Wasanii wa bongo movie wakishiri kufanya usafi
katika eneo la mnara wa askari makutano ya barabara ya Samora na Azikiwe jijini Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON-FULLSHANGWEBLOG
katika eneo la mnara wa askari makutano ya barabara ya Samora na Azikiwe jijini Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON-FULLSHANGWEBLOG
Wasanii wa bongo movie wakishiri kufanya usafi
katika eneo la mnara wa askari makutano ya barabara ya Samora na Azikiwe jijini Dar es Salaam.
katika eneo la mnara wa askari makutano ya barabara ya Samora na Azikiwe jijini Dar es Salaam.
Mbunge wa jimbo la Ilala,Mhe.
Mussa Azzan Zungu , akihojiwa na waandishi wa habari wakati aliposhiriki
siku ya usafi kitaifa, katika eneo la mnara wa askari makutano ya
barabara ya Samora na Azikiwe jijini Dar es Salaam .
Wasanii wa Bongo Muvie,
wakishiriki kupakia taka kwenye gari lenye namba za usajili Su 39012
mali ya shirika la Nyumba Taifa NHC katika eneo la Posta jijini Dar es
Salaam.
Wauza matunda wakiendelea na biashara hiyo mtaa wa Zanaki jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wananchi wa Manispaa ya
Temeke wakifanya usafi katika dampo lililopo Mwembe yanga ambalo
limekuwa kero kwa wakazi wake kutokana na kutoa harufu kali na kupelekea
wasiwasi wa wakazi kupata ugonjwa wa kipindupinndu kama walivyokutwa na
kamera yetu jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wafanyakazi wa kitengo
cha madawa ya binadamu, bohari kuu, wakifanya usafi wa mazingira
kandokando mwa jengo hilo kama walivyonaswa na kamera yetu jijini Dar es
Salaam jana, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John
Pombe Magufuli.
Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange na Mkuu wa Brigedi ya Chui Brigedia Jenerali Sharif Othman wakishiriki kufanya usafi maadhimisho ya uhuru
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali
Davis Mwamunyange(kulia), Mkuu wa Brigedi ya Chui Brigedia Jenerali
Sharif Othman(kushoto) pamoja na Maafisa na Askari wakishiriki zoezi la
usafi katika kambi ya Lugalo, jijini Dar es Salaami wakati wa
kuadhimisha miaka 54 ya Uhuru kama alivyoagiza Rais na Amiri Jeshi Mkuu
Dkt. John Pombe Magufuli
MABONDIA ZUMBA KUKWE NA SELEMANI GALILE WATAMBIANA KUZIDUNDA JANUARR 2, MANZESE
Mabondia Seleman Galile kushoto na Zumba Kukwe wakitunishiana misuli baada ya kusaini makubaliano ya kupigana january 2 katika ukumbi wa Frends Corner Manzese Dar es salaam Picha na SUPER D BOXING NEWS |
Mabondia Seleman Galile kushoto na Zumba Kukwe wakitunishiana misuli baada ya kusaini makubaliano ya kupigana january 2 kwenye mpambano wa kufungulia mwaka utakaofanyika katika ukumbi wa Frends Corner Manzese Dar es salaam Picha na SUPER D BOXING NEWS |
Bondia Hussein Mbonde kushoto wakitunishiana misuli na Shomari Milundi wakati wakitambulisha mpambano wao utakaofanyika january 2 katika ukumbi wa Frends Corner Manzese Dar es salaam Picha na SUPER D BOXING NEWS |
Bondia Hussein Mbonde kushoto wakitunishiana misuli na Shomari Milundi wakati wakitambulisha mpambano wao utakaofanyika january 2 katika ukumbi wa Frends Corner Manzese Dar es salaam katikati ni Pembe Ndava Picha na SUPER D BOXING NEWS |
Bondia Hussein Mbonde kushoto wakitunishiana misuli na Shomari Milundi wakati wakitambulisha mpambano wao utakaofanyika january 2 katika ukumbi wa Frends Corner Manzese Dar es salaam Picha na SUPER D BOXING NEWS |
Mabondia Hussein Mbonde wa pili
kulia na Shomari Milundi wakiwa na makocha wao kushoto ni Cristopher
Mzazi na Mohamed Mbade mbade wakati wa utambulisho wa mpambano wao
utakaofanyika january 2 katika ukumbi wa Frends Corner Manzese Dar es
salaam Picha na SUPER D BOXING NEWS
DK. SHEIN AJUMUIKA WATANZANIA KATIKA WAZANZIBARI KUADHIMISHA DISEMBA 9KWA KUFANYA USAFI LEO
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Mstahiki Meya wa
Manispaa ya Zanzibar Khatib Abrahman Khatib wakati alipowasilikati eneo
la Malindi Mjini Zanzibar katika zoezi ka Usafi wa mazingira katika
kuadhimisha miaka 54 ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
lililoshirikisha Viongozi na Wananchi mbali mbali nchini.[Picha na
Ikulu.]
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akizoa taka katika zoezi ka Usafi wa mazingira katika kuadhimisha miaka
54 ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania eneo la Malindi Mjini
Unguja leo zoezi ambalo liliwashirikisha Viongozi na Wananchi mbali
mbali nchini (kushoto) Waziri wa Ardhi,Maji,Makaazi na Nishati Ramadhan
Abdalla Shaaban,[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizoa taka katika zoezi ka
Usafi wa mazingira katika kuadhimisha miaka 54 ya Muungano wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania eneo la Malindi Mjini Unguja leo zoezi ambalo
liliwashirikisha Viongozi na Wananchi mbali mbali nchini (kushoto)
Waziri wa Ardhi,Maji,Makaazi na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban,[Picha
na Ikulu.]
Baadhi ya Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ walishiriki katika zoezi
ka Usafi wa mazingira katika kuadhimisha miaka 54 ya Muungano wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania eneo la Malindi Mjini Unguja leo zoezi
ambalo liliwashirikisha Viongozi na Wananchi mbali mbali nchin,[Picha na
Ikulu.]
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(katikati) akimimina taka katika kontena baada ya kufanya usafi wa
madhingira leo wakati wa zoezi hilo lililofanyika nchi nzima katika
kuadhimisha miaka 54 ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
ikiwemo eneo la Malindi Mjini Unguja,ambapo viongozi mbali mbali
walijumuika katika kufanikisha kazi hiyo,[Picha na Ikulu.]
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(katikati) akitoa nasaha zake baada ya kumalizika kwa zoezi la kufanya
usafi wa madhingira leo wakati wa zoezi hilo lililofanyika nchi nzima
katika kuadhimisha miaka 54 ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ikiwemo eneo la Malindi Mjini Unguja,ambapo viongozi mbali
mbali walijumuika katika kufanikisha kazi hiyo,(kushoto)Mstahiki Meya wa Manispaa ya Zanzibar Khatib Abrahman Khatib, [Picha na Ikulu.]
Baadhi ya Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ walishiriki katika zoezi
ka Usafi wa mazingira katika kuadhimisha miaka 54 ya Muungano wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania eneo la Malindi Mjini Unguja leo zoezi
ambalo liliwashirikisha Viongozi na Wananchi mbali mbali nchin,[Picha na
Ikulu.]
Wizara ya Fedha yaadhimisha sherehe za Uhuru kwa kufanya usafi
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt.
Servacius Likwelile (wa tatu kulia) akielekea eneo la kufanya usafi
kuzunguka maeneo ya ofisi za wizara hiyo leo jijini Dar es salaam ikiwa
ni mwitikio na utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli la kufanya usafi katika eneo ya
kazi wakati wa maadhimisho ya sherehe za Uhuru mwaka huu.
Mkurugenzi wa Utawala na
Rasilimali Watu (DHRM) Wizara ya Fedha Deodata Makani akitoa maelekezo
ya kufanya usafi kuzunguka ofisi za Wizara hiyo leo jijini Dar es
salaam.
Baadhi ya watumishi wakikata
matawi ya miti kwa makini bila kuharibu nya za simu yaliyokuwa kizuizi
katika barabara eneo la ofisi za wizara ya fedha kwa lengo la kufanya
usafi leo jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt.
Servacius Likwelile akiendelea kufanya usafi katika moja ya sehem ya
kuzunguka maeneo ya ofisi za wizara hiyo leo jijini Dar es salaam ikiwa
ni mwitikio na utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli la kufanya usafi katika eneo ya
kazi wakati wa maadhimisho ya sherehe za Uhuru mwaka huu.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt.
Servacius Likwelile akiongea na watumishi wa wizara hiyo leo jijini Dar
es salaam mara baada ya kumaliza zoezi la kufanya usafi ikiwa ni
mwitikio na utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli la kufanya usafi katika eneo ya kazi
wakati wa maadhimisho ya sherehe za Uhuru mwaka huu.
…………………………………………………………………………………………..
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt.
Servacius Likwelile leo ameiongoza wizara hiyo katika kuitikia na
kutekeleza agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli la kufanya usafi katika eneo lao la kazi katika
maadhimisho ya sherehe za Uhuru ya mwaka huu.
Akiongea na watumishi wa Wizara
hiyo, Dkt. Likwelile alisema kuwa maadhimisho ya siku ya uhuru yaendelee
kutumika kama kichocheo cha kujenga tabia ya kufanya kazi ikizingatiwa
dhana iliyokuwepo tangu uhuru ilikuwa “Uhuru na Kazi” ambapo kwa sasa
kaulimbiu ya Rais Dkt. Magufuli inasema “Hapa Kazi Tu”
“Ni uamuzi mzuri wa Rais, ni wa
busara na unaendana na tulipotoka ambapo Tanzania inaamini katika “Uhuru
na Kazi”, huu ni mwanzo wa kusimama kwa miguu yetu wenyewe ili
kujiletea maendeleo kwa kuendelea kuwapiga vita maadui watatu wa taifa”
alisema Dkt. Likwelile.
Dkt. Likwelile aliwataja maadui
hao kuwa ni ujinga, maradhi na umasikini ambao ndiyo wamekuwa chanzo cha
kurudisha nyuma juhudi za maendeleo, kwa kuimarisha suala la usafi
katika mazingira yote nchini, itakuwa mwanzo wa kupambana na suala
magonjwa milipuko ikiwemo kipindupindu ambao asili yake ni uchafu.
Aidha, Dkt. Likwelile aliwaasa
watumishi wa wizara hiyo na Watanzanaia kwa ujumla kuenzi kazi
iliyonzishwa na Mhe. Rais Dkt. Magufuli ya kufanya usafi na zoezi hilo
liwe endelevu na la kudumu ambapo ameahidi kuwa wizara yake itapanga
siku ya kufanya usafi mara kwa mara katika maeneo ya kazi ili kudumisha
usafi ambao ni suala muhimu katika kuimarisha afya zao na ikizingatiwa
watumishi hutumia muda mwingi wakiwa katika maeneo ya kazini.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
Utawala na Rasilimali Watu (DHRM) Wizara ya Fedha Deodata Makani alisema
kuwa mwitikio wa watumishi katika zoezi la usafi umekuwa mkubwa na
wanapendekeza zoezi hilo liwe endelevu maana watumishi hutumia muda
mwingi katika maeneo ya kazini hivyo ni vema kuyaweka mazingira hayo
katika hali ya usafi ili yawe rafiki wakati wote wa kutekeleza majukumu
yao.
Naye mmoja wa watumishi wa
Wizara hiyo William Muhoja alisema kuwa zoezi la kufanya usafi katika
maeneo ya kazi linatakiwa kufanywa kila wakati ambapo itakuwa ni sehemu
ya watumishi kuwajibika kwa jamii katika maeneo yao wanapoishi na
wanapofanya kazi.
Sherehe za uhuru mwaka huu
nchini zimeadhimishwa kwa namna tofauti na ilivyozoeleka miaka iliyopita
ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe
Joseph Magufuli kwa mamlaka aliyonayo kikatiba alitangaza maadhimisho ya
Sherehe za Uhuru na Jamhuri ya 9 Disemba mwaka huu, Watanzania wote
waitumie kwa kufanya kazi mbalimbali kama vile, mashambani, maofisini,
sokoni, viwandani na usafi wa miji yao katika kutimiza dhana ya Uhuru na
Kazi kwa vitendo.
Maadhimisho hayo yanaendelea
nchi nzima ambapo kila halmashauri inatekeleza agizo la Mhe. Rais kwa
vitendo kwa kufanya usafi katika maeneo yao, zoezi linashirikisha
Wizara, idara, taasisi za Kiserikali na zisizo za kiserikali, maeneo ya
viwanda, shule, vyuo, maeneo ya biashara, masoko na kuzunguka maeneo
yote ya makazi ya watu.
TAMASHA KUBWA LA MSAFARA LINALOWAHUSISHA VIJANA KUFANYIKA JUMAMOSI HII IFAKARA MOROGORO.
Kutoka
kushoto ni Manoah William Waziri wa Elimu Serikali ya wanafunzi Chuo
Kikuu cha Dar es salaam, Agnes Inocent wa YFF, James Isdore Mwenyekiti
wa Msafara,Fadhiri Meta kutoka Youth can na Batseba Modest kutoka Ngao
youth wakiongea katika mkutano huo na waandishi wa Habari leo 9.12.2015
James Isdore Mwenyekiti wa Msafara akizungumzia Shughuli ya msafa kwa ujumla
Fadhiri
Meta kutoka Youth can akizungumzia jinsi Msafara ulivyopokelewa vizuri
na mpaka sasa wamepata zaidi ya vijana 500 ambao wanajifunza
ujasiliamali na kuibua vipaji na ubunifu mbalimbali.
Agnes Inocent akizungumzia jinsi watakavyo hamasisha wanawake wengine kujitambua na kuwa wanaweza.
Batseba Kassanga (Kulia) akitoa wito kwa vijana namna wanavyoweza kujikomboa kupitia Msafara
Noah William akifafanua jambo kuhusiana na Msafara
Mkutano ukiendelea
Programu ya
Msafara inayoendeshwa asasi tano za kiraia ambazo ni; YouthCAN, TYDC, DARUSO,
NGAO YOUTH na Young Feminist Forum kwa uratibu wa Shirika la Oxfam, inatarajiwa
kufanyika mapema kesho kutwa katika Mkoa wa Morogoro wilayani Ifakara.

Programu
inayolenga kuwahamasisha vijana kubuni njia za kujikwamua kiuchumi kupitia
wenzao waliofanikiwa, itafanyika kwa njia ya tamasha kubwa katika eneo la
Uwanja wa Taifa, Ifakara mkoani Morogoro ambapo ndani ya tamasha hilo mitaji na
motisha ya kukabidhiwa vitendea kazi itagaiwa kwa vijana wenye umri kuanzia
miaka 15 hadi 24.

Mbali na
kutoa elimu na motisha hiyo, tamasha hilo litapambwa na burudani za aina mbalimbali
huku pia kukiwa na vijana waliofanikiwa watakao wahamasisha wenzao kupitia kauli
mbiu ya Inspire, Aspire and Activate.

Bayport yamuunga mkono Dr Magufuli kwa vitendo, yapaka rangi, yafagia shule ya msingi Hekima
Mkurugenzi
Mkuu wa Bayport Financial Services, John Mbaga, akipaka rangi katika
ukuta wa shule ya Msingi Hekima, iliyopo Tandale, wilaya ya Kinondoni,
jijini Dar es Salaam leo mchana. Picha zote kwa Hisani ya Bayport
Financial Services.
Meneja wa Oparasheni wa Bayport Financial Serviices, Charles Mgeta, akizungumza na waandishi wa habari juu ya taasisi yao kuamua kufanya usafi, kutunza mazingira na kuipaka rangi shule ya msingi Hekima, iliyopo Kata ya Tandale, Wilaya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, kushoto mwenye kofia na miwani akishiriki kufanya usafi katika shule ya Msingi Hekima, iliyopo Tandale, wilayani Kinondoni, jijini Dar es Salaam, asubuhi.
Wafanyakazi wa Bayport, walimu na wanafunzi wakijiandaa kufanya usafi mbele ya jengo la shule ya Hekima, kabla ya kuanza kupakwa rangi.
Mchambuzi wa Miradi wa Bayport Financial Services, Joseph Munga, kulia akishiriki kupaka rangi katika shule hiyo ya msingi Hekima.

………………………………………………………………………………….
TAASISI ya
Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na utoaji wa mikopo, jana
imemuunga mkono kwa vitendo Rais wa Jamhuri ya Muungano Dr John Pombe Magufuli
kwa kufanya usafi, kutunza mazingira na kupaka rangi shule ya Msingi Hekima,
iliyopo Kata ya Tandale, wilaya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, huku wakianza
kwanza kusafisha eneo la Makao Makuu ya ofisi yao, kabla ya kuelekea hapo. Tukio hilo
liliongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Bayport, John Mbaga, pamoja na zaidi
ya wafanyakazi 80 kwenye taasisi hiyo inayotoa mikopo ya fedha kwa watumishi wa
umma na wafanyakazi wa kampuni binafsi, bila kusahau wajasiriamali katika mradi
wao wa mikopo ya viwanja vilivyopo Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani. Shughuli
hiyo Ilianza mishale ya saa tatu asubuhi ambapo Mkurugenzi huyo na wafanyakazi
wa Bayport walianza kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya shule hiyo,
pamoja na upakaji wa rangi katika baadhi ya madarasa katika shule hiyo yenye
wanafunzi zaidi 1900, ukiacha idadi kubwa ya wanafunzi wa darasa la kwanza
watakaonza shule mapema mwakani.

Wafanyakazi wa Bayport Financial Services wakiendelea na usafi katika shule ya msingi Hekima.
Akizungumza
katika tukio hilo leo asubuhi, Mkurugenzi wa Bayport Financial Servivces, John Mbaga,
alisema kwamba wameamua kuchagua shule ya Tandale kwa sababu inahitaji kuungwa
mkono kutokana na eneo iliyopo pamoja na changamoto mbalimbali za kimaisha. Alisema
baada ya rais kuagiza kwamba Sikukuu ya Uhuru 9 Desemba iendane na kazi ya
kufanya usafi na utunzaji wa mazingira, Bayport iliamua kwenda mbali zaidi kwa
kuhakikisha kwamba wanaipaka rangi shule hiyo ili ionekane safi, tofauti na
ilivyokuwa awali.

Usafi ukiendelea shuleni hapo
Usafi ukiendelea
“Tunamuunga
mkono Dr Magufuli na serikali yake kwa vitendo, hivyo si usafi tu, ila
tumeirudisha shule ya Msingi Hekima kwenye upya wake, huku tukiamini kuwa
tutaendelea kujikita zaidi katika mambo ya kijamii, hususan katika suala zima
la elimu kwa kusaidia kila kilichokuwa ndani ya uwezo wetu” alisema Mbaga.

Naye Meneja
Masoko na Mawasiliano wa Bayport, Ngula Cheyo, alisema kwamba wamefurahia
kushirikiana na walimu na wanafunzi wa shule ya Msingi Hekima kufanya nao usafi
na kutunza mazingira ya eneo la shule hiyo inayotumiwa na watoto wengi kutoka
kwenye Kata hiyo ya Tandale. “Bayport ni
taasisi ya Watanzania wote, wakiwamo watumishi wa umma na wafanyakazi wa
kampuni binafsi, hivyo naamini itaendelea kutoa huduma bora zenye kuwakwamua
wateja wetu,” alisema Cheyo.

Naye Mwalimu
Mkuu wa shule ya Msingi Hekima, Hussein Mohamed, aliishukuru Bayport kwa
kujitolea kurudisha upya wa shule yao kwa kuamua kuipaka rangi, pamoja na
kushirikiana nao katika 9 Desemba kufanya usafi, jambo ambalo ni muhimu ili
kujiepusha na magonjwa ya miripuko, ukiwamo ugonjwa wa Kipindupindu.

“Hatuna cha
kuwalipa Bayport kwa kujitolea kwao kwetu, hivyo tunawaombea kwa Mungu, ingawa
tunazidi kuwaomba waendelee kuwa karibu na sisi kwa kutusaidia mambo mbalimbali
ili tufanikishe kwa vitendo kuwapatia watoto wetu elimu bora ili kuwaandalia
maisha bora wanafunzi hawa ambao licha ya changamoto kadhaa zinazotukabili, ila
ufaulu wao umekuwa ni mkubwa, jambo linalotutia moyo,” alisema Mohamed. Bayport ni
moja ya taasisi zinazofanya juhudi kubwa kuwakwamua wateja wao, wakiwamo
watumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni binafsi kwa kupewa mikopo isiyokuwa
na amana wala dhamana, huku huduma hizo zikipatikana kwa urahisi kutokana na
kuenea kwa matawi zaidi ya 80 katika wilaya na mikoa mbalimbali ya Tanzania
Bara.

WAFANYAKAZI WA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII WAFANYA USAFI MAENEO MBALIMBALI JIJINI DAR ES SALAAM
Wafanyakazi wa Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii wakifanya usafi katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road
ikiwa ni kutekeleza agizo la Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli la
kufanyika kwa usafi wa mazingira nchi nzima ikiwa ni maadhimisho ya
miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Makatibu wakuu wa Wizara ya Afya
na Ustawi wa Jamii Dkt .Donan Mmbando (wapili kulia) na Ofisi ya Waziri
Mkuu Tawala za Mikoa na Seikali za Mitaa (TAMISEMI) Ndg. Jummanne
Sagini (watano kulia) wakifanya usafi katika Soko la Samaki la Feri
jijini Dar es Salaam. Wengine walioshirikia kazi ya kufanya usafi ni
wafanyakazi wa wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii wakifanya usafi wa mazingira leo katika soko la
samaki la Feri ikiwa ni kutekeleza agizo la Mhe. Rais Dkt. John Pombe
Magufuli la kufanyika kwa usafi wa mazingira nchi nzima ikiwa ni
maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii Dkt. Donan Mmbando akiongea na waandishi wa Habari
waliofika katika soko la samaki la Feri jijini Dar es Salaam kuona jinsi
usafi wa mazingira ulivyokuwa unafanyika sokoni hapo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii wakifanya usafi wa mazingira leo katika soko la
samaki la Feri ikiwa ni kutekeleza agizo la Mhe. Rais Dkt. John Pombe
Magufuli la kufanyika kwa usafi wa mazingira nchi nzima ikiwa ni
maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii Dk.Donan Mmbando akiongea na wafanyakazi wa wizara
hiyo mara baada ya kumalizika kwa kazi ya kufanya usafi wa mazingira
katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam. Wafanyakazi wa wizara
hiyo walifanya usafi katika mahabusu ya watoto Kisutu, Makazi ya Wazee
ya Nunge, Taasisi za Mifupa MOI na Saratani ya Ocean Road, Hospital ya
Taifa Muhimbili, Masoko ya Kariakoo na Feri, na Mbagala Zakhem.
Wafanyakazi wa Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii wakiwa na nyuso za furaha mara baada ya kumaliza kazi
ya kufanya usafi wa mazingira katika maeneo mbalimbali jijini Dar es
Salaam. Wafanyakazi wa wizara hiyo walifanya usafi
Picha na Anna Nkinda – Maelezo
Kwaya ya Kinondoni Revival Tamasha la Krismasi
Na Mwandishi Wetu
KWAYA mahiri ya nyimbo za Injili, Kinondoni Revival ni
mojawapo ya watakaosindikiza Tamasha la Krismasi linalotarajia kufanyika
Desemba 25 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE ASHIRIKI ZOEZI LA USAFI SOKO KUU LA CHALINZE
Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho
Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng.
Evarist Welle Ndikilo wakielekea soko kuu la Chalinze kushirikiana na
wananchi kufanya usafi wa mazingira leo Desemba 9, 2015 ikiwa ni
kuadhimisha miaka 54 ya UHURU kama ilivyoagizwa na Rais Dkt John Pombe
Joseph Magufuli
Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho
Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakifanya usafi katika soko kuu la
Chalinze leo Desemba 9, 2015 ikiwa ni kuadhimisha miaka 54 ya UHURU kama
ilivyoagizwa na Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli

Kikwete na wananchi wa Chalinze baada ya kushirikiana nao kufanya usafi
wa mazingira ya soko kuu la Chalinze leo Desemba 9, 2015 ikiwa ni
kuadhimisha miaka 54 ya UHURU kama ilivyoagizwa na Rais Dkt John Pombe
Joseph Magufuli
Mkuu wa Mkoa azindua kampeni ya upigaji dawa mabasi ya mikoani
Na Immaculate Makilika, MAELEZO
Mkuu wa Mko wa Dar es Salaam
Saidi Meck Sadick leo katika eneo la Standi ya mabasi Ubungo,
amezindua kampeni ya upigaji dawa ya kuuwa wadudu kwa mabasi yaendayo
mikoani na nchi jirani.
Uzinduzi huo umefanyika ikiwa ni
sehemu ya kuunga mkono jitihada za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli ambaye aliamua maadhimisho ya
sherehe za miaka 54 kwa mwaka huu yafanyike kwa wananchi kushiriki
kufanya usafi katika maeneo yao.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya kuwa
na ongezeko kubwa la idadi ya wagonjwa wa kipindupindu ambapo imefikia
idadi ya zaidi ya vifo 165 nchi nzima, na kupelekea Mheshimiwa Rais
kufikia uamuzi huo.
Aidha, zoezi hilo la upigaji dawa
ya kuuwa wadudu kwa mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani limeanza
tangu tarehe 7/12/2015 ambapo hadi sasa mabasi zaidi ya 70 tayari
yameshapigwa dawa, huku matarajio ni kufikia mabasi 1,000.
Mkuu wa Mkoa alipongeza jitihada
zilizofanywa na Chama cha wamiliki wa mabasi Tanzania (TABOA) kwa
kuandaa utaratibu huu kwa kushirikian na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri
wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) pamoja na Jeshi la Polisi kikosi cha
Usalama Barabarani na kusema kuwa “ usafi huu ni endelevu usisubiri
matukio kama haya peke yake, anagalau ufanyike kila baada ya miezi 4
au 6”.
Aliendelea kwa kusema kuwa,
baadae utaratibu huo utafanyika pia kwa daladala zote zinazofanya
safari zake katika jiji la Dar es salaam ili kuhakikisha afya za
wasafiri zinakuwa katika hali ya usalama, na pia aliwataka wamiliki
kuweka vifaa vya kutupa taka katika daladala zao.
Naye, Kamanda wa Polisi wa
kikosi cha usalama Barabarani Mohammed Mpinga amesema zoezi hili ni
zuri kwa kuwa linasaidia kuhakikisha usalama wa abiria kwa kuzuia
kupata magonjwa kutokana na maambukizi yanayotokana na wadudu kama
kunguni na mende.
Aidha, mmoja wa wamikili wa mabasi
Bwana. Issa Nkya amesema zoezi hili linaendelea vizuri, na
kuhakikisha kuwa mabasi yote yatapigwa dawa kufikia tarehe 15/12/2015
hadi tarehe 20/12/1015, pia ametoa wito kwa kwa wamiliki wa mabasi
kuhakikisha mabasi yao yanapigwa dawa.
Huku, mmoja wa abiria Bwana. Thabiti Mfaume naye amesema amefurahishwa na zoezi hilo na kuomba liwe endelevu.
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
imekua ikiadhimisha sherehe za Uhuru kila mwaka tangu Uhuru wa nchi hii
tarehe 9 Desemba, 1961. Ambapo mwaka huu imekua tofauti baada ya Rais
John Magufuli kuwataka wananchi kushiriki katika kampeni ya usafi kwa
kufanya usafi katika maeneo mbalimbali nchi nzima.
Ambapo, wananchi katika maeneo
yao nchi nzima wameitikia wito wa kampeni hiyo kwa kushiriki kwa
kufanya usafi na kuungwa mkono na viongozi mbalimbali akiwemo Rais
Magufuli ambaye amefanya usafi katika eneo la soko la samaki Feri,
Waziri Mkuu Mheshimiwa Majaliwa Khasim Majaliwa naye ameshiriki
kufanya usafi katika eneo la soko kuu la Kariakoo jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo afungua maoyesho ya 10 ya filamu za Asia.
: Balozi wa Japan nchini Tanzania
Bw,Masaki Okada(wa kwanza kushoto) akizungumza jambo na Katibu Mkuu
Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole
Gabriel(katikati) wakati wa uzinduzi wa maonyesho ya 10 ya filamu za
Asia.Aliyesimama pembeni yao ni katibu mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini
Tanzania Bi.Joyce Fisoo.
Katibu Mkuu Wizara ya
Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel(wa tano
kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na mabalozi wa nchi za
Asia katika uzinduzi wa maonyesho ya 10 ya filamu za Asia.
Katibu Mkuu Wizara ya
Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel
akifungua maonyesho ya 10 ya Filamu za Asia.Pembeni yake ni mabalozi wa
nchi mbalimbali za Asia walihoudhuria uzinduzi huo.Maonyesho Hayo
yatafanyika kuanzia tarehe 8-17 desemba katika ukumbi wa Century
Cinemax Dar Free Market Oysterbay.
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu
Bi.Joyce Fisoo akifurahia jambo wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya 10
ya Filamu za Asia katika ukumbi wa Dar free Market jijini Dar es salaam.
TPB YASAFISHA SOKO LA FERI, YATOA VIFAA VYA USAFI, NI KATIKA KUUNGA MKONO UAMUZI WA RAIS MAGUFULI WA UHURU NI KAZI
Kaimu
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, TPB, Henry Bwogi, akizibua
chemba ya kupitisha maji taka kwenye zoni 3 ya soko la samaki la kimataifa Feri
jijini Dar es Salaam Desemba 9, 2015. TPB imeungana na watanzania katika kuunga
mkono agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuwataka wananchi
kusherehekea sikukuu ya Uhuru wa Tanganyika kwa kufanya usafi ili kutekeleza
zana ya “Uhuru ni Kazi” badala ya kufanya sherehe na matamasha huku nchi
ikakabiliwa na ugonjwa wa Kipindupindu

………………………………………………………………………
Na
K-Vis Media/Khalfan Said)
K-Vis Media/Khalfan Said)
KATIKA
kuunga mkono maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa wananchi
na taasisi za serikali kufanya usafi siku ya maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru
wa Tanganyika, Benki ya Posta Tanzania, TPB, nayo iliungana na wananchi hususan
eneo la soko la kimataifa la samaki Feri, katika kutekeleza agizo hilo.

Wakati
Mh. Rais alishirikiana na majirani zake, wavuvi na wachuuzi wa samaki pale nje
kidogo ya uzio wa Ikulu, hali ilikuwa hivyo hivyo kwenye maeneo mengi, ya nchi
ambapo katika eneo hilo la soko la Feri, TPB walipewa eneo la kufanyia usafi
kwenye zoni namba 1 na eneo la kuegeshea mitumbwi maarufu kama “Lebanon” ambapo
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Bw. Henri Bwogi, aliwaongoza
wafanyakazi wa benki hiyo katika kufagia, kuzibua mitaro na chemba za maji
taka, hali kadhalika kupakia taka kwenye malori ya kubebea taka.

Katika
hatua nyingine Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Bw. Bwogi, alikabidhi
vifaa vya kufanyia uasafi viliovyokuwa vikitumiwa na wafanyakazi wa benki hiyo
kwa uongozi wa soko ili waendelee na kazi ya usafi siku za usoni.

wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli,
aliagiza sherehe za mwaka huu za Uhuru wa Tanganyika, zisherehekewe kwa kufanya
kazi ili kutekeleza zana ya “Uhuru ni Kazi” badala ya kufanya matamasha na shamra
shamra kwenye viwanja mbaklimbali nchini.

“
Nimefurahishwa sana na wananchi jinsi walivyojitokeza kwa wingi kwenye maeneo
mbaklimbali ya nchi katika kufanya usafi ili kuiweka nchi yetu safi na
kujikinga na maradhi kama Kipindupindu.” Rais Magufukli aliwaambia majirani
zake baada ya zoezi la kufanya usafi.

Naye
Kaimu Afisa Myendaji Mkuu wa TPB, Bw. Bwogi, alisema TPB kama taasisi ya
serikali iliamuru wafanyakazi wake, wafike kazini na kushiriki katika kufanya
usafi na sisi tumeona tuje kuungana na wenzetu wa feri ili kutekeleza maelekezo
ya Rais wetu.” Alisema.

Mfanyakazi wa TPB, akizibua chemba katika kutekeleza zana ya Uhuru ni Kazi
Usafi wa Disemba 9 wang’arisha Soko la Tandale
Na Jacquiline Mrisho
Mazingira ya Soko la Tandale jijini Dar r
es salaam yamekua safi baada ya usafi mkubwa kufanywa leo na
wafanyabiashara pamoja na Makampuni mbalimbali yaliyojitolea kusaidia
kusafisha mazingira hayo.
Akiongea na mwandishi, Mtendaji
wa Kata ya Tandale Bw.Ole Losai amesema kuwa usafi wa kawaida huwa
unafanyika sokoni hapo ila changamoto kubwa ni ukosefu wa vifaa pamoja
na magari ya kubebea uchafu kutokuja kwa wakati kwakua soko la Tandale
linapokea zaidi ya tani 28 za uchafu kwa siku kutoka kwenye vifungashio
vya bidhaa mbalimbali ziletwazo sokoni hapo.
“Tamko la Muheshimiwa Rais ni zuri
sana maana sherehe za uhuru zimesherehekewa na watu wote kwa kufanya
usafi wa mazingira “alisema Bw. Losai.
Aliongeza kuwa ,kwa Wilaya ya
Kinondoni hasa Kata ya Tandale usafi ulianza kufanyika tangu Disemba 1
baada ya kufanya uzinduzi wa usafi katika Wilaya hiyo ambapo Mtendaji wa
Kata pamoja na watendaji wa Manispaa ya Kinondoni walipita kila mtaa
kuwahamasisha wananchi kufanya usafi katika maeneo yao.
Aidha Mwenyekiti wa Soko
hilo,Bw.Mohamedi Mwekya ametoa salamu za pongezi kwa Muheshimiwa Rais
John Pombe Magufuli kwa kutoa tamko la kufanya usafi wa mazingira pamoja
na kulisimamia hadi kukamilika kwake hivi leo.
“Matamko mengi huwa yanatamkwa na
viongozi mbalimbali lakini hayafanyiwi utekelezaji ila hili la
Muheshimiwa Rais,watu wamelipokea na wamefanya usafi kwa bidii hata hali
ya soko letu inaridhisha”amesema Bw. Mwekya.
Pia Bw. Mwekya aliyapongeza
makampuni na vikundi mbalimbali vya kijamii ambavyo vimejitolea kusaidia
kufanya usafi katika Soko la Tandale ambapo aliyataja baadhi ya
Makampuni na vikundi hivyo vya Kijamii vilivyoshiriki kuwa ni chombo
cha habari cha Clauds Media Group, Msalaba Mwekundu,Max Malipo, Benki ya
Biashara ya Akiba (ACB), Watendaji wa Manispaa,Shirika la Afya Duniani
(WHO) na Kliniki ya tiba mbadala ya Ifakara Herbalist Clinic iliyopo
Tandale.
Akiongea na mwandishi,mmoja wa
wafanyabiashara wa soko hilo Bw.Gasper Muhumba alisema,wito wa wananchi
umekua mkubwa na wamewahi kuanza usafi kabla hata ya muda uliopangwa (sa
moja asubuhi) na hii inaonyesha kuwa watu wamependa na wamekubaliana na
wazo la Muheshimiwa Rais John Pombe Magufuli ndio maana wamefanya kazi
ya kusafisha mazingira kwa juhudi.
Tamko hili lilitolewa na Rais John
Pombe Magufuli kuwa badala ya wananchi kujumuika uwanjani kuazimisha
siku ya Uhuru,maadhimisho hayo yatafanyika kwa kufanya usafi katika
maeneo yetu yanayotuzunguka ili kuzuia magonjwa ya milipuko kama
kipindupindu.
Wananchi wazingatie Mipango Miji kudumisha Usafi
Diwani
wa kata ya Kawe Mhe. Muta Rwakatare akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa
habari (hawapo pichani) kuhusu usafi katiak kata ya ya kawe ikiwa ni
utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais Dkt Magufuli kufanya usafi siku ya
Disemba 9.
……………………………………………………………………………………………..
Na Raymond Mushumbusi -Maelezo
Hayo yamesemwa
leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Bw. Alphayo Kidatu aliposhiriki
kufanya usafi katika eneo la mto Mbezi maarufu kwa jina la darajani kwa
Malecela ikiwa ni kuunga mkono tamko la Mhe Rais Dkt John Pombe Joseph
Magufuli la kuitangaza siku ya Disemba 9 kuwa ni siku ya uhuru na kazi.
Katibu Mkuu
Alphayo Kidatu amesema kuwa usafi sio kusafisha maeneo tu ya makazi na
sehemu za huduma pia ni kuzingatia mipango miji kwa kutovamia maeneo ya
wazi, kujenga kiholela bila mipango na kuvamia sehemu za vyanzo vya maji
kwa kuchimba mchanga na kufanya yale yote yanayohatarisha usafi wa
mazingira.
“ kwa sasa
wizarani tunahakikisha tunatoa ramani za mipango miji kwenda mpaka
serikali za mitaa ili wananchi na watendaji wa serikali za mitaa wajue
maeneo ya wazi yako wapi ili waweze kuyasimamia.” Alisema Kidatu.
Naye Diwani wa
kata ya Kawe Mhe. Muta Rwakatare amesema kata yake inachangamoto za
kukosa huduma ya kukusanya taka na kwa sasa wameamua kufunga dampo
ndogol ililopo pembezoni mwa mto Mbezi ili kuepusha magonjwa ya mlipuko.
“ kama viongozi
hatuwezi kusubiri Manispaa waleta magari ya kuzoe taka mimi kama diwani
nitahakikisha anakuwepo mkandarasi wa kuzoa taka katika kata yangu na
swala hili nitalisimamia kwa karibu” Alisema Rwakatare.
Naye mtendaji wa
kata ya kawe Bw. Raymond Chimbuya amesema wanaunga mkono siku ya leo na
halitaishia leo tu bali watajiwekea utaratibu kwa kushirikia na diwani
na wananchi kufanya usafi kuwa ni desturi na sio mpaka walazimishwe.
Akizungumza mmoja
ya wananchi wa kata yak awe Bw. Hussein Bana amesema wanapenda kufanya
usafi ila changamoto zimekuwa ni vifaa vya usafi, watu kutojitoa kufanya
usafi maeneo yao na ufatiliaji mbovu katika serikali za mitaa hivyo
watendaji wafatilie kwa karibu ili kunusuru afya za wa watanzania na
watanzania tuwe na desturi ya usafi.
Disemba 9
ilitangazwa rasmi na Mhe rais dkt John Pombe Joseph Magufuli kuwa ni
siku ya uhuru na kazi na wananchi wafanye usafi katika maeneo yao ili
kupiga vita ugonjwa wa kipindipindu unaoenea kwa kasi nchini.
MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN ASHIRIKI NA WANANCHI WA ENEO LAKE KUFANYA USAFI WA MAZINGIRA, MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akishiriki kufagia na baadhi ya wananchi wakazi wa eneo lake la
Oysterbay Karume Raod, wakati wa zoezi la kufanya usafi wa mazingira
ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania kama
alivyoagiza Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo zoezi hilo
limefanyika nchini kote hii leo Dec 9, 2015. Picha na OMR

akishiriki kuzoa taka na baadhi ya wananchi wakazi wa eneo lake la
Oysterbay- Karume Raod, wakati wa zoezi la kufanya usafi wa mazingira
ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania kama
alivyoagiza Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo zoezi hilo
limefanyika nchini kote hii leo Dec 9, 2015. Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akiwasili eneo la Kituo cha Daladala cha Morocco, kwa ajili ya kuendelea
kushiriki na wananchi wa eneo hilo kufanya usafi wa mazingira ikiwa ni
sehemu ya maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania kama alivyoagiza
Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo zoezi hilo limefanyika nchini
kote hii leo Dec 9, 2015. Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akiingia kukagua eneo la kuhifadhia Taka lililopo eneo la Kituo cha
Daladala cha Morocco, wakati alipofika eneo hilo kwa ajili ya kuendelea
kushiriki na wananchi kufanya usafi wa mazingira ikiwa ni sehemu ya
maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania kama alivyoagiza Mhe Rais
Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo zoezi hilo limefanyika nchini kote hii
leo Dec 9, 2015. Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akishiriki kuzoa taka na baadhi ya wananchi wa eneo Morocco, wakati wa
zoezi la kufanya usafi wa mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya
miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania kama alivyoagiza Mhe Rais Dkt. John Pombe
Magufuli, ambapo zoezi hilo limefanyika nchini kote hii leo Dec 9, 2015.
Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wananchi na wasanii mbalimbali
waliojitokeza kushiriki naye katika zoezi hilo baada ya kuhitimisha
zoezi la usafi eneo la Morocco, jijini Dar es Salaam, leo Dec 9, 2015.
Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wananchi na wasanii mbalimbali
waliojitokeza kushiriki naye katika zoezi hilo baada ya kuhitimisha
zoezi la usafi eneo la Morocco, jijini Dar es Salaam, leo Dec 9, 2015.
Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wananchi na wasanii mbalimbali
waliojitokeza kushiriki naye katika zoezi hilo baada ya kuhitimisha
zoezi la usafi eneo la Morocco, jijini Dar es Salaam, leo Dec 9, 2015.
Picha na OMR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akiondoka eneo la Morocco, baada ya kushiriki zoezi hilo na wananchi wa
eneo hilo la kufanya usafi wa mazingira leo Dec 9, 2015. Picha na OMR
KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO AKIFANYA USAFI NA WANANCHI WA UPANGA MASHARIKI
PIcha na Benjamin Sawe
MH. NAPE NNAUYE ASHIRIKI KUFANYA USAFI MTAMA
Mbunge
wa Jimbo la Mtama Ndugu Nape Nnauye akishiriki kufanya usafi jimboni
kwake ikiwa sehemu ya kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dk. John Pombe Magufuli inayowataka wananchi kushiriki usafi
wa mazingira kwenye siku ya kilele cha kusheherekea uhuru wa Tanzania,
Desemba 9.
Wakazi wa jimbo la Mtama wakijitokeza kufanya usafi
Wakazi wa jimbo la Mtama wakishiriki usafi
Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe. Yahaya Nawanda (mwenye fulana nyeusi) akishiriki usafi pamoja Mbunge wa Jimbo la Mtama Ndugu Nape Nnauye na wakazi wa jimbo hilo ikiwa sehemu ya kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli inayowataka wananchi
kushiriki usafi wa mazingira kwenye siku ya kilele cha kusheherekea
uhuru wa Tanzania, Desemba 9.
Usafi ukiendelea Mtama ambapo wananchi wamesafisha mitaro yote pamoja na maeneo ya sokoni.
Mbunge wa Jimbo la Mtama Ndugu Nape Nnauye akishiriki kufanya usafi
jimboni kwake ikiwa sehemu ya kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli inayowataka wananchi
kushiriki usafi wa mazingira kwenye siku ya kilele cha kusheherekea
uhuru wa Tanzania, Desemba 9.
Mbunge wa Jimbo la Mtama Ndugu Nape Nnauye akizungumza na wananchi wa jimbo lake waliojitokeza kushiriki usafi

WAFANYAKAZI NHC WAUNGA MKONO AGIZO LA RAIS DK MAGUFULI, WASHIRIKI KWA VITENDO KUSAFISHA MITAA NHC UPANGA
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akiongoza kwa vitendo zoezi la kufanya usafi katika majengo ya NHC na maeneo yanayozunguka barabara za Ali Hassan Mwinyi, Alikhan, Barak Obama na Magore UPANGA jijini Dar es Salaam leo. Menejimenti ya NHC imeamua kuwa kufanya usafi kwenye majengo ya Shirika ili kuonyesha kwa vitendo utekelezaji wa agizo la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli wa kuitumia Sikukuu ya Uhuru na Jamhuri ambayo hufanyika kila ifikapo Desemba 9 ya kila mwaka kwa gwaride na shamrashamra za halaiki, kufanya usafi wa mazingira.
Mkurugenzi wa Ubunifu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Issack Peter na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi TAMICO, NHC, Lilian Reuben wakishiriki katika zoezi la kufanya usafi katika majengo ya NHC yaliyopo barabara za Ali Hassan Mwinyi, Alikhan, Barak Obama na Magore jijini Dar es Salaam leo
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akiongoza kwa vitendo zoezi la kufanya usafi katika majengo ya NHC yaliyopo barabara za Ali Hassan Mwinyi, Alikhan, Barak Obama na Magore jijini Dar es Salaam leo.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akiwa amebeba reki kushiriki katika zoezi la kufanya usafi katika majengo ya NHC yaliyopo barabara za Ali Hassan Mwinyi, Alikhan, Barak Obama na Magore jijini Dar es Salaam leo.
Wafanyakazi wa NHC wakishiriki katika zoezi la kufanya usafi katika majengo ya NHC yaliyopo barabara za Ali Hassan Mwinyi, Alikhan, Barak Obama na Magore jijini Dar es Salaam leo.
Yamlihery Ndullah wa NHC akishiriki katika zoezi la kufanya usafi katika majengo ya NHC na maeneo yanayozunguka barabara za Ali Hassan Mwinyi, Alikhan, Barak Obama na Magore jijini Dar es Salaam leo.
Wafanyakazi wa NHC wakishiriki katika zoezi la kufanya usafi katika majengo ya NHC yaliyopo barabara za Ali Hassan Mwinyi, Alikhan, Barak Obama na Magore jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi
wa Uendelezaji Miliki wa NHC, Haikamen Mlekio akishiriki katika zoezi
la kufanya usafi katika majengo ya NHC na maeneo yanayozunguka barabara
za Ali Hassan Mwinyi, Alikhan, Barak Obama na Magore jijini Dar es
Salaam leo.
Mkurugenzi wa Fedha wa NHC, Felix Maagi akishiriki katika zoezi la kufanya usafi katika majengo ya NHC na maeneo yanayozunguka barabara za Ali Hassan Mwinyi, Alikhan, Barak Obama na Magore jijini Dar es Salaam leo.

Wafanyakazi wa NHC wakiwa na zana za usafi wakielekea kwenye wakishiriki katika zoezi la kufanya usafi katika majengo ya NHC yaliyopo barabara za Ali Hassan Mwinyi, Alikhan, Barak Obama na Magore jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Ubunifu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Issack Peter na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi TAMICO, NHC, Lilian Reuben wakishiriki katika zoezi la kufanya usafi katika majengo ya NHC yaliyopo barabara za Ali Hassan Mwinyi, Alikhan, Barak Obama na Magore jijini Dar es Salaam leo
Mkurugenzi wa Fedha wa NHC, Felix Maagi akishiriki katika zoezi la kufanya usafi katika majengo ya NHC na maeneo yanayozunguka barabara za Ali Hassan Mwinyi, Alikhan, Barak Obama na Magore jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Fedha wa NHC, Felix Maagi akishiriki katika zoezi la kufanya usafi katika majengo ya NHC na maeneo yanayozunguka barabara za Ali Hassan Mwinyi, Alikhan, Barak Obama na Magore jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akiongoza kwa vitendo zoezi la kufanya usafi katika majengo ya NHC yaliyopo barabara za Ali Hassan Mwinyi, Alikhan, Barak Obama na Magore jijini Dar es Salaam leo.
Kutoka
kushoto Meneja wa Fedha wa NHC, Albinus Manumbu, Mwenyekiti wa Chama
cha Wafanyakazi TAMICO, NHC, Lilian Reuben, Meneja wa Huduma kwa Jamii,
Muungano Saguya na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa,
Nehemia Kyando Mchechu wakishiriki katika zoezi la kufanya usafi katika
majengo ya NHC yaliyopo barabara za Ali Hassan Mwinyi, Alikhan, Barak
Obama na Magore jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akiongoza kwa vitendo zoezi la kufanya usafi katika majengo ya NHC yaliyopo barabara za Ali Hassan Mwinyi, Alikhan, Barak Obama na Magore jijini Dar es Salaam leo.
Mojawapo ya majengo ya NHC yaliyopo katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi lililofanyiwa usafi a wafanyakazi wa NHC.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akiwa na wadau walioshiriki katika zoezi la kufanya usafi katika majengo ya NHC yaliyopo barabara za Ali Hassan Mwinyi, Alikhan, Barak Obama na Magore jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akiongoza kwa vitendo zoezi la kufanya usafi katika majengo ya NHC yaliyopo barabara za Ali Hassan Mwinyi, Alikhan, Barak Obama na Magore jijini Dar es Salaam leo.
NHIF YAADHIMISHA 9 DESEMBA KWA KUFANYA USAFI WA MAZINGIRA
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko
Michael Mhando akikabidhi mashuka 100 kwa Hospitali ya Jeshi la Polisi
Kilwa Road baada ya kuwaongoza watumishi wa mfuko NHIF kwa kufanya
usafi maeneo yanayozunguka makao makuu ya Mfuko na hatimaye kutoa
mashuka 100 kwa jeshi la Polisi
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko
Michael Mhando akishiriki kufanya usafi pamoja na wafanyakazi wa mfuko
wa NHIF kuzunguka maeneo ya majengo ya mfuko hu.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko Michael Mhando akiwaelekeza wafanyakazi wa NHIF mahali pengine ambapo panatakiwa kufanyiwa usafi.
Wafanyakazi hao wakiendelea na kazi ya kuzoa taka.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko
Michael Mhando wa pili kutoka kushoto akiongozana na maofisa wa shirika
hilo kuelekea ofisini baada ya kumalizika leo.
Baadhi ya wafanyakazi wakiendelea ksafisha mitaro.
WAKAZI WA KITUNDA JIJINI DAR ES SALAAM WAITIKIA WITO WA KUFANYA USAFI KATIKA MAENEO YAO KATIKA KUADHIMISHA SIKU YA UHURU 9 DESEMBA MWAKA HUU.
Baadhi
ya Wakazi wa Kitunda jijini Dar es Salaam wakiitikia wito wa Rais John
Pombe Magufuli wa kuadhimisha siku ya Uhuru wa Tanzania Bara unafanyika
kila mwaka tarehe 9 Desemba kwa kufanya usafi katika maaeneo yao.
Mmoja
wa Wakazi wa Kitunda jijini Dar es Salaam akiitikia wito wa Rais John
Pombe Magufuli wa kuadhimisha siku ya Uhuru wa Tanzania Bara unafanyika
kila mwaka tarehe 9 Desemba kwa kufanya usafi katika maaeneo yao.
…………………………………………………………………………………………
Na Benedict Liwenga
Wakazi wa Kata ya Kitunda
Kati Jijini Dar es Salaam wameitikia wito wa kufanya usafi katika
maeneo yao ikiwa ni siku ya Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Tanzania
inayofanyika kila mwaka tarehe 9 Desemba.
Akiongea leo kwa niaba ya wakazi
wa eneo lake, Mjumbe wa Nyumba Kumi Bi. Zahara Idrissa ameeleza kuwa
kauli ya Mhe. Rais John Pombe Magufuli la kuwataka Watanzania wote
nchini kuadhimisha Sherehe za Siku ya Uhuru kwa kufanya usafi katika
maeneo yao ni suala muhimu kwakuwa linasaidia katika kuepukana na
magonjwa ya milipuko ukiwemo ugonjwa wa Kipundipindu ambao umeshika kasi
nchini.
Bi. Idrissa amesema kuwa kwa
kufanya usafi katika maeneo ya makazi kutawafanya watu wengi kujitambua
na kuachana na tabia ya kutupa taka ovyo ili kuepukana na magonjwa
hatari, hivyo wao wameamua kuitikia wito huo kwa dhati na kushirikiana
kwa bidiii kuifanya kazi hiyo.
Ameongeza kuwa, suala la kufanya
usafi katika makazi nchini kote liwe endelevu kwani haitakuwa na maana
kufanya hivyo siku moja tu ya Uhuru kama kumpendezesha Rais.
‘’Hili suala la usafi ni zuri
sana na linaboresha mazingira yetu na linawafanya watu wajielewe kwa
kuishi katika mazingira yaliyosafi na salama ili kujikinga na maambukizi
ya magonjwa hasa ya milipuko, lakini kuna watu wengine wanakuwa wabishi
wa kufanya usafi hivyo hatunabudi kuwahimiza watu wa namna hii’’,
alisema Bi. Idrissa.
Aidha, ametoa ushauri kwa
Serikali ya Awamu ya Tano ya kutaka suala la usafi liwe la mara kwa mara
ikiwezekana kila siku za Jumamosi watu wawe wanafanya usafi na kwa
kufanya hivyo magonjwa kama vile Kipindupindu na malaria vitatoweka.
Makzi wa Kivule Bwana Yusuph
Mateka ambaye ni Fundi pikipiki katika eneo la Kitunda Shule anafafanua
kuwa, suala la kufnya usafi ni jambo zuri lakini changamoto iliyopo ni
magari ya kuzoa taka yamekuwa hakuna katika maeneo yao hali ambayo
inawafanya wafanya usafi kulindika taka eneo moja bila kuzipeleka
kunakohusika.
‘’Kwa kifupi hali iliyoko ya
uchafu jijini Dar es Salaa imekithiri lakini kama zoezi hili la ufanyaji
wa usafi litakuwa enedelevu basi litasaidia kuondokana na maradhi hasa
ya kipindupindu, hivyo mimi nampa pongezi sana Mhe. Magufuli kwa wazo
hili zuri alilotuletea sisi Watanzania.
Watanzania leo wanashiriki
katika kufanya usafi kwenye maeneo yao ikiwa ni Maadhimisho ya Siku ya
Uhuru wa Tanzania Bara ambayo kwa mwaka huu Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliamua itumike kwa
kufanya usafi nchini kote ili kuepukana na magonjwa ya kipindupindu
yatokanayo na uchafu.
FILAMU YA ‘Going Bongo’ KUZINDULIWA MLIMANI CITY JIJINI DAR ES SALAAM
FILAMU mpya
inayokwenda kwa jina la ‘Going Bongo’ ambayo iliyokuwa ikisubiriwa kwa
hamu na mashabiki wa filamu ndani na na nje ya nchi imekamilika sasa
kuzinduzliwa rasmi kesho Ijumaa kwenye ukumbi wa sinema wa Century
Cinemax uliopo Mlimani City, Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Dar es Salaam
kuhusu uzinduzi huo mtunzi na muandishi ambaye pia ameisimamia katika
kuitengeneza na kuigiza filamu hiyo,Ernest Napoleon alisema, “Naamini
kuonyeshwa kwa filamu hii kutaandika historia muhimu kwenye tasnia ya
filamu nchini Tanzania”
“Tunashukuru kupata nafasi hii
kwani tunategemea tutaweza kubadilisha utamaduni wa kuangalia filamu
haswa pale filamu nyingi za hapa nyumbani zikipana nafasi ya kuonyeshwa
kwenye majumba ya majumba ya sinema” alisema.
Filamu hiyo ambayo mpaka sasa
imetwaa tunzo kadhaa, ina maudhui ambayo yanonyesha maisha ya Daktari
aliyejitolea kwenda kufanya huduma nchini Tanzania kwa muda wa mwezi
mmoja.
Filamu hii imerekodiwa majiji
makubwa mawili ambayo ni Dar es Salaam na California Marekani,
inaelezea sehemu ya maisha ya kweli aliyonayo Daktari mwenye asili ya
nchini Ufaransa aliyeondoka Ulaya na kwenda kufanya kazi barani
Afrika.
Kati ya tuzo ambazo filamu hii
imeshinda ni pamoja na, Filamu Bora Afrika Mashiriki katika tamasha la
Zanzibar International Film Festival (Ziff) na Filamu Bora ya Kimataifa
katika tamasha la ‘Black Entertainment Fashion’, ‘Film and Television
Awards’ (BEFTA)
Amewaomba mashabikmi wa filamu
kujitokeza kwa wingi kesho kwenye uzinduzi huo ambapo tiketi zimeshaanza
kuuzwa Century Cinemax Theaters Mlimani City.
WAFANYAKAZI HOSPITALI YA MUHIMBILI WAFANYA USAFI
Baadhi
ya Wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) wakifanya usafi
leo nje ya jengo la Kibasila akiwamo Mwenyekiti wa Khoja Shia
Ithnashery Jamaat ya jijini Dar es Salaam, Dewji Azim (katikati).
Kushoto
ni Mwanasheria wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Veronica Hillary,
Mkuu wa Idara ya Upasuaji, Dk Julieth Magandi, Mkurugenzi wa Upasuaji,
Dk John Kimario na Mwenyekiti wa Khoja Shia Ithnashery Jamaat ya jijini
Dar es Salaam, Dewji Azim wakifanya usafi leo Desemba 9 ambayo ni siku
ya kuadhimisha Uhuru wa Tanzania. Usafi huo umefanyika katika Jengo la
Kibasila.
Mkurugenzi
wa Upasuaji katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk John
Kimario akisomba takataka ikiwa ni sehemu ya kutekeleza agizo la Rais
John Pombe Magufuli kwamba leo Desemba 9, siku ya Uhuru watu wote
wajumuike kufanya usafi.
Mkuu
wa Idara ya Mawasiliano na Huduma kwa Wateja, Aminiel Aligaesha (wa
pili kulia) akishiriki kufanya usafi katika hospitali hiyo leo Desemba
9, 2015.
Mkuu
wa Idara ya Sheria, Veronica Hillary, Ofisa Uhusiano Msaidizi, John
Stephen, Mkurugenzi wa Upasuaji, Dk John Kimario na Mkuu wa Idara ya
Upasuaji, Dk Julieth Magandi wakijumuika pamoja kufanya usafi leo katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) ikiwa ni kuitikia agizo la Rais
John Pombe Magufuli la kufanya usafi leo Desemba 9, siku ya Uhuru.
Mwenyekiti wa Khoja Shia Ithnashery Jamaat ya jijini Dar es Salaam, Dewji Azim akifanya usafi leo katika hospitali hiyo.
WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFANYA USAFI SOKO KUU LA KARIAKOO
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisafisha mtaro wa maji machafu kwenye soko kuu
la Kariakoo jijini Dar es salaam Desemba 9, 2015. Kulia ni Mkuu wa Mkoa
wa Dar es salaam Meck Sadiki.(Pichana Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akielekea eneo la shimoni kwenye soko kuu la
Kariakoo kufanya usafi Desemba 9, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majliwa akitoka eneo la shimoni kwenye soko kuu la
Kariakoo kufanya usafi Desemba 9, 2015. Kulia kwake ni Mkuu wa wilaya
ya Ilala, Raymond Mushi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na umati ulioshiriki katika kufanya
usafi kwenye soko kuu la Kariakoo jijini Dar es salaam Desemba 9, 2015.
kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Meck Sadiki na Kulia
kwake ni Mkuu wa wilaya ya Ilala, Raymond Mushi.(Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Baadhi
ya washiriki wa zoezi la usafi kwenye soko kuu la Kariakoo jijini Dar
es salaam wakipiga picha kwa kutumia simu wakati Waziri Mkuu, Kasim
Majaliwa alipozunguza nao baada ya kufanya usafi sokoni hapo Desemba
9, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na umati ulioshiriki katika kufanya
usafi kwenye soko kuu la Kariakoo jijini Dar es salaam Desemba 9, 2015.
.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Gari
alilopanda Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa likitoka kwenye eneo la soko
kuu la Kariakoo alikokwenda kushiriki katika kufanya usafi Desemba 9,
2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI MKUU Kassim
Majaliwa amesema zoezi la usafi lililofanyika leo nchini kote lisiishie
hapo bali liwe endelevu ili Tanzania iwe na taswira nzuri kwa wageni
wanaoingia nchini.
Ametoa wito huo leo
kwenye soko la Kariakoo wakati akishiriki zoezi la kufanya usafiikiwa ni
utekelezaji wa agizo la Rais John Pombe Magufuli la kutaka maadhimisho
ya miaka 54 ya Uhuru yasiwepo na badala yake watu wote washiriki kufanya
usafi katika maeneo mbalimbali.
Waziri Mkuu Majaliwa pia
amewataka viongozi wa soko la Kariakoo wafike ofisini kwake Jumatatu
ijayo (Desemba 14, 2015) saa 4 asubuhi ili wamueleze wana mikakati gani
ya kuboresha utoaji huduma kwenye soko hilo.
“Natambua kuwa siyo
sahihi kupanga chini biashara tulizonazo. Nataka hawa viongozi waje
wanieleze wana mpango gani endelevu wa kuboresha soko hili,” alisema
Waziri Mkuu huku akishangiliwa.
Waziri Mkuu ambaye
alienda kufanya usafi kwenye soko hilo, alilazimika kuzungumza na mamia
ya wananchi waliofika kushiriki zoezi hilo. Pia alikagua maeneo
mbalimbali ya soko hilo hadi shimoni na kusema aneridhika na usafi
uliofanyika bali amesisitiza usafi huo uendelezwe.
“Kaulimbiu ya Mheshimiwa
Rais Magufuli ya HAPA KAZI TU inatupa ari ya kufanya kazi. Fanyeni
kazi. Watanzania mko huru kufanya kazi yoyote lakini cha msingi fuateni
taratibu na kanuni. Serikali hii tumamua kuwajali watu wa chini.
Tutahakikisha wajasiriamali wadogo, akinamama lishe na wamachinga
mnafanya kazi kwa amani na utulivu, ” alisema.
Rais Magufuli aliamua
kuitangaza siku ya leo (Desemba 9, 2015) ambayo ni maadhimisho ya miaka
54 ya Uhuru iwe ni siku ya kufanya usafi nchi nzima ili kuepukana na
magonjwa mbalimbali na hasa kipindupindu..
Rais Magufuli afanya usafi katika Ufukwe wa Ferry jijini Dar es Salaam
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
pamoja na Mama Janeth Magufuli wakielekea eneo la ufukwe wa Ferry
kufanya usafi katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru tarehe 9 Desemba.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizoa taka katika eneo la ferry jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizoa taka katika eneo la ferry jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizoa taka
katika eneo la ufukwe wa ferry jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka
taka ndani ya ndoo ya Taka katika eneo la Magogoni jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kulia akiwa
pamoja na Mke wake Mama Janeth Magufuli wakifanya usafi katika eneo la
ufukwe wa ferry jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka
taka taka kwenye dastibin wakati akifanya zoezi la kufanya usafi katika
eneo la ufukwe wa Ferry jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiokota
takataka katika eneo la Ferry katika zoezi la kufanya usafi nchi nzima.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiokota
takataka katika eneo la Ferry katika zoezi la kufanya usafi nchi nzima.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
na Wavuvi wa ferry huku akiwa ndani ya Mtumbwi. Rais Magufuli
alizisikiliza kero zao na kuahidi kuzitatua ndani ya muda mfupi.
Rais
Magufuli akifanya usafi pamoja na wavuvi wa eneo la ferry waliojitokeza
kuungamkono zoezi hilo. Rais Magufuli amewataka Watanzania kuwa na
Utamaduni wa kufanya Usafi kila wakati ili kuweka mazingira katika hali
nzuri. PICHA ZOTE NA IKULU
Matukio ya picha za usafi siku ya Uhuru kutoka Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira
Katibu
wa Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw.
Xavier Daudi (katikati) akiwaongoza watumishi wa ofisi yake Kufanya
usafi eneo la Maktaba Kuu ya Taifa ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya
Siku ya Uhuru wa Tanzania.
Watumishi
wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma wakiwa katika Picha ya
pamoja baada ya kumaliza zoezi la usafi katika eneo la Maktaba kuu ya
Taifa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Tanzania.
Sehemu ya Watumishi wa Sekretarieti ya Ajira wakishiriki katika zoezi la usafi kuadhimisha siku ya Uhuru.
SSRA emerged the First winner in the National Board of Accountants and Auditors (NBAA) – Best presented Financial Statements Competitionusing IPSAS
THE Social Security Regulatory Authority (SSRA) has emerged the
First winner in the National Board of Accountants and Auditors (NBAA)
Best presented financial statements competition. SSRA competed in the
International Public Sector Accounting Standards (IPSAS) category with other public entities using IPSAS.
It’s the fourth year consecutively since SSRA started
participating in the competition and throughout the period the Authority became
number one for the all four years. It’s the Authority’s pleasure to be
associated and acknowledged in this prestigious and highly recognized best
financial statements competition.

SSRA Board Chairman( at the
center) with SSRA staff in a jovial mood after emerging theFirst winner in the
National Board of Accountants and Auditors (NBAA) Best presented Financial
Statements Competition from left Ms. Lightness Mauki Director of Compliance and Registration; Mr. Emil Mkaki –
Finance Manager; Mr. Mohamed Nyasama –Director of Finance & Administration
& Mr. Peter Mbelwa – Chief Internal Auditor.

SSRA Director of Compliance &
Registration Ms. Lightness Mauki receiving award trophy from Dr. Hamis Mwinyimvua Deputy Permanent Secretary-
Ministry of Finance looking from left is Mr. Peter Mbelwa – Chief Internal
Auditor.
Registration Ms. Lightness Mauki receiving award trophy from Dr. Hamis Mwinyimvua Deputy Permanent Secretary-
Ministry of Finance looking from left is Mr. Peter Mbelwa – Chief Internal
Auditor.
SSRA Director of Compliance & Registration Ms. Lightness
Mauki receiving award trophy from Dr.
Hamis Mwinyimvua Deputy Permanent Secretary- Ministry of Finance.
Mauki receiving award trophy from Dr.
Hamis Mwinyimvua Deputy Permanent Secretary- Ministry of Finance.
SSRA
Director of Finance & Administration Mr. Mohamed Nyasama in a
jovial mood holding a trophy with Ms. Lightness Mauki – Director of
Compliance and Registrations.
SSRA
Director of Finance & Administration Mr. Mohamed Nyasama in a
jovial mood holding a trophy with Ms. Lightness Mauki – Director of
Compliance and Registrations.
MASHINDANO BAISKELI KILOMITA 115 YAKUZA VIPAJI VYA VIJANA
Washindi wa kwanza wa
mashindano.ya baiskeli, ya Rift Valley
Odyssey ya liyofanyika jijini arusha DEC 6 Mwaka huu Sophia Husseni wa kwanza
(kulia) na Sophia Adson wa (pili) kutoka kulia wakiwa na Mkurugenzi wa 6degrees
Simone Paine wa pili kutoka kulia yaliyo fanyika Arusha ambapo wachezaji
toka ndani nan je ya nchi wameshirikai kwa takriban siku mbili kuendesha kwa
umbali wa kilomita 115. Masindano ambayo yanawapa ushindi timu ya Warriors
ambao wametumia masaa matano na dakika 28

Mshindi wakwanza wa mashindano ya
kuendesha baiskeli ya Rift Valley Odyssey Sophia Husseni ya liyofanyika jijini arusha DEC Jijini Arusha
kuendesha baiskeli ya Rift Valley Odyssey Sophia Husseni ya liyofanyika jijini arusha DEC Jijini Arusha
Washiriki wa mashindano ya baiskeliya Rift Valley Odyssey yaliyofanyika
jijini arusha ambapo wachezaji toka ndani nan je ya nchi wameshirikai
kwa takriban siku mbili kuendesha kwa umbali wa kilomita 115
jijini arusha ambapo wachezaji toka ndani nan je ya nchi wameshirikai
kwa takriban siku mbili kuendesha kwa umbali wa kilomita 115
Mkurugenzi wa 6degrees
Simone Paine akizungumza na washiriki wa shindano hilo.
Simone Paine akizungumza na washiriki wa shindano hilo.
Mshindi wakwanza wa mashindano ya
kuendesha baiskeli ya Rift Valley Odyssey Sophia Husseni
kuendesha baiskeli ya Rift Valley Odyssey Sophia Husseni
NAPE AWAPA PIKIPIKI MAKATIBU KATA WA JIMBO LAKE
Mbunge
wa Jimbo la Mtama Ndugu Nape Nnauye akimkabidhi Katibu wa kata ya Mtua
Kilimahewa funguo ya pikipiki kwa niaba ya makatibu kata 20 wa jimbo
hilo ambao wote wamewezeshwa usafiri wa pikipiki ili kurahisisha ufanisi
wa kazi zao.
Mbunge
wa Jimbo la Mtama (CCM) Nape Nnauye akijaribu moja ya pikipiki kati ya
20 alizowapa makatibu kata ili ziweze kuwasaidia kufanya kazi kwa
ufanisi kwenye shughuli zao za kujenga na kuimarisha Chama Cha
Mapinduzi.
Sehemu ya pikipiki zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Mtama Ndugu Nape Nnauye kwa makatibu kata 20 wa jimbo hilo.
Mbunge
wa Jimbo la Mtama Ndugu Nape Nnauye akizungumza mbele ya viongozi wa
CCM wilaya ya Lindi vijijini ambapo aliwaambia viongozi hao kuwa
amejipanga kufanya kazi katika jimbo hilo zenye kuleta tija na
kuhakikisha anatekeleza ahadi zote alizozitoa wakati wa kampeni na
kuwata makatibu kata waliokabidhiwa pikipiki 20 kuzitumia katika kazi za
kujenga na kuimarisha chama.
No comments :
Post a Comment