Makamu
wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed
Gharib Bilal, akimkabidhi Kombe Nahodha wa timu ya VPO Sports Club,
Nehemia Mandia, baada ya kuibuka na ushindi katika Bonanza maalum la
kumuaga Dkt. Bilal, lililofanyika jana Nov 28, 2015 kwenye Uwanja wa
Jakaya Kikwete uliopo Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam. VPO
waliibuka kidedea baada ya kuwafunga timu ya Wizara ya Mambo ya Nje kwa
mikwaju ya penati 5-4. Picha na OMR
Katibu
Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Sazi Salula, akizungumza wakati wa
Bonanza maalum la kumuaga Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, liliandaliwa na timu ya timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais (V.P.O
Sports Club) lililofanyika kwenye Uwanja wa Jakaya Kikwete, uliopo
Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam jana Nov 28, 205. Katika Bonanza
hilo lililoshirikisha jumla ya timu Nne za VPO Sports Club, Wizara ya
Mambo ya Nje, Kamati ya Amani waliochanganyika na Mabalozi na Amana Bank
waliochanganyika na Zanzibar Fc, Timu ya VPO Sports Club iliibuka na
ushindi kwa kuwafunga Mambo ya nje kwa jumla ya mikwaju ya penati 5-4 na
kutwaa kombe la Bonanza hilo. Picha na OMR
Makamu
wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed
Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti cha kushiriki Nahodha wa timu ya Kamati
ya Amani Tanzania, Sheikh Alhad Mussa Salum, katika Bonanza maalum la
kumuaga Dkt. Bilal, lililofanyika jana Nov 28, 2015 kwenye Uwanja wa
Jakaya Kikwete uliopo Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam. VPO
waliibuka kidedea baada ya kuwafunga timu ya Wizara ya Mambo ya Nje kwa
mikwaju ya penati 5-4. Picha na OMR
Makamu
wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed
Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti cha kushiriki Nahodha wa timu ya Mambo
ya Nje, Christopher Mwitula, katika Bonanza maalum la kumuaga Dkt.
Bilal, lililofanyika jana Nov 28, 2015 kwenye Uwanja wa Jakaya Kikwete
uliopo Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam. VPO waliibuka kidedea
baada ya kuwafunga timu ya Wizara ya Mambo ya Nje kwa mikwaju ya penati
5-4. Picha na OMR
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akizungumza na kutoa
nasaha zake katika bonanza hilo la kumuaga rasmi katika utumishi wa
umma.
Nahodha
wa timu ya VPO Sports Club, Muhidin Sufiani, akimtoka beki wa timu ya
Kamati ya Amani, Mhungaji Amos Nene, wakati wa Bonanza maalum la kumuaga
Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, lililofanyika
kwenye Uwanja wa Jakaya Kikwete,uliopo Kidongo Chekundu jijini Dar es
Salaam jana Nov 28, 2015. Katika Mchezo huo VPO walishinda kwa bao 1-0
na kutinga fainali na Timu ya Mambo ya Nje ambapo pia waliibuka kidedea
kwa mikwaju ya penati 5-4 baada ya mchezo kumalizika bila kufungana.
Picha na OMR
Nahodha
wa timu ya Kamati ya Amani Tanzania, Sheikh Alhad Mussa Salum,
akimiliki mpira mbele ya beko wa VPO Sports Club, Kibiti wakati wa
Bonanza maalum la kumuaga Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, lililofanyika kwenye Uwanja wa Jakaya Kikwete,uliopo Kidongo
Chekundu jijini Dar es Salaam jana Nov 28, 2015. Katika Mchezo huo VPO
walishinda kwa bao 1-0 na kutinga fainali na Timu ya Mambo ya Nje ambapo
pia waliibuka kidedea kwa mikwaju ya penati 5-4 baada ya mchezo
kumalizika bila kufungana. Picha na OMR
Makamu
wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed
Gharib Bilal akisalimiana na Nahodha wa timu ya VPO kabla ya kuanza kwa
mchezo huo.
………………………………………………………………………………………………….
Na Muhidin Sufiani, Dar
Timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais,
VPO Sports Club, jana Nov 28, 2015 imetwaa kombe la bonanza maalum
lililoandaliwa kwa ajili ya kumuaga rasmi Makamu wa Rais Mstaafu Dkt.
Mohammed Gharib Bilal, kwa kuifunga kwa mikwaju ya penati 5-4 timu ya
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika mchezo wa
fainali.
Katika bonanza hilo lililofanyika
kwenye viwanja vya Jakaya Mrisho Kikwete Park (JMK Park) zamani Kidongo
Chekundu, timu hiyo iliianza kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kamati ya
Amani Tanzania iliyoongozwa na Sheikh Mkuu wa Dar es Salaam, Alhaj Mussa
Salum.
Baada ya mechi hiyo, Timu ya Ofisi
ya Makamu wa Rais ilicheza mchezo wa fainali dhidi ya Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambayo ilimaliza katika nafasi ya
pili, ilifuzu katika hatua hiyo baada ya kuifunga timu ya Amana Benki
kwa mabao 2-1.
Katika mchezo wa kutafuta mshindi
wa tatu, timu ya Amana Benki iliifunga timu ya Kamati ya Amani kwa mabao
2-0. Makamu Rais Mstaafu Dk Bilal alishuhudia michezo yote hiyo na
kukabidhi vikombe kwa washindi.
Akizugumza baada ya michezo hiyo,
Dkt. Bilal, aliwashukuru waandaaji wa bonanza hilo kwa kumuaga rasmi na
kusema michezo ina umuhimu mkubwa sana katika maisha ya kila siku ya
binadamu ikiwa ni pamoja na kujenga afya, kuhimarisha na kuanzisha
urafiki na vile vile kuburudisha.
“Nimefurahi sana kuona jinsi
mlivyoonyesha ushindani mkubwa na vipaji vya hali ya juu, sikujua kama
kuna wachezaji wazuri namna hii, nawapa pongezi sana na msiache kuandaa
mabonanza mengine kama haya mara kwa mara, mnatakiwa kufanya kila mara
ili kujenga afya zenu na kuanzisha na kudumisha urafiki na amani”
alisema Dkt Bilal.
Aidha Dkt. Bilal alitoa wito kwa
wanamichezo nchini kutumia uwekezaji huo mkubwa kutoka kwa Rais Mstaafu,
Jakaya Mrisho Kikwete kuendeleza vipaji. “Hapa kuna viwanja vya mpira
wa miguu, mpira wa kikapu, netiboli, mpira wa mikono, mpira wa wavu,
tumieni fursa hii kwa ajili ya kuendeleza vipaji na kuiwezesha nchi
kufanya vyema katika michuano ya Kimataifa,” alisema.
HAPA KAZI TU” YAWAWEKA SAWA WAFANYAKAZI WA DAWASCO
Ofisa
Mtendaji wa Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (Dawasco),
Mhandisi Cyprian Luhemeja, akizungumza katika mkutano na wafanyakazi
uliofanyika hivi karibuni Makao Makuu ya Dawasco jijini Dar es Salaam
kuhusu utendaji kazi wa kazi.
Wafanyakazi wa Dawasco wakimsikiliza Ofisa Mtendaji
Mkuu wao.
…………………………………………………………………………………….
CHAMA CHA WASHIRIKA-WAUGUZI TANZANIA KUKUTANA DESEMBA 12, 2015 JIJINI DAR ES SALAAM KUJADILI MAENDELEO NA CHANGAMOTO ZAO
Ofisa
Ushirika wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Omary Mkamba
(kulia), akimkabidhi cheti cha Usajili wa Chama cha Ushirika -Wauguzi
Tanzania (Tanna Saccos Ltd) , Mwenyekiti wa chama hicho, Kapteni Adam
Leyna katika mkutano uliofanyika hivi karibuni. Mkamba ni mlezi wa chama
hicho.
Mwenyekiti
wa chama hicho, Kapteni Adam Leyna (katikati), akizungumza na wanachama
wapya waliojiunga na chama hicho mkoani Kagera.
Wanachama wakijadiliana.
Wanachama wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa wamevalia fulana rasmi mkoani Kagera
Viongozi wa chama hicho na wanachama wakiwa katika picha ya pamoja.
……………………………………………………………………………
Na Dotto Mwaibale
CHAMA cha Washirika-Wauguzi Tanzania (Tanna Saccos Ltd) kinatarajia kujadili mafanikio na changamoto zao mbalimbali katika mkutano wao mkuu , utakaofanyika Desemba 12, mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana,
Mwenyekiti wa Tanna Saccos Ltd, Kapteni Adam Leyna alisema mkutano huo ni muhimu sana kwao kwani unawakutanisha wauguzi washirika nchi nzima na kuweza kujadili mafanikio, changamoto mbalimbali na maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
“Ni mkutano muhimu sana kwetu kwani unatusaidia kubadilishana
uzoefu wa ushirika kutoka kwa washirika wenzetu kama Ngome Saccos,
Walimu Saccos na Magereza Saccos na kujua changamoto zetu ikiwa ni
pamoja na kuzitafutia ufumbuzi’ alisema Leyna.
Aliongeza
kuwa mkutano huo ambao utafanyika Ukumbi wa Makuti katika Kambi ya
Jeshi la Kujenga Taifa Mgulani ni mikutano ambayo hufanyika kila mwaka
ili
kuzungumzia maendeleo ya chama na uboreshaji wa uchumi wa muuguzi na ustawi wa jamii kwa ujumla.
Leyna alisema pamoja na mambo mengine katika mkutano huo
watajadili taarifa ya maendeleo ya chama na kuweka mpango
kazi wa kutekeleza mwaka wa fedha 2016.
Mwenyekiti huyo ametumia fursa hiyo kuwaomba wauguzi washirika wa tanna saccos ltd kujitokeza kwa wingi katika mkutano huo muhimu kwao.
Chama cha Ushirika -Wauguzi Tanzania (Tanna Saccos Ltd) ni
chama cha ushirika kinachowaunganisha wauguzi na wakunga
Tanzania ambacho kinasimamia utoaji wa mikopo, elimu ya ujasiriamali na maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wauguzi.
MSD YAKARABATI JENGO LA DUKA LA DAWA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI KWA KASI KUBWA KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS DK.MAGUFULI
Mafundi
wakikarabati jengo ambalo Bohari ya Dawa (MSD), itafungua duka la dawa
katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MSD) Dar es Salaam jana kwa
ajili ya kuhudumia wananchi kwa karibu zaidi vikiwemo vifaa tiba. Duka
hilo linatarajiwa kufunguliwa kesho kutwa.
Fundi akitoboa ukuta sehemu litakapo fungwa beseni la kunawia katika duka hilo.
Mafundi wakiendelea na ukarabati wa jengo hilo lililopo jirani na wodi ya Kibasila linalotizamana na maegesho ya magari.
Fundi akipaka rangi ndani ya jengo hilo.
Jengo la duka hilo la MSD linavyoonekana kwa nje. Hapa mafundi wakiendelea na kazi ya ukarabati.
………………………………………………………………………………..
Na Dotto Mwaibale
BOHARI
ya Dawa (MSD) imejiimarisha na kuhahikisha inatekeleza kwa wakati agizo
la Rais Dk. John Magufuli la kuweka maduka ya dawa katika hospitali za
rufaa na kanda nchini.
Katika
kutekeleza agizo hilo MSD imeanza kwa kasi kubwa ya kukarabati jengo la
duka la dawa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), ambalo
linatarajiwa kufunguliwa kesho.
Mwandishi
wa habari hii alishuhudia jana kasi kubwa ya mafundi ujenzi
wakikarabati jengo hilo ambalo awali lilikuwa likitumika kama stoo ya
kuhifadhi vitu mbalimbali vya hospitali hiyo.
Akizungumza
na vyombo vya habari hivi karibuni kuhusu ufunguzi wa maduka hayo,
Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laureane Bwanakunu alisema agizo la Rais la
kuitaka MSD kuanzisha duka la dawa karibu na hospitali limekuja wakati
muafaka kwani kwenye mpango mkakati wa miaka sita wa MSD tayari ilikuwa
na mpango wa kufungua maduka hayo kwa ajili ya kusogeza huduma karibu a
wananchi.
Alisema
maduka ya MSD ambayo yatafunguliwa kwenye hospitali za rufaa na kanda
yatafanya kazi masaa 24 na kuuza dawa na vifaa tiba chini ya bei ya
soko pia yatahudumia watu binafsi na wale waliopo kwenye taratibu za
Bima ya afya kote nchini.
“Ili
kudhibiti watumishi wasio waaminifu kuiba dawa MSD inafanya kazi za
uagizaji, uhifadhi na usambazaji kwa kutumia mfumo wa mtandao wa E9 na
tangu mwaka wa fedha uliopita tumeanza kuziwekea alama ya GOT bidhaa
zetu ikiwa ni pamoja na vidonge.” alisema Bwanakunu.
Alisema
vidonge ambavyo tayari vimewekewa nembo ya GOT vipo 45 na wanaendelea
kuwapa maelekezo wazabuni ili vyote viwekwe alama hizo..,nembo ya
serikali inaonekana kwenye dawa za serikali kama Diclofenac, moxillin,
iprofloxacin, Contrimoxale,paracetamol,
na magnesium.
Alisema
wanatarajia kuanzisha huduma ya kutoa taarifa kwa njia ya simu pale
wananchi watakapoona kuna wizi wa dawa za serikali na kwamba wananchi
wanaelimishwa kutoa taarifa pale wanapoona dawa za serikali mitaani.
Alisema, pamoja na serikali kuanza kupunguza deni lake linalodaiwa na MSD bado inadaiwa Sh.bilioni 53.
BOMOBOMOA SALASALA ILI KUPISHA UJENZI WA BOMBA LA MAJI -RUVU CHINI
Katapila
likiwa ndani ya gari tayari kwa kazi ya bomobomoa eneo la Salasala
jijii Dar es salaam ili kupisha ujenzi wa bomba la maji kutoka Ruvu
Chini hadi jijini Dar es salaam.
Kazi
ya kubomoa baadhi ya nyumba ikiendelea mwishoni mwa wiki eneo la
Salasala jijii Dar es salaam ili kupisha ujenzi wa bomba la maji kutoka
Ruvu Chini.
Baadhi
ya wakazi wa eneo la Salasala jijini Dar es salaam wakishuhudia
kazi ya kubomoa baadhi ya nyumba mwishoni mwa wiki ili kupisha ujenzi
wa bomba la maji kutoka Ruvu Chini.
Kazi
ya kubomoa baadhi ya nyumba ikiendelea mwishoni mwa wiki eneo la
Salasala jijii Dar es salaam ili kupisha ujenzi wa bomba la maji kutoka
Ruvu Chini.
Mafundi
wakiendelea kubomoa nyumba iliyopo eneo la Salasala kwa hiyari ya
mmiliki wa nyumba hiyo ili kupisha ujenzi wa bomba la maji kutoka Ruvu
Chini.
(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
………………………………………………………………………………………………..
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Zoezi la kubomoa nyumba na
majengo yaliyoingia ndani ya ya hifadhi ya miundombinu ya bomba la maji
kutoka Ruvu Chini limeendelea mwishoni mwa wiki ili kuhakikiha
kunakuwepo usalama wa bomba hilo na kuwapatia wakazi wa jiji la Dar es
salaam na maeneo ya mkoa wa Pwani uhakika wa maji ifikapo Februari,
2016.
Bomo bomoa hiyo ya mwishoni mwa
wiki ilihusisha maeneo ya Salasala ambapo baadhi ya nyumba, karakana na
uzio vyote viljengwa ndani ya hifadhi ya miundombinu hiyo ya maji.
Akizungumzia ubomoaji huo,
Mkurugenzi wa Usimamizi na Ufundi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka
Dar es Salaam (DAWASA), Romanus Mwang’ingo alisema kuwa ni wajibu wa
wakazi wa maeneo hayo kuvunja sehemu za makazi yao yaliyoingia ndani ya
hifadhi ya mradi kwa hiyari ama nyumba hizo kuvunjwa baada ya kukaidi
agizo la kubomoa ili kupisha ujenzi wa bomba la maji kutoka Ruvu Chini
hadi jijini Dar es salaam.
“Umbali sahihi unaopaswa wakazi
hao kujenga makazi yao kutoka lilipo bomba la maji ni mita 15 kila
upande ambapo hatua hiyo inapelekea kuwa jumla ya mita 30 ya umbali
unaotakiwa ili kuhakikisha kunakuwepo na usalama na kuruhusu matengenezo
mengine tofauti na hali ya awali ambayo huwezi hata kufanya kazi maana
bomba limepita ndani ya uzio na makazi ya watu ambayo ni hatari kwa
usalama wa maisha yao na mali zao” alisema Mwang’ingo.
Vile vile Mwang’ingo alizitaja
changamoto zilizochangia kuchelewesha kukamilika kwa mradi huo kwa
wakati ni kuwepo kwa kesi zilizofunguliwa na wananchi kuzuia ufanisi wa
kazi hiyo ambapo kulikuwa na kesi 17 katika mahakama mbalimbali katika
maeneo hayo ikiwemo mahakama ya ardhi.
Kwa mujibu wa Mwang’ingo hadi
sasa DAWASA imeshinda kesi 13 na kupewa haki ya kutumia njia hiyo
kukamilisha upanuzi wa mradi na zimebaki kesi nne ambazo bado zipo
mahamani na zimefikia hatua mbalimbali kulingana na taratibu za
kimahakama.
Kwa upande wake mkazi wa
Salasala Mhandisi Josephat Nakapange ambaye sehemu ya nyumba yake pamoja
na uzio vipo ndani ya hifadhi hiyo ya bomba la maji kutoka Ruvu Chini
hadi Dar es salaam alisema kuwa yeye hana tatizo wala ugomvi na mradi
huo, wamepokea maelekezo na wanayafanyia kazi.
“Hivi sasa ninavyoongea mafundi
wapo kwenye eneo langu wanaendelea na zoezi la kutoa mabati na baadaye
kuvunja kuta zilizo ndani ya umbali unaotakiwa kuachwa wazi kwa ajili ya
mradi wa bomba la maji” alisema Josephat.
Aidha, Josephat aliongeza kuwa
ni vema ziwekwe alama katika maeneo yote yanayotakiwa kuachwa wazi
ambayo yapo ndani ya hifadhi ya mradi ili kuepusha usumbufu na gharama
zisizo za lazima kwa wakazi ulipopita mradi huo.
Maeneo yaliyohusishwa na
ubomoaji huo mwishoni mwa wiki ni pamoja na Bunju, Bondeni, Boko,
Tegeta, Mbezi Intacheki, na Mbezi Tangibovu ili kuruhusu kukamilisha
ujenzi wa bomba hilo la maji kutoka Ruvu Chini ha jijini Dar es salaam.
Watakaokwamisha juhudi za Rais Dkt. Magufuli katika sekta ya elimu kukiona
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. George Mcheche Masaju akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wahitimu wa kidato cha nne wa shule za Fedha. |
(Picha/Habari na Hassan Silayo)
……………………………………………………………………………………………
Wananchi wameshauriwa
kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano za kuendeleza sekta
ya elimu kwa maslahi na maendeleo ya watoto na nchi kwa ujumla.
kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano za kuendeleza sekta
ya elimu kwa maslahi na maendeleo ya watoto na nchi kwa ujumla.
Hayo yamesemwa
na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. George Mcheche Masaju wakati wa Mahafali ya
Shule za Sekondari za Wavulana na Wasichana za Feza leo Jijini Dar es Salaam.
na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. George Mcheche Masaju wakati wa Mahafali ya
Shule za Sekondari za Wavulana na Wasichana za Feza leo Jijini Dar es Salaam.
Bw. Masaju
alisema kuwa anatambua Serikali inayoongozwa na Rais John Pombe Joseph Magufuli
imeamua na kuelekeza kwamba kuanzia Januari 2016 elimu itolewe bure kuanzia
ngazi ya awali (Kindergarten) hadi kidato cha nne ikiwa ni njia ya
kuwafanya watoto wa shule za msingi au watoto waliofalu na kupata nafasi ya
kusoma elimu ya sekondari kutokusoma.
alisema kuwa anatambua Serikali inayoongozwa na Rais John Pombe Joseph Magufuli
imeamua na kuelekeza kwamba kuanzia Januari 2016 elimu itolewe bure kuanzia
ngazi ya awali (Kindergarten) hadi kidato cha nne ikiwa ni njia ya
kuwafanya watoto wa shule za msingi au watoto waliofalu na kupata nafasi ya
kusoma elimu ya sekondari kutokusoma.
Masaju alisema
kuwa Asiwepo mtu atakayesababisha mtoto kukosa haki yake ya kupata elimu kwa
sababu yoyote ile ikiwemo kuwaozesha watoto, kuwapa ujauzito, kuwaficha
majumbani, kuwaachisha masomo, kuwatorosha shule, utoro kwani kama nilivyoeleza
awali kufanya hivyo ni kutenda kosa la jinai chini Sheria ya Elimu na Kanuni
zake hivyo serikali itachukua hatua dhidi yake.
kuwa Asiwepo mtu atakayesababisha mtoto kukosa haki yake ya kupata elimu kwa
sababu yoyote ile ikiwemo kuwaozesha watoto, kuwapa ujauzito, kuwaficha
majumbani, kuwaachisha masomo, kuwatorosha shule, utoro kwani kama nilivyoeleza
awali kufanya hivyo ni kutenda kosa la jinai chini Sheria ya Elimu na Kanuni
zake hivyo serikali itachukua hatua dhidi yake.
“Kama tunavyofahamu
Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Pombe Joseph Magufuli imeamua
na kuelekeza kwamba kuanzia Januari 2016 elimu itolewe bure kuanzia ngazi ya
awali (Kindergarten) hadi kidato cha nne, hivyo asiwepo mtu atakayekwamisha juhudi hizi
kwa njia yoyote ile kwani ni kuwanyima watoto haki yao ya kikatiba kwani Serikali
haitasita kuchukua hatua stahiki za kisheria dhidi ya watu wanaojihusisha na
vitendo hivyo” Alisema Masaju.
Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Pombe Joseph Magufuli imeamua
na kuelekeza kwamba kuanzia Januari 2016 elimu itolewe bure kuanzia ngazi ya
awali (Kindergarten) hadi kidato cha nne, hivyo asiwepo mtu atakayekwamisha juhudi hizi
kwa njia yoyote ile kwani ni kuwanyima watoto haki yao ya kikatiba kwani Serikali
haitasita kuchukua hatua stahiki za kisheria dhidi ya watu wanaojihusisha na
vitendo hivyo” Alisema Masaju.
Pia Bw. Masaju alizitaka shule na taasisi za elimu kutoa fursa sawa
kwa wanafunzi wote kutumia haki ya uhuru wa kuabudu kulingana na imani za dini
zao kwa kupanga mitihani au vipindi kwa muda au siku za kuabudu kwani ni kukiuka
masharti ya Ibara ya 19 inayotoa haki ya uhuru wa kuabudu
kwa wanafunzi wote kutumia haki ya uhuru wa kuabudu kulingana na imani za dini
zao kwa kupanga mitihani au vipindi kwa muda au siku za kuabudu kwani ni kukiuka
masharti ya Ibara ya 19 inayotoa haki ya uhuru wa kuabudu
Aidha Masaju
alizipongeza sekta binafsi za elimu kwa kutoa mchango mkubwa katika utoaji wa
elimu hapa nchini kwa kuongeza wigo wa utoaji wa elimu ya msingi na elimu ya
sekondari; kuongeza vyanzo vya kodi na hivyo kukuza uchumi na huduma za kijamii
kutokana na kodi inayolipwa na shule zinazotoa huduma ya elimu; kutunza na
kuendeleza utamaduni wa Kitanzania kwa kuwezesha watoto kusoma hapa Tanzania
badala ya kupelekwa kusoma nje ya nchi; na kuongeza ajira kwa walimu na watu wa
kada mbalimbali wanaoajiriwa na shule binafsi
alizipongeza sekta binafsi za elimu kwa kutoa mchango mkubwa katika utoaji wa
elimu hapa nchini kwa kuongeza wigo wa utoaji wa elimu ya msingi na elimu ya
sekondari; kuongeza vyanzo vya kodi na hivyo kukuza uchumi na huduma za kijamii
kutokana na kodi inayolipwa na shule zinazotoa huduma ya elimu; kutunza na
kuendeleza utamaduni wa Kitanzania kwa kuwezesha watoto kusoma hapa Tanzania
badala ya kupelekwa kusoma nje ya nchi; na kuongeza ajira kwa walimu na watu wa
kada mbalimbali wanaoajiriwa na shule binafsi
Wadau wa Filamu waiomba Serikali kuanzisha kiwanda cha kuzalisha DVD tupu na Vifungashio vya kazi za filamu
Katibu
Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fisoo (kushoto) akisisitiza jambo
wakati wa kongamano la wadau wa filamu lililofanyika Jana Mkoani
Morogoro kujadili changamoto na namna ya kukuza tasnia ya filamu nchini.
kulia ni Katibu kutoka Filmmaking Clinic of Tanzania (FCoT) Bw. Ignas
Mkindi
Katibu
kutoka Filmmaking Clinic of Tanzania (FCoT) Bw. Ignas Mkindi (Kulia)
akizungumza na wadau wa filamu (hawapo pichani) wakati wa kongamano la
wadau hao jana Mkoani Morogoro. Kushoto ni mdau wa filamu na mratibu wa
kongamano Bw. Kheri Mkamba
Mkurugenzi
kutoka Tansquare Film House Bi. Christina Mroni akichangia mada wakati
wa kongamano la wadau wa filamu lililofanyika Jana Mkoani Morogoro
kujadili changamoto na namna ya kukuza tasnia ya filamu nchini
Picha na: Genofeva Matemu -Maelezo.
Picha na: Genofeva Matemu -Maelezo.
…………………………………………………………………………………………………………….
Na:Genofeva Matemu – Maelezo
Wadau wa filamu nchini wameiomba Serikali ya awamu ya tano kutoa kipaumbele kwa viwanda vitakavyofufuliwa kuzalisha DVD tupu na vifungashio vya kazi za filamu vyenye kiwango hivyo kuinua sekta ya filamu kwa kasi.
Rai hiyo imetolewa na mdau wa filamu nchini Bw. Luhende Richard Luhende wakati wa kongamano la wadau wa filamu lililoudhuriwa na watayarishaji na wazalishaji wa filamu jana Mkoani Morogoro.
Bw. Luhende amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano imelenga kukuza sekta ya filamu kwa kuandaa ilani inayojali wasanii kama ilani hiyo ilivyoainisha katika ukurasa wake wa 219 pamoja na 220.
“Ilani ya chama cha mapinduzi imelenga kukuza sekta ya fulamu hususani katika eneo la miundombinu, ubora na weledi katika sekta na bidhaa zinazozalishwa pamoja na uimarishwaji wa chombo chenye dhamana na filamu kwa maana ya bodi ya filamu, uanzishwaji na uratibu wa mfuko ambao utawawezesha wasanii kupata mitaji hivyo kuzalisha bidhaa zenye ubora” alisema Bw. Luhende.
Aidha Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu bibi. Joyce Fisoo amesema kuwa Serikali imekua ikitoa wito kwa wawekezaji ambao wako tayari kujitokeza kuwekeza katika miundombinu ya filamu hususani jumba changamani la filamu kwa lengo la kuinua wasanii na kukuza tasnia ya filamu.
Bibi. Fisoo amewataka wasanii kushirikiana, kutumia fursa za mikopo zinazotolewa na wadau mbalimbali, kujiunga na mafunzo ya muda mfupi kuongeza ujuzi, na kupunguza utamaduni wa kuongelea masuala yasiyokua na tija bali kutumia muda walionao kufanya kazi kwa bidii kama hari iliyotolewa na Mheshimiwa Rais wa Serikali ya awamu ya tano.
Naye mwakilishi kutoka Proin Promotion Bw. Josephat Lukaza ameipongeza bodi ya filamu kushirikisha wadau wa filamu kwenye matamasha mbalimbali yakiwemo matamasha ya JAMA Festival, Nepal Afrika inayotarajia kufanyika Februari 2016, pamoja na kwenda Misri kwa ajili ya tamasha la Script Writers litakalofanyika Desemba mwaka huu, matamasha ambayo yanatoa fursa kwa wadau wa filamu kupata mbinu mpya za kuendeleza tasnia ya filamu nchini.
Na:Genofeva Matemu – Maelezo
Wadau wa filamu nchini wameiomba Serikali ya awamu ya tano kutoa kipaumbele kwa viwanda vitakavyofufuliwa kuzalisha DVD tupu na vifungashio vya kazi za filamu vyenye kiwango hivyo kuinua sekta ya filamu kwa kasi.
Rai hiyo imetolewa na mdau wa filamu nchini Bw. Luhende Richard Luhende wakati wa kongamano la wadau wa filamu lililoudhuriwa na watayarishaji na wazalishaji wa filamu jana Mkoani Morogoro.
Bw. Luhende amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano imelenga kukuza sekta ya filamu kwa kuandaa ilani inayojali wasanii kama ilani hiyo ilivyoainisha katika ukurasa wake wa 219 pamoja na 220.
“Ilani ya chama cha mapinduzi imelenga kukuza sekta ya fulamu hususani katika eneo la miundombinu, ubora na weledi katika sekta na bidhaa zinazozalishwa pamoja na uimarishwaji wa chombo chenye dhamana na filamu kwa maana ya bodi ya filamu, uanzishwaji na uratibu wa mfuko ambao utawawezesha wasanii kupata mitaji hivyo kuzalisha bidhaa zenye ubora” alisema Bw. Luhende.
Aidha Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu bibi. Joyce Fisoo amesema kuwa Serikali imekua ikitoa wito kwa wawekezaji ambao wako tayari kujitokeza kuwekeza katika miundombinu ya filamu hususani jumba changamani la filamu kwa lengo la kuinua wasanii na kukuza tasnia ya filamu.
Bibi. Fisoo amewataka wasanii kushirikiana, kutumia fursa za mikopo zinazotolewa na wadau mbalimbali, kujiunga na mafunzo ya muda mfupi kuongeza ujuzi, na kupunguza utamaduni wa kuongelea masuala yasiyokua na tija bali kutumia muda walionao kufanya kazi kwa bidii kama hari iliyotolewa na Mheshimiwa Rais wa Serikali ya awamu ya tano.
Naye mwakilishi kutoka Proin Promotion Bw. Josephat Lukaza ameipongeza bodi ya filamu kushirikisha wadau wa filamu kwenye matamasha mbalimbali yakiwemo matamasha ya JAMA Festival, Nepal Afrika inayotarajia kufanyika Februari 2016, pamoja na kwenda Misri kwa ajili ya tamasha la Script Writers litakalofanyika Desemba mwaka huu, matamasha ambayo yanatoa fursa kwa wadau wa filamu kupata mbinu mpya za kuendeleza tasnia ya filamu nchini.
Chanzo cha maji cha Ruvu Chini kuwatua akina mama ndoo za maji.
Meneja
Mradi Ruvu chini Mhandisi Emmanuel Makasa akiwaonesha waandishi wa
habari sehemu ya bomba la kusafirisha maji kutoka chanzo cha Ruvu chini
kwenda jijini Dar es salaam.
Sehemu
ya bomba la kusafirisha maji kutoka chanzo cha Ruvu chini kwenda jijini
Dar es salaam lilivyozamishwa chini tayari kwa kusafirisha maji ambayo
yatawanufaisha wananchi wa mikoa ya Dar es salaam na Pwani kwa matumizi
mbalimbali.
Baadhi ya mitambo ya kusafisha maji ambayo yamesafishwa tayari kwa matumizi ya wananchi wa mikoa ya Dar es salaam na Pwani.
Baadhi ya waandishi wa habari na viongozi kutoka Wizara ya Maji wakiwa eneo la chanzo cha maji cha Ruvu Chini.
Fundi
akiendelea na kazi ya kuunganisha na kuchomelea bomba la maji ambalo
litasafirisha maji kutoka Ruvu Chini kwenda jijini Dar es salaam.
Muonekano wa maji yakiwa mtoni kabla ya kuanza kusafishwa kupitia hatua mbalimbali kwa matumizi.
(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
…………………………………………………………………………………………….
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA)
inaendelea kuboresha na kuimarisha miundombinu ya maji ili kuwanufaisha
wakazi wa mikoa ya Dar es salaam na Pwani kupata maji kwa mahitaji yao
ya kila siku.
Mioundombinu hiyo inayoboreshwa ni pamoja na bomba la Ruvu
Chini lenye urefu wa Jumla ya km 55 ambapo hadi sasa km 52.6
zimekamilika na zimebaki km 2.4 ili kukamilisha mradi huo ambao
utasaidia kusimamia moja ya sentensi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ya “Kuwatua akina mama ndoo za
maji kichwani”
Ili kufikia azma hiyo ya kuwapatia maji safi na salama
wakazi wa mikoa hiyo, Mkurugenzi wa Usimamizi na Ufundi wa DAWASA,
Romanus Mwang’ingo alisema kuwa upanuzi wa mtambo wa Ruvu Chini na
ujenzi wa bomba kuu kutoka Ruvu Chini hadi matanki ya Chuo Kikuu cha
Ardhi ndiyo utakuwa suluhisho la tatizo la maji katika jiji la Dar es
salaam na maeneo ya mkoa wa Pwani.
Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake kabla ya
waandishi hao kwenda kujionea hatua iliyofikiwa, Mwang’ingo alisema kuwa
ujenzi wa mradi huo unatarajiwa kukamilika ifikapo Februari 2016 na
kuondoa adha ya maji kwa wananchi na kuwaunganishia wengine ambao
hawakuwa na huduma ya maji.
“Tumelazimika kufikia hatua ya kupanua huduma ya
upatikanaji wa maji katika mikoa ya Dar es salaa na Pwani kutokana na
ongezeko la watu kulingana na sensa ya watu ya mwaka 2012, mkoa wa Dar
es salaam una jumla ya zaidi ya watu milioni 5 ambao watatumia maji
zaidi ya lita milioni 5 kwa siku”,
“Katika upanuzi huo, kumekuwa na changamoto ya makazi ya
watu kuwa ndani ya mradi ambapo kulikuwa na kesi 17 katika mahakama
mbalimbali katika maeneo hayo ikiwemo mahakama ya ardhi, hadi sasa
DAWASA imeshinda kesi 13 na kupewa haki ya kutumia njia hiyo kukamilisha
upanuzi wa mradi” alisema Mwang’ingo.
Kwa mujibu wa Mwang’ing’o kesi nne bado zipo mahamani na ambazo zimefikia hatua mbalimbali kulingana na taratibu za kimahakama.
Lengo la mradi huu ni kuongeza uzalishaji wa maji kutoka
lita milioni 182 hadi 270 kwa siku. Mradi ambapo awamu itakayofuata ni
lita milioni 360 kwa siku.
Chanzo cha maji cha Ruvu Chini ndiyo chenye kiwango kikubwa
ambacho kina wapatia maji wakazi wa Dar es salaam kwa zaidi ya asilimia
75 ikilinganishwa na asilimia 25 kutoka Ruvu Juu.
Mradi wa upanuzi wa mtambo wa Ruvu Chini unalenga kuongeza
uzalishaji maji na kuwahudumia wakazi wa maeneo ya uwekezaji (EPZ)
Bagamoyo, Chasimba, Buma, Zinga, Kerege na Mpiji mkoa wa Pwani
Maeneo mengine yatakayonufaika na mradi huo kwa Mkoa wa Dar
es salaam ni Bunju, Wazo, Salasala, Madale na Kinzudi Mbezi Juu, Goba,
Kawe, Makongo, Mwenge, Msasani, Mikocheni, Mlalakua, Masaki, Sinza,
kijitonyama, Manzese, Konondoni, Magomeni, Kigogo, Vingunguti, Buguruni,
Kariakoo na Ilala.
RAIS DK.SHEIN ATEMBELEA KIWANDA CHA SUKARI MAHONDA LEO.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Bw, Mahesh Patel Mwenyekiti wa Kiwanda cha Sukari cha Mahonda kiliopo katika Wilaya ya Kaskazini B. Unguja alipofanya ziara maalum ya kutembelea kiwanda hicho leo,ambacho kinachofanyiwa ukarabati na Kampuni ya Shanta Sugar Holding Ltd kutoka nchini India,[Picha na Ikulu.]
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akisalimiana na Viongozi mbali mbali wakati alipowasili katika Kiwanda
cha Sukari cha Mahonda kiliopo katika Wilaya ya Kaskazini B. Unguja alipofanya ziara maalum ya kutembelea kiwanda hicho leo,ambacho kinachofanyiwa ukarabati na Kampuni ya Shanta Sugar Holding Ltd kutoka nchini India,[Picha na Ikulu.]
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akisalimiana na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Maliasili Bw,Afani
Othman Maalim mara alipowasili katika Kiwanda cha Sukari cha Mahonda kiliopo katika Wilaya ya Kaskazini B. Unguja alipofanya ziara maalum ya kutembelea kiwanda hicho leo,ambacho kinachofanyiwa ukarabati na Kampuni ya Shanta Sugar Holding Ltd kutoka nchini India,[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi mbali mbali wa Kiwanda cha Sukari cha Mahonda kiliopo katika Wilaya ya Kaskazini B. Unguja alipofanya ziara maalum ya kutembelea kiwanda hicho leo,ambacho kinachofanyiwa ukarabati na Kampuni ya Shanta Sugar Holding Ltd kutoka nchini India,[Picha na Ikulu.]
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(katikati) akipata maelezo wakati alipofuatana Meneja wa Kiwanda cha Sukari cha Mahonda Bw.Rajesh Kumar (wa pili kulia) kiliopo katika Wilaya ya Kaskazini B. Unguja alipofanya ziara maalum ya kutembelea kiwanda hicho leo,ambacho kinachofanyiwa ukarabati na Kampuni ya Shanta Sugar Holding Ltd kutoka nchini India,(kulia ni ) Waziri wa Fedha Omar Yussuf Mzee,[Picha na Ikulu.]
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(wa pili kulia) akiangalia hatua ya ujenzi na kupata maelezo katika Kiwanda cha Sukari cha Mahonda kiliopo katika Wilaya ya Kaskazini B. Unguja alipofanya ziara maalum ya kutembelea kiwanda hicho leo,ambacho kinachofanyiwa ukarabati na Kampuni ya Shanta Sugar Holding Ltd kutoka nchini India,[Picha na Ikulu.]
Hili
ni jengo la Kiwanda cha Sukari cha Mahonda ambalo linamitambo mbali
mbali ambayo inafanyiwa ukarabati wa hali ya juu na Kampuni ya Shanta Sugar Holding Ltd kutoka nchini India,na baadae mitambo hiyo iweze kuzalisha Sukari itakayouzwa ndani na Nje ya Nchi,Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Sheinleo alitembelea na kuona hali ya ukarabati huo akiwa katika ziara
maalum,[Picha na Ikulu.]
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(wa pili kulia) akipata maelezo wakati alipofuatana Meneja wa Kiwanda
cha Sukari cha Mahonda Bw.Rajesh Kumar (katikati) alipotembelea kiwanda hicho leo,ambacho kinachofanyiwa ukarabati na Kampuni ya Shanta Sugar Holding Ltd kutoka nchini India,kiliopo katika Wilaya ya Kaskazini B. Unguja,(kulia) Meneja mradi Tushar MEHTA,[Picha na Ikulu.]
Baadhi ya Mashine katika kiwanda cha Sukari cha Mahonda Wilaya ya Kaskazini B. Unguja,ambacho kinachofanyiwa ukarabati na Kampuni ya Shanta Sugar Holding Ltd kutoka nchini India,Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akiambatana na Viongozi mbali mbali wa Serikali alitembelea kiwanda
hicho leo,[Picha na Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akionesha kitu wakati alipotembelea kiwanda cha Sukari cha Mahonda Wilaya ya Kaskazini B. Unguja leo ambacho kinachofanyiwa ukarabati na Kampuni ya Shanta Sugar Holding Ltd kutoka nchini India,akiwa katika ziara aliyofuatana na Viongozi mbali mbali wa Serikali,[Picha na Ikulu.]
Majengo
ya Kiwanda cha Sukari cha Mahonda kiliopo Wilaya ya Kaskazini B.Unguja
yakiwa katika hali hiyo inanyoonekana pichani katika ukarabati
unaofanywa na Kampuni ya Shanta Sugar Holding Ltd kutoka nchini India,[Picha na Ikulu.]
KOMBE AMUUNGA MKONO RAIS MAGUFULI KWA KUWAPATIA JAMBO LEO FAGIO ZA USAFI SIKUKUU YA UHURU
Waandishi wa habari wa gazeti la
Jambo Leo, wakifurahia kupata fagio walizokabidhiwa na Mwenyekiti wa
Bodi ya Zahanati ya Mji Mwema Kigamboni, Dar es Salaam, Omary Kombe
(kulia), katika hafla iliyofanyika katika chumba cha habari cha gazeti
hilo, Dar es Salaam. Kombe ametoa msaada huo kuunga mkono maelekezo ya
Rais Dk. John Magufuli ya kufuta sherehe za Sikukuu ya Uhuru ili
wananchi washiriki siku hiyo kufanya usafi wa mazingira kwa lengo la
kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu nchini. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
KOCHA SUPER D AMNOA BONDIA IBRAHIMU CLASS KING CLASS MAWE
Bondia Ibrahimu Class ‘King Class Mawe’ akifundishwa jinsi ya kupiga ngumi za mkunjo wa chini ‘UpCat’ wakati wa mazoezi ya bondia huyo kujiandaa na mpambano wake na Twaha Kassimu utakaofanyika Desemba 25 katika uwanja wa Jamhuri Morogoro Picha na SUPER DBOXING NEWS |
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila ‘Super D’ juu akimfanyisha mazoezi ya misuli ya shingo kupandisha na kushusha shingo huku akiwa juu ya bondia Ibrahimu Class ‘King class Mawe’ wakati wa mazoezi ya kujiandaa na mapambano ya kitaifa na kimataifa ya bondia huyo Picha na SUPER DBOXING NEWS |
…………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu
KOCHA wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila ‘Super D’ amendelea kuwamwagia sumu mabondia Ibrahimu Class ‘king Class Mawe’ na Vicent Mbilinyi wakati wa mazoezi yao ya kujiandaa na mapambano yao yatakayofanyika desemba 25 katika uwanja wa Jamhuri Morogoro
KOCHA wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila ‘Super D’ amendelea kuwamwagia sumu mabondia Ibrahimu Class ‘king Class Mawe’ na Vicent Mbilinyi wakati wa mazoezi yao ya kujiandaa na mapambano yao yatakayofanyika desemba 25 katika uwanja wa Jamhuri Morogoro
Wakati Class akimvaa Twaha Kassimu bondia vicent Mbilinyi atavaana na bondia mkongwe kabisa Deo Njiku wa Morogoro
Akizungumzia mazoezi ambayo
anampa bondia huyo bingwa wa mikanda miwili ya U.B.O na WPBF Afrika
Ibrahimu Class ambapo kwa sasa anamfanyisha mazoezi ya kumjengea nguvu
pamoja na akili kwa ajili ya mchezo wake ujao
Kocha huyo akimfanyisha mazoezi
mbalimbali ya nguvu yakiwemo ya kujenga misuli ya tumbo pamoja na shingo
ambapo bondia huyo kwa sasa anafanya mazoezi mara tatu kwa siku na
kusimamiwa vizuri na kocha wake tayari kwa pambano hilo.
Ni kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili
SERIKALI imewasimamisha kazi
watumishi watatu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambao jana
iliamriwa kwamba watahamishiwa mikoani. Watumishi hao ni Bw. Anangisye
Mtafya, Bw. Nsajigwa Mwandengele na Bw. Robert Nyoni.
Uamuzi huo umetolewa leo
(Jumamosi, Novemba 28, 2015), na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa
ili kupisha uchunguzi zaidi wa tuhuma zinazowakabili. Kama ilivyo kwa
wenzao sita waliosimamishwa kazi jana (akiwemo aliyekuwa Kamishna Mkuu),
nao pia hawaruhusiwi kusafiri kwenda nje ya nchi hadi uchunguzi
utakapokamilika.
“Kazi ya kuwachunguza ilianza
jana ileile na sasa, tumeona hawa watu wanapaswa kuwa nje ya utumishi
ili kupisha uchunguzi ufanyike kwa uhuru zaidi,” alisema Waziri Mkuu.
Pia Waziri Mkuu amemuagiza Kaimu
Kamishna Mkuu wa TRA, Dkt. Philip Mpango atekeleze maagizo hayo kwa
kuwaandikia barua watumishi hao.
Jana mchana, Waziri Mkuu alifanya
ziara ya kushtukiza kwenye bandari ya Dar es Salaam akiwa na nia ya
kukagua namna shughuli zinavyoendelea kwenye bandari hiyo hasa kwenye
maeneo ya kupokelea mizigo kutoka nje ya nchi.
Katika kikao kilichofanyi ka
bandarini hapo na kuhudhuriwa na baadhi ya viongozi wa Serikali, Waziri
Mkuu aliamua kuwasimamisha kazi maafisa watano na TRA kutokana na
‘upotevu’ wa makontena 349 yenye thamani ya zaidi ya sh. bilioni 80/-.
Waziri Mkuu alisema upotevu huo
unasababishwa na mchezo unaofanyika baina ya wafanyabiashara na
watumishi wa TRA ambao wanaruhusu makontena kupita bila kulipiwa ushuru
na hivyo kuikosesha Serikali mapato.
JNIA YAONGEZA UKAGUZI MIZIGO YA POSTA, SASA KUKAGULIWA MARA YA PILI KABLA YA KUPAKIZWA KWENYE NDEGE
Mkurugenzi
wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es
Salaam, Bw.Injinia Thomas Haule, (katikati), akizungumza kwenye mkutano
na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa uwanja huo leo
Ijumaa Novemba 27, 2015. Utawala wa uwanja huo ulio chini ya Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege Tanzania, TAA, umejipanga upya katika kuimarisha
ulinzi ambapo kuanzia sasa, vifurushi na mizigo yote kutoka posta
itakaguliwa kwa mara ya pili kabla ya kupakiwa ndani ya ndege, ikiwa ni
hatua ya kudhibiti vifurushi na mizigo haramu kupenya kwenye ndege.
Kushoto ni Kaimu Meneja Usalama wa Uwanja huo, Bw.David Ngaragi,
(kushoto) na Afisa Usalama Mwandamizi wa Uwanja huo, Dorice Uhagile.
(Picha na K-Vis Media/Khalfan Said)
Na K-Vis Media
UONGOZI wa Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere unaomilikiwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
Tanzania, TAA, umetangaza leo Ijumaa Novemba 27, 2015 kuwa kuanzia sasa
vifurushi na mizigo mingine yote ya Shirika la Posta Tanzania,
itakaguliwa kwa mara ya pili kama mizigo mingine yoyote kabla ya
kupakiwa ndani ya ndege.
Uamuzi huo umetangazwa na
Mkurugenzi wa Uwanja huo, (JNIA), Injinia Thomas Haule, wakati
akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa
mikutano wa VIP ulioko uwanjani hapo.
Alisema, uamuzi huo ni baada ya
Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege, TAA, kutoa maonyo kadhaa, kwa Shirika la
Posta, kuimarisha ukaguzi wa vifurushi na mizigo itokayo Posta kwa vile
imekuwa ikikamatwa na mizigo ambayo ni tofauti na iliyokusudiwa.
Alitaja mizigo hiyo kuwa ni pamoja
nabangi, na kwamba, Uholanzi wamekuwa wakilalamika mara kadhaa kuwa
wamekuwa wakikamata vifurushi vya Posta vikiwa na mizigo
iliyoharamishwa.
“Sisi Kama Mamlaka, wajibu wetu
mkubwa ni kuzuia kitu au vitu vyovyote vinavyoweza kuhatarisha usalama
wa abiria wawapo ndani ya ndege au ndege yenyewe haviingii ndani ya
ndege.” Alianza kwa kusema Injinia Haule na kuongeza kuwa, vitu vingine
kama madawa ya kulevya, pembe za ndovu, na vingine vingi, ,
vinashughulikiwa na mamlaka nyingine ambazo zina maafisa wake hapa JNIA
wakishirikiana na maafisa wetu.
Hata hivyo makosa yafanywayo na
idara Fulani ya serikali yenye afisa wake hapa JNIA, ni wazi kwamba
watakaonyooshewankidole ni TAA, alisema na kubainisha kuwa Mamlaka
haitavumilia tena uzembe utakaofanywa na taasisi nyingine ya serikali
katika kuhakikisha zinatekeleza wajibu wake ipasavyo
Meneja
wa Usalama wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, TAA, kwenye uwanja
wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Bw.David
Ngaragi, akifafanua jambo kwenye mkutano huo na waandishi wa habari
Waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, JNIA, Injinia Thomas Haule
Injinai
Haule akiteta jambo na Afisa Habari wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
Tanzania, Bw. Godfrey Lutego, muda mfupi kabla ya kuanza kwa mkutano huo
Amos Makalla apiga marufuku likizo za Ma dc, Wakurugenzi na wakuu wa idara mkoani Kilimanjaro
Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro
KATIKA hali inayoonyesha ni joto kali la kuwatumikia Watanzania, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makalla, amepiga marufuku likizo za Wakuu wa wilaya, Wakurugenzi na Wakuu wa Idara kwenye mkoa wake ili kutekeleza kwa vitendo hotuba na maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli.
RC Makalla aliyasema hayo juzi katika kikao cha kazi na wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri, wakuu wa idara wa halmashauri na Kamati ya Ulinzi na usalama ya mkoa huo kwa ajili ya kupeana mikakati ya majukumu ya kuwatumikia Wana Kilimanjaro na Watanzania kwa ujumla, ikiwa ni hatua nzuri ya kwenda na kasi ya Dr Magufuli.
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makalla, akizungumza na Wakuu wa Wilaya,
Wakurugenzi na Wakuu wa Idara katika Mkoa huo ili kujipanga katika
majukumu mbalimbali ya kuwatumikia wana Kilimanjaro na Watanzania kwa
ujumla. Picha na Mpiga Picha Wetu.
Baadhi
ya watendaji wa Mkoa Kilimanjaro wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa
huo, Aamos Makalla alipozungumza nao jana. Katika kikao hicho, RC
Makalla alipiga marufuku likizo kwa Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na
Wakuu wa Idara ili kujipanga na maagizo yaliyotolewa na Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli.
Alisema
kuwa Dr Magufuli ameagiza mambo mengi mazuri na yenye kuhitaji utendaji
uliotukuka, ikiwamo elimu bure, mikakati ya kubana matumizi, kupambana
na maradhi mbalimbali, ugonjwa wa kipindupindu, usimamizi wa pembejeo na
kuzuia pia matukio mbalimbali yenye kugharimu pesa, sanjari na
mapambano ya dawa za kulevya na uwadijibikaji kazini.
“Hakuna muda wa kupoteza katika kufanyia kazi maagizo ya rais Magufuli, hivyo sote kwa pamoja tunapaswa kujipanga na kwenda na kasi ya serikali yetu ili kuhakikisha kwamba nchi yetu inapiga hatua kubwa kama yalivyokuwa makusudio yetu ya kuhakikisha watoto wanasoma bure, hivyo sitaki kusikia likizo kutoka kwa Ma DC, Wakurugenzi na Wakuu wa Idara katika Mkoa wetu wa Kilimanjaro. “Suala la kubana matumizi, pembejeo kwa wakulima, vita ya madawa ya kulevya na mengineyo yanapaswa kuanza sasa, huku tukihakikisha kwamba maadhimisho ya siku ya Uhuru yanajikita zaidi kwenye suala zima la usafi kuanzia kaya, mtaa au kijiji na kwingineko,” Alisema Makalla.
Katika hatua nyingine, RC Makalla alionyesha kukerwa na ugonjwa wa kipindu kipindu na kusema kuwa kamwe hataki kuona ugonjwa huo unaingia kwenye Mkoa wake wa Kilimanjaro, akiwataka wataalamu wa afya na watendaji wa serikali kujipanga kikamilifu.
Kwa mujibu wa Makalla, endapo watajipanga imara katika suala zima la usafi, usimamizi wa rasilimali na utendaji uliotukuka katika maeneo yao, Mkoa huo utazidi kupiga hatua kubwa kiuchumi, hivyo kufanikisha kwa vitendo dhamira kubwa ya Dr Magufuli ya kuwakwamua wananchi wake na Watanzania kwa ujumla. RC Makalla ni miongoni mwa viongozi wa juu wanaopambana kwenda na kasi ya Rais Magufuli, ikiwa ni siku chache tangu alipoapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, huku wananchi wengi wakionyesha kuwa na Imani kubwa na rais huyo wa awamu ya tano.
“Hakuna muda wa kupoteza katika kufanyia kazi maagizo ya rais Magufuli, hivyo sote kwa pamoja tunapaswa kujipanga na kwenda na kasi ya serikali yetu ili kuhakikisha kwamba nchi yetu inapiga hatua kubwa kama yalivyokuwa makusudio yetu ya kuhakikisha watoto wanasoma bure, hivyo sitaki kusikia likizo kutoka kwa Ma DC, Wakurugenzi na Wakuu wa Idara katika Mkoa wetu wa Kilimanjaro. “Suala la kubana matumizi, pembejeo kwa wakulima, vita ya madawa ya kulevya na mengineyo yanapaswa kuanza sasa, huku tukihakikisha kwamba maadhimisho ya siku ya Uhuru yanajikita zaidi kwenye suala zima la usafi kuanzia kaya, mtaa au kijiji na kwingineko,” Alisema Makalla.
Katika hatua nyingine, RC Makalla alionyesha kukerwa na ugonjwa wa kipindu kipindu na kusema kuwa kamwe hataki kuona ugonjwa huo unaingia kwenye Mkoa wake wa Kilimanjaro, akiwataka wataalamu wa afya na watendaji wa serikali kujipanga kikamilifu.
Kwa mujibu wa Makalla, endapo watajipanga imara katika suala zima la usafi, usimamizi wa rasilimali na utendaji uliotukuka katika maeneo yao, Mkoa huo utazidi kupiga hatua kubwa kiuchumi, hivyo kufanikisha kwa vitendo dhamira kubwa ya Dr Magufuli ya kuwakwamua wananchi wake na Watanzania kwa ujumla. RC Makalla ni miongoni mwa viongozi wa juu wanaopambana kwenda na kasi ya Rais Magufuli, ikiwa ni siku chache tangu alipoapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, huku wananchi wengi wakionyesha kuwa na Imani kubwa na rais huyo wa awamu ya tano.
AFISA MATEKELEZO NA URATIBU WA BIMA YA AFYA (NHIF) SALVATORY OKUMU AKITOA MADA KATIKA KONGAMANO LA WADAU WA BIMA YA AFYA DAR ES SALAAM
Afisa Matekelezo na Uratibu wa Bima ya Afya Salvatory Okumu, akitowa mada katika kongamalo hili (PICHA NA KHAMISI MUSSA)
Mhadhiri
wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi Muhimbili, Dereck Chitama
akizungumza na washiriki wa kongamano la Bima ya Afya lililoandaliwa na
Policy Forum Dar es Salaam, ambapo -upatikanaji wa huduma za Afya kwa
jamii kupitia Bima hiyo ni miaka zaidi zaidi ya Ishirini imepita tangu
kuanzishwa kwa bima ya Afya nchini lakini mpaka leo zaidi ya robo tatu
ya watu Tanzania hawana bima ya Afya, Hata wale waliyonayo bado wanapata
huduma duni hasa kwa wale walioko vijijini, kutumia dawa na vifaa tiba
ni kawaida malengi,Malengo ya Dunia yametamka wazi kwamba kila mwananchi
aweze kupata huduma bora za Afya na akahoji, je, kwa mwenendo huu wa
sasa ambapo watu wengi hawana bima ya Afya Tunafika?
Programu Afisa Mfuko wa Afya ya Jamii, Kidani Magwila akizungumza katika kongamano hilo
Balozi Sefue kuhusu kusimamishwa kazi Kamishna Mkuu TRA
Katibu
mkuu kiongozi balozi Ombeni Sefue akizungumza na waandishi kutoka
vyombo mbalimbali vya habari hawapo pichani kuhusu upotevu wa makontena
zaidi ya 349 huku akiwa ameshika nyaraka yenye orodha ya makontena hayo.
Katibu mkuu kiongozi balozi Ombeni Sefue akionesha nyaraka hiyo mbele ya waandishi wa habari waliofika kwenye mkutano huo.
Katibu mkuu kiongozi balozi Ombeni Sefue wakwanza kushoto akifafanua jambo mbele ya wanahabari.
RAIS DK. JOHN POMBEA MAGUFULI AMSIMAMISHA KAZI KAMISHNA WA TRA
Rais
wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
amemsimamisha kazi kuanzia leo tarehe 27.Nov 2015 Kamishna mkuu wa TRA
nchini ndugu Rished Bade kufuatia ziara ya kushitukiza ya waziri mkuu
Mh. Majaliwa Kassimu Majaliwa mapema leo asubuhi baada ya kubaini
bandari ya Dar es salaam kupitisha makontena zaidi ya miatatu na
kusababisha hasara ya zaidi ya shilingi bilioni 80.
Rais Dkt John Pombe Magufuli
amemteua Katibu mtendaji wa tume ya mipango Dkt. Philip Mpango kukaimu
nafasi hiyo taarifa hiyo iliyosomwa na Katibu mkuu Kingozi Balozi
Ombeni Sefue ikiwataka maofisa wote wa TRA kutosafiri nje ya nchi mpaka
pale uchunguzi dhidi yao utakapo kamilika.
MWILI WA MAWAZO KUAGWA KITAIFA KATIKA UWANJA WA FURAHISHA JIJINI MWANZA.
Mkutano wa Naibu Katibu Mkuu Chadema Salum Mwalimu na Wanahabari Jijini Mwanza hii leo.
Na:Binagi Media Group
BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUSIKILIZA
Naibu
Katibu Mkuu Chadema, Salum Mwalimu akionyesha kibali kilichotolewa na
Manispaa ya Ilemela ili kuruhusu ibada ya kumuaga Marehemu Mawazo
Kufanyika kesho katika Uwanja wa Furahisha
Mkutano wa Naibu Katibu Mkuu Chadema Salum Mwalimu na Wanahabari Jijini Mwanza hii leo (hawapo pichani).
Kushoto ni Ezekiel Wenje na Kulia ni Grace Kihwelu ambae ni Mbunge Viti Maalumu Chadema Mkoani Kilimanjaro
Singo
Kigaila Benson ambae ni Mkurugenzi wa Mafunzo Chadema (Kushoto) akiwa
na Peter Mekele ambae ni Mwenyekiti Chadema Kanda ya Ziwa Victoria
(Kulia)
Husna Amri Said ambae ni Mwenyekiti BAWACHA Wilayani Geita
Viongozi na Makada wa Chadema
Mkutano wa kutoa ratiba za kuuaga mwili wa Marehemu Mawazo kwa wanahabari Jijini Mwanza hii leo
Wanahabari
KAMPENI YA ABIRIA PAZA SAUTI YAZINDULIWA RASMI JIJINI DAR ES SALAAM LEO
Mkuu wa
Kitengo cha Elimu kwa Umma wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mrakibu
Msaidizi wa Polisi (ASP), Abel Swai (kulia), akizungumza katika mkutano
na waandishi wa habari Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo, kuhusu kampeni ya
Abiria Paza Sauti iliyozinduliwa Dar es Salaam leo asubuhi.i kote kwa
njia ya kutoa elimu, haki na wajibu wa raia wanapokuwa safarini.
No comments :
Post a Comment