Kampuni ya Tana Communication
Media inayomiliki kituo cha Radio 5 pamoja na mfuko wa kijamii wa PSPF
imewafikia wadau wa mfuko huo kwa kuwapa elimu kupitia kipindi cha
“Good-Morning Tanzania
Mkurugenzi mkuu wa mfuko huo
Bw.Adam Mayingu akiongozana na Afisa mahusiano wa mfuko huo Bw.Abdul
Njaidi walipokelewa na meneja Masoko na Mahusiano wa Radio 5 Bi.Sarah
Keiya pamoja na Meneja Biashara wa kituo hicho Bi.Angela Maina
Akizungumza katika kipindi hicho
kinachorushwa na kituo hicho Bw.Adam alisema kuwa ni wajibu wao kutoa
elimu kwa jamii ili iweze kupata fursa ya kufahamu vema mfuko huo pamoja
na kufaidika na huduma za afya za PSPF kupitia NHIF
Kwa upande wake Meneja masoko na
mahusiano wa Radio 5 Bi.Sarah alisema uwepo wa mifuko ya kijamii
inawezesha wananchi kupanga maisha yao ya sasa na baadae na ndio maana
Radio 5 imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha mipango ya mifuko hii
inawafikia walengwa
Bi,Sarah alisema kuwa Mkurugenzi
wao Bw.Robert Francis amekuwa akiwezesha idara yao ya masoko na
biashara kwa kutoa bei nafuu ya matangazo kwa mifuko hii ya kijamii ili
kuwezesha kuwafikia wananchi kwa wingi na urahisi
No comments :
Post a Comment