Friday, November 27, 2015

SERIKALI YACHARUKA, WAZIRI MKUU MAJALIWA AAMURU MAAFISA WA TRA KUKAMATWA MARA MOJA

Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa leo ameamuru kukamatwa kwa maafisa kadhaa  wa Mamlaka ya Mapato (TRA) na wengine kufukuzwa kazi  baada ya kufanya ziara ya kushtukiza Bandarini na kukuta madudu ambayo hakuyafurahia.
Maafisa hao, ambao kwa sasa tunahifadhi majina ili Jeshi la Polisi liweze kuwashughulikia, wametakiwa pia kusalimisha hati zao za usafiri.
Hii imekuja baada ya kugundulika kwamba kuna makontena 349 yenye thamani ya zaidi ya bilioni 80 ambayo data za Mamlaka ya Bandari inazo lakini katika mtandao wa TRA hayaonekani.
Habari kamili inaandaliwa. Fanya subira....
Kwa sasa anza na picha....


Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na uongozi wa TRA na TPA alipofanya ziara ya kustukiza Bandarini leo asubuhi.
 Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa akiongea na viongozi wa TRA na TPA
Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa akikabidhi orodha ya makontena yaliyopotea na ambayo TRA haina taarifa nazo
Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa 
akiagana na viongozi wa TRA na TPA.


 
Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, Bw.Injinia Thomas Haule, (katikati), akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa uwanja huo leo Ijumaa Novemba 27, 2015. Utawala wa uwanja huo ulio chini ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, TAA, umejipanga upya katika kuimarisha ulinzi ambapo kuanzia sasa, vifurushi na mizigo yote kutoka posta itakaguliwa kwa mara ya pili kabla ya kupakiwa ndani ya ndege, ikiwa ni hatua ya kudhibiti vifurushi na mizigo haramu kupenya kwenye ndege. Kushoto ni Kaimu Meneja Usalama wa Uwanja huo, Bw.David Ngaragi, (kushoto) na Afisa Usalama Mwandamizi wa Uwanja huo, Dorice Uhagile. (Picha na K-Vis Media/Khalfan Said)
Na K-Vis Media
UONGOZI wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere unaomilikiwa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, TAA, umetangaza leo Ijumaa Novemba 27, 2015 kuwa kuanzia sasa vifurushi na mizigo mingine yote ya Shirika la Posta Tanzania, itakaguliwa kwa mara ya pili kama mizigo mingine yoyote kabla ya kupakiwa ndani ya ndege.
Uamuzi huo umetangazwa na Mkurugenzi wa Uwanja huo, (JNIA), Injinia Thomas Haule, wakati akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa VIP ulioko uwanjani hapo.
Alisema, uamuzi huo ni baada ya Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege, TAA, kutoa maonyo kadhaa, kwa Shirika la Posta, kuimarisha ukaguzi wa vifurushi na mizigo itokayo Posta kwa vile imekuwa ikikamatwa na mizigo ambayo ni tofauti na iliyokusudiwa.
Alitaja mizigo hiyo kuwa ni pamoja nabangi, na kwamba, Uholanzi wamekuwa wakilalamika mara kadhaa kuwa wamekuwa wakikamata vifurushi vya Posta vikiwa na mizigo iliyoharamishwa.
"Sisi Kama Mamlaka, wajibu wetu mkubwa ni kuzuia kitu au vitu vyovyote vinavyoweza kuhatarisha usalama wa abiria wawapo ndani ya ndege au ndege yenyewe haviingii ndani ya ndege." Alianza kwa kusema Injinia Haule na kuongeza kuwa, vitu vingine kama madawa ya kulevya, pembe za ndovu, na vingine vingi, , vinashughulikiwa na mamlaka nyingine ambazo zina maafisa wake hapa JNIA wakishirikiana na maafisa wetu.
Hata hivyo makosa yafanywayo na idara Fulani ya serikali yenye afisa wake hapa JNIA, ni wazi kwamba watakaonyooshewankidole ni TAA, alisema na kubainisha kuwa Mamlaka haitavumilia tena uzembe utakaofanywa na taasisi nyingine ya serikali katika kuhakikisha zinatekeleza wajibu wake ipasavyo
 Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, Injinia Thomas Haule, akizungumza kwenye mkutano huo
 Meneja wa Usalama wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, TAA, kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Bw.David Ngaragi, akifafanua jambo kwenye mkutano huo na waandishi wa habari
 Waandishiw a habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, JNIA, Injinia Thomas Haule

Injinia Haule akiteta jambo na Afisa Habari wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, Bw. Godfrey Lutego, muda mfupi kabla ya kuanza kwa mkutano huo

Mteja wa muda mrefu wa bemki ya Amana Bw Masoud Khalfan ambaye akizindua wiki ya huduma kwa wateja katika tawi la Main la benki ya Amana jijini Dar ka kukata utepe. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa benki hiyo Dk Muhsin Masoud, Kulia ni mkuu wa idara ya masoko Bw Dassu Mohamed Mussa, kushoto ni mteja wa siku nyingi wa benki hiyo Bw Dossa.
Mkuu wa idara ya masoko Bw. Dassu Mussa kushoto akiwa na mkuu wa kitengo cha fedha Bw. Fahad Hamid siku ya uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja.
Benki ya kwanza ya kiislamu Tanzania, Amana Bank imeadhimisha miaka minne tangu kuanza rasmi kutoa huduma zake kwa wateja mnamo 24 Novemba 2011. Wakuu wa idara Mameneja na wafanyakazi siku ya jumatatu wote walikutana na wateja na kuwapatia huduma mbalimbali kupitia matawi yetu yote ya Dar es salaam, Arusha na Mwanza.
Meneja wa tawi la Main,  Bi Aisha Awadh akimwelekeza kitu mteja wa benki hiyo mama Sangawe.
Amana Bank ambayo kwa sasa ina wateja zaidi ya 20,000 na matawi 7 Tanzania nzima, inachukua fursa katika maadhimisho haya kuwashukuru wateja wake wote kwa kuwa wazalendo na kuichagua Amana Bank kama pendekezo lao kwa huduma za kibenki. Amana Bank inaahidi kuendelea kuwekeza na kukuza mtandao wake na kuleta bidhaa na huduma bora Zaidi na za kisasa. Amana Bank mpaka sasa ina matawi saba ambapo manne yapo jijini Dar nayo ni Tandamti, Lumumba, Nyerere na main ambapo ndipo makao makuu ya benki hiyo ya aina yake nchini.
Mfanyakazi wa benki ya Amana (Kushoto) akiwahudumia wateja kwa viburudisho katika siku ya wiki ya huduma kwa wateja wiki hii.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Amana wakipata picha ya pamoja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Amana Bank, Dr. Muhsin Salim Masoud amesema, “Katika kipindi hiki maalum kwa benki yetu, tutashirikiana na wateja wetu wa ndani na wa nje kwa kuwapatia huduma bora zaidiTunaamini wateja wetu ndio muhimili wa mafanikio yetu, lengo letu kubwa ni kuwaridhisha wao hivyo tumejidhatiti kuwapa huduma bora muda wote bila kujali mahali walipo. Tunawaahidi wateja wetu  huduma za kiwango cha juu kwa ajili ya mahitaji yao ya binafsi au kibiashara muda wote.
Mtoa huduma kwa wateja Bi. Zainab wa tawi la Mwanza akimhudumia kwa viburudisho mteja wa benki hiyo.

Mteja huyu akijipatia huduma katika tawi la Mwanza
Huduma kwa wateja.
Maadhimisho haya yatahitimishwa ijumaa ya 27/11/2015, kwa hafla ya  kuwazawadia wateja na wafanyakazi katika matawi ya Amana Bank ambapo mkurugenzi wa benki hiyo  Dk Muhsin Masoud atakuwa katika tawi la jijini Mwanza mjini kukutana na wateja na kupokea maoni na ushauri wa kila aina utakaotolewa na wateja wao.
Baadhi ya wateja wakijipatia huduma katika benki ya Amana tawi la jijni Arusha.

Huduma kwa wateja zikiendelea jijini Arusha.
DSC_0928
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu, Mh. Idd Ramadhan Mapuri (katikati) akizindua taarifa ya Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kuhusu utafiti wa Hali ya Haki za watu wenye kuishi maisha asilia Tanzania. kushoto kwake ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bi. Mary Massay na (kulia) ni mmoja wa wajumbe walioshiriki kuandaa ripoti hiyo, kutoka nchini Kenya katika taasisi ya ACHPR, Dk. Naomi Kipuri.(Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog).
Na Andrew Chale, Modewjiblog
[DAR ES SALAAM-TANZANIA] Jamii ya watu wa asili na makundi yao wameiomba Serikali ya Tanzania kutambua uwepo wao hapa nchini ikiwemo kuwatangaza kwa mema na kuwasaidia kwa misingi ya haki, hutu na kimaendeleo kama watu wengine wanaotambulika ndani na nje ya mipaka yao.
Hayo yameelezwa mapema leo jijini hapa wakati wa uzinduzi wa taarifa ya Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kuhusu utafiti wa Hali ya Haki za watu wenye kuishi maisha asilia Tanzania wakiwemo makabila ya Wa-Akiye,Wa- Hadzabe,Wa- IIparakuyio Masai na wengine wengi.
Akielezea katika uzinduzi huo mmoja wa wajumbe walioandaa taarifa ya Tume hiyo, ambaye anatoka nchini Kenya, katika taasisi ya African Commission on Human and Peoples Rights (ACHPR), Dk. Naomi Kipuri amebainisha kuwa jamii ya watu asilia wamekuwa na kilio cha muda mrefu cha kutaka kupata haki zao zao msingi na kutambulika zaidi.
“Utafiti tuliofanya jamii ya watu asilia wamekuwa katika malalamiko ya muda mrefu ikiwemo kutaka haki zao za msingi. Ikiwemo masuala ya elimu, makazi na haki zingine. Pia wameomba Serikali kuwatangaza watu hawa wa asilia ili wasionekane wageni kwani jamii nyingi bado hazijawatambua na hata kupelekea kuwavunjia hutu wao” alieleza Dk. Naomi.
Aidha, Dk. Naomi katika uwakilishi wake wa mada kwenye mkutano huo amelezea namna ya jamii inavyoendelea kuwaona watu hao ni tofauti kiasi cha kupelekea watu hao kudumaa na maisha yale yale ya asilia.
DSC_0961
Mtangazaji wa radio Deutsche Welle (DW) ya Ujerumani, George Njogopa akifanya mahojiano na Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bi. Mary Massay. Kushoto ni Mratibu wa NGONET Ngorongoro, Samweli Nangiria “Jamii zingine zinawatenga watu wa jamii ya Wamasai, tumeshuhudia lugha na matamshi kwenye mizunguko ya watu ikiwemo kwenye madaladala, mitaani huku wakimuona Mmasai kama mtu tofauti, sasa katika ripoti hii imeweza kuelezea mambo mengi sana. Ikiwemo suala la Haki ya kuishi, kufanya kazi na mambo yote kama watu wengine” alimalizia Dk. Naomi. Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu, Mh. Idd Ramadhan Mapuri ameeleza kuwa kupitia ofisi yake itahakikisha inashughulikia suala hilo la kuwa karibu na watu asilia na kutambua misingi ya haki zao ambapo amebainisha watu hao wa asilia kwa Tanzania wanafikia makundi zaidi ya sita. Kwa upande wao baadhi ya wawakilishi wa watu hao wa watu asilia wakielezea katika mkutano huo, waliomba na wao na wapate wawakilishi maalum ikiwemo Bungeni ama sehemu za maamuzi ikiwemo Halmashauri na maeneo mengine ya Serikali ilikutambua michakato ya Kimaendeleo kwa kina. “Jambo la ardhi, ndilo linalotuumiza kwa sasa. Sie tunaporwa ardhi yetu kila siku na kesi nyingi ni za kuporwa ardhi na migogoro ya wakulima na wafugaji, ndani ya migogoro hii ina siri kubwa bila kujua kiini chake ni wakati wa kufika kule na kupata ukweli zaidi” alielezea Adam Ole Mwarabu Kwa upande wake, Mratibu wa NGONET Ngorongoro, Samweli Nangiria ambaye anawakilisha watu hao asilia anaeleza kuwa, wao wamekuwa wakitambuana kwa desturi ikiwemo suala la ufugaji na maisha mengine, Jamii nyingine imekuwa wakiwaona wao ni watu wa tofauti kiasi cha kupora mali zao ikiwemo ardhi, mifugo na mambo mengine ya msingi.
DSC_0953
Baadhi ya wawakilishi wa Jamii za watu asilia wakiwemo Wahadzabe, Masai, Wabarabaig na wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na wadau wengineo wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo juu ya usawa na kutambulika kama jamii asilia yenye tamaduni na desturi zake.
“Sie watu asilia tuna mahusiano mbalimbali na jamii zetu za kifugaji licha ya jamii zingine kutuingilia kwenye maeneo yetu na kupora ardhi yetu. Watu asilia tunahitajika kutambulika zaidi na hata kupatiwa huduma muhimu ikiwemo kujengewa shule, vyuo na mahitaji mengine ikiwemo haki na hutu kama watu wengine.” Alieleza Samweli Nangiria.
Kwa upande wake, .. ameweza kuipongeza tume ya Haki za Binadamu kwa kuweza kushughulikia suala hilo na hata kuandaa tukio hilo kwa kushirikisha wadau wengine wakiemo wao wa asilia.
“Tanzania ndio nchi ya kwanza kuaandaa kikao cha Afrika kwa watu hawa wa makundi maalum wa asilia, kilichofanyika mwaka uliopita. Hili ni jambo bora sana kwani watu asilia tunaendelea kutambulika zaidi.
Ripoti hiyo iliyozinduliwa ya taarifa ya Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kuhusu utafiti wa Hali ya Haki za watu wenye kuishi maisha asilia Tanzania, imeweza kuangalia mambo mbalimbali ikiwemo suala la haki ya kuishi, Utawala bora na namna ya jamii hizo zinapotokea katika maeneo yao hapa nchini.
DSC_0944
Wadau wa haki za binadamu wakiwa katika picha ya pamoja katika mkutano huo baada ya uzinduzi wa ripoti hiyo ya kuwatambua watu wa makundi asilia. Mkutano unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Blue Pearl Ubungo jijini Dar es Salaam.
DSC_2541
Mmoja wa washiriki wa mkutano huo Mhifadhi Mkuu, kutoka ofisi ya Makamu wa Rais, Bw. Seleman Kisimbo akichangia mada juu ya hali iliyopo sasa ikiwemo jamii hiyo ya watu asilia na changamoto za Mabadiliko ya tabia nchi ikiwemo suala la ukame inayowakabili katika maisha yao ya vijijini.
DSC_0946
Dk. Naomi Kipuri wa taasisi ya ACHPR, ya nchini Kenya akijadiliana jambo na Mhadhiri wa Sheria Chuo Kikuu cha Tumaini-Makumira, Bw. Elifuraha Laltaika.
DSC_0955
Baadhi ya wawakilishi wa Jamii za watu asilia wakiwemo Wahadzabe, Masai, Wabarabaig na wengineo wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye mkutano huo.

No comments :

Post a Comment