Waziri
Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa leo ameamuru kukamatwa kwa maafisa
kadhaa wa Mamlaka ya Mapato (TRA) na wengine kufukuzwa kazi baada ya
kufanya ziara ya kushtukiza Bandarini na kukuta madudu ambayo
hakuyafurahia.
Maafisa
hao, ambao kwa sasa tunahifadhi majina ili Jeshi la Polisi liweze
kuwashughulikia, wametakiwa pia kusalimisha hati zao za usafiri.
Hii imekuja baada ya kugundulika kwamba kuna makontena 349 yenye thamani ya zaidi ya bilioni 80 ambayo data za Mamlaka ya Bandari inazo lakini katika mtandao wa TRA hayaonekani.
Hii imekuja baada ya kugundulika kwamba kuna makontena 349 yenye thamani ya zaidi ya bilioni 80 ambayo data za Mamlaka ya Bandari inazo lakini katika mtandao wa TRA hayaonekani.
Habari kamili inaandaliwa. Fanya subira….
Kwa sasa anza na picha….
Kwa sasa anza na picha….
Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na uongozi wa TRA na TPA alipofanya ziara ya kustukiza Bandarini leo asubuhi.
Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa akiongea na viongozi wa TRA na TPA
Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa akikabidhi orodha ya makontena yaliyopotea na ambayo TRA haina taarifa nazo
Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa
akiagana na viongozi wa TRA na TPA.
Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa akiongea na viongozi wa TRA na TPA
Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa akikabidhi orodha ya makontena yaliyopotea na ambayo TRA haina taarifa nazo
Waziri Mkuu Mhe Majaliwa Kassim Majaliwa
akiagana na viongozi wa TRA na TPA.
MWILI WA MAWAZO KUAGWA KITAIFA KATIKA UWANJA WA FURAHISHA JIJINI MWANZA.
Mkutano wa Naibu Katibu Mkuu Chadema Salum Mwalimu na Wanahabari Jijini Mwanza hii leo.
Na:Binagi Media Group
Mwili wa aliekuwa
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Mkoa wa Geita Marehemu
Alphonce Mawazo, kesho unatarajiwa kuagwa Jijini Mwanza kabla ya kusafirisha
kwenda Mkoani humo kwa ajili ya Mazishi.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Mkoa wa Geita Marehemu
Alphonce Mawazo, kesho unatarajiwa kuagwa Jijini Mwanza kabla ya kusafirisha
kwenda Mkoani humo kwa ajili ya Mazishi.
Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema Salum Mwalimu, amesema Marehemu Mawazo
ataagwa Kitaifa kwa taratibu za chama hicho, katika uwanja wa Furahisha Jijini
Mwanza.
ataagwa Kitaifa kwa taratibu za chama hicho, katika uwanja wa Furahisha Jijini
Mwanza.
Amesema ratiba hiyo itatanguliwa na ratiba ya kifamilia ya kuuaga
mwili huo, ambayo itafanyika asubuhi Nyegezi Jijini Mwanza ambako ni nyumbani
kwa Mchungaji Charles Lugiko ambae ni baba mdogo wa Marehemu Mawazo hiyo ikiwa
ni baada ya mwili wake kutolewa katika Hospitali ya Rufaa Bugando
ulikohifadhiwa.
mwili huo, ambayo itafanyika asubuhi Nyegezi Jijini Mwanza ambako ni nyumbani
kwa Mchungaji Charles Lugiko ambae ni baba mdogo wa Marehemu Mawazo hiyo ikiwa
ni baada ya mwili wake kutolewa katika Hospitali ya Rufaa Bugando
ulikohifadhiwa.
Mwalimu amebainisha kwamba mwili huo utasafirishwa hiyo kesho
kwenda Mkoani Geita kuanzia majira ya saa nane mchana ambapo wakazi wa Mkoa huo
pia watapata fursa ya kuuagwa kesho kutwa jumapili.
kwenda Mkoani Geita kuanzia majira ya saa nane mchana ambapo wakazi wa Mkoa huo
pia watapata fursa ya kuuagwa kesho kutwa jumapili.
Ameeleza kwamba kuanzia majira ya saa mbili asubuhi, shughuli za
kuuaga mwili huo zitafanyika Kimkoa katika Uwanja wa Magereza Mjini Geita na
baadae kusafirisha kwenda Katoro ambapo wakazi wa Jimbo lake la Busanda
watapata fursa ya kuuaga mwili huo.
kuuaga mwili huo zitafanyika Kimkoa katika Uwanja wa Magereza Mjini Geita na
baadae kusafirisha kwenda Katoro ambapo wakazi wa Jimbo lake la Busanda
watapata fursa ya kuuaga mwili huo.
Mwalimu ametanabaisha kwamba, baada ya shughuli zote hizo
kukamilika, mazishi ya Marehemu Mawazo yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumatatu
katika Kijiji cha Chikobe Jimbo la Busanda Mkoani Geita.
kukamilika, mazishi ya Marehemu Mawazo yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumatatu
katika Kijiji cha Chikobe Jimbo la Busanda Mkoani Geita.
Shughuli zote hizo zinatarajiwa kuongozwa na Mwenyekiti wa Chadema
Taifa Freeman Mbowe, Viongozi waandamizi wa Chama hicho akiwemo Frederick
Sumaye, aliekuwa mgombea urais wa Ukawa Edward Lowasa, wabunge pamoja na makada
wa Chadema.
Taifa Freeman Mbowe, Viongozi waandamizi wa Chama hicho akiwemo Frederick
Sumaye, aliekuwa mgombea urais wa Ukawa Edward Lowasa, wabunge pamoja na makada
wa Chadema.
Ratiba za Mazishi ya Marehemu Mawazo ambae aliuawa Novemba 14
mwaka huu na watu wasiojulikana, zimejiri baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza
jana kuondoa zuio la Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza, lililokuwa zinazuia mwili
huo kuagwa Jijini Mwanza kutokana na hofu ya kiusalama pamoja na uwepo wa
mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu ambapo zuio hilo liliondolewa katika kesi
iliyofunguliwa na baba mlezi wa Mawazo, Mchungaji Charles Lugiko baada mvutano
mkali wa siku nne mahakamani hapo.
BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUSIKILIZA
mwaka huu na watu wasiojulikana, zimejiri baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza
jana kuondoa zuio la Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza, lililokuwa zinazuia mwili
huo kuagwa Jijini Mwanza kutokana na hofu ya kiusalama pamoja na uwepo wa
mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu ambapo zuio hilo liliondolewa katika kesi
iliyofunguliwa na baba mlezi wa Mawazo, Mchungaji Charles Lugiko baada mvutano
mkali wa siku nne mahakamani hapo.
BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUSIKILIZA
Naibu
Katibu Mkuu Chadema, Salum Mwalimu akionyesha kibali kilichotolewa na
Manispaa ya Ilemela ili kuruhusu ibada ya kumuaga Marehemu Mawazo
Kufanyika kesho katika Uwanja wa Furahisha
Mkutano wa Naibu Katibu Mkuu Chadema Salum Mwalimu na Wanahabari Jijini Mwanza hii leo (hawapo pichani).
Kushoto ni Ezekiel Wenje na Kulia ni Grace Kihwelu ambae ni Mbunge Viti Maalumu Chadema Mkoani Kilimanjaro
Singo
Kigaila Benson ambae ni Mkurugenzi wa Mafunzo Chadema (Kushoto) akiwa
na Peter Mekele ambae ni Mwenyekiti Chadema Kanda ya Ziwa Victoria
(Kulia)
Husna Amri Said ambae ni Mwenyekiti BAWACHA Wilayani Geita
Viongozi na Makada wa Chadema
Mkutano wa kutoa ratiba za kuuaga mwili wa Marehemu Mawazo kwa wanahabari Jijini Mwanza hii leo
Wanahabari
KAMPENI YA ABIRIA PAZA SAUTI YAZINDULIWA RASMI JIJINI DAR ES SALAAM LEO
Mkuu wa
Kitengo cha Elimu kwa Umma wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mrakibu
Msaidizi wa Polisi (ASP), Abel Swai (kulia), akizungumza katika mkutano
na waandishi wa habari Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo, kuhusu kampeni ya
Abiria Paza Sauti iliyozinduliwa Dar es Salaam leo asubuhi.
…………………………………………………………………………….
Na Dotto Mwaibale
MKUU wa
Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna wa Polisi, Mohamed
Mpinga amesema kila mwananchi anawajibu kuzuia ajali za barabarani
badala ya kudhani kazi hiyo ni ya polisi pekee.
Mpinga
alitoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Abiria Paza Sauti
iliyozinduliwa Stendi Kuu ya Mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam leo
asubuhi, ambao ulikwenda sanjari na mabalozi wa Usalama barabarani
(RSA) ambao walitoa elimu kwa abiria kuhusu usalama barabarani.
“Abiria
pazeni sauti pale mtakapoona dereva anaendesha gari lake ndivyo sivyo na
kama mtapaza sauti itasaidia kupunguza ajali hapa nchini” alisema
Kamanda Mpinga.
Mwakilishi
wa Mwenyekiti wa Usalama Barabarani ambaye ni Mratibu wa kampeni hiyo ,
Jackson Kalikuntima, alisema kampeni hiyo itaendelea nchini kote kwa
njia ya kutoa elimu, haki na wajibu wa raia wanapokuwa safarini.
Alisema abiria wanaowajibu wa kuzuia ajali wakishirikiana na mabalozi watakao kuwa ndani ya mabasi kuhimiza abiria kupaza sauti.
Kwa
upande wake Mkuu wa Kitengo cha Elimu kwa Umma wa Kikosi cha Usalama
Barabarani, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Abel Swai alisema kumekuwa
na changamoto kubwa kwa baadhi ya madereva kukiuka sheria na
kusababisha ajali kwa makusudi.
Alisema
kampeni hiyo inalengo la kutoa elimu kwa abiria waweze kujiamini na
kutoa taarifa pale wanapoona dereva anakwenda kinyume na sheria kwa
kutumia namba za kutoa taarifa kwa polisi na Mamlaka ya Udhibiti wa
Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) ambazo ni 0800110019 au
0800110020.
Swai
alisema madereva wanapaswa kutii sheria bila shuruti na kuwa wana amini
kila mmoja atakuwa makini na kuzingatia sheria ajali zitapungua kama sio
kuisha kabisa.
NHIF Yakabidhiwa Kituo cha Matibabu cha Mfano Dodoma
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa
Bima ya Afya ya Taifa Bw. Michael Muhando akionyesha funguo za majengo
ya kituo chake cha matibabu kilicho katika Chuo Kikuu cha UDOM mkoani
Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa
Bima ya Afya ya Taifa Bw. Michael Muhando akizungumza na waandishi wa
habari wakati wa kukabidhiwa majengo ya kituo chake cha matibabu kilicho
katika Chuo Kikuu cha UDOM mkoani Dodoma.
Majengo yenyewe yanavyoonekana.
Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa Bw. Michael Muhando akikagua majengo hayo.
……………………………………………………………………………………………………..
MFUKO wa taifa wa bima ya afya (NHIF) umekabidhiwa kituo chake cha
matibabu cha mfano mara baada ya ujenzi wa kituo hicho kukamilika.
Makadhiano hayo yamefanyika mjini hapa jana (leo) katika hafla fupimatibabu cha mfano mara baada ya ujenzi wa kituo hicho kukamilika.
iliyohudhuriwa na Uongozi wa nhif, hospitali ya mkoa na timu ya
wakandarasi akiwemo mshauri mkuu wa mradhi huo kampuni ya Nosuto
Associates.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Michael Mhando amesema kukamilika kwa
jengo hilo ni hatua kubwa iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na kazi
iliyoko sasa ni ya ununuzi wa vifaa na samani za jengo ili lianza
kutoa huduma kabla ya sikukuu ya Krismasi.
Amesema timu ya wataalamu kutoka Sekteratarieti ya mkoa tayari iko
jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuchagua vifaa tiba mbalimbali
vitakavyotumika. Ameongeza kuwa vifaa vyote hivyo pamoja na samani za
jengo hili vitalipiwa na Mfuko wa NHIF.
Kituo hicho cha matibabu cha kisasa kinayo mifumo mbalimbali ya TEHAMA
katika utoaji wake wa huduma ikiwemo miito kwa wauguzi, utayarishaji
wa madai na utambuzi wa wagonjwa.
Amesema malengo makuu ya ujenzi wa kituo hicho ni kuwa na kituo cha
kisasa kitakachowezesha wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na
umma wa watanzania kwa ujumla kupata huduma bora za matibabu
wanapokuwa Dodoma katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa Taifa.
Naye Mkurugenzi wa fedha,mipango na uwekezaji wa nhif bw Desudedit
Rutazaa amesema Kituo hicho vilevile kitasaidia kuwepo na watalamu
wenye uzoefu nchini kwani itakuwa ni sehemu ya kujifunzia kwa
wataalamu wa kada mbalimbali za udaktari na utabibu wawapo masomoni
katika mkoa wa Dodoma na mikoa mingine ya Tanzania.
KAMANDA MPINGA AZINDUA OPERESHENI PAZA SAUTI,JIJINI DAR ES SALAAM LEO
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani,DCP Mohamed
Mpinga, akisalimiana na Mabalozi wa Usalama Barabarani, muda mfupi
kabla ya kuzindua Operesheni ijulikanayo kwa jina la “Paza Sauti” yenye
lengo la kuwaelimisha abiria ili waweze kutoa taarifa mara wanapoona
kuna viashiria vya uvunjifu wa sheria za barabarani. Operesheni hii
ilizinduliwa jijini Dar es Salaam leo.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, DCP Mohammed
Mpinga, akitoa maelekezo ndani ya moja ya basi linalofanya safari zake
mkoani wakati wa kuzindua wa Operesheni Paza Sauti yenye lengo la
kuwaelimisha abiria ili waweze kutoa taarifa mara wanapoona viashiria
vya uvunjifu wa sheria za barabarani. Operesheni hii ilizinduliwa
jijini Dar es Salaam leo.
Wadau
wanaotumia usafiri wa barabara, wakiwemo madereva na abiria
wakimsikiliza Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed
Mpinga(hayupo pichani) alipozindua Operesheni Paza Sauti, yenye lengo
la kuwaelimisha abiria ili waweze kutoa taarifa wanapoona kuna
viashiria vya uvunjifu wa sheria za barabarani,Operesheni hii
ilizinduliwa jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Tuzo na Matukio wa Mabalozi wa Usalama Barabarani,Jackson
Kalikumtima(kulia), akitoa elimu kuhusiana na Operesheni ya Paza Sauti
kwa mmoja wa wadau wanaotumia usafiri wa barabara, Operesheni hii
ilizinduliwa Stendi ya Mabasi yaendayo mikoani ya Ubungo, jijini Dar es
Salaam leo.(Picha zote na Abubakari Akida,Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
MAHAKAMA YA TANZANIA YAFUNGUA MILANGO KWA WANAHABARI.
Jaji
Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Shaban Ally Lila akitoa ufafanuzi
kuhusu Kichwa cha Habari ya Mahakamani kilichoandikwa bila kuzingatia
Weledi na moja ya Gazeti la Kila siku wakati wa mafunzo ya siku mbili
ya Waandishi wa Habari za Mahakama yaliyofanyika jijini Dar es salaam.
Picha/Aron Msigwa –MAELEZO.
…………………………………………………………………………………….
Na. Aron Msigwa –MAELEZO.
.Dar es salaam.
Mahakama ya Tanzania imesema
kuwa itendelea kufanya kazi na vyombo vya Habari nchini katika
kuuhabarisha umma kuhusu utekelezaji wa jukumu la Kikatiba ililonalo la
kutafsiri sheria mbalimbali na kuzitolea maamuzi ili kuwawezesha
wananchi kujua na kupata Haki zao kwa wakati.
Akifunga Mafunzo ya siku 2 ya
waandishi wa Habari za Mahakama jana jijini Dar es salaam Jaji Kiongozi
wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Shaban Ally Lila aliwataka waandishi hao
kutimiza wajibu wao wa kuueleza umma taarifa sahihi za mashauri
mbalimbali yanayotokea mahakamani kwa kuzingatia sheria.
Alisema vyombo vya habari na
mahakama vinahitajiana, vinafanya kazi pamoja kwa manufaa ya umma huku
akieleza kuwa mikutano ya mara kwa mara kati ya wanahabari na mahakama
kunaongeza kuaminiana na kujenga mahusiano mazuri.
Alifafanua kuwa kazi ya Mahakama
kikatiba ni kutafsiri sheria mbalimbali na kuzitolea maamuzi kwa mujibu
wa sheria kulingana na mashauri yananayowasilishwa Mahakamani na
kuongeza kuwa hakuna Jaji wa Mahakama ya Tanzania anayeamua kesi bila
nje ya utaratibu wa sheria zilizopo.
Alisema wao kama majaji hutumia
sheria zilizopo katika kutoa maamuzi hata kama haziwapendezi wahusika na
kuongeza kuwa jambo wanalolifanya ni kutoa maoni na mapendekezo kwa
mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa hatua zaidi.
” Sisi kama Majaji hutumia
sheria zilizopo kutoa maamuzi,hatutungi sheria jukumu letu kikatiba ni
kutafsiri sheria mbalimbali na kuzitolea maamuzi pia tunatumia fursa ya
maamuzi tunayoyatoa kuelimisha jamii kuhusu sheria iliyotumika kutoa
haki katika kesi husika” Alisema.
Aliwataka waandishi wa Habari za
Mahakama kujipa muda wa kutosha pindi wanapofika Mahakamani kufuatilia
mashauri yanayoendeshwa ili waweze kuwa na taarifa za kutosha pindi
shauri linapofunguliwa na kutolewa hukumu ili kuwawezesha wananchi
kupata taarifa za kutosha za mwenendo wa Mashauri.
Aliongeza kuwa Mahakama ya
Tanzania imedhamiria kufanya kazi na waandishi wa habari nchini kwa
kuzingatia kwamba wakati majaji wanapotoa hukumu mahakamani kunakuwa na
idadi ndogo ya wananchi wanaoshuhudia kuliko ile iliyo nje ila vyombo
vya habari kutokana na umuhimu wake huwapasha habari mamilioni ya
watanzania walio nje ya Mahakama.
Alisema Mahakama itaendelea
kujenga mahusiano mazuri na Vyombo vya Habari hususan waandishi wa
Habari za Mahakama kwa kutenga maeneo ndani ya Mahakama yatakayotumiwa
na waandishi hao kuwawezesha kufanya kazi zao bila vikwazo kwa mujibu wa
sheria, kanuni na taratibu zilizopo.
Pia alieleza kuwa Mahakama,
itaendelea kutoa taarifa za ufafanuzi wa hukumu mbalimbali
zitakazotolewa kwa vyombo vya habari pia Nakala za taarifa za Hukumu kwa
waandishi wa habari ili kuwawezesha wananchi kujua ukweli wa yale
yanayojili mahakamani kuondoa upotoshaji unaotokea.
Majaliwa azindua ununuzi wa hisa za Benki ya Walimu- MCB
Waziri
Mkuu, Majaliwa Kassim Majliwa akigonga kengelle kuashiria uzinduzi wa
ununuzi wa hisa za Benki ya Walimu- MCB kwenye soko la hisa la Dar es
salaam. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es salaam Novemba 27, 2015.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua
uuzaji wa hisa za Benki ya Walimu MCB kwenye soko la hisa la Dar es
salaam, uliofanyika jijini Dar es salaam Novemba 27, 2015. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akiteta na baadhi ya Viongozi wa Benki
ya Walimu- MCB baada ya kuzindua uuzaji wa hisa za Benki hiyo katika
soko la hisa la Dar es salaam. Uzinduzi huo uliyofanyika jijini Dar es
salaam Novemba 27, 2015 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu,Majaliwa Kassim Majlaiwa akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya
Fedha Dkt. Servacius Likwelile baada ya kuzindua mpango wa Benki ya
Walimu MCB – MCB kuanza kuuza hisa zake kwenye soko la hisa la Dar es
salaam Novemba 27, 2015. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dares
salaam.3065 (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WAZIRI MKUU AWASIMAMISHA KAZI MAAFISA WATANO WA TRA
Waziri
Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akisalimiana na Kamishina Mkuu wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Rished Bade na Naibu wake, Lusekelo
Mwaseba (wapili kulia ) baada ya kuwasili kwenye bandari ya Dar es
salaam kutaka maelezo kuhusu upotevu wa makontena 349 yenye kodi ya
serikali ya thamani ya shilingi bilioni 80, Novemba 27, 2015. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akimwonyesha orodha ya makontena 349
yenye kodi ya serikali ya thamani ya shilingi bilioni 80 yaliyotoka
kwenye bandari ya Dar es salaam bila kulipiwa kondi, Kamishina Mkuu wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania , Rished Bade wakati alipotaka maelezo kuhusu
upotevu wa makontena hayo, bandarini jijini Dar es slaam Novemba 27,
2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akimkabidhi Kamishina Mkuu wa Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA), Rished Bade orodha ya makontena 349 yenye
kodi ya serikali ya thamani ya shilingi bilioni 800 yalitoka kwenye
bandari ya Dar es salaam bila kulipiwa kodi. Mheshimiwa Majaliwa
alikwenda kwenye bandari ya Dar es salaam Novemba 27, 2015 kutaka
maelezo kuhusu kupotea kwa makontena hayo. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Waziri
Mkuu, Majliwa Kassim Majaliwa akizungumza kwenye bandari ya Dar es
salaam alikokwenda Novemba 27, 2015 kutaka maelezo ya makontena 349
yaliyotoka kwenye bandari ya Dar es salam bila kulipiwa kodi na
kuikosesha serikali shilingi billioni 80. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
…………………………………………………………………………
*Ni kwa upotevu wa makontena 349, yana thamani ya sh. bilioni 80/-
WAZIRI MKUU Majaliwa Kassim
Majaliwa amewasimamisha kazi maafisa watano na watumishi watatu wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutokana na upotevu wa makontena 349
yenye thamani ya zaidi ya sh. bilioni 80/-.
Akizungumza na viongozi wa Mamlaka
ya Bandari pamoja na viongozi wa TRA katika ziara ya kushtukiza leo
mchana (Ijumaa, Novemba 27, 2015), Waziri Mkuu amewataka Kamishna Mkuu
wa TRA, Bw. Rished Bade na Naibu Kamishna Mkuu wa TRA, Bw. Lusekelo
Mwaseba wahahakikishe wanashirikiana na polisi kufuatilia upotevu huo na
kwamba fedha hizo zinapatikana na zinarudi Serikalini.
Akitangaza uamuzi huo baada ya
kufanya kikao na baadhi ya viongozi wa Serikali bandarini hapo, Waziri
Mkuu aliwataja maafisa waliosimamishwa kazi kuwa ni Kamishna wa Forodha,
Bw. Tiagi Masamaki na Mkuu wa Kituo cha Huduma kwa Wateja, Bw. Habibu
Mponezya.
“Hawa wanasimamishwa kazi. IGP
ninaagiza hawa watu wakamatwe na kuisaidia polisi. Hati zao za kusafiria
zikamatwe na mali zao zikaguliwe kama zinaendana na utumishi wa umma,”
alisema Waziri Mkuu.
Maafisa wengine waliosimamishwa
kazi ni Mkuu wa kitengo cha TEHAMA, Bw. Haruni Mpande, Bw. Hamisi Ali
Omari (hakutaja ni wa idara gani), na Mkuu wa Kitengo cha Bandari Kavu
(ICD In-Charge), Bw. Eliachi Mrema. “Hawa wanasimamishwa kazi hadi
uchunguzi utakapokamilika na pia wawe mikononi mwa polisi,” alisema.
Pia aliagiza watumishi watatu wa
mamlaka hiyo wahamishwe kutoka Dar es Salaam na kupelekwa mikoani.
Watumishi hao ni Bw. Anangisye Mtafya, Bw. Nsajigwa Mwandengele na Bw.
Robert Nyoni.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu
amemwagiza Katibu Mkuu wa Hazina, Dk. Servacius Likwelile ambaye
alikuwepo kwenye kikao hicho, kuhakikisha kuwa anapeleka wataalamu
kutoka Wakala wa Serikali Mtandao (e-Govt) haraka iwezekanavyo ili
wakakague mifumo ya taarifa na kubaini jinsi ambavyo wizi huo
unafanyika.
“Ninataka uchunguzi uanze
kufanyika mara moja, tafuteni njia ambazo zinatumika kama mianya ya wizi
kutokea hapa bandarini hadi kwenye ICDs. Nataka hayo makontena
yatafutwe hadi yajulikane yako wapi, na fedha hiyo ihakikishwe inarudi
serikalini,” alisema.
Kikao hicho kilihudhuriwa pia na
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Bw. Ernest Mangu, Katibu Mkuu wa Ofisi
ya Waziri Mkuu, Dkt. Florens Turuka, Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi,
Dkt. Shaaban Mwinjaka, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya DSM, Suleiman
Kova, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari (TPA), Bw. Awadh Massawe na
viongozi mbalimbali kutoka TRA na TPA.
Mapema akijibu maswali ya Waziri
Mkuu, Kamishna Mkuu wa TRA, Bw. Bade alikiri kwamba kuna upotevu wa
makontena ambao huwa unafanyika kati ya bandarini na ICDs na hasa ICD ya
Ubungo. Akitoa ufafanuzi, alisema kwamba walifanya ukaguzi kwenye ICD
moja na kukuta makontena 54 yamepotea kwa njia za wizi. “Hata hivyo,
tulipoendelea na ukaguzi, namba iliongezeka na kufikia 327. Tunaendelea
kufuatilia kwa kushirikiana na TAKUKURU. Mmiliki wa ICD ametakiwa kulipa
faini sh. bilioni 12.6/- na ameshalipa sh. bilioni 2.4/-,” alifafanua.
Alipoulizwa na Waziri Mkuu kama
ana majina ya watumishi wanaohusika na wizi huo, Bw. Bade akakiri kwamba
anayo lakini siyo kwa wakati huo labda ayapate kutoka kwa wasaidizi
wake. Ndipo Waziri Mkuu akamuonyesha orodha ya makontena 349 yenye
taarifa zote hadi namba za magari yaliyobeba mizigo hiyo na Bw. Bade
akakiri kwamba orodha hiyo ni ya kweli.
“Kwa utaratibu huo hatuwezi
kufika, labda baadhi ya watu waondolewe kazini”. Ndipo akaanza kutaja
majina ya maafisa hao waliosimamishwa kazi.
…………………………………
KITUO CHA KILIMO N AUFUGAJI KUJENGWA WILAYANI KIBAHA KUUNGA JUHUDI ZA SERIKALI KATIKA SEKTA YA KILIMO
KATIKA kuunga mkono juhudi za
serikali katika kukuza sekta ya kilimo Chama cha wakinamama wataalamu
katika sekta za kilimo mifugo pamoja na mazingira Tanzania (TAWLAE)
wamejiwekea mikakati ya kujenga kituo maalumu cha kilimo na ufugaji
katika kata ya Pangani iliyopo Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani.
Makumbusho ya Taifa yazindua maonyesho ya picha za matukio yanayohusu Albino nchini
Mratibu
wa Maonyesho ya Picha za Alibino kutoka Makumbusho ya Taifa Bibi. Flora
Vicent akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa
hafla ya uzinduzi wa maonyesho hayo jana jijini Dar es Salaam. Maonyesho
hayo yanafanyika kuanzia tarehe 26 Novemba 2015 hadi tarehe 26 Januari
2016
Mkurugenzi
Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Profesa Audax Mabulla (kushoto), Afisa
Mtendaji Mkuu wa Under The Same Sun Bw. Peter Ash, Mwakilishi wa Benki
ya Dunia Dkt. Yutaka Yoshino wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa
maonyesho ya Picha za matukio ya watu wa jamii ya Albino zilizo pigwa
katika kambi ya kuwahudumia Albino ya Kabanga.
Mkurugenzi
Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Profesa Audax Mabulla (kushoto), Afisa
Mtendaji Mkuu wa Under The Same Sun Bw. Peter Ash, Mwakilishi wa Benki
ya Dunia Dkt. Yutaka Yoshino wakipongezana mara baada ya kukata utepe
kuashiria uzinduzi rasmi wa maonyesho ya Picha za matukio ya watu wa
jamii ya Albino zilizo pigwa katika kambi ya kuwahudumia Albino ya
Kabanga.
Mkurugenzi
Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Profesa Audax Mabulla (kushoto), Afisa
Mtendaji Mkuu wa Under The Same Sun Bw. Peter Ash, Mwakilishi wa Benki
ya Dunia Dkt. Yutaka Yoshino wakifurahia mara baada ya kukata utepe
kuashiria uzinduzi rasmi wa maonyesho ya Picha za matukio ya watu wa
jamii ya Albino zilizopigwa katika kambi ya kuwahudumia Albino ya
Kabanga
Katibu
Mtendaji wa Bodi ya Filamu akifuatilia maelekezo ya Picha wakati hafla
ya uzinduzi wa mmaonyesho ya picha maonyesho ya Picha za matukio ya watu
wa jamii ya Albino zilizopigwa katika kambi ya kuwahudumia Albino ya
Kabanga.
Wakiwa katika picha ya pamoja.
Tigo yazindua mtandao wenye kasi zaidi wa 4G LTE jijini Tanga.
Mkurugenzi
wa Tigo kanda ya Mashariki, Goodluck Charles (wa pili kulia)
akimkabidhi zawadi ya simu, James Marwa ambaye aliibuka mshindi wa
kwanza wa bahati nasibu iliyochezeshwa jana sambamba na uzinduzi wa
intaneti yenye kasi zaidi ya 4G LTE jijini Tanga.
Wadau
mbalimbali wakimsikiliza mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa
uzinduzi wa mfumo wa intaneti wenye kasi zaidi wa 4G LTE, uliozinduliwa
na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, jijini Tanga jana.
Mkuu wa
kitengo cha biashara (B2B) katika kampuni ya simu za mkononi ya Tigo
Rene Bascope, akihutubia hadhira iliyohudhuria uzinduzi wa mfumo wa
intaneti wenye kasi zaidi (4G LTE) uliozinduliwa jana jijini Tanga.
Wadau
mbalimabli wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, wakihudumiwa na watoa
huduma wa kampuni hiyo sambamba na uzinduzi wa huduma ya intaneti yenye
kasi zaidi (4G LTE) uliofanyika jijini Tanga jana.
Kamanda
wa kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Tanga, Nassor Sisiwaya (wa
pili kushoto) akibadilishana mawazo na Meneja Mawasiliano ya Umma wa
kampuni ya simu za mkononi ya Tigo John Wanyancha (wa kwanza kulia)
wakati wa uzinduzi huo.
Mkuu wa wilaya ya Tanga, Abdullah Lutavi akihutubia wakati wa uzinduzi huo.
No comments :
Post a Comment