TBS KUFANYA MSAKO MKALI NCHI NZIMA KUWABAINI WAUZAJI WA UMEME NURU 'SOLAR POWER PANELS' ZILIZO CHINI YA KIWANGO
Katibu
Mtendaji wa Taasisi ya Nishati Jadidifu (TAREA), Mhandisi Mathew
Matimbwi (katikati), akiwaonesha wanahabari Dar es Salaam leo asubuhi
Umeme Nuru (Solar Power panels) ambazo hazina ubora zilizokamatwa zikiwa
katika soko la Tanzania baada ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa
kushirikiana na Taasisi hiyo, kufanya uchunguzi na kubaini kuwepo katika
soko solar hizo. Kulia ni Ofisa Viwango wa TBS, Henry Massawe na Ofisa
Uhusiano, Roida Andusamile.
Katibu
Mtendaji wa Taasisi ya Nishati Jadidifu (TAREA), Mhandisi Mathew,
akiwaonesha wanahabari Solar Power panels zinazotakiwa kuwa kwenye soko
ambazo ni bora.
Ofisa Uhusiano wa TBS, Roida Andusamile (kushoto), akizungumza katika
mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya Shirika la Viwango
Tanzania (TBS), Ubungo Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu shirika hilo
kuanza msako mkali wa kuwabaini wafanyabiashara wanaouza Umeme Nuru
(Solar Power Panels), zilizochini ya kiwango. Kulia ni Ofisa Viwango wa
TBS, Henry Massawe na Ofisa Udhibiti Ubora wa TBS, Ashura Katunzi.
MAKAMU WA RAIS DKT. AFUNGUA KONGAMANO LA AFRIKA KUHUSU MAKUBALIANO YA RASIMU MPYA YA DUNIA, JIJINI DAR ES SALAAM.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akihutubia wakati akifungua rasmi Kongamano la Afrika kuhusu
Makubaliano ya Rasimu mpya ya Dunia inayohusu Usimamizi wa Masuala ya
Tabianchi. Kongamano hilo lilianza jana Sept 3, 2015 kwenye Ukumbi wa
Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar esSalaam. Picha na
OMR
Picha na – OMPR – ZNZ.
Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya usafiri na matengenezo ya Ndege la avic kutoka Jamuhuri ya Watu wa China limejitolea kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuanzisha mradi wa Kiuchumi wa pamoja wa Shirika la Ndege la Zanzibar.
Naibu Mkurugenzi wa Shirika hilo lenye Makao Makuu yake Mjini Beijing China Bwana Duan Bao Rong alieleza hayo wakati alipokuwa akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwa Balozi Seif Vuga Mjini Zanzibar.
Bwana Duan Bao Rong alisema Uongozi wa Shirika hilo hivi sasa uko katika hatua za awali za kuwasiliana na Viongozi Waandamizi wa Taasisi zinazohusika na Sekta ya Mawasiliano na Uwekezaji kwa nia ya kuandaa taratibu zinatakazofanikisha kuanzishwa kwa Shirika hilo katika mfumo wa Ubia na Serikali.
Alisema Wataalamu wa Shirika hilo kwa kushirikiana na wale wa Zanzibar wataendelea kufanya utafiti wa pamoja katika kuona namna gani mradi huo mkubwa unatekelezwa ili kusaidia kuongeza mapato ya Taifa ambapo pia alieleza kuwa Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China itakuwa tayari kuunga mkono uanzishwaji wa mradi huo.
SECRETARY GENERAL ON A WORKING VISIT TO ROOFINGS GROUP UGANDA
The Secretary General of the East African Community, Amb. Dr Richard Sezibera, on Thursday paid a working visit to Roofings Group Uganda at its 2nd plant located in Namanve, Uganda's
upcoming Industrial Area on the outskirts of the capital, Kampala.
Welcoming the Secretary General to the Plant, the Chairman and Managing Director of the Roofings Group, Mr. Sikander Lalani, said it was gratifying that Amb. Sezibera's visit to the plant came immediately after the 1st East African Manufacturing Business Summit held from 1st to 2nd September, 2015 in the Ugandan capital.
TIMU YA TAIFA YA WANAWAKE YAONDOKA KUELEKEA CONGO BRAZAVILLE KATIKA MASHINDANO YA ALL AFRICAN GAMES
Mkurugenzi
Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Leonard Thadeo (kushoto)
akimkabidhi mmoja wa wanariadha Bendera ya Taifa tayari kwa safari
yakuelekea nchini Congo Brazaville kwenye mashindano ya Afrika (All
African Games), Timu hiyo iliondoka jana jioni na ndege ya Shirika la
Ndege la Tanzania. (Pichana Benjamin Sawe- WHVUM)
Afisa Michezo Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Gordon Nsajigwa akimpatia mmoja wa wachezaji wa Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wanawake tiketi jana jioni tayari kwa safari yakuelekea Congo Brazaville kwenye mashindano ya Afrika (All African Games), kushoto aliyevaa sutini Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Leonard Thadeo.
Wachezaji wa Timu ya Taifa wakipanda ndege ya Shirikia la Ndege la Tanzania (Air Tanzania) jana jioni tayari kwa kuanza safari ya kuelekea nchini Congo Brazaville kwaajili ya Mashindano ya Afrika (All African Games).
A BAADA YA KUMTUMIA MENEJA UHUSIANO PICHA ZA UTUPU
Afisa Michezo Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Gordon Nsajigwa akimpatia mmoja wa wachezaji wa Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wanawake tiketi jana jioni tayari kwa safari yakuelekea Congo Brazaville kwenye mashindano ya Afrika (All African Games), kushoto aliyevaa sutini Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Leonard Thadeo.
Wachezaji wa Timu ya Taifa wakipanda ndege ya Shirikia la Ndege la Tanzania (Air Tanzania) jana jioni tayari kwa kuanza safari ya kuelekea nchini Congo Brazaville kwaajili ya Mashindano ya Afrika (All African Games).
Mwanaume mmoja huko
Chicago Marekani amepoteza nafasi ya kupata ajira baada ya kumtumia
kimakosa picha za utupu meneja uhusiano wa kampuni aliyoomba ajira.
Polisi wamesema
mwanaume huyo ambaye jina lake limehifadhiwa alituma picha za utupu
kati ya Agosti 11 na 13 kwa meneja uhusiano huyo mwanamke na baadae
kumpigia simu.
Meneja huyo mwanamke wa
kampuni mojawapo ya St Charles alipokea picha hizo zilizotumwa kama
ujumbe wa simu mara mbili akiwa nyumbani na kuwasiliana na polisi.
Msemaji wa polisi
amesema mwanaume huyo alikiri kutuma jumbe hizo lakini amesema picha
hizo alikuwa amelenga kumtumia mtu mwingine.
Mgombea
wa Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. John Pombe
Magufuli akiingia kwenye Ukumbi wa Karemjee kuzungumza na Wajumbe wa
Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi CCM.
Mgombea
wa Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. John Pombe
Magufuli akizungumza na wajumbe hao. Dkt. Magufuli amewaomba wajumbe hao
kufanya kazi kwa uadilifu na kuihubiri Amani ya nchi yetu ili maendeleo
bora yaweze kupatikana.MUIGIZAJI FILAMU EMMA THOMPSON ADAI KUWA UK WABAGUZI
Muigizaji filamu Emma
Thompson amedai kuwa Uingereza haichukui kiasi kikubwa cha wakimbizi
kutoka mataifa ya Ulaya kutokana na umma wake kuwa ni wabaguzi.
Mshindi huyo wa tuzo ya
Oscar, amesema namna Uingereza inavyoshughulikia mgogoro wa wahamiaji
ni aibu, na kusema kuna nafasi ya kutosha kuhifadhi maelfu ya
wakimbizi.
Hatua hiyo ya muigizaji
huyo nyota imekuja huku kukiwa na shinikizo kwa serikali ya Uingereza
kutoa hifadhi kwa familia zaidi za wakimbizi wa Syria wanaokimbilia
mataifa ya Ulaya.








No comments :
Post a Comment