Mratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri
Mkuu, Edgar Senga akieleza uratibu wa shughuli za maafa kwa wananchi
waliotembelea Banda hilo katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea
katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi, Tarehe 7 Agosti , 2015.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya
Wavulana ya Ndada wakipata maelezo juu ya sera baina ya Ubia kati ya
Sekta ya Umma na Sekta Binafsi kutoka kwa Mchumi wa Ofisi ya Waziri
Mkuu, Idara ya Maendeleo ya Sekta Binafsi, Uwekezaji na Uwezeshaji ,
Vedastus Manumbu walipotembelea Banda hilo katika Maonesho ya Nane Nane
yanayoendelea katika viwanja vya Ngongo mkoani Lindi, Tarehe 7 Agosti ,
2015
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, SEIF SHARIF HAMAD, ashiriki Uvunaji wa Matikiti
![]() |
|
| Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizindua uvunaji wa matikiti maji kwa wakulima wa shehia ya Donge Muwanda. |
![]() |
||||
| Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizindua uvunaji wa matikiti maji kwa wakulima wa shehia ya Donge Muwanda. |
![]() |
|
| Mkulima wa matikiti maji na pilipili boga Bw. Salum Khamis Kiregu akitoa maelezo mbele ya Makamu wa Kwanza wa Rais kuhusiana na changamoto zinazowakabili katika kilimo hicho. |
Na:Hassan Hamad (OMKR)
…………………………
Makamu wa Kwanza wa
Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amesifu juhudi zinazochukuliwa
na wananchi wa Donge katika kuendeleza kilimo cha matunda na mboga mboga.
Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amesifu juhudi zinazochukuliwa
na wananchi wa Donge katika kuendeleza kilimo cha matunda na mboga mboga.
Amesema iwapo kilimo
hicho kitawekeza mikakati imara, kinaweza kuwa mkombozi wa kweli kwa wakulima
na kuweza kuweza kuongeza kipato chao.
hicho kitawekeza mikakati imara, kinaweza kuwa mkombozi wa kweli kwa wakulima
na kuweza kuweza kuongeza kipato chao.
Maalim Seif ameeleza
hayo wakati akizindua uvunaji wa matikiti maji na pilipili boga katika shehia
za Donge mchangani na Muwanda katika Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja.
hayo wakati akizindua uvunaji wa matikiti maji na pilipili boga katika shehia
za Donge mchangani na Muwanda katika Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja.
Amesema katika siku
za hivi karibuni, kilimo hicho kimepata mafanikio makubwa na kupunguza
uagiziaji wa bidhaa hizo nje ya Zanzibar kutoka asilimia 80 hadi asilimia 20.
za hivi karibuni, kilimo hicho kimepata mafanikio makubwa na kupunguza
uagiziaji wa bidhaa hizo nje ya Zanzibar kutoka asilimia 80 hadi asilimia 20.
Amefahamisha kuwa
lengo la Serikali ni kuimarisha zaidi kilimo cha matunda na mboga mboga ili
kuweza kukidhi soko la ndani na kuacha kuagizia bidhaa hizo kutoka nje ya
Zanzibar.
lengo la Serikali ni kuimarisha zaidi kilimo cha matunda na mboga mboga ili
kuweza kukidhi soko la ndani na kuacha kuagizia bidhaa hizo kutoka nje ya
Zanzibar.
Amesema
kinachohitajika hivi sasa ni kwa Serikali kuongeza mashirikiano na wakulima,
ili kusaidia kuwatatulia kero zinazowakabili ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa
maji pamoja na pembejeo.
kinachohitajika hivi sasa ni kwa Serikali kuongeza mashirikiano na wakulima,
ili kusaidia kuwatatulia kero zinazowakabili ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa
maji pamoja na pembejeo.
Makamu huyo wa Kwanza
wa Rais wa Zanzibar ameiagiza Wizara ya Kilimo kupeleka mabwana na mabibi
shamba wa kutosha katika shehia hizo za Mchangani na Muwanda, ili kusaidia
utaalamu kwa wakulima hao na kuweza kuzalisha zaidi.
wa Rais wa Zanzibar ameiagiza Wizara ya Kilimo kupeleka mabwana na mabibi
shamba wa kutosha katika shehia hizo za Mchangani na Muwanda, ili kusaidia
utaalamu kwa wakulima hao na kuweza kuzalisha zaidi.
Nae Katibu Mkuu
Wizara ya Kilimo na Maliasili Zanzibar Bw. Affan Othman Maalim, amesema tayari
Serikali imeanza kufanya utafiti kujua maeneo ya kuchimba visima ili kuwasaidia
wakulima hao kuondokana na tatizo la upungufu wa maji.
Wizara ya Kilimo na Maliasili Zanzibar Bw. Affan Othman Maalim, amesema tayari
Serikali imeanza kufanya utafiti kujua maeneo ya kuchimba visima ili kuwasaidia
wakulima hao kuondokana na tatizo la upungufu wa maji.
Hata hivyo
amewashauri wakulima hao kujikusanya pamoja ili kurahisisha miundombinu ya maji
kuweza kuwafikia walengwa.
amewashauri wakulima hao kujikusanya pamoja ili kurahisisha miundombinu ya maji
kuweza kuwafikia walengwa.
Kuhusu tatizo la
pembejeo, Bw. Affan amesema Wizara ya Kilimo inaandaa utaratibu wa kulipeleka
suala hilo katika ngazi za juu, ili kuwawezesha wakulima wa matunda na mboga
mboga kuweza kupatiwa ruzuku za pembejeo za kilimo kama wanavyopatiwa wakulima
wa mpunga.
pembejeo, Bw. Affan amesema Wizara ya Kilimo inaandaa utaratibu wa kulipeleka
suala hilo katika ngazi za juu, ili kuwawezesha wakulima wa matunda na mboga
mboga kuweza kupatiwa ruzuku za pembejeo za kilimo kama wanavyopatiwa wakulima
wa mpunga.
Mapema mmoja kati ya
wakulima hao Bw. Salum Khamis Kiregu, amemueleza Makamu wa Kwanza wa Rais kuwa
licha ya mafanikio wanayoyapata, bado wanakabiliwa na tatizo la soko la kuuzia
bidhaa hizo, na kuiomba serikali kuandaa mazingira bora ya soko kwa wakulima
hao.
wakulima hao Bw. Salum Khamis Kiregu, amemueleza Makamu wa Kwanza wa Rais kuwa
licha ya mafanikio wanayoyapata, bado wanakabiliwa na tatizo la soko la kuuzia
bidhaa hizo, na kuiomba serikali kuandaa mazingira bora ya soko kwa wakulima
hao.
Amesema hivi sasa wanalazimika kuuza bidhaa zao kwa bei ya chini kupitia kwa wafanyabiashara,
jambo ambalo limekuwa likipunguza kipato chao licha ya kuzalisha bidhaa hizo
kwa wingi.
jambo ambalo limekuwa likipunguza kipato chao licha ya kuzalisha bidhaa hizo
kwa wingi.
Bw. Kiregu ameeleza matatizo mengine yanayowakabili kuwa ni pamoja wadudu
waharibifu na maradhi ya mimea, na kuwaomba wataalamu wa kilimo kuwa karibu na
wakulima ili kusaidia kukabiliana na changamoto hizo.
waharibifu na maradhi ya mimea, na kuwaomba wataalamu wa kilimo kuwa karibu na
wakulima ili kusaidia kukabiliana na changamoto hizo.
TGDC yaendelea na Kampeni ya kuelimisha Umma kuhusu Jotoardhi mkoani Mbeya.
Meneja
Mkuu Shirika la Uendelezaji Nishati ya Jotoardhi Tanzania (TGDC),
Mhandisi Boniface Njombe (aliyesimama) akielimisha Umma wa Kata ya Swaya
wakati walipotembelea eneo la kata hiyo ikiwa ni sehemu ya Kampeni ya
uelimishaji kuhusu manufaa ya Jotoardhi hivi karibuni mkoani Mbeya. Kushoto ni Mkurugenzi wa masuala ya Ufundi wa TGDC, Bwana Karamaeli Mnjokava.
Mkurugenzi
wa masuala ya Ufundi wa TGDC, Bwana Karamaeli Mnjokava.(aliyesimama
mbele) akichangia mada kuhusu jotoardhi na manufaa yake kwa wakazi wa
Kata ya Swaya hivi karibuni mkoani Mbeya.
Baadhi
ya Wakazi wa Kata ya Swaya pamoja na baadhi ya Watendaji wa Kampuni ya
Uendelezaji Nishati ya Jotoardhi (TGDC) wakifuatilia uwasilishwaji wa
mada toka kwa Meneja Mkuu wa TGDC hivi karibuni mkoani Mbeya.
………………………………………………………………………………….
Habari Picha na Benedict Liwenga, Maelezo-Mbeya.
Mkoa wa Mbeya unasemekana kuwa
ni moja ya maeneo yaliyobarikiwa kuwa miongoni mwa maeneo ambayo Shirika
la Uendelezaji wa Jotoardhi Tanzania (TGDC) linatarajia kuanza shughuli
ya uchimbaji jotoardhi kutokana na tafiti za awali kuhusu nishati hiyo
kuanza katika mkoa huo.
Kauli hiyo imetolewa na Meneja
Mkuu wa TGDC, Mhandisi Boniface Njombe wakati wa Kampeni ya Uelimishaji
kuhusu Jotoardhi kwa viongozi katika ngazi za Kata za Ilomba katika
Vijiji vya Ituha, Tonya pamoja na Kata nyingine ya Nanyala iliyoko Mbozi
Mkoani Mbeya.
Mhandisi Njombe amesema kuwa,
TGDC ina malengo ya kuzalisha zaidi ya megawati 200 kwa mkoa huo licha
ya mkoa huo kwa sasa kutumia megawati 40 jambo ambalo linaweza kupelekea
nishati hiyo itakayozalishwa kupeleka katika mikoa mingine ya jirani
kwani kiasi hiko cha umeme kitakuwa ni kikubwa.
Aidha, amewataka wakazi wa Mbeya
kuonyesha ushirikiano kati ya Serikali yao pamojana TGDC ili zoezi hilo
lenye manufaa kwao liweze kufikiwa kwa maendeleo ya mkoa na vijijini
ambako kuna changamoto ya ukosefu wa nishati ya umeme pia kutatua tatizo
la mgao wa umeme katika mkoa huo.
“Tuunge mkono jitihada hizi za
Serikali ili walau nishati hii izidi kuendelezwa na ituokoe dhidi ya
hali ya umeme isiyokuwa na uhakika kwani tukishakuwa na uelewa na
kuelimisha wananchi na kutoa ushirikiano, tutakaa mkao wa kula kutokana
na nishati hii”, alisema Njombe.
Kwa upande wake Mjiolojia
Mwandamizi kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Bwana Jacob Mayalla
ameeleza kuwa kutokana na juhudi za Serikali, tafiti za jotoardhi nchini
zilizanza miaka ya 1976 hadi mwaka 1978 zikiwa kama tafiti za awali
ambazo ziliweza kubainisha maeneo katika nchi ya Tanzania kwenye maeneo
yaliyopitiwa na Bonde la Ufa ambapo viashiria vya jotoardhi vipo.
“Kwa Mkoa wa Mbeya, tafiti za
jotoardhi zilifanywa na Serikali kwa kushirikiana na Wakala wa Jiolojia
Tanzania”, alisema Mayalla.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa masuala
ya Kiufundi toka Kampuni ya TGDC, Bwana Taramaeli Mnjokava ameyataja
baadhi ya matumizi ya moja kwa moja ya jotoardhi nchini ikiwemo matumizi
ya kiutalii ambapo maji ya jotoardhi huwekwa kwenye mabwawa hivyo
huvutia watalii wa ndani na nje ya nchi kwa kuyaoga na kuyaangalia jambo
ambalo linaongeza pato la taifa.
Aliongeza kuwa, maji ya
jotoardhi hufaa kwa matumizi ya uzalishaji wa samaki kwani samaki
hupenda maji yenye hali ya uvuguvugu kuliko yenye baridi hasa kwa maeneo
yenye baridi kama mkoa wa Mbeya, hivyo pindi mabwawa ya samaki
yanapotengenezwa na kuwekewa maji ya jotoardhi yanasaidia kuzalisha
samaki kwa wingi jambo ambalo nalo litakuza pato kwa taifa na kwa eneo
husika ambalo uzalishaji unafanyika.
“Maji ya jotoardhi yanaweza
kutumika katika uzalishaji wa mboga mboga au maua kwa njia ya Vitalu
Nyumba kwa Kiingereza huitwa Green Houses lakini ni vitalu hutengenzwa
kwa plastiki au kioo, hivyo watu hutumia vitalu hivi jambo ambalo
linavutia sana soko la nje kwani huwa hawapendi mboga zilizopigwa dawa
wala maua yaliyopigwa dawa, niwahamasishe kujiandaa kwa kuupokea mradi
huu kwani utawanufaisha vyakutosha nyie wakazi wa Mbeya na taifa kwa
ujumla,” alisema Mnjokava.
Mnamo tarehe 19 Disemba, 2013
Serikali ya Tanzania kupitia Shirika la Ugavi wa Umeme (TANESCO)
ilisajiri kampuni ya kuendeleza nishati itokanayo na Jotoardhi, jina la
kampuni likiitwa “Tanzania Geothermal Development Company Limited
(TGDC).
Kampuni hii ilianzishwa kama
kampuni tanzu ya Shirika la TANESCO ambalo linamilikiwa na Serikali kwa
asilimia 100 na mnamo mwezi Julai 2014 TGDC ilianza kazi zake rasmi
ikipewa jukumu la kuharakisha uendelezaji wa nishati ya jotoardhi
nchini.
MTANGAZAJI WA RADIO FREE AFRICA APITA KURA ZA MAONI UDIWANI SASA KUSUBIRI KURA ZA UBUNGE.
……………………………………………………………..
SHINYANGA
Mwandishi wa habari na mtangaaji
wa Radio Free Africa William Bundala (KIJUKUU CHA BIBI K) ameshinda
kura za maoni katika nafasi ya Udiwani katika kata ya Ulowa jimbo la
Ushetu.
Akitangaza matokeo hayo
Msimamizi wa uchaguzi huo Sangoma amesema kuwa Bundala ameshinda nafasi
hiyo kwa kupata kura 46 dhidi ya Wagombea wenzake Charles Bahati
aliyepata kura 14 na Marco Matheo ambaye hakupata kura yoyote katika
kinyang’anyiro hicho.
Kuelekea uchaguzi mkuu Bundala
alitangaza nia ya Kugombea Ubunge katika jimbo la Ushetu na udiwani
katika kata ya Ulowa huku akisimamia kauli mbiu yake kuwa “Tunahitaji
mawazo na nguvu mpya za vijana kuleta mabadiriko ya maendeleo”.
Akiongea kwa njia ya simu akiwa
jimboni Bundala amesema kuwa huu ni mwanzo na kuongeza kuwa kwa sasa
anasubiri kura za maoni za ubunge ili kuchaguliwa kupeperusha bendera ya
Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema katika uchaguzi mkuu wa mwaka
2015.
Sambamba na hayo Bundala amesema
kuwa Tanzania ilipofikia kwa sasa inahitaji viongozi wazalendo wenye
uchungu na rasilimali za wananchi na siyo kiongozi mwenye uchu wa
madaraka anayetaka uongozi kwa rushwa.
Kwa upande wao wagombea
waliokuwa katika kinyang’anyiro hicho cha udiwani wamesema kuwa
wameridhika na matokeo na kwamba lengo la CHADEMA ni moja kuleta
mabadiriko katika jimbo la Ushetu na kata ya ulowa kwa Ujumla.
Kwa sasa Bundala anasubiri kura
za maoni za Ubunge zinazotarajiwa kufanyika wiki ijayo huku akiwa katika
kinyang’anyiro hicho na watia nia wengine wawili ambao ni Mabula Nkwabi
na John Kitibu ambaye alipata kura 45 katika kura za maoni za jimbo la
Kahama Mjini katika uchaguzi ambao James Lembeli aliibuka mshindi.
ADC YAFANYA MKUTANO WA HADHARA KUWATAMBULISHA WAGOMBEA WA URAIS KUELEKEA UCHAGUZI MKUU
Mgombea
urais wa Tanzania kupitia Chama cha Alliance for Democratic Change
(ADC), Lutasola Yemba (katikati), akimtambulisha kwa wananchi mgombea
mwenza Said Miraj (kulia) na mgombea urais wa chama hicho, Zanzibar,
Hamad Rashid Hamad kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Buguruni Sheli
Dar es Salaam jana.
Mgombea
urais wa Tanzania kupitia Chama cha Alliance for Democratic Change
(ADC), Lutasola Yemba (katikati), akimtambulisha kwa wananchi mgombea
mwenza Said Miraj (kushoto), baada ya kuchukua fomu Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) Dar es Salaam leo. Kulia ni mke wake, Mwanaisha Lutasola.
Mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama hicho, Hamad Rashid Hamad akizungumza na wananchi katika mkutano huo.
Mgombea
urais wa Tanzania kupitia Chama cha Alliance for Democratic Change
(ADC), Lutasola Yemba, akihutubia katika mkutano huo Buguruni Sheli
jana.
Wanachama wa chama hicho na wananchi wakisikiliza sera za viongozi hao watakao peperusha bendera ya ADC kwenye uchaguzi mkuu.
Rais Kikwete azindua benki ya kwanza ya Wakulima Tanzania-Agosti 7, 2015
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akihutubia wadau wa kilimo na taasisi za fedha wakati akizindua rasmi
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) leo Agosti 7, 2015 katika
Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere jijini Dar es
salaam.
Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo
ya Kilimo, Thomas Samkyi akizungumza wakati wa uzinduzi wa benki ya
wakulima Tanzania (TADB), uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa
Mwalimu JK Nyerere.
Mwenyekiti wa Bodi ya benki ya Maendeleo ya Kilimo, Bi Rosebud Kurwijila, akizungumza wakati wa uzinduzi wa benki.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akifuatilia uzinduzi wa benki
ya Maendeleo ya Kilimo, kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya benki hiyo
Bi Rosebud Kurwijila, akifuatiwa na Mkurugenzi Mkuu wa benki, bwana
Thomas Samkyi, na kutoka kushoto ni Waziri wa Kilimo, Stephen Wasira
akifuatiwa na Waziri wa Fedha, Bi Saada Mkuya.
Wageni waalikwa wakifuatilia uzinduzi wa benki ya Maendeleo ya Kilimo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akizindua rasmi Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) leo Agosti
7, 2015 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere
jijini Dar es salaam.
………………………………………………………………………………………
Na Mwandishi wetu-Dar es Salaam
Rais Jakaya Kikwete leo amezindua
benki ya kwanza ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania, ambayo inalenga
kuanzisha mtizamo mpya wa kukiendeleza kilimo kupitia kushirikisha wadau
mbali mbali, kuangalia kila mnyororo wa thamani kwa ukamilifu wake,
pamoja na kuwa na ubunifu katika kuchangia kifedha kwenye miradi ya muda
mrefu, ya kati na muda mfupi kwenye sekta ya kilimo. Benki hiyo
inatarajiwa kutoa mchango mkubwa katika ukuzaji wa sekta ya kilimo
ambayo imeajiri zaidi ya aslimia 70 ya Watanzania.
Akizungumza katika uzinduzi huo
uliofanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere, Rais Kikwete amesema changamoto zinazowakabili
wakulima nchini ndizo zilizosababisha serikali yake kuanzisha benki hii
ili kuwakomboa wakulima kwenye umaskini ili waweze kuzalisha kibiashara
na sio kwa kwa kujikimu.
‘Awali huduma za kifedha na mikopo
kwa wakulima hazikuwepo kabisa na hivyo kupelekea tija kwenye kilimo
kuwa chini, uzalishaji wa mazao ya kilimo na mifugo nao ukawa chini ya
viwango vya Afrika na hata dunia, hivyo ya uzinduzi wa benki hii
unafungua ukurasa mpya wa mapinduzi ya kilimo nchini’ alisema Rais
Kikwete.
Rais Kikwete pia aliwaasa wakulima
kutumia vyema fursa ya uanzishwaji wa benki hii akisema kwa sasa kilimo
kinachangia asilimia 25 ya pato la taifa, huku asilimia 35 ya bidhaa
tunazouza nje ni za kilimo.
‘Serikali imetoa mtaji wa
kuanzisha benki wa jumla ya shilingi bilioni 60, na tunatarajia kuingia
hati fungani ili kuiongezea benki mtaji kwa jumla ya shilingi bilioni
800’ anasisitiza Waziri wa Fedha, Saada Mkuya.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu
wa benki, Bwana Thomas Samkyi, alisema dhumuni kuu la uanzishaji wa
benki hiyo ni kuboresha tija katika uzalishaji kwenye sekta ya kilimo
kwa kuunganisha nguvu za wadau mbalimbali ili kuwezesha uendelezaji wa
miundombinu ya kilimo kama miradi ya umwagiliaji, usafirishaji,
uhifadhi, mindombinu ya masoko, n.k. ambayo inachangia maendeleo ya
sekta ya kilimo.
‘Uanzishwaji wa benki hii unalenga
kuziba mianya mikubwa ya ukopeshaji kwenye kilimo ambayo inaachwa na
benki za biashara, ili kuchochea kukua kwa sekta ya kilimo, kwa kutoa
mikopo na huduma nyingizezo za uwezeshaji wa kilimo kwa wakulima, ambao
wengi wao hawana uwezo wa kupata huduma za kibenki’ alisema Bw. Samkyi.
Akieleza zaidi kuhusu uanzishwaji
wa benki hiyo, Bwana Samkyi alisema Benki ya Wakulima itakuwa msitari wa
mbele katika kusukuma shughuli za kilimo pamoja na kuchagiza benki na
taasisi nyingine za kifedha kushiriki katika kuwezesha shughuli za
kilimo.
‘Benki hii imeundwa ili kutoa
mikopo kwa masharti nafuu, pamoja na kutoa huduma nyinginezo
zitakazoongeza uwezo wa wakulima kukopa na kuzalisha. Ili kufanikisha
haya, benki inabidi iwe na vyanzo endelevu vya fedha za kutosha kwani
nchi hii ni kubwa na wadau wa benki ni wengi sana. Lengo kuu ni kubadili
kilimo cha Tanzania kutoka kilimo cha kujikimu kwenda kilimo cha
kibiashara’ alisema Bw. Samkyi.
Benki hii pia inatarajiwa kuwa ni
kiungo muhimu cha utekelezaji wa mageuzi ya awamu ya pili ya sekta ya
kifedha, na vile vile kuboresha maendeleo ya kilimo nchini ikizingatia
Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025 pamoja na mipango mbalimbali ya
maendeleo ya miaka mitano mitano, Mkakati wa Maendeleo wa Sekta ya
Kilimo, na Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini (MKUKUTA),
pamoja na sera mbali mbali za Serikali zinazohusu sekta ya kilimo.
KAMATI MAALUM YA HALMASHAURI KUU YA CCM NEC ZANZIBAR
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti
wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) mara walipoingia katika
ukumbi wa mikutano wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja leo
katika kikao cha kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM NEC ya
Zanzibar,(kulia) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai na
Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi(kushoto)
Picha zote na Ikulu.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai alipokuwa akitoa taarifa ya kikao kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM NEC ya Zanzibar kwa
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo
Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein katika ukumbi wa
mikutano wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja leo kbla ya
kukifungua kikao hicho,
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti
wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akikifungua kikao cha kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM NEC ya Zanzibar leo katika
ukumbi wa mikutano wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja,(kulia)
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai na Makamo wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi(kushoto)
Baadhi ya wajumbe wa kikao
cha kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM NEC ya Zanzibar
wakifuatuilia kwa makini ratiba ya kikao hicho kilichofanyika leo katika
ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja,
Baadhi ya wajumbe wa kikao
cha kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM NEC ya Zanzibar
wakifuatuilia kwa makini ratiba ya kikao hicho kilichofanyika leo katika
ukumbi wa Ofisi ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja,
Naibu waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene atembeleakiwanda cha kutengeneza vigae mkoani mbeya
Naibu waziri wa Viwanda na
Biashara Janet Mbene akizungumza, mmoja wa viongozi wa kampuni ya Marmo
and Garnito Mines wakati alipokuwa kwenye ziara ya viwanda mkoani mbeya
hivi karibuni.
Naibu Waziri wa Viwanda na
Biashara,Janet Mbene,akiangalia baadhi ya bidhaa zilizotengenezwa na
kampuni ya Marmo and Garnito Mines kwa ajili ya matumizi mbalimbali
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara , Janet Mbene, akitembelea sehemu ya kiwanda cha Marmo anda Granito Mines
TOTO AFRICAN KUCHAGUANA OKTOBA 2015
Klabu ya Toto African ya Mwanza
inatarajiwa kufanya uchaguzi wa kujaza nafasi zilizo wazi katika kamati
yake ya utendaji ifikapo tarehe 11 Oktoba 2015. Katika barua yake kwa
Katibu Mkuu wa Toto African, Katibu Mkuu wa TFF ameuagiza uongozi wa
Toto African kuwasiliana na Kamati yao ya Uchaguzi ili tangazo la
uchaguzi litolewe si chini ya siku sitini (60) kabla ya tarehe ya
kufanyika uchaguzi.
Kwa muda mrefu kumekuwa na
mvutano katika klabu ya Toto na suala kubwa likiwa ni kuhusu ujazaji wa
nafasi zilizo wazi. Awali TFF ilipokea maombi ya wanachama na wadau wa
Toto African wakitaka ufanyike uchaguzi ili kumaliza mvutano ndani ya
klabu.
TFF ilishauri uchaguzi huo kusubiri klabu kukamilisha mchakato wa usajili.
Vilevile TFF imewataka wadau wote
wa klabu hiyo kongwe ya mjini Mwanza kuheshimu uongozi uliopo
madarakani kwani ndio unaotambulika na ndio utaendelea kuiongoza Toto
African katika kipindi cha kuelekea uchaguzi uchaguzi.
TWIGA STARS YAELEKEA ZANZIBAR
Timu ya Twiga Stars ikiondoka kwenda Zanzibar kwa ajili ya kambi ya mazoezi
Wachezaji wa Tiga Stars wakiwa Feri wakisubiri boti ya kwenda Zanzibar kwa ajili ya kupiga kambi ya mazoezi.
……………………………………………………………………
Kikosi cha timu ya Timu ya Taifa
ya Wanawake (Twiga Stars) kimeodoka leo saa 6 mchana jijini Dar es
salaam kuelekea kisiwani Zanzibari, ambapo kitaweka kambi ya mwezi mmoja
kujiandaa na fainali za Michezo ya Afrika (All Africa Games) mwezi
Septemba.
Msafara wa Twiga Stars umeondoka
na boti ya Azam (Kilimanjaro) ukiwa na watu 32, wakiwemo wachezaji 25,
benchi la ufundi 6 pamoja na kiongozi wa msafara, ambapo TFF imegharamia
kambi hiyo ya mwezi mmoja
Wachezaji waliosafiri leo ni
Fatuma Omari, Belina Julius, Happiness Hezron, Fatuma Hassan, Anastazia
Anthony, Fatuma Bashiru, Fatuma Issa, Fatuma Khatibu, Maimuna Hamis,
Donizia Daniel, Sofia Mwasikili, Etoe Mlenzi.
Wenigine ni Amina Ally, Thereza
Yonna, Mwanahamisi Omari, Stumai Abdallah, Shelder Boniface, Asha
Rashid, Najiat Abbas, Estha Chabruma, Mwajuma Abdallah na Fatuma
Mustapah.
Twiga Stars itakua kambini
kisiwani Zanzibar kwa kipindi cha mwezi mmoja, kujiandaa na fainali hizo
za michezo ya afrika, ambapo imepangwa kundi A pamoja na wenyeji Congo –
Brazzavile, Ivory Coast na Nigeria.
Fainali za Michezo ya Afrika (All Africa Games) zinatarajiwa kuanza kutivua vumbi Septemba 4 – 19 nchini Congo-Brazzavile.
MABONDIA RAMA SHAURI NA LULU KAYAGE WAPAA KWENDA AFRIKA KUSINI
| Rais wa TPBO Yassin Abdallah ‘Ustaadhi’ katikati akiwa na mabondia Lulu Kayage kulia na Ramadhani Shauri wakienda kupanda ndege kwenda Afrika ya Kusini mabondia hawo wanapanda uringoni agost 9 Picha naSUPER D BOXING NEWS |
EUROPEAN UNION STATEMENT
Declaration by the High
Representative, Federica Mogherini, on behalf of the European Union on
the occasion of the International Day of the World’s Indigenous Peoples,
9 August 2015.
…………………………………………………………………..
While we celebrate today the
International Day of the World’s Indigenous Peoples, we take stock of
the progress achieved towards ending all forms of discrimination and in
ensuring that indigenous peoples’ rights are respected, protected and
fulfilled. In September of last year, the EU contributed to the success
of the World Conference on Indigenous Peoples and promoted equal
participation of indigenous peoples in preparation of this meeting. We
supported the Outcome Document of the conference which serves as a
blueprint for actions at international and national level, bringing
positive changes to the lives of indigenous peoples. As follow up to the
World Conference, the EU is further developing its policy in line with
the United Nations Declaration on the Rights of Indigenous Peoples and
in close consultation with their representatives. Despite the many
positive examples of progress achieved around the world, indigenous
peoples, particularly women and girls, continue to experience multiple
forms of discrimination, vulnerability and marginalisation in their
lives. We are therefore committed to their empowerment. By reaffirming
its support to the UN declaration on the Rights of Indigenous Peoples,
the EU restates its determination to work closely with indigenous
peoples, along with other partners and stakeholders in its endeavour to
promote the recognition that human rights are equally guaranteed to all
men and women.
RAIS KIKWETE AZINDUA RASMI BENKI YA MAENDELEO YA KILIMO TANZANIA (TADB)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akihutubia wadau wa kilimo na taasisi za fedha wakati akizindua rasmi
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) leo Agosti 7, 2015 katika
Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere jijini Dar es
salaam
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akihutubia wadau wa kilimo na taasisi za fedha wakati akizindua rasmi
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) leo Agosti 7, 2015 katika
Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere jijini Dar es
salaam
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akizindua rasmi Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) leo Agosti
7, 2015 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere
jijini Dar es salaam
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akizindua rasmi Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) leo Agosti
7, 2015 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere
jijini Dar es salaam
Vifijo baada ya Rais Jakaya
Mrisho Kikwete kuzindua rasmi Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania
(TADB) leo Agosti 7, 2015 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa
Mwalimu JK Nyerere jijini Dar es salaam
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika
picha ya pamoja na Waziri wa Kilimo, Mhe Stephen Wasira, Waziri wa
Fedha Mhe Saada Mkuya na viongozi na watendaji wa Benki ya Maendeleo ya
Kilimo Tanzania (TADB) leo Agosti 7, 2015 katika Ukumbi wa Mikutano wa
Kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere jijini Dar es salaam
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
katika picha ya pamoja na Waziri wa Kilimo, Mhe Stephen Wasira, Waziri
wa Fedha Mhe Saada Mkuya, Katibu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue,
Mkurugenzi Mkuu wa TIB Bank Bw. Peter Noni na viongozi na watendaji wa
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) leo Agosti 7, 2015 katika
Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere jijini Dar es
salaam
Msanii akiburudisha kwa ngoma
kutoka Zanzibar baada ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuzindua rasmi
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) leo Agosti 7, 2015 katika
Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere jijini Dar es
salaam
PICHA NA IKULU
TFDA YAWATAKA WAFANYABISHARA KUZINGATIA SHERIA YA CHAKULA NA VIPODOZI NA MWANDISHI WETU, ARUSHA
NA MWANDISHI WETU, ARUSHA
Mamlaka ya chakula na dawa hapa
nchini TFDA imewataka wafanya biashara kuzingatia sheria ya chakula na
vipodozi kwa kutoingiza nchini bidhaa ambazo hazidhibitishwa na mamlaka
hiyo ili kulinda afya za watumiaji
Hayo yamesema na mkurugenzi wa
mmalaka hiyo hapa nchini Hiiti Baran Sillo alipokuwa akizungumza na
vyombo vya habari wakati akitoa elimu kwa wananchi na wafanyabaishara
katika maonesho ya nane nane
Amesema kuwa wafanyabishara na
wananchi wanapaswa kuwa makini wanaponunua vipodozi venye sumu pamoja na
vyakula vilivuyuopita muda wake kwani kwa kufanya hivyo wanavunja
sheria za mamlka hiyo huku wauzaji nao wakiwa wanahatarisha usalama wa
watumiaji.
Ameeeleza kuwa ameona umhimu wa
kushiriki katika maonesho ya nane nane ili watoe elimu kwa wananchi na
wafanyabiashara ambao wanaingiza bidhaa zenye sumu au ambazo zimepita
muda wake kwani zimekuwa zikihatrarisha maisha ya binadamu
Amedai kuwa kupitia maonesho
hayo wananchi wataelewa bidhaa bora na salama pamoja na kubaini zile
ambazo zimepigwa marufuku kwa matumizi ya binadamu kwani wapo
wanaozituimia kwa kutokuwa na elimu ya kutosha.
Aidha Baram amewataka wananchi
kuhakikisha kuwa wananunua bidhaa ambazo zimedhibitishwa na
mamlaka hiyo na kuepuka kununua bidhaa ambazo zimepia muda wa uhai wake
na endapo kama watabaini wafanyabishara wanaouza bidhaa zilizopita basi
watoe taarifa katika mamlaka hiyo ili hatua za kisheria zichukuliwe
dhidi yao.
KAMISHNA CHAGONJA AWAPOKEA WANAMICHEZO WALIOTOKA SWAZILAND NA KUWAHUTUBIA
Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo
wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja akiwa katika picha ya pamoja na
wanariadha wa Jeshi la Polisi walioshiriki Michezo ya Majeshi ya Polisi
kwa nchi za kusini mwa Afrika (SARPCCO).Wengine ni Viongozi wa Michezo
wa Jeshi la Polisi (Picha na Alexander Mpeka-Jeshi la Polisi)
Kamishna wa Oparesheni na
Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja akizungumza na Wanariadha wa
Jeshi la Polisi, Wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza iliyofanyika Makao
Makuu ya Polisi Jana baada ya kufanya vizuri katika Michezo ya Majeshi
ya Polisi kwa nchi za kusini mwa Afrika (SARPCCO).Kushoto ni Mkuu wa
Kitengo cha Michezo, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Jonas Mahanga (Picha
na Alexander Mpeka-Jeshi la Polisi)
Kamishna wa Oparesheni na
Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja akimpongeza Mwanariadha wa
Jeshi la Polisi, PC Basil John aliyeshinda medali tatu za dhahabu katika
Michezo ya Majeshi ya Polisi kwa nchi za kusini mwa Afrika (SARPCCO),
Wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza iliyofanyika Makao Makuu ya Polisi
Jana.(Picha na Alexander Mpeka-Jeshi la Polisi)
……………………………………………………………………………………….
Michezo ya SARPCCO ilianzishwa
kwa lengo la kuwakutanisha Maafisa na Askari Polisi ili kuweza
kubadilishana mbinu za kukabiliana na uhalifu pamoja na kuwasaidia
kujenga afya na kuwa wakakamavu katika kutekeleza majukumu yao ya kila
siku.
Michezo ni sehemu ya
kuitambulisha nchi yoyote kama Taifa huru lenye utamaduni wake. Michezo
ni mojawapo ya viungo muhimu katika utamaduni wa kila jamii ya binadamu
duniani. Michezo ni chombo muhimu sana katika kuiendeleza jamii. Aidha,
michezo huweza kuwa kielelezo na utambulisho wa Taifa kwa kutoa
burudani, kujenga na kukomaza afya ya mwili na akili, kujenga nidhamu,
kujitangaza kiuwezo na vipaji. Ushiriki katika michezo ya kimataifa
husaidia kulitangaza Taifa nje ya mipaka yetu. Vile vile michezo
huwaweka pamoja Askari na kuwawezesha kufahamiana na kuondoa misongo ya
mawazo “STRESS”. Hivyo Ni wazi kuwa mmetumia vyema fursa mliyoipata
katika michezo hiyo ikiwemo ya kubadilishana mawazo na uzoefu katika
kutenda kazi za polisi, Hongereni sana.
Nimepewa taarifa kuwa kulikuwa na
ushindani mkubwa katika michezo hiyo na ninyi pamoja na uchache wenu
mmfenakiwa kupata medali 12, 6 za dhahabu, 4 za fedha na 2 za shaba, Pia
timu yetu ya riadha (wanaume) ya mbio ndefu imefanikiwa kuwa timu bora
katika mashindano hayo na Askari PC Basil John aliibuka mchezaji bora wa
mashindano baada ya kushinda medali 3 za dhahabu katika mbio za mita
800, 1500 na mbio za nyika (Km 12 cross country).Nawapongeza sana
walioshinda
Mmefanya kazi kubwa na
mmehakikisha kuwa heshima ya Jeshi letu la Polisi iliyojijengea katika
michezo hiyo tangu kuanzishwa kwake inaendelea kudumu pamoja na uchache
wenu kutokana na wanamichezo wengine kutofanikiwa kwenda kutokana na
sababu mbalimbali.
Aidha nawapongeza sana kwa
nidhamu mliyoionyesha katika kipindi chote cha michezo hiyo, Nidhamu na
kujituma kwa juhudi ndio msingi wa kufanikiwa katika mchezo wowote hivyo
ninyi mmekuwa mabingwa katika kipengele hicho.
Aidha, napenda pia kutumia fursa
hii kuwashukuru wadhamini waliotuwezesha kwa kutupatia vifaa vya michezo
ambao ni Benki ya CRDB, NMB, African Life Assuarance, na PPF, kwani kwa
ufadhili wao walioutoa umefanyiwa kazi na hivyo kupata mafanikio ya
ushindi, Hivyo wakati mwingine wasisite kuiunga mkono timu yetu ya
Polisi.
napenda kuwaahidi kuwa
tutaendelea kuipa kipaumbele michezo ili kuweza kuwaimarisha kiafya na
kuwakutanisha na wenzenu katika mataifa mengine na nawatakieni
maandalizi mazuri katika michezo mingine iliyopo mbele yenu na safari
njema ya kurudi katika mikoa yenu.
AHSANTENI SANA KWA KUNISIKILIZA.
UTUMISHI YAKABIDHIWA ZAWADI YA USHIRIKI WA TANZANIA KATIKA MAONYESHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA BARANI AFRIKA YALIYOFANYIKA CONGO BRAZAVILLE
Kaimu Katibu Mkuu Utumishi Bw.HAB
Mkwizu (wa pili kutoka kushoto) akipokea zawadi ya Tanzania kutoka kwa
mmoja wa Washiriki wa Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Barani
Afrika Bw. William Budoya yaliyofanyika nchini Congo Brazaville hivi
karibuni. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Ofisi
ya Rais-Utumishi Bw.Aloyce Msigwa (kushoto) na Mkurugenzi wa Mipango
Ofisi ya Rais- Utumishi Bw. Cosmas Ngangaji (wa pili kutoka kulia).
Kaimu Katibu Mkuu Utumishi Bw.HAB
Mkwizu (katikati) akipokea cheti cha ushiriki wa Tanzania kutoka kwa
Mmoja wa Washiriki wa Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Barani
Afrika Bw. William Budoya yaliyofanyika nchini Congo Brazaville hivi
karibuni. Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. Florence Temba (wa kwanza
kushoto), Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Ofisi ya Rais-Utumishi
Bw.Aloyce Msigwa (wa pili kutoka kushoto) na Mkurugenzi wa Mipango
Ofisi ya Rais- Utumishi Bw. Cosmas Ngangaji (wa pili kutoka kulia).
Kaimu Katibu Mkuu Utumishi
Bw.HAB Mkwizu (katikati) akionyesha cheti cha ushiriki wa Tanzania
katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika nchini Congo
Brazaville hivi karibuni. Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Kitengo cha
Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. Florence Temba (wa
kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Ofisi ya
Rais-Utumishi Bw.Aloyce Msigwa (wa pili kutoka kushoto), Mkurugenzi wa
Mipango Ofisi ya Rais- Utumishi Bw. Cosmas Ngangaji (wa pili kutoka
kulia) na mmoja wa washiriki wa maonyesho hayo kutoka Wizara ya Uchukuzi
Bw. William Budoya (wa kwanza kulia).
MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA UZINDUZI WA MFEREJI MPYA WA SUEZ
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Balozi
wa Tanzania, nchini Misri, Balozi Mohammed Hamza, wakati wakitoka kwenye
Boti baada ya kuhudhuria hafla ya uzinduzi wa Mfereji mpya wa Suez
Canal, kwa ajili ya meli za mizigo. Hafla hiyo ilifanyika jana Agosti 6,
2015 jijini Ismailia. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Balozi
wa Tanzania, nchini Misri, Balozi Mohammed Hamza, wakati wakitoka kwenye
Boti baada ya kuhudhuria hafla ya uzinduzi wa Mfereji mpya wa Suez
Canal, kwa ajili ya meli za mizigo. Hafla hiyo ilifanyika jana Agosti 6,
2015 jijini Ismailia. Picha na OMR
ISIMAILIA AGOSTI 06, 2015
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal jana ameiwakilisha
Tanzania katika uzinduzi wa mfereji mpya wa Suez unaounganisha mabara ya
Ulaya, Afrika na Asia. Mfereji huu mpya ambao Misri inauita “zawadi
mpya kwa Dunia” unalenga kukuza uchumi katika usafiri wa maji na
utarahisisha usafirishaji wa mizigo kwa mabara haya matatu, huku Misri
ambayo kijiografia iko jangwani ikitegemea kukuza uchumi wake kutokana
na meli zitakazopita katika mfereji huo.
Mradi wa ujenzi wa Mfereji huu
mpya umejengwa kwa mwaka mmoja licha ya kupangwa kukamilika baada ya
miaka mitatu na umetumia kiasi cha dola za Marekani Bilioni Nane ambazo
zimechangwa kwa njia ya Hisa na wananchi wa Misri kwa kipindi
kisichozidi siku tisa. Mfereji huu ambao umezinduliwa jana, unatoa fursa
kwa Meli kupita bila usumbufu tofauti na zamani ambapo ilipaswa Meli
kusimama ili kupishana lakini sasa kila upande wa Meli utapita bila
kuathiri upande mwingine.
Sherehe hizo za aina yake
zimehudhuriwa na viongozi kadhaa wa nchi mbalimbali na kupata kuripotiwa
na vyombo vyote vikubwa duniani na hivyo kutoa picha ya kuwa Afrika
inapiga hatua katika kukuza uchumi wake pamoja na kuonesha dunia kuwa
fursa mpya za maendeleo zipo Afrika.
Sherehe hizo za aina yake
zilipambwa na maonesho ya ndege za kivita zilizotanda anga la Mfereji
mpya wa Suez huku zingine zikiruka kwa kasi na kutoa moshi ulioakisi
bendera ya Misri, zingine zikipeperusha bendera ya nchi hiyo.
Katika tukio hilo la kuathimisha
tukio hilo la kihistoria serikali ya Misri ilitangaza kuwa siku hiyo
ni ya mapumziko huku ulinzi mkali ukiimarishwa katika miji yote mikuu ya
nchi hiyo huku jiji la Cairo walipofikia viongozi mbalimbali wa
kimataifa likiwa chini ya uangalizi wa kijeshi kwenye maoneo yote
muhimu. Barabara ya kwenda eneo la Islamelia zilikofanyika sherehe hizo
ilifungwa kwa siku nzima, walioruhusiwa kupita ni viongiozi na wageni
mbalimbali waalikwa waliotakiwa kuhudhuria tukio hilo la kihistoria.
Rais wa Misri Abdel Fatah Sisi
alisema kufunguliwa kwa Mfereji ni uthibitisho kwamba Misri inaweza na
kueleza kwamba njia hiyo itaimarisha zaidi shughuli za usafirisha na
kufungua fursa zaidi kwa mataifa duniani.
Katika moja ya matukio ya
uzinduzi huo Rais Fatah na viongozi mbalimbali waliohudhuria sherehe
hizo walisafiri katika meli za kifahari huku kiongozi huyo wa Misri
akivalia mavazi maalumu ya kijeshi akiwa juu ya sehemu ya uwazi wa meli
hiyo pamoja na kijana mdogo mwanafunzi wa miaka tisa aliyevalia kijeshi
na kupeperusha bendera ya Misri kama ishara ya kufunguliwa rasmi kwa
mfereji huo.
Shughuli ilimazika usiku kwa
maonesho mbalimbali ya sanaa na utamaduni wa Misri na kuhudhuriwa na
viongozi na wageni wote waalikwa.
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais
Cairo Misri Agosti 7, 2015
TCRA YAWAHIMIZA WANANCHI KUTUMIA KWA USAHIHI MAWASILIANO
TBL YAFANIKISHA UPIMAJI AFYA ZA MADEREVA WA MASAFA MAREFU WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI
Mganga kutoka kitengo cha afya
makao makuu ya jeshi la polisi Tanzania, Dk Issa Ndimila akimchukua damu
dereva wa magari makubwa, Benedicti Samuel kwa ajili ya kumpima
magonjwa katika uzinduzi wa upimaji wa afya kwa madereva wa mabasi na
malori ya masafa marefu ikiwa sehemu ya maadhimisho ya wiki ya nenda kwa
usalama barabarani katika kituo cha mizani cha Mikese mkoa wa Morogoro
mpango ulioanzishwa na TBL na jeshi la polisi nchini.
Mganga kutoka kitengo cha afya
makao makuu ya jeshi la polisi Tanzania, Dk Issa Ndimila akimchukua damu
dereva wa magari makubwa, Kanai John kwa ajili ya kumpima magonjwa
katika uzinduzi wa upimaji wa afya kwa madereva wa mabasi na malori ya
masafa marefu ikiwa sehemu ya maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama
barabarani katika kituo cha mizani cha Mikese mkoa wa Morogoro mpango
ulioanzishwa na TBL na jeshi la polisi nchini.
Katibu Tawala wilayaa ya
Morogoro, Emmanuel Nzunda akimkabidhi zawadi ya fulana na cheti dereva
wa magari makubwa baada ya kupima afya wakati wa maadhimisho ya wiki ya
nenda kwa usalama barabarani katika kitucha mizani cha Mikese mkoa wa
Morogoro, mpango ulioanzishwa na
TBL na jeshi la polisi nchini.
TBL na jeshi la polisi nchini.
Askari wa kikosi cha usalama
barabarani mkoa wa Morogoro, Silve Massawe akijaza taarifa za dereva
Edward Sanga baada ya kupima afya katika uzinduzi wa upimaji wa afya kwa
madereva wa mabasi na malori ya masafa marefu ikiwa sehemu ya
maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani katika kituo cha
mizani cha Mikese mkoa wa Morogoro mpango ulioanzishwa na TBL na jeshi
la polisi nchini.
Askari wa kikosi cha usalama
barabarani mkoa wa Morogoro, Silve Massawe akijaza taarifa za dereva
Abdallah Rajabu baada ya kupima afya katika uzinduzi wa upimaji wa afya
kwa madereva wa mabasi na malori ya masafa marefu ikiwa sehemu ya
maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani katika kituo cha
mizani cha Mikese mkoa wa Morogoro mpango ulioanzishwa na TBL na jeshi
la polisi nchini.
KATA YA MWASANGA NA TEMBELA MKOANI MBEYA ZAPATIWA ELIMU KUHUSU JOTOARDHI
Afisa Mawasiliano wa Kampuni ya
Kuendeleza Jotoardhi Tanzania (TGDC) Bi. Johari Kachwamba akiwaelimisha
Viongozi wa Kata ya Mwasanga na Tembela kuhusu majukumu ya TGDC leo 7
Agosti, 2015 Mkoani Mbeya.
Mhandisi Mwandamizi toka Wizara
ya Nishati na Madini, Bwana. Jacob Mayalla akiwaelimisha Viongozi wa
Kata ya Mwasanga na Tembela kuhusu historia ya tafiti za jotoardhi kwa
mkoa wa Mbeya leo 7 Agosti, 2015 Mkoani Mbeya.
Baadhi ya Viongozi wa Kata
ya Mwasanga na Tembela wakifuatilia kwa makini elimu ikiyotolewa na
Wayendaji wa TGDC leo 7 Agosti, 2015 Mkoani Mbeya.
PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA.
………………………………………………………………………………………………………..
NA BENEDICT LIWENGA, MAELEZO, MBEYA.
Nishati ya jotoardhi imeelezwa
kuwa ni nishati usiyokuwa na kikomo kwani pindi inapovunwa huwa haiishi
na matumizi yake yanakuwa endelevu kwasababu pindi mvuke unapopatikana
toka katika maji ya jotoardhi, maji yake hutumiwa kwa shughuli za moja
kwa moja ikiwemo ukaishaji wa mazao, uzalishaji samaki ikiwemo na
utalii.
Hayo yameelezwa leo na Mhandisi
Mwandamizi toka Wizara ya Nishati na Madini, Bwana Jacob Mayalla wakati
Timu ya Shirika la Uendelezaji wa Nishati ya Jotoardhi Tanzania (TGDC)
ikiendelea na kampeni yake ya kuelimisha viongozi pamoja na wanavijiji
kuhusu faida ya jotoardhi nchini.
Mayalla amesema kuwa utafiti
kuhusu upatikanaji wa jotoardhi ulianza miaka ya nyuma ya 1976 hadi 1978
ambapo mkoa wa Mbeya umekuwa miongoni mwa mikoa ambayo jotoardhi
inasemekana ipo kutokana na tafiti hizo.
“Mkoa wa Mbeya ni miongoni mwa
mikoa iliyobarikiwa kuwa na jotoardhi, hivyo Serikali kupitia Kampuni
hii ya TGDC inakusudia kuanza shughuli za upimaji ili kuweza kupata
nishati hii na kuweza kutatua changamoto za upatikanaji wa umeme katika
mkoa huu”, alisema Mayalla.
Akitaja baadhi ya matumizi ya
moja kwa moja, Mhandisi Mipango toka TGDC, Bwana Chagaka Kalimbia
ameeleza kuwa, jotoardhi ina matumizi mbalimbali ikiwemo kupadha nyumba
joto, kuzalisha mazao ya mbogamboga kwa kutumia Vitalu Nyumba, vyanzo
vya kitalii kwa nchi pamoja na matumixi mengineyo ambayo yanapelekea
kuongeza vipato vya wananchi na taifa kwa ujumla.
“Mradi huu una manufaa kwa
wananchi kwa mfano kwa mkoa wa Mbeya ambao kuna baridi kali, jotoardhi
inaweza kutatua changamoto hii kwa kutengeneza miundombinu ambayo
itasaidia kupasha nyumba joto, lakini pia kwasababu mkoa huu unategemea
kilimo, basi jotoardhi hii itakuwa mkombozi kwa uzalishaji mkubwa wa
mazao mbalimbalu kwa kukaushia maxso yao kwani nishati ya jua katika
maeneo haya siyo ya uhakika”.
Naye Afisa Mawasiliano wa TGDC,
Bi. Johari Kachwamba ameeleza mandhari nzima wa madhumuni ya TGDC kwa
wananchi na kwa Taifa zima ikiwemo hali ya uzalishaji wa umeme hapa
nchini, historia ya TGDC, Dira na dhamira kuu ya TGDC ili kuifanya jamii
ipate uelewa mzuri kuhusu majukumu ya Kampuni hiyo.
Kwa upande wake Afisa Sayansi
ya Jamii, Bi. Eva Nyantori ameeleza masuala mbalimbali kuhusu namna gani
jamii inashitikishwa na mradi huo kwa manufaa ya wananchi hususani
fursa mbalimbali ambazo jamii inatarajiwa kuzipata zikiwemo fursa za
ajira ambazo huleta kipato hali ambayo inapelekea uchumi wa eneo kukua
kwa kasi kutokana na na nishati hiyo.
“Jamii itarajie kupata fursa
mbalimbali mfano sekta za barabara, ajira kwa wananchi, kodi itokanayo
na mradi huo, upatikanaji wa umeme wa nafuu kwa wakazi wa eneo husika,
hivyo ni matumaini yetu kuwa nishati hii itapunguza gharama kwa wananchi
wa mkoa huu”, alisema Nyantori.
Akizitaja changamoto za mradi
huo, amesema kuwa kuna Sheria namba 4 na 5 ya 1999 ili kuweza kufanya
fidia kwa maeneo yayaksyohusika na mradi ambapo Sheria hiyo inaitaka
kufanya fidia hiyo ndani ya miezi Sita kabla ya mradi huo kuanza rasmi
kuchimbwa, lakini elimu kuhusu fidia hiyo itatolewa ili kumfanya
mwananchi apate kuelewa.
TGDC inatarajia kuzalisha zaidi
ya Megawati 200 za nishati ya umeme kwa mkoa wa Mbeya ambao utatokana
na nishati ya jotoardhi ambapo kwa sasa mkoa huo unatumia Megawati 40.
MBUNIFU WA MITINDO AMINA PLUMMER ATOA MADA NAMNA KUJITAMBUA KWENYE SEMINA YA KUWAWEZESHA WANAWAKE WAJASIRIAMALI
Mbunifu na Mmiliki wa Maduka ya Amina Design Ambaye pia ni Mentor wa Taasisi ya Manjano Foundation Amina Plummer Akitoa
Mada kwenye Semina ya Kuwawezesha Wanawake Kuwa Wajasiriamali kupitia
Vipodoz Vya Luv Touch Manjano Iliyoandaliwa na Manjano Foundation Kwa
Lengo la Kuwajengea Udhubutu Wanawake Kufanya biashara pia namna ya
Kujiwekea Akiba na Kutumiza Malengo yao. Taasisi
ya Manjano Foundation, ambayo imeanzisha jukwaa kwa ajili ya kuandaa
Miradi ambayo itamuinua mwanamke wa Kitanzania kwa kumwondolea
umasikini wa kipato na ambayo itakuwa ni chachu ya kubadili yale yote
yaliyoyazunguka maisha yake. Taasisi hii limekwishazindua mradi wenye
kubeba bendera yake, Manjano Dream-Makers, mradi unaokusudia kuzaa
kizazi kipya cha wajasiriamali wanawake kwa kutumia kipodozi cha
LuvTouch Manjano tu
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd Mama Shekhar Nasser (Katikati) Akiwa na Mbunifu Amina Plummer (Kushoto ) Pamoja Afisa Mtendaji Mkuu wa Women an Youth Empowerment Program Kutoka Uganda Dada Remmie Male.
Mbunifu na Mmiliki wa maduka ya Amina Design Amina Plummer ni mmoja
kati ya Mentors 15 watakao wapa muongozo washiriki 30 wa mradi wa
Manjano Foundation. Amina aliwapa somo la kujifahamu kama wajasiriamali
chipukizi kuwa wasilimbuke pale ambapo mafanikio yanapo anza kuja.
Aliwaeleza kuhusu umuhimu wa kujiamini, kumuamini Mungu, kuwakarimu
wateja, kuweka akiba Akiwa Sambamba na Afisa Mtendaji Mkuu wa Women an Youth Empowerment Program Kutoka Uganda Dada Remmie Male
Mbunifu Amina Plummer ni mmoja
katika Picha ya Pamoja na Baadhi ya washiriki wa Semina hiyo
inayoandaliwa na Taasisi ya Manjano Kupitia Bidhaa za Luv Touch
Manjano.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd Mama Shekhar Nasser na Mbunifu Amina Plummer Pamoja
Afisa Mtendaji Mkuu wa Women an Youth Empowerment Program Kutoka
Uganda Dada Remmie Male. Katika Picha ya Pamooja na Washiriki wa Semina
hiyo..
NISHATI YA JOTOARDHI KUNUFAISHA BAADHI YA VIJIJI MKOANI MBEYA
Mkurugenzi wa masuala ya Kiufundi
toka TGDC, Bwana Karamaeli Mnjokava akiwaeleza wanakijiji cha Ituha na
Itonyajuu ya faida za jotoardhi nchini 6 Agosti, 2015 mkoani Mbeya.
Meneja Mkuu wa Shirika la
Uendelezaji wa Nishati ya Jotoardhi, Mhandisi Boniface Njombe
akiwaelimisha wanakijiji cha Ituha na Tonya juu ya jotoardhi nchini 6
Agosti, 2015 mkoani Mbeya.
Mjiolojia Mwandamizi toka Wizara
ya Nishati na Madini, Bwana Jacob Mayalla akiwaelezea wanakijiji wa
Ituha na Tonya hitoria ya tafiti za jotoardhi nchini 6 Agosti, 2015.
Baadhi ya wanakijiji wa Ituha na
Tonya wakifuatilia mada kwa makini zikizotolewa na watendaji wa TGDC 6
Agosti, 2015 mkoani Mbeya.
……………………………………………………………………………..
NA BENEDICT LIWENGA, MAELEZO, MBEYA.
Nishati ya Jotoardhi imeelezwa
kuwa muhimu kwa maeneo ambayo utafiti ulishafanywa hapo awali kwani ina
faida lukuki kwa maendeleo ya nchi hususani katika kutatua changamoto ya
ukosefu wa nishati ya umeme ikiwemo umeme wa mgao ambao unazikumba
baadhi ya mikoa hapa nchini.
Akiongea wakati wa Kampeni
endelevu kuhusu jotoardhi 6 Agosti, 2015 katika Kata za Ilomba vijiji
vya Ituha na Tonya pamoja na Kata ya Nanyala iliyopo Wilaya ya Mbozi
mkoani Mbeya, Meneja Mkuu wa Shirika la Uendelezaji wa Jotoardhi (TGDC),
Mhandisi Boniface Njombe amesema kuwa jamii hainabudi kuonyesha
ushirikiano na Serikali pamoja na Kampuni ya TGDC ili kuwepo na uelewa
juu ya nishati hiyo na kuleta maendeleo nchini.
“Niwahakikishie kuwa nishati hii
ni nzuri kwani itasaidia kutatua changamoto tulizonazo katika uoande wa
nishati, hivyo niwasihi kuonyesha ushirikiano baina ya Serikali yetu
pamoja na Kampuni hii ili juhudi hizi zizidi kuendelea na kutuletea
maendeleo katika maeneo yetu”, alisema Njombe.
Mhandisi Njombe aliongeza kuwa
TGDC imedhamiria kuzalisha umeme wa Megawati 200 jambo ambalo litasaidia
upatikanaji wa umeme wa uhakika na kuuondoa mgao kwani kwa sasa mkoa wa
Mbeya pekee unatumia Megawati 40.
Naye Mkurugenzi wa Masuala ya
Kiufundi toka TGDC, Bwana Taramaeli Mnjokava ameeleza kuwa, jotoardhi
ina matumizi mengi ikiwemo matumizi ya moja kwa moja kama vile katika
uzalishaji wa samaki kwani samaki hupendelea maji yenye uvuguvugu kiasi,
hivyo endapo wanambeya watajikita katika kutengeneza mabwawa ya samaki,
maji ya jotoardhi yanasaidia katika kuzalisha samaki kwa wingi na
hatimaye kuongeza pato kwa taifa.
“Matumizi mengine ya maji
yatokanayo na jotoardhi ni kwamba, maji haya yanaweza kutumika katika
Vitalu shamba kwa kiingereza huitwa Green Houses, sasa kwa maji haya
tunaweza kuzalisha mboga mboga pamoja na maua jambao ambalo litaweza
kutuongezea kipato.
WENGI WAJIUNGA NA NSSF MAONYESHO YA NANENANE
Meneja
Kiongozi wa Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii
(NSSF), Eunice Chiume akiwaelezea faidaza kujiunga na mfuko huo wakazi
wa Mkoa wa Lindi waliofika kwenye banda la NSSF kwenye maonesho ya
Nanenane yanayofanyika kitaifa mkoani humo.
Meneja
Kiongozi wa Masoko Na Uhusiano Eunice Chiume akiwapa Maelezo ya Faida
za kuwa Mwanachama wa NSSF wanachama waliotembelea banda la NSSF mkoani
Lindi.
Mwanachama wa Hiari, Mrisho Mpoto akilipia michango yake kwenye maonesho ya Nanenane Mkoani Lindi.
Afisa Uendeshaji
Muandamizi Kabona Kandoro akimkabidhi zawadi mmoja wa wanachama waliotembelea
banda la NSSF kwenye maonesho ya nanenane mkoani Lindi.
Muandamizi Kabona Kandoro akimkabidhi zawadi mmoja wa wanachama waliotembelea
banda la NSSF kwenye maonesho ya nanenane mkoani Lindi.
Mwanachama mpya wa NSSF akipigwa picha kwa ajili ya kadi ya uanachama baada ya kujiunga na mfuko huo.
UMOJA WA WASANII WA FANI MBALIMBALI WAMTANGAZA RAIS DR. JAKAYA KIKWETE KUWA SHUJAA WA SANAA YA MUZIKI NCHINI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Jakaya Kikwete akizungumza
mbele ya wageni waalikwa mbalimbali (hawapo pichani),waliofika ndani ya
ukumbi wa Mlimani City katika hafla ya kuagwa kwake ilioandaliwa na
Muungano wa Wasanii kwa ajili ya kumshukuru kwa namna alivyowasaidia
tangu alivyoingia madarakani kwa miaka 10 na pia kumtambulisha Mgombea
wa Urais wa chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli,Dkt Jakaya Kikwete
alizungumza mambo mbalimbali zikiwemo haki na hatimiliki za wasanii wa
muziki pamoja na Bongomovie na pia alikubali kuwa mlezi wa tasnia hizo
na kuhakikisha mambo yanakwenda sawa ndani ya tasnia hizo mbili adhimu
kwa sasa hapa nchini.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Jakaya Kikwete katikati pichani
akiserebuka na wadau wa muziki na huku akipiga nao picha,ndani ya ukumbi
wa Mlimani City katika hafla ya kuagwa kwake ilioandaliwa na Muungano
wa Wasanii kwa ajili ya kumshukuru kwa namna alivyowasaidia tangu
alivyoingia madarakani kwa miaka 10 na pia kumtambulisha Mgombea wa
Urais wa chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli.
Mgombea
Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akipiga ngoma huku akishirikiana
na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipiga gitaa ndani ya
ukumbi wa mlimani City jijini Dar.
Mwanadada Wema Sepetu akimtunza midola Dkt John Magufuli alipokuwa akipiga ngoma jukwaani kwa ustadi mkubwa.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Jakaya Kikwete akiwa ameambatana
na Mgombea Urais wa chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli pamoja na
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,Katibu wa NEC Itikadi na
Uuenezi Nape Nnauye na pamoja na Januari Makamba wakifurahia jambo kwa
pamoja na wageni waalikwa mbalimbali waliofika ndani ya ukumbi wa
Mlimani City kushiriki hafla ya kuagwa kwake ilioandaliwa na Muungano wa
Wasanii kwa ajili ya kumshukuru kwa namna alivyowasaidia tangu
alivyoingia madarakani kwa miaka 10.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Jakaya Kikwete akiwa ameambatana
na Mgombea Urais wa chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli pamojoa na
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (mwisho kushoto) na Mkuu wa
Wilaya ya Ilala Mh.Paul Makonda wakiwasili ndani ya ukumbi wa Mlimani
City kushiriki hafla ya kuagwa kwake ilioandaliwa na Muungano wa Wasanii
kwa ajili ya kumshukuru kwa namna alivyowasaidia tangu alivyoingia
madarakani kwa miaka 10.
SELEMANI RASHIDI MKAZI WA KITONGOJI CHA LUGONGONI (A) NGURUKA MKOA WA KIGOMA ANAOMBA MSAADA WA MATIBABU KWA MWENYE KUGUSWA
Selemani
Rashidi, naomba msaada kwa yeyote anisaidie niweze kufanyiwa matibabu
kwa kinyama kilicho jitokeza kichwani mwangu toka nilipo zaliwa.
Selemani Rashidi, anapoishi na mama yake mzazi
Selemani
Rashidi (kushoto), akiwa na mama yake mzazi pichani, ambaye alisimulia
mkasa mzima wa mwanaye, alizaliwa akiwa mzima na baada ya kuzaliwa
alipatwa na matatizo ya ugonjwa wa Degedege na alimpeleka kwa mganga wa
kienyeji na kupona matatizo hayo na ndipo kikaota kipele kichwani cheusi
na kikawa kinakuwa na kushikana na sikio, kutokuwa na uwezo wa kipesa
hakuweza mpeleka popote, Baba yake yapata Miaka kumi na tano toka
afariki na ukizingatia ni pesa inayo hitajika, hayo yalisemwa na mama
yake mzazi ambaye anaitwa Zamda Kibosha, wakiwa wamekaa kwao maeneo ya
kitongoji cha Lugongoni, (A) Kataa ya Nguruka Wilaya ya Uvinza Mkoa wa
Kigoma, Mama yake anasema mwanaye baada ya kuota kinyama hicho, kauli
kutoka ni kwa shida, akijibu maramoja harudii tena kuongea na chooni
anakwenda mwenyewe na kula anakula kama kawaida, mama anaomba kwa mtu
yoyote mwenye kuona na kusia anaomba msaada wa hali na mali ili mwanaye
apate matibabu, kwa mawasiliano mwenye chochote kitumwe kwenye namba 0687946492, Mariam Hamza Thabiti, Nguruka kigoma.
(PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
Mmiliki wa ujijirahaa blog.
Maonesho ya Nane Nane kitaifa yanayofanyika mkoani Lindi yafikia siku ya sita.
Wananchi wote mnakaribishwa
kutembela banda la Wizara ya Fedha na taasisi zilizo chini yake ikiwemo
UTT AMIS, Mfuko wa Pensheni PPF, GPSA na UTT PID uwanja wa maonesho ya
kilimo ya Nane Nane Kitaifa Ngongo mkoani Lindi.
Mwenyekiti wa Chama cha Kilimo
Taifa (TASO) Englebert Moyo akiuliza swali kuhusu masuala ya pensheni
kwa Mhasibu kutoka Idara ya Pensheni Wizara ya Fedha Imelda Mzatulla
wakati alipotembelea Banda la Wizara ya Fedha.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma
ya Ununuzi Serikalini (GPSA) Josephat Mwambega akiongea na Afisa Msoko
na Uhusiano Rahimu Mwanga kutoka taasisi ya UTT AMIS kwenye Uwanja wa
maonesho ya Kilimo ya Nane Nane Ngongo Mkoani Lindi.
Mhasibu kutoka Idara ya Pensheni
Wizara ya Fedha Imelda Mzatulla akiongea na baadhi ya wageni waliofika
kujionea kazi mbalimbali zinazofanywa na Wizara ya Fedha wakati wa
maonesho ya Kilimo ya Nane Nane uwanja wa Ngongo Mkoani Lindi. Continue reading →
TFF YATUMA SALAM ZA RAMBIRAMBI
Shirikisho la Mpira wa Miguu
nchini (TFF) limetuma salam za rambi rambi kwa familia ya Muro, kufutia
kifo cha Mzee Cornel Muro kilichotokea mwishoni mwa wiki jijini Dar s
salaam na mazishi kufanyika Machame mkoani Kilimanjaro.
Katika salamu zake za rambirambi
kwa familia ya marehemu Muro, TFF imewapa pole wafiwa, ndugu jamaa na
marafiki na kusema wako pamoja katika kipindi hiki cha maombelezo na
kuomba mwenyezi Mungu awajilie nguzu wafiwa
Marehemu Cornel Muro ni baba mzazi wa Afisa Habari wa klabu ya Young Africans, Jerry Muro.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
WASANII WAMUAGA DR. JAKAYA KIKWETE NA KUMKARIBISHA DR JOHN POMBE MAGUFULI MLIMANI CITY
Rais Dr. Jakaya Kikwete
akifurahia jambo na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr
John Pombe Magufuli kupitia CCM wakati alipowasili Mlimani City jijini
Dar es salaam kwa ajili ya kushiriki hafla ya chakula cha jioni
kilichondaliwa na Muungano wa wasanii Kumshukuru Mh. Dr. Jakaya Kikwete
kwa jinsi alivyowasaidia katika uongozi wake wa miaka 10 kama Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kumkaribisha Mgombea wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dr. John Pombe Magufuli, Hafla hiyo
imehudhuriwa na wasanii mbalimbali wakiwemo waigizaji wa filamu,
wachezaji na wanamuziki wakishiriki kwa pamoja kumshukuru Dr. Jakaya
Kikwete, Kulia ni Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Mh. Januari
Makamba(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MLIMANI CITY-DAR ES SALAAM)

Rais Dr. Jakaya Kikwete
akiongozana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kushoto,
Mgombea wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dr. John Pombe
Magufuli na Mwigizaji Jacob Steven JB wakati alipowasili kwenye ukumbi
wa Diamond.
Rais Dr. Jakaya Kikwete
akiongozana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinanawa pili kutoka
kushoto ar es salaam Mh Meck Sadik na Muigizaji Jacob Steven JB.
Mwanamuziki Nasib Abdul aka Diamond Platnumz akiwasili na Meneja wake wa Shughuli za kimataifa Bw.Salam.
Rais Dr. Jakaya Kikwete akiongozana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kushoto wakati wakiigia ukumbini.
Rais Dr. Jakaya Kikwete akiwa na
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kushoto,Mgombea wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dr. John Pombe Magufuli wa pili
kutoka kulia na Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Mh. Januari
Makamba.
Rais Dr. Jakaya Kikwete akiwa na
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kushoto,Mgombea wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dr. John Pombe Magufuli kulia na
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Ndugu Nape Nnauye wakipiga makofi
wakati wimbo maalum ukiimbwa.
Davis Mosha kulia akiwa pamoja na Mboni Masimba wa The Mboni Show wakiperuzi kwenye simu.
Rais Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na Davis Mosha na Mboni Masimba
Rais Dr. Jakaya Kikwete akina baadhi ya viongozi wa bendi za muziki wa Taarab.
Rais Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na Bw. Godfrey Kusaga mmoja wa wakurugenzi wa kampuni ya Primetime.

Rais Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na Adam Mchomvu mtangazaji wa kipindi cha XXL cha Clouds Radio.
Mgombea wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kupitia CCM Dr. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi
wa mtandao huu Bw. John Bukuku kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam
Mh. Meck Sadik Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Davis Mosha kushoto ni msanii Mwana FA.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akizungumza na wasanii mbalimbali kutoka kushoto ni
Mwigizaji Jacob Steven, Mwanamuziki Jose Mara na Mwana FA.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akifurahia jambo na wasanii mbalimbali kutoka kushoto
ni Mwigizaji Jacob Steven, Mwanamuziki Jose Mara, Mwigizaji Monalisa
aka Yvone Cherry na Mwana FA, kulia ni Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh.
Meck Sadik.
Kutoka kulia ni Mama Monalisa . Juma Kaseja, Dokii na Monalisa wakiwa katika hafla hiyo.
Ali Choki kushoto na anayefuatia ni msanii Kitale pamoja na wasanii wenzao wakiwa katika hafla hiyo.
Kutoka kushoto ni Mabosi wangu Edward Mpogole, Daniel Chongolo na Juma Kengele wakipozi kwa picha.
TAARIFA KWA WAANDISHI WA HABARI KUTOKA CHAMA CHA WANANCHI CUF KUHUSU KUJIUZULU KWA PROFESA LIPUMBA
Leo tarehe 6 Ago
sti,
2015 Profesa Ibrahim Lipumba aliitisha mkutano na waandishi wa habari
katika Hoteli ya Peacock, mjini Dar es Salaam na kutangaza kwamba
amejizulu nafasi yake kama Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Wananchi
(CUF).
Sisi kama Chama
tumezipokea taarifa hizo na tunayaheshimu maamuzi yake. Ni haki yake ya
kikatiba na haki ya kidemokrasia kufanya maamuzi anayoyaona yana maslahi
kwake.
Bila shaka, Profesa
Ibrahim Lipumba amekifanyia kazi kubwa Chama chetu katika miaka 16
ambayo alikuwa Mwenyekiti wetu, nafasi iliyomfanya awe kiongozi wetu
mkuu. Kwa nafasi yake hiyo, pia ametoa mchango mkubwa katika ujenzi wa
demokrasia katika nchi yetu. Tunaithamini kazi hiyo na tutaendelea
kumheshimu kwa utumishi wake mkubwa kwa Chama chetu na nchi yetu.
Tunamtakia kila la kheri katika mipango yake ya baadaye.
Chama Cha Wananchi
(CUF) ni taasisi na kinaendeshwa kitaasisi. Ndiyo maana maamuzi yake
yote yamekuwa yakifanywa kitaasisi kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za
Chama. Kwa msingi huo, pamoja na ukweli kwamba kuondoka kwa Profesa
Lipumba katika safu ya uongozi kutaacha pengo hasa katika kipindi hichi
ambacho tunaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu, tunawahakikishia wanachama na
wapenzi wa CUF na wananchi wa Tanzania kwa ujumla kwamba Chama hichi
hakitayumba.
Katika historia yake,
CUF imepita katika dhoruba na misukosuko mingi lakini mara zote
kimeonesha uwezo mkubwa wa kuhimili dhoruba na misukosuko hiyo na
kukabiliana na athari zake. Hatuna chembe ya wasiwasi kwamba hata
mtihani huu tutauvuka na tunaamini tutaibuka tukiwa Chama imara zaidi.
Katibu Mkuu ameagiza
kuitishwa kwa vikao vya dharura vya Kamati ya Utendaji ya Taifa na
Baraza Kuu la Uongozi la Taifa siku ya Jumapili, tarehe 9 Agosti, 2015
ili kujadili hatua hiyo na kufanya maamuzi juu ya hatua muafaka
zinazopaswa kuchukuliwa katika kipindi hiki hadi hapo Chama
kitakapomchagua mwanachama mwengine kujaza nafasi hiyo ya Mwenyekiti.
Katika kipindi hiki,
Chama kinawataka wanachama na wapenzi wake wote kuwa watulivu na
wavumilivu na kusubiri maelekezo ya vikao vya juu vya kitaifa vya Chama.
Mwisho kabisa,
tunawahakikishia wanachama wetu na Watanzania wote kwa ujumla kwamba CUF
itaendelea na shughuli zake kama Chama na pia kama mshirika katika
UKAWA ambayo CUF ilikuwa ni katika waasisi wake. Tunawahakikishia
wanachama wetu na Watanzania wote kwa ujumla kwamba CUF itatumia nguvu,
uwezo, juhudi na maarifa yake yote kuhakikisha kwamba inaulinda UKAWA
ambao unaonekana kuwa mwiba kwa CCM. Tunatambua kwamba kuna njama na
mbinu kubwa na nyingi zinazofanywa na watawala kutaka kuuvuruga na
kuuhujumu UKAWA wakidhani kwamba watapata manusura. Tumesema na
tunaendelea kusema CCM mwaka huu hawana manusura. Watanzania wameamua
kuwan’goa, na watan’goka Tanzania Bara na Zanzibar kupitia sanduku la
kura tarehe 25 Oktoba, 2015. Wimbi hili kubwa la mabadiliko halizuiliki
tena.
HAKI SAWA KWA WOTE
ISMAIL JUSSA
KAIMU MKURUGENZI WA HABARI, UENEZI NA MAWASILIANO NA UMMA
06 AGOSTI, 2015
KAIMU MKURUGENZI WA HABARI, UENEZI NA MAWASILIANO NA UMMA
06 AGOSTI, 2015






























No comments :
Post a Comment