Tathimini inaonesha mfuko utakuwa imara bila kuteteleka kwa muda wa
miaka 50 ijayo.
Mkurugenzi wa fedha wa NSSF ndugu
Ludovick Mrosso alipokuwa Kaimu mkurugenzi mkuu wa Mfuko akitoa maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Kigamboni linalojengwa na NSSF kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania kwa waziri wa ujenzi na miundo mbinu Mh.Dakt John Pombe Makufuli
Christian Gaya Arusha
Alhamis Juni 4, 2015
Mkurugenzi wa fedha wa NSSF ndugu
Ludovick Mrosso alisema ya kuwa thamani ya mfuko iliongezeka na kufikia
shilingi milioni 2,759,555 mpaka mwezi Juni 2014 ukilinganisha na shilingi
milioni 2,551,227 kutoka mwezi Juni 2013, sawa na ongezeko la shilingi 208,328
likiwa sawa na ongezeko la asilimia 8.17 kwa mwaka.
Alitaja ya kuwa vitega uchumi
viliongezeka kutoka shilingi milioni 2,295,251 za kitanzania kwa mwaka wa fedha 2012/2013 mpaka kufikia
shilingi milioni 2,403.606 kwa mwaka wa fedha 2013/2014. Hii ikiwa sawa na
ongezeko la asilimia la shilingi milioni 108,355 ambapo ni sawa na asilimia
4.72 ukilinganisha na mwaka 2012/2013.
“Aidha lengo lilikuwa kufikia
vitega uchumi vyenye thamani ya shilingi 2,484,533, hivyo lengo lilifikiwa kwa
asilimia 96.70” Mrosso aliyasema haya
siku ya ufunguzi wa mkutano mkuu wa wadau uliofanyika ndani ya ukumbi wa Simba
Hall Arusha ulioanza tarehe 2-4 June, 2015
Alisema kwa ujumla kumekuwepo na
ongezeko la uwekezaji kwenye nyanja mbalimbali isipokuwa kwenye dhamana za
serikali, amana za mabenki ambazo zinaonesha kupungua. upungufu mkubwa katika
amana za mabenki umetokana na amana zilizowekezwa mwaka uliopita kuiva ndani ya
mwaka huu, na kuwa mwaka huu uwekezaji ulifanyika kidogo katika amana za
kibenki kutokana na mahitaji makubwa ya fedha kwa ajili uwekezaji wa fedha vya
muda mrefu
Akizungumzia rasilimali zingine
Mroso alisema ziliongezeka kutoka shilingi milioni 255, 976 kwa mwaka 2013 na
kufikia shilingi milioni 355,949 kwa mwaka 2014 ongezeko likiwa ni asilimia
39.06 wakati kwa upande wa rasilimali halisi ziliongezeka kutoka milioni
2,378,068 toka Juni 2013 na kufikia milioni 2,582,921 mwezi Juni 2014 likiwa
sawa na ongezeko la shilingi milioni 204, 853 sawa na asilimia 8.61
“Pato kutokana na vitega uchumi
kwa mwaka 2013/2014 lilifikia shilingi
milioni 222.160 ukilinganisha na shilingi milioni 252.547 kwa mwaka 2012/2013 na
pungufu ukiwa ni sawa na asilimia 12.03. aidha kulikuwa na ongezeko la thamani
ya hisa za kampuni zilizosajiriwa katika soko la hisa la Dar es Salaam kwa
kiasi cha shilingi milioni 29.490” mkurugenzi wa fedha alifafanua.
Akifafanua juu ya ukusanyaji wa michango
Mrosso alisema ya kuwa mpaka kufikia mwaka 2013/2014 mfuko uliweza kukusanya
shilingi milioni 548.472 ukilinganisha na shilingi milioni 476.107 mwaka
2012/2013. ongezeko hili lilikuwa sawa shilingi milioni 72.365 sawa na asilimia
15.20. Wakati kwaupande wa mafao alisema
ya kuwa kwa mwaka 2013/2014 mfuko uliweza kulipa wanachama kiasi cha milioni 344,787 ukilinganisha na
shilingi milioni 228.049 mwaka 2012/2013, ongezeko likiwa ni shilingi milioni
116,738 sawa na asilimia 51.19
Kwa upande wa hali ya ukwasi na
thamani ya mfuko wa NSSF mkurugenzi aliwaambia wadau ya kuwa hali ya ukwasi kwa
ujumla kwa mwaka 2013/2014 ilikuwa nzuri kwa sababu mpaka ilipofikia tarehe 30
Juni 2014 shirika ilikuwa na shilingi milioni 59,890. Tathimini ya uimara
(solvency) wa mfuko ilifanywa na bwana George Langi’s wa Canada kwa kipindi
kilichoishia tarehe 30.06.2009 na inaonesha mfuko utakuwa imara bila kuteteleka
kwa muda wa miaka 50 ijayo. Pia tathimini iliyofanywa na kampuni ya Genesis
Solution ya Africa kusini inaonesha ya kuwa rasilimali kwa ajili ya kulipa
mafao ni asilimia 75.5 na kwa wanachama kuendelea kuchangia asilimia 20 ya
mshahara na hivyo mfuko uko imara kabisa kwa miaka mingi ijayo alisisitiza.
No comments :
Post a Comment