KOMREDI KINANA ALAKIWA KWA SHAMRA SHAMRA ZA SUNGUSUNGU JIMBO LA KWIMBA
BOTI YA KILIMANJARO V KUANZA SAFARI MWISHONI MWA WIKI HII
Kampuni
ya Boti za Azam Marine Zanzibar yatowa Boti Mpya ya Kilimanjaro
V,iliowasili juzi katika bandari ya Zanzibar na inategemewa kuaza kutoa
huduma ya Usafiri kati ya Zanzibar na Dar-es-Salaam mwishoni mwa wiki
hii baada ya kukamilisha taratibu zote za kisheria na kuaza kutowa
huduma hiyo. Ikiwa katika bandari ya Zanzibar leo.Ina uwezo wa kuchukua
Abiria 550, inachukua masaa maskamu lisaa moja na nusu mpaka Dar.
Sehemu ya VIP One ikiwa na Video katika viti vyake vyenye uwezo wa kulala wakati abiria wakiwa safarini.
Sehemu ya VIP kama inavyoonekana
Kepteni wa Boti Mpya ya Kilimanjaro V Thomas Buhatwa akizungumza na
waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya Zanzibar kuhusiana na
huduma zinazopatikana katika boti hiyo mpya na kutowa maelezo ya vyombo
vya kisasa viliomo katika boti hiwa wakati wa kuitembelea boti hiyo
ikiwa katika bandari ya Zanzibar leo mchana.
WAWAKILISHI WA CHAMA CHA WANANCHI ( CUF ) WAZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI
Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar Mhe. Nassor Mazrui akizungumza na
waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar kuhusiana na
kutoka katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi kwa kudai furugu iliotokea
katika kituo cha uandikishaji cha skuli ya mto pepo.kwa kudai kuzuiwa
wanachama wao kuandikisha.
Makamu
Mwenyekiti wa CUF,Mhe Juma Duni akijibu maswali ya Waandishi wa habari
kuhusiana na kuchukua uamuzi wa kususia Kikao cha Baraza las Wawakilishi
wakati wa ichangoo ya Wizara ya Fedha kwa kudai kufganyika kwa vurugu
katika zioezi la uandikishaji wa wapiga kura katika kituo cha skuli ya
mto pepo.
WAWEKEZAJI KUTOKA CHINA WAVUTIWA NA ENEO LA VIWANDA WILAYANI KISARAWE MKOANI PWANI
Kibao kinacho elekeza eneo la mradi wa viwanda wilayani Kisarawe mkoani
Pwani lililopo Visegese. Mradi huo unaendeshwa na Halmshauri hiyo na
wabia wa Kampuni ya World Map
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),
Brendan Maro (kushoto), akizungumza na viongozi wa Halmshauri ya Wilaya
ya Kisarawe, Wabia wa eneo la mradi wa Kampuni ya World Map na
wawekezaji kutoka nchini China waliofika wilayani humo jana kuangalia
fursa za kuwekeza viwanda katika eneo hilo. Kulia ni Ofisa Mipango Miji
Mwandamizi kutoka TIC, Elibariki Ngorovily.
Wawekezaji kutoka China wakiwa katika mkutano na uongozi wa wilaya ya
Kisarawe na wabia wa mradi huo kutoka Kampuni ya World Map kabla ya
kwenda kuona eneo la mradi wa viwanda. Kutoka kushoto ni Makamu wa Rais
wa Umoja wa Makampuni ya Huallan ‘Huallan Group’, Tu Huobao, Mkurugenzi
wa Masoko wa Kampuni hiyo, Apple Ye, Huang Haitao na Meneja Masoko, Nara
Zhou.
Mkurugenzi wa Halmshauri ya Kisarawe, Mwanamvua Mrindoko (kulia),
akizungumza katika mkutano huo wakati akiwakaribisha wawekezaji hao.
Kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji
Tanzania (TIC), Brendan Maro, Ofisa Mipango Miji Mwandamizi kutoka TIC,
Elibariki Ngorovily, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Subira Kigalu,
Mwenyekiti wa Halmshauri hiyo, Adam Ng’imba.
MAWAKALA WA FORODHA NCHINI WAASWA KUJISAJILI KWENYE MFUMO WA HIMAYA MOJA YA FORODHA YA AFRIKA MASHARIKI ( SINGLE CUSTOM TERRITORY )
Kamishna
wa Forodha Kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Tiagi Kabisi
akiongea na viongozi wa Chama cha Mawakala wa Forodha na kuwataka
mawakala wa Tanzania kujisajili katika mfumo wa uondoshaji wa Himaya
moja ya Forodha(SINGLE CUSTUM TERRITORY) ili kuwezesha uondoshwa wa
mizigo kwa haraka zaidi pindi mfumo huo utakapoanza kutumika kwani
mifumo huo na watanzania tayari zinawasiliana mpaka sasa, Wakati wa
Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam Kushoto ni Naibu Kamishna
wa Forodha Dkt. Patrick Mugoya.
Rais
wa Chama cha Mawakala wa Forodha (TAFA) Bw. Stephen Ngatunga akiongea
na viongozi wa Chama cha Mawakala wa Forodha na wawakilishi wa Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) ambapo aliipongeza serikali kupitia Mamlaka
hiyo katika kuhakikisha wanaweka mazingira mazuri kwa mawakala wa
forodha na kuiasa kuendelea kushughulikia changamoto mbalimbali katika
sekta hiyo ili kuiwezesha serikali kupata mapato kwa maendeleo ya Taifa,
Wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam Kulia ni
Kamishna wa Forodha Kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Tiagi
Kabisi.
Baadhi
ya Viongozi na wanachama wa Chama cha Mawakala wa Forodha (TAFA)
wakimsikiliza Kamishna wa Forodha Kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA) Bw. Tiagi Kabisi, Wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es
Salaam.
RAIS KIKWETE NA DKT. REGINALD MENGI IKULU, DAR ES SALAAM
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo
vya Habari (MOAT) Dkt Reginald Mengi wakiongea na kubadilishanma mawazo
Ikulu, Jijini Dar es salaam katika hafla ya kutunuku nishani kwa
watumishi wa umma na wananchi waliofanya vyema na kwa uadilifu kwenye
sehemu zao za kazi. Dkt Mengi alikuwa mmoja wa watu mashuhuri
walioalikwa hapo Ikulu.
PICHA NA IKULU















No comments :
Post a Comment