Na Suzan Mwillo, Mwananchi
Kwa ufupi
- Serikali imeiagiza Tanesco kumtafuta mzabuni mwingine wa kuuza umeme kwa wateja kwa kushirikiana na Maxcom
Dar es Salaam. Serikali imefuta
mkataba wake na kampuni ya Selcom iliyokuwa inauza umeme wa Luku kwa
kile kilichodaiwa kuwa ni ubabaishaji katika kutoa huduma hiyo.
Pia kampuni hiyo, ambayo imekuwa ikinunua umeme wa
jumla kutoka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) imesitishiwa mkataba
huo kutokana na kukiuka sheria na taratibu za ulipaji wa kodi.
Hata hivyo, mkurugenzi mtendaji wa Selcom, Sameer Hirji hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo.
“Siwezi kuzungumzia chochote kuhusu hilo (mkataba). Tutakuwa na mkutano na waandishi wa habari kesho (leo),” alisema.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene
aliitaka Tanesco kufuata uamuzi wa Serikali kwa kuwa Selcom imekuwa
ikilalamikiwa na wateja kuwa na matatizo ya kiufundi kila wanaponunua
umeme, hasa ifikikapo mwisho wa mwezi.
“Hatuwezi kuendelea kuvumilia hali hii kwa sababu
hafai. Hiyo nafasi tumeiondoa, tunawapa wengine. Utendaji wao mbovu na
umekuwa ukisababisha wananchi kukosa umeme.
“Mteja anafika kwa wakala kununua umeme, anaambiwa hakuna, tunarekebisha mitambo yetu,” alisema.
Selcom na Maxcom ndiyo kampuni pekee zilizoshinda
zabuni za kuuza nishati hiyo na kuingia mkataba na Tanesco wa kununua
umeme wa jumla na kuuza kwa rejareja. Hata hivyo imeelezwa kuwa Maxcom
imekuwa ikifanya vizuri kuliko Selcom.
Simbachawene, ambaye amechukua nafasi iliyoachwa
na Profesa Sospeter Muhongo, alisema pia wameichukulia hatua za kisheria
kampuni hiyo kutokana na kukuika taratibu za kulipa kodi.
“Kwa mujibu wa sheria za kodi hawawezi kuendelea
kutoa huduma na hili wala halina athari zozote kwa sababu wao ndiyo
wamevunja sheria... naomba wananchi wanunue umeme katika vituo vya
Maxcom hadi pale tutakapopata muuzaji mwingine,” alisema
Mkurugenzi wa Tanesco, Felchesmi Mramba alisema
kabla ya kuchukua uamuzi huo walipokea barua kutoka Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) wakiwataka wasitishe mkataba wao na Selcom.
“Ukiachilia mbali malalamiko yaliyokuwa yanatolewa
na wananchi. TRA walituambia tusifanye kazi na hao jamaa huku
wakiwatuhumu kwa kugushi nyaraka na kukiuka taratibu za kulipa kodi.
No comments :
Post a Comment