Na Na Julius Mtatiro
Kwa ufupi
Mzee Nchimbi pia amewahi kuwa Mjumbe wa Halmashauri
Kuu ya CCM (NEC) kwa vipindi viwili kupitia kundi la majeshi na baadaye
katibu wa CCM wa mkoa, alikoma kushiriki masuala ya kisiasa mfumo wa
vyama vingi ulipoanzishwa.
Historia yake
Dk Emmanuel Nchimbi alizaliwa Desemba 24, 1971
mkoani Mbeya, (atafikisha miaka 44 Desemba mwaka huu). Elimu yake ya
Msingi aliianzia jijini Dar es Salaam katika Shule ya Msingi Oysterbay
kati ya mwaka 1980 – 1986.
Baba yake mzazi, Mzee John Nchimbi kutoka wilayani
Songea ni askari mstaafu wa Jeshi la Polisi na wakati anastaafu alikuwa
Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara.
Mzee Nchimbi pia amewahi kuwa Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) kwa vipindi viwili kupitia kundi la majeshi
na baadaye katibu wa CCM wa mkoa, alikoma kushiriki masuala ya kisiasa
mfumo wa vyama vingi ulipoanzishwa.
Dk Nchimbi alijiunga na elimu ya sekondari kwenye
Shule ya Sekondari Uru kati ya mwaka 1987 – 1989 (kidato cha I – III)
halafu akahamia Shule ya Sekondari Sangu na kukamilisha kidato cha nne
mwaka 1989 – 1990.
Nchimbi alisoma Shule ya Sekondari ya Forest Hill,
Mbeya masomo ya kidato cha V na VI mwaka 1991 – 1993. Alijiunga katika
Chuo cha IDM Mzumbe (Morogoro) na kuhitimu Stashahada ya Juu ya Utawala
(mwaka 1994 – 1997).
Wakati anahitimu IDM, pia alichaguliwa kuwa Mjumbe
wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) na mwaka uliofuatia (1998),
alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi
(UVCCM).
Dk Nchimbi amewahi kuajiriwa na Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kati ya mwaka 1998 – 2003.
Alisoma shahada ya uzamili ya usimamiz wa biashara
Chuo Kikuu cha Mzumbe mwaka 2001 – 2003 akibobea kwenye maeneo ya
(benki na fedha).
Dk Nchimbi aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda
(mwaka 2003–2005) na (mwaka 2008 – 2011) alisoma na kufanikiwa kuhitimu
shahada ya uzamivu (PhD) katika Chuo Kikuu cha Mzumbe.
Dk Nchimbi amemuoa Jane na wana watoto watatu.
Mbio za ubunge
No comments :
Post a Comment