Monday, April 6, 2015

Ufahamu umuhimu wa mikataba ya huduma kwa wateja


Retired teachers. About 50,000 civil servants are set to retire over the next one year. FILE


Baadhi ya wanachama wakishauri mifuko ya hifadhi ya jamii kuanzisha mikataba ya huduma  bora yenye misingi ya uwazi na uwajibikaji na kufahamu matarajio  na viwango vya mafao yao
Unafikiri kwa nini kuna umuhimu mkubwa kwa mifuko ya pensheni ya hifadhi ya jamii kuwekea maanani sana juu ya huduma kwa wanachama, wastaafu pamoja na wategemezi wao na hata kwa waajiri. Kwa sasa kampuni na taasisi nyingi zinaendeshwa kwenye mazingira ya ushindani ambao kila siku unaongezeka.  Na ushindani huu ni wa kimataifa na wakati huo huo na masoko ulimwenguni yanaendelea kuongezeka.

Leo gharama za kumpata mwanachama au mteja mpya mara nyingi zinazidi hata gharama za kumbakiza mwanachama au mteja wa siku nyingi. Mteja aliyeridhika na huduma huwa habishana na bei za huduma au bidhaa unazotoza na kwa maana hiyo kunakuwepo na shughuli au kazi ndogo sana za kufanya masoko na za uuzaji za kumhudumia mteja wa namna hii kuliko utekelezaji au shughuli ambazo ungefanya kwa kumtafuta mteja mpya.

Matokeo yake kwa sasa wakati wa teknolojia na habari na mawasiliano shughuli za biashara zaidi humgusa mteja. Kwa kuongezeka kwa ushindani mifuko ya pensheni ya hifadhi ya jamii inahitaji kuunganisha aina zote za mitandao ili kuboresha mawasiliano na hatimaye kumridhisha mteja. Mifuko ya pensheni ya hifadhi ya jamii lazima iweke malengo na mikakati ya rasilimali zao kwa nguvu zote kwa ajili ya kuwalenga na kuwabakisha wateja bora na wanaovutia na kuhakikisha ya kuwa wanapanua msingi wa wateja ambao wataleta faida kubwa ndani ya mfuko hasa kukusanya michango itakayotunisha mfuko kwa muda marefu ili kutimiza ahadi za mafao ya muda mrefu na ya muda mfupi. Faida kubwa kwa mwanachama kama atapatiwa huduma bora anakuwa amezoea na huduma ya hali juu kwa kuridhika na kiwango cha huduma na jinsi mfuko unavyomjali. 

Matokeo yake ni kwamba mteja anakuwa hana muda wa kuhangaika wa kutafuta mfuko mwingine wa pensheni wa hifadhi ya jamii wa kuhamia wa kumpatia huduma bora zaidi hiyo anayopata. Gharama au bei ya huduma au bidhaa  siyo kwa kila kitu, mteja yaani mwanachama anabaki kuwa mwaminifu wa mfuko wa pensheni wa hifadhi ya jamii unaomridhisha na huduma anazotaka hata kama kutatokea na mfuko mwingine wa pensheni wa hifadhi ya jamii unaotoa huduma na bidhaa zinazofanana na kwa bei au gharama za chini. Na faida kubwa kwa mfuko wa kutoa huduma bora na hali ya juu ya kumjali mteja ni kwamba mteja aliyeridhika mara nyingi ni mtu ambaye atabaki kuwa mteja wako. Na jinsi ya kumpata mteja au mwanachama mpya kwa kawaida ni gharama za hali ya juu sana kuliko kumtunza na kumbakiza mteja au mwanachama uliyekuwa nawe tangia muda mrefu

Hivyo Mifuko ya Pensheni ya hifadhi ya jamii nchini inatakiwa kujiwekea malengo na mikakati mbalimbali ili kuleta ufanisi na tija katika shughuli za ulipaji wa mafao. Kwa mfano mfuko wa pensheni wa PSPF tangu kuundwa kwake umejiwekea malengo na mikakati mbalimbali ili kuleta tija na ufanisi katika shughuli za ulipaji mafao. ili kuweza kulibainisha hili, mfuko umeona ni muhimu kuwepo na mapatano ya utoaji wa huduma baina yake na mteja kwa kuanzisha mkataba wa huduma kwa wateja.

Mkataba huu wa PSPF unasema mapatano haya ni hatua muhimu sana katika utoaji wa huduma bora katika misingi ya uwazi na uwajibikaji. Kwa kufanya hivyo wateja wa PSPF watapata uhuru na uelewa wa kufahamu matarajio yake katika huduma fulani  na hasa viwango vya muda ambavyo vitamwezesha mwanachama kupanga mambo yake vyema badala ya kusubiri huduma bila kufahamu upatikaji wa huduma hizo na kwa viwango vipi.
Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa PSPF ndugu Adam Mayingu anasema mapatano haya yatamwezesha mwanachama kufahamu huduma za mfuko, viwango vya huduma na hatua atakazoweza kuzichukua iwapo viwango vya huduma vitakuwa kinyume na matarajio ya mkataba. 

“Hata hivyo, ili mfuko uweze kutoa huduma bora kwa wakati kama ilivyokusudiwa katika mapatano haya, tunategemea zaidi kupata mwitikio na ushirikiano kutoka kwa wateja ili kutimiza makubaliana haya. Mteja ndiyo kiungo muhimu katika kufanikisha utekelezaji wa malengo ya kila siku ya mfuko, kwa kuwa taarifa anazotoa ndizo zinazouwezesha mfuko kutoa huduma stahiki” Mayingu anasema.

Mkurugenzi mkuu anasema wana imani ya kwamba, kila mwanachama atatimiza wajibu wake ipasavyo ili aweze kupata huduma bora zinazotolewa kwa wakati muafaka, kwa heshima na kwa unyenyekevu. Hivyo, maoni ya mteja yatauwezesha mfuko kuongeza ubora wa huduma unazozitoa. 

Mfuko wa pensheni wa PSPF ulianzishwa kwa sheria ya mafao ya hitimisho la kazi kwa watumishi wa umma namba 2 ya mwaka 1999, sura ya 371. Tangu kuundwa kwake mfuko umejiwekea malengo na mikakati mbalimbali ili kuleta tija na ufanisi katika shughuli za ulipaji mafao ili kuweza kulibainisha hili, mfuko umeona ni muhimu kuwepo  mapatano ya utoaji wa huduma baina yake na mteja kwa kuanzisha mkataba wa huduma kwa mteja.  Dira ya mfuko ni “kuwa mtoa huduma bora kwa huduma za hifadhi ya jamii nchini”, wakati kwa upande wa dhima ni “kutoa huduma zenye ushindani katika sekta za hifadhi ya jamii kwa wateja kwa kutumia watumishi wenye ari ya kazi na teknolojia inayofaa”.

No comments :

Post a Comment