Monday, April 6, 2015

Mpango wa uchangiaji hiari kwa wote

Mmojawapo wa wajasiriamali wa maduka ya nguo nchini akijaza fomu ya kujiunga kuwa mwanachama wa mpango wa hiari wa mfuko wa pensheni wa PSPF ili kunufaika na mafao ya muda mrefu na mafao ya mfupi kama vile mikopo ya kukuza biashara na mikopo ya ada za shule na chuo
Idadi kubwa ya watanzania hawana elimu ya hifadhi ya jamii inayoweza kuwaelemisha juu ya mafao yanayotolewa, wajibu wao, na haki zao za pensheni kwa ujumla. Hivyo kuna haja kubwa hata kuelemishwa umma juu ya kujiunga na mifuko ya pensheni ya ziadi ya kujiunga kwa hiari hata kama ni wanachama wa wachangiaji wa mifuko hii ya lazima kisheria. 

Kufuatia kupitishwa na sheria ya mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii Sheria Na. 8 ya mwaka, 2008 mtu yeyote anaweza kujiunga na mfuko wowote wa pensheni ya hifadhi ya jamii. Uanachama kwenye mifuko ya ziada iliyoruhusiwa na SSRA kuanzishwa na mifuko hii ya pensheni ya hifadhi ya jamii ni ya hiari kwa mtu yeyote aliyeajiriwa au kujiajiri mwenyewe, mwanachama aliye katika mifuko mingine, na kwamba mwanachama wa mpango wa hiari anayo fursa ya kuhamia kwenye mpango wa uchangiaji kwa mujibu wa sheria.

Kila binadamu ana uhusiano mkubwa na hifadhi ya jamii iwe kinadharia au kivitendo kutoka kuzaliwa kwake mpaka kufa, binadamu mwenyewe lazima ajishughulishe na kazi hatarishi na kuugua magojwa mbalimbali   na kwa hiyo binadamu lazima akumbane na majanga mbalimbali kama vile majanga ya kiuchumi na ya kijamii yanayosababishwa na kukoma au kupungua kipato kutokana na maradhi, kujifungua mtoto, ajali za kuumia kazini, ukosefu wa ajira, ulemavu, uzee, kifo na kuongezeka kwa gharama za matibabu haya majanga yote ni matukio ya kila siku kwa binadamu ambayo hayatabiriki na yote yanaaangukia kwenye mpango wa hifadhi ya jamii. Hivyo ni kitu cha asili ya kwamba kila mtu lazima apewe hifadhi ya jamii na lazima aijue inamsaidiaje katika maisha yake ya kila siku kama sehemu ya maisha ya mwanadamu

Pamoja na hayo ikumbukwe ya kuwa pensheni zinazotolewa na mifuko iliyopo hapa nchini hazitoshelezi mahitaji ya watanzania wakiwemo wastaafu na familia zao.  Takwimu zilizotolewa mwaka 2012 zinaonesha ya kuwa ni watu milioni 1.7 tu ndio waliojiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii wakati idadi ya watanzania wote ni milioni 44.9 hii ikiwa ni asilimia 6.5 tu ya nguvu kazi yote ya watu milioni 23.7.  Hivyo ni kwamba asilimia 93.5 ya watanzania wote wanaotegemewa kuwa ni milioni 44.9 hawana kinga ya hifadhi ya jamii ya aina yeyote.

Hifadhi ya Jamii ni haki ya kila Mtanzania. Haki hii imeanishwa wazi katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 11(1) na Sera ya Taifa ya Hifadhi ya Jamii ya mwaka 2003. Haki hii pia imeiainishwa kwenye mkataba wa kimataifa wa haki za binadamu wa mwaka 1948 pamoja na mikataba ya shirika la kazi duniani (ILO) ibara ya 102 ya mwaka 1952.
Mfuko wa pensheni wa PSPF ni taasisi ya hifadhi ya jamii iliyoanzishwa kwa sheria Namba 2 ya mafao la hitimisho la kazi kwa watumishi wa umma ya mwaka 1999

Mabadiliko katika sekta ya hifadhi ya jamii nchini yamepelekea kuwepo na mabadiliko ya sheria ya mfuko wa pensheni wa (PSPF). Sheria ya Mfuko wa pensheni wa PSPF sasa unaruhusu kusajili wanachama katika sekta zote za umma na binafsi. Na kwa sasa mfuko una mipango miwili ya uchangiaji wa lazima yaani PSPF Mandatory Scheme na mpango wa uchangiaji wa hiari yaani PSPFSupplementary Scheme yaani kwa kifupi PSS

Mwanachama wa mpango huu anastahili kulipwa michango pamoja na faida itakayopatikana kutokana uwekezaji ambayo huwekwa katika akiba mara mbili kwa mwaka yaani kwa mwezi wa Januari na Julai.

Mpango huu wa hiari ni mahususi kwa ajili ya kuwapatia huduma ya hifadhi ya jamii wale wote ambao awali kutokana na matakwa ya kisheria hawakuweza kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii. Watanzania wanatakiwa kuitumia fursa hii kujiwekea akiba ya ziada hata kwa wale ambao tayari wamo katika mifuko mbalimbali ya hifadhi ya jamii hii itawasaidia kujiongezea na kutunisha na hivyo kunufaika na mafao ya muda mrefu na ya muda mfupi wakati wanapoendelea kufanya kazi na kuweza kuwa na akiba za ziada baada ya kustaafu.
.
Katika mpango huu wa uchangiaji wa hiari wa wa pensheni wa PSPF, mwanachama anapaswa kuchangia si chini ya Tshs 10,000 au zaidi kwa mwezi. Michango inaweza kuwasilishwa kwa siku, wiki, mwezi au awamu. Mwanachama anawekewa gawio la akiba yake kwa kila mwaka mara moja. Uanachama ni kwa watanzania wote na wasio watanzania wanaofanya kazi nchini na hata waliopo nje ya nchi.

Mpango huu wa hiari umeanzishwa na mfuko wa pensheni wa PSPF kwa ajili ya kupanua wigo wa uwanachama kwa kuandikisha wananchi waliojiajiri au kuajiriwa katika sekta rasmi na isiyo rasmi na kuwawezesha wale wote ambao hapo awali hawakuweza kupata huduma ya hifadhi ya jamii kutokana na kutokua na ajira

Hifadhi ya jamii ni haki ya kila mtu na si kwa wale tu walio katika ajira rasmi ila hata kwa wale waliojiajiri wenyewe na hata kwa wale ambao ni wanachama wa katika mifuko ya hifadhi ya jamii nchini kuweza kuwa na akiba ya ziada. 

Kwa sababu mpaka sasa kulingana na takwimu zilizotolewa mwaka 2012 idadi ya watanzania wote ni milioni 44.9 ambao kati yao watu milioni 1.7 tu ndio waliojiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii, hii ikiwa ni asilimia 6.5 tu ya nguvu kazi yote ya watu milioni 23.7 na ndiyo maana mfuko wa pensheni PSPF wana mpango wa uanachama wa hiari kama mkakati wa makusudi juu ya kupanua wigo wa hifadhi ya jamii ili kuhakikisha ya kuwa hata wale waliojiajiri kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii kwa hiari na hata wale wanachama wa mifuko iliyopo kuweza kuwa na akiba ya ziada ya kutosha kwa baadaye.

Uanachama wa mpango huu wa hiari wa PSPF ni kwa raia na asiye raia wa Tanzania anayefanya kazi nchini na nje ya nchi hivyo hauna ubaguzi nchi wala wa rangi ya mtu. Mfanyakazi anapaswa kuwa mwanachama wa mfuko mmoja tu katika mpango wa lazima, lakini ana haki ya kujiunga na mpango wa hiari zaidi ya mmoja kama huu wa mfuko wa pensheni wa PSPF.

Aina za mafao yanayo tolewa na mpango huu wa hiari chini ya mfuko wa pensheni wa PSPF ni kama vile fao la uzeeni, fao ya kuumia kazini, fao la kifo, fao la elimu, fao la ujasiriamali, fao ya urithi, fao ugonjwa/ulemavu, na fao la kujitoa. Mafao haya hutolewa na kunufaika sawasawa bila kujali ya kuwa mwanachama anachangia kwa hiari au kwa lazima kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii.

Hivyo mtu yeyote aliyejiajiri, mkulima, mvuvi, mfanyakazi wa ndani, wafanya biashara wadogo wanaweza kujiandikisha kwa hiari na kulipa kadri ya uwezo wake wa mapato kwenye mfuko wa pensheni wa PSPF. Uchangiaji katika mpango huu wa hiari wa PSPF wanachama wana uhuru wa kuchagua jinsi ambavyo wanaweza kuwasilisha michango yao, iwapo ni kwa wiki Mwezi au kwa msimu kutegemea na upatikanaji wa kipato cha ziada kwa ajili ya akiba na michango huwasilishwa moja kwa moja kupitia akaunti ya benki au wakala wa malipo wa M-pesa, Tigo-pesa na Airtel money.
“Nimejiunga kuwa mwanachama wa hiari katika Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kwa kuwa kuna utaratibu baada miezi 12 ambapo unaweza kuchukua fedha zako za kuanzishia biashara au kulipia ada za watoto shuleni au chuoni,” anaanza kueleza mfanyakazi wa shirika la  bandari Tanzania ambaye hakutaka kutaja jina lake alipozungumza na gazeti hili la majira
Mwanachama huyu ambaye ni mwanachama wa mfuko wa hiari wa PSPF ambaye yuko kituo cha bandari ya Mtwara, anasema ni muhimu kwa wajasiriamali na watu wengine walio katika sekta isiyo rasmi kujiunga na mfuko huu wa PSPF ili waweze  kunufaika na fursa mbalimbali zilizopo kwa kwamba yeye ana wasilisha michangi yake kwa wiki, mwezi au msimu kutegemeana na upatikanaji wa kipato cha ziada kwa ajili ya akiba.

Mtu yeyote anaweza kuwa mwanachama kwa kujiunga na mpango huu wa hiari kwa kujaza formu PSS FN.1 na kuambatanisha picha moja ya rangi yaani passport size pamoja na taarifa muhimu za wanachama kama vile; majina; tarehe ya kuzaliwa;  anwani na nambari za simu; shughuli au kazi na mara baada ya kukamilisha usajili, mwanachama hupewa kitambulisho na nambari ya uanachama

Katika mpango huu wa uchangiaji hiari wa mfuko wa pensheni wa PSPF mwanachama akisha anza kuchangia naye anakuwa na haki ya kupata mafao yote yatolewayo na mpango huu wa hiari wa PSPF. 

Mafao katika mpango huu wa hiari mwanachama huwa anastahili kulipwa michango pamoja na riba inayokokotolewa kwa mujibu wa viwango vya riba vilivyoko katika soko kulingana na mfumuko wa bei na kwamba riba ambayo ni asimilia sita (6) huongezwa katika akiba ya mwanachama mara mbili kwa mwaka katika miezi ya Januari na Julai. Mwanachama wa mpango huu wa hiari wa PSPF anapolazimika kuchukua michango yake yote na faida kutokana na sababu zozote zile, anaweza tena kuchangia upya bila masharti yoyote.

Tangu kuzinduliwa kwake mapema machi 7 mwaka 2013 tayari wanachama zaidi ya 5,000 wamejiunga na mpango huo wa hiari ambapo makundi zaidi ya 25 yamejiunga na mfuko huu kutokana na ubora wa mafao yake na mikopo inayotolewa kwa wanachama waliojiunga na mfuko huo kwa miaka mitano tofauti na wakati wa nyuma ambapo mikopo ya nyumba ilitolewa kwa wanachama waliobakiza miaka mitano ya kustaafu

No comments :

Post a Comment