Saturday, April 4, 2015

KUZUIA IRAN KURUTUBISHA NYUKLIA


MIILI YA WATU WANNE YAKUTWA KATIKA GHOROFA LILILOANGUKA

BAHARIA AISHI BAHARINI MIEZI MIWILI KWA KULA SAMAKI WABICHI BAADA YA BOTI YAKE KUPINDUKA

Baharia mmoja wa Marekani ameishi kwa miezi miwili baharini baada ya kupotea huku akiishi kwa kula samaki wabichi na kunywa maji ya mvua.

Baharia huyo Louis Jordan mwenye umri wa miaka 37, alipatikana na meli ya Ujerumani iliyokuwa ikipita umbali wa maili 200 kutoka pwani ya North Carolina siku ya Alhamisi.

Baharia huyo alipotea baharini baada ya boti lake la futi 35, kupinduliwa na mawimbi, ambapo Jordan alikutwa ameka juu ya boti hilo lililopinduka juu chini.

AMBER ROSE ATAKA KURUDIANA NA MUMEWE WIZ KHALIFA

Inaonekana mbunifu wa mavazi, modo, rapa na muigizaji Amber Rose na mumewe rapa Wiz Khalifa wanaweza kumaliza tofauti zao kwa ajili ya manufaa ya mtoto wao ambaye walikuwa wakigombea kumlea.

Amber Rose ametumia Instagram yake kutoa ujumbe mzito wa mahaba kwa mumewe huyo mtata akisema kuwa Wiz Khalifa ndiye mpenzi wa maisha yake.

Amber aliyeomba talaka mwezi Septemba ikiwa ni chini ya mwaka mmoja tu tangu waoane, lakini sasa ameonyesha kubadili moyo wake kutokana na kusema hamna mwanaume anayemfanya awe na furaha kama Wiz Khalifa.


No comments :

Post a Comment