Sunday, June 29, 2014

PSPF, TPB Wazindua mpango wa kukopesha wanachama wastaafu


Mstaafu ambaye pia ni Mwanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Eunice Temu, akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa huduma ya "Wastaafu Loan" itakayotolewa na Mfuko huo kwa wanachama wake wastaafu kupitia benki ya Posta Tanzania (TPB). Hafla hiyo iliyoongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi (Mstaafu), Philemon Luhanjo, ilifanyika kwenye ukumbni wa nhoteli ya Belmonte iliyoko jengo la PSPF Jubilee Tower katikati ya jiji Ijumaa Juni 29, 2014. Huduma hiyo ni ya kwanza kutolewa na Mifuko ya Pensheni hapa nchinina una lengo la kutoa mikopo nafuu ili kuwawezesha wastaafu kukidhi mahitaji ya kifedha na kuboresha maisha yao, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Adam Mayingu alizungumza katika hotuba yake

Baadhi ya maafisa wa benki ya posta Tanzania (TPB) na wenzao wa PSPF, wakifuatilia magtukio yaliyokuwa yakitokea kwenye uzinduzi huo

Katibu Mkuu Kiongozi (Mstaafu), Philemon Luhanjo (Kulia), akiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu (Kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, mara baada ya kumalizika kwa hafla ya uzinduzi wa huduma ya "Wastaafu Loan" jijini Dar es Salaam Juni 20, 2014

Katibu Mkuu Kiongozi (Mstaafu), Philemon Luhanjo (Wapili kushoto-Waliokaa), Mkurugenzi Mkuu wa TPB, Sabasaba Moshingi (Wakwanza kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu (Watatu kushoto) na Mstaafu Eunice Temu, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wastaafu wa kwanza kufaidika na mikopohiyo

Mgeni rasmi na viongozi wa PSPF na TPB akiwa katika pichas ya pamoja na wakurugenzi wa idara wa PSPF, na TPB.

Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa PSPF na TPB


Katibu Mkuu Kiongozi (Mstaafu), Philemon Luhanjo, akitoa hotuba ya uzinduzi wa mpango huo


Katibu Mkuu Kionmgozi (Mstaafu), Philemon Luhanjo (Wapili kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayigu(Wapili kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, (TPB), Sabasaba Moshingi), Wakwanza kulia) na Mstaafu Eunice Temu, wakiwa wamenyanyua juu mikono kuashiria uzinduzi wa mpango wa mfuko huo kuwakopesha wastaafu amabao ni wanachama wake kupitia benki ya Posta "Wastaafu Loan",. Hafla ya uzinduzi huo ulifantyika jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, akitoa hotuba kuelezea huduma hiyo mpya ya "Wastaafu Loan"

Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi, akitoa hotuba yake.

No comments :

Post a Comment