Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya
wasichana, Marian, iliyoko Bagamoyo mkoani Pwani, ambao wanasoma na kulipiwa
ada na PPF kupitia fao la elimu baada ya wazazi wao kufariki dunia, kutoka
kushoto na madarasa yao kwenye mabano ni Debora Kibona (Kidato cha tatu),
Eileen Amon Urio, (Kidato cha tatu) na Rosalia Faustin Madulu (Kidato cha
Kwanza)
Na Christian Gaya, majira machi 17, 2014
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Kanisa Katoliki, Muadhama Policarp Kadinali Pengo ameupongeza mfuko wa pensheni wa PPF kwa udhamini wa siku ya familia wa shule za Marian zilizopo Bagamoyo mkoa wa Pwani, na jinsi alivyofurahishwa na juhudi za Marian zilizoanza kujenga chuo kikuu cha sayansi cha Marian Bagamoyo
Na Christian Gaya, majira machi 17, 2014
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Kanisa Katoliki, Muadhama Policarp Kadinali Pengo ameupongeza mfuko wa pensheni wa PPF kwa udhamini wa siku ya familia wa shule za Marian zilizopo Bagamoyo mkoa wa Pwani, na jinsi alivyofurahishwa na juhudi za Marian zilizoanza kujenga chuo kikuu cha sayansi cha Marian Bagamoyo
Shule ya Marian iliyoko Bagamoyo mkoa wa Pwani imeshaanza tayari kujenga chuo kikuu cha sayansi ikiwa na lengo la kuwapa motisha kwa wanafunzi wanaopenda kujiendeleza na masomo ya sayansi na kutimiza ndoto zao za kuwa wanasayansi wanaotegemewa na jamii ya Kitanzania. Haya yalitamkwa na meneja wa shule za marian nchini padri Valentiono Bayo Siku ya Familia ya Marian iliyokuwa imedhaminiwa na Mfuko wa Pensheni wa PPF.
Alisema wazo la kuanzisha chuo kikuu cha sayansi lilianza
tangia miaka 13 iliyopita (2003) na kwa miaka yote utawala na uongozi wa marian
umekuwa ukiandaa na kutimiza mipango na kwamba mpaka sasa majengo ya kemia,
fizikia na bailojia yako hatua ya juu zaidi
“Tunalenga kutoa wanasayansi wa kutosha kwa siku zijazo.
Kwa kufanya hivi tunaiunga mkono serikali kwa vitendo katika zake juhudi na
nguvu zake za kuendeleza sekta ya sayansi na kuwa na wanasayansi wa kuaminika
nchini” anasema Bayo.
Kulingana na Bayo chuo kikuu kitakuwa sehemu ya shule za
marian nchini ili kuwezesha kutoa elimu kutoka shule ya awali mpaka hatua ya
juu
“Chuo kikuu hiki kitaanza chini ya mwavuli wa chuo kikuu
cha St Augustine Tanzania (SAUT). Shule
ya marian ilianza na wanafunzi 42 na wanafunzi 4 kwa mwaka 2007 lakini mpaka
sasa shule za marian imeandikisha
wanafunzi wapatao zaidi ya 1,000.” Alibainisha.
Kwa upande wa meneja wa uhusiano na masoko wa PPF Bi Lulu
Mengele anasema mpaka sasa mfuko wa pensheni wa PPF umetumia shilingi za
kitanzania zipatazo bilioni 4.6 kutoka katika mfuko wa elimu wa kudhamini
watoto wa wanachama wa PPF waliofiwa na wazazi wao wanaosoma shule mbalimbali hapa nchini
zikiwemo shule za Marian tangia mwaka 2003
Lulu anasema PPF ni mfuko wa pekee nchini unaotoa fao
hili la elimu ambalo hutolewa kwa watoto wa mwanachama anayefariki akiwa katika
akiwa katika ajira na tayari amekwisha changia miaka 3 au zaidi.
“Kwa muda wa miaka ipatayo 11 sasa tumekuwa tukitoa
udhamini wa elimu kwa wanafunzi. Kwa mfano mwaka jana 2013 mfuko ulitumia
shilingi milioni 813 kwa ajili ya kununuliwa vifaa na kulipia ada za wanafunzi
wapatao 1,467 kuanzia shule ya awali mpaka sekondari” alisema. Wakati kwa mwaka
2012 pekee Mfuko ulisomesha watoto 1,333 kwa kuwalipia jumla ya shilingi
milioni 682 katika shule 765 kutoka Tanzania Bara na Visiwani katika shule za
msingi na sekondari.” Lulu anabainisha
“Elimu
ni nyezo muhimu katika maisha ya binadamu. Kutokana na nguvu ya elimu katika
kukuza uchumi wa nchi, mataifa mengi duniani yaliyopata maendeleo ya kijamii na
kiuchumi yamewekeza katika sekta ya elimu. Hakuna taifa lolote duniani ambalo
linaweza kupata maendeleo bila watu wake kuwa na elimu na kwa maana hiyo hakuna
maendeleo bila elimu. Elimu ndiyo inamfanya binadamu kuwa daktari, rubani,
mhandisi na mtaalamu katika nyanja mbalimbali. Kwa kutambua hilo uwekezaji
katika sekta hiyo umekuwa ukiongezeka. Leo hii kumesikika vilio vingi nchini
vikilenga mazingira bora na fursa zaidi katika sekta ya elimu vinavyotokana na
watu wengi kutambua nguvu ya elimu kwa vizazi vijavyo. Mfuko wa Pensheni wa PPF
kwa kutambua umuhimu wa elimu mwaka 2003 ulianzisha fao la elimu. Sababu ya
msingi iliyousukuma Mfuko huo kuanzisha fao hilo ni kutokana na umuhimu wa
watoto wa mwanachama kuendelea kupata elimu hata baada ya mzazi wao kufariki”
Anasema.
Lulu anaeleza ya
kuwa Mfuko wa pensheni wa PPF ulianzisha fao la elimu kwa kuanza na watoto
watatu ambao wazazi wao walifariki wakiwa katika ajira. Kuweza kubuni na kutoa
fao la elimu kwa watoto wa Wanachama wenu waliofariki wakiwa kazini kwa kipindi
cha miaka 11 sasa. Kwa kufanya hivi
mfuko wa pensheni wa PPF umewezesha watoto hawa kupata elimu, ambayo huenda
wengeikosa kwa vile tu wazazi wao wametangulia mbele ya haki, na kwa rasilimali
watu iliyoelimika kwa siku za usoni kwa taifa.
Anaendelea
kufafanua ya kwamba fao la elimu ni kati ya mafao saba yanayotolewa na
Mfuko. Anasema fao hili hujumuisha
ulipaji wa karo za shule na mahitaji mengine ya mwanafunzi husika yaani
kwa mtoto wa mwanachama aliyefariki kama vile sare, vifaa, usafiri na
chakula kwa kuzingatia mshahara wa mzazi aliyekuwa mwanachama wa PPF.
“Gharama za ada na matumizi mengine
hulipwa moja kwa moja kwenye shule ambazo watoto wanasoma bila kupitia kwa
mzazi aliyebaki au mlezi, jambo ambalo linatoa uhakika kwamba fedha zinatumika
kwa matumizi yaliyokusudiwa. Sababu za mfuko kuamua kuanzisha fao la elimu ni
baada ya mfuko wa PPF kufanya utafiti yakinifu na kugundua kuwa watoto wengi wa
wanachama wao wanashindwa kuendelea na masomo baada ya wazazi wao kufariki kwa
kushindwa kulipa ada za shule na mahitaji mengine muhimu. Na imechangiwa na kwamba
wengi wa ndugu wa marehemu na wasimamizi wa mirathi kuwa na vipaumbele vyao
tofauti, ikiwemo kugawa urithi bila kuwawekea elimu kama kipaumbele kwa watoto
wengi wa wanachama aliyefariki wakati yuko kazini.” Lulu anasema ambaye ndiye
meneja uhusiano na masoko wa PPF.
Anabainisha ya kuwa fao la elimu
hutolewa kwa watoto wasiozidi wanne wa mwanachama aliyefariki akiwa katika
ajira baada ya kuchangia katika mfuko huo kwa miaka mitatu au zaidi. Fao hilo la
elimu ni kati ya mafao saba yanayotolewa na mfuko wa pensheni wa PPF na
limewavutia wengi wanaotambua nguvu ya elimu na kujiunga na PPF ili
waweze kufaidika na fursa zinazotolewa na Mfuko huo likiwamo fao la elimu
linalotolewa baada mwanachama kufariki.
Ikumbukwe katika
sherehe ya kutimiza miaka kumi tangia kuanzishwa kwa fao hilo pia kulikuwa na
shuhuda za wanafunzi waliosomeshwa na wanaosomeshwa na Mfuko akiwemo Pascalia
Thobias (19) wakati huo ambaye alikuwa amekata tamaa baada ya baba yake
kufariki akiwa darasa la nne. Alisema, “Baba alipofariki nilijua ndio mwisho
wangu wa kupata elimu kwa sababu baba ndiye aliyekuwa akifanya kazi na mama
hakuwa na kazi ya kumuingizia kipato, nilijua kuwa huo ndiyo mwisho wa elimu
yangu. Ila PPF ilianza kunilipia ada toka mwaka 2003 nikiwa darasa la nne mpaka
kidato cha nne ambapo niliweza kufaulu vizuri” kwa kupata daraja la kwanza.
Rosalia Madulu
mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Marian ambaye alihudhuria Siku ya Familia ya
Marian naye anaushukuru mfuko wa PPF kwa kuendelea kumdhamini katika masomo
yake tangia mwaka 2007 wakati yuko darasa la II mara tu baba yake alipofariki.
“Baada ya kufa
baba yangu mama alikata tamaa juu ya kunisomesha mimi pamoja na ndugu zangu
wengine, lakini tunashukuru PPF kwa kutushika mikono yetu wanafamilia wote na
kutupa nguvu kuanzia wakati huo mpaka leo.” Rozalia anasema.
Lulu anasema suala la maamuzi ya mirathi limeendelea kusababisha
ucheleweshaji wa mafao yanayotakiwa kutolewa na Mfuko kwa wasimamizi wa mirathi
au wategemezi pale mwanachama anapofariki akiwa katika ajira. Hivyo basi, ni
vyema wanachama wetu wote wajenge tabia ya kuandika wosia na hii itasaidia
kupunguza na kuondoa malumbano ya mirathi ambayo imekuwa ni kero kwa wajane na
watoto wa marehemu
“Fao la elimu hutolewa ili
kugharamia sehemu au gharama zote zinazohitajika katika elimu ya mtoto wa
mwanachama aliyefariki na gharama hizi
ni kuanzia elimu ya chekechea hadi kidato cha sita. Mfuko
huu ulifikia uamuzi wa kuwasomesha watoto hao kutokana na kuwepo kwa tatizo kwa
wasimamizi wa mirathi pindi wazazi wa watoto hao wanapopoteza maisha”. Lulu
anasema.
Anasema ili fao hilo litolewe kinachohitajika ni kwa
mwajiri anatakiwa kutoa taarifa PPF pindi mfanyakazi wake aliyekuwa mwanachama wa mfuko wa
pensheni wa PPF anapofariki dunia pamoja na nakala ya cheti cha kifo na maelezo
muhimu kuhusu mtoto au watoto wa marehemu majina kamili na majina ya shule .
Lulu anasema ya kuwa kila mtoto anagharamiwa na mfuko wa
pensheni wa PPF kiasi kisichozidi 1/12 ya mshahara wa mwaka wa mwanachama
aliyefariki akiwa katika ajira. Na kiasi hicho hutolewa kila mwaka kwa kila
mtoto katika shule anayosoma mtoto ili kugharamia mahitaji ya elimu ya mtoto
yanayohitajika katika shule hiyo
Sifa na utaratibu wa utoaji wa fao la elimu pamoja na
nyaraka zinazohitajika ni rahisi sana kwa wanachama na familia zao
kuzipata kwa “mfano mara wanapopata fomu
ya maombi ya mafao ya elimu kutoka kwa mwajiri wa marehemu aliyekuwa mwanachama
wa mfuko, maelezo ya shule anayosoma kila mtoto ikiwemo pia akaunti ya shule
hiyo pamoja na nakala ya cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa kwa kila mtoto
malipo yanaandaliwa mara moja na kuingizwa kwenye akaunti husika” Bi Lulu
anasema
Anaeleza kuwa gharama za ada na matumizi
mengine hulipwa moja kwa moja kwenye shule ambazo watoto wanasoma bila kupitia
kwa mzazi aliyebaki au mlezi, jambo ambalo linatoa uhakika kwamba fedha
zinatumika kwa matumizi yaliyokusudiwa.
Lulu anasema PPF imekuwa ikibeba
majukumu ya mzazi ambaye amefariki akiwa kazini, kwa kuhakikisha watoto wake
wanaendelea kupata elimu. Anatoa wito kwa wananchi kujiunga na PPF ili waweze
kufaidika na mafao yanayotolewa na mfuko huo, likiwamo fao la elimu kwani
limekuwa mkombozi kwa wanafunzi wengi nchini
Anaongeza kuwa mafanikio ya fao hilo
hayapo tu katika idadi ya wanafunzi wanaowasomesha, bali pia katika matokeo ya
mitihani yao baadhi ya watoto wanaofaidika na fao hilo hufaulu vizuri. "Kwa
mfano katika matokeo ya mitihani ya kidato cha nne mwaka 2012 na 2013 miongoni
mwa wanafunzi waliofaulu kwa kiwango cha daraja la kwanza na la pili wapo
wanaosomeshwa na PPF," anasema.
Anabainisha kuwa mbali na mafanikio
hayo, pia fao hilo linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwamo baadhi ya
shule kushindwa kutuma ripoti za mitihani kwa PPF ambazo zingesaidia kutambua
maendeleo ya wanafunzi hao, ili kujua namna bora zaidi ya kuboresha utoaji wa
fao hilo
Lulu anawaomba
wananchi wote kutoka katika sekta iliyo rasmi na isiyo rasmi na hata kwa wale
waliojiajiri wenyewe na hata ambao ni wanachama wa mifuko mengine ya hifadhi ya
jamii kujiunga na Mfuko wa Pensheni wa PPF kwa kutumia mfumo wa uwekezaji amana
kama mfumo wa ziada kwa wanachama walio katika mfumo wa asili wa pensheni au
walio katika mifumo ya lazima ya hifadhi ya jamii ili waweze kufaidika na fao
la elimu na kuhakikisha maisha bora ya sasa na ya baadaye.
Changamoto nyingine ni katika kupata
uhakika kuwa wanaosomeshwa ni watoto wanaostahili na si watoto wengine kwa
majina ya watoto wa marehemu, hivyo inalazimu PPF kufanya uhakiki wa mara kwa
mara jambo ambalo ni gharama kubwa.
Anasema waajiri wanatakiwa kutokuchelesha
kutuma taarifa za vifo vya wafanyakazi wao mara wanapofariki. "kwa
sababu wasipotuma mapema inasababisha watoto wa marehemu wanachama kuchelewa
kulipiwa ada, hususan pale kifo kinapotokea wakati mwaka mpya wa masomo” Lulu
anasisitiza. Na changamoto nyingine ni kupata uhakika kuwa wanaosomeshwa ni
watoto wanaostahili na si watoto wengine kwa majina ya watoto wa marehemu hivyo
inalazimu PPF kufanya uhakiki wa mara kwa mara jambo ambalo ni gharama kubwa.
Lulu ambaye ni meneja wa mawasiliano na
masoko kwa niaba ya mkurugenzi mkuu wa
mfuko wa pensheni wa PPF anawashauri watanzania ambao hawajajiunga na Mfuko huu
kufanya hivyo mapema ili waweze kuwa sehemu ya wale wanaofaidika na mafao
yanayotolewa ikiwa ni pamoja na fao la elimu. Anasema pia kwa ushirikiano wa
uongozi, wafanyakazi, wanachama na wadau wote wa sekta ya hifadhi ya jamii
nchini PPF itaendelea kuboresha huduma zake kwa wateja kama ilivyo kawaida yake
kama ilivyofanya kwa kipindi chote chote cha miaka 35, tangu ilipoanzishwa
mwaka 1978 hasa kwa kuhakikisha ya kuwa fao la elimu linatolewa kwa wakati na
linaendelea kuwa bora zaidi.
Mfuko wa Pensheni wa PPF ulianzishwa
Julai 1978 kwa sheria Namba 14 ya mwaka 1978 ambayo sasa inafahamika kama mfuko
wa pensheni wa PPF yaani “PPF Pensions Fund Act” Sura ya 372 ya sheria
za nchi yetu kama ilivyorekebishwa na sheria namba 5 ya mwaka 2012 kwa
madhumuni ya kutoa mafao ya uzeeni na mafao mengine kwa wanachama wa
Mfuko. PPF ilianza ikiwa chini ya
usimamizi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) kama Mfuko wa kwanza wa kuchangia wa Pensheni Tanzania kwa madhumuni ya
kuandikisha wanachama, kukusanya michango, kuiwekeza pamoja na kulipa mafao ya
muda mrefu na ya muda mrefu.
Mfuko huu wa PPF ulianzishwa ili kutoa huduma ya
pensheni kwa wanachama katika utaratibu wa kuchangia. Huu ndio Mfuko wa kwanza
wa pensheni Tanzania ulioanzishwa katika misingi ya kuchangia. Sheria ya Mfuko
inaruhusu wanachama kutoka katika sekta rasmi na sekta isiyo rasmi kujiunga na
Mfuko.

No comments :
Post a Comment