Na Idda Mushi: 4th November 2012
Maoni
Nicholaus Mgaya
Sera za mifuko mingi ya hifadhi ya jamii nchini,
zimewekwa kwa ajili ya kulinda maslahi ya mifuko hiyo na si
kuwanufaisha wafanyakazi .
Hayo yalielezwa na Katibu Mkuu wa
Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA) Nicholaus Mgaya
kwenye warsha ya viongozi wa juu wa chombo hicho inayofanyika mjini
Morogoro.
Alisema sera ya Shirika la Kazi Duniani
(ILO) inasema kwa mifuko ya hifadhi ya jamii kukidhi mahitaji ya
wafanyakazi ni lazima kuwa na mafao yasiyopungua tisa, lakini kwa
Tanzania mifuko mingi ina mafao matatu pekee.
Alisema isipokuwa Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) ndilo pekee lenye mafao saba.
Alisema mifuko inakinzana na mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umaskini (MKUKUTA ).
Mgaya alilizungumzia fao la kujitoa kuwa
ni suluhisho pekee la kumkomboa mfanyakazi kutoka katika umaskini pale
anapoachishwa au kufukuzwa kazi .
Katika hatua nyingine, Mwenyekiyi wa
Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Dk Diwani Mrutu
aliwataka watendaji wakuu wa vyama vya wafanyakazi nchini kuhakikisha
wanakusanya michango na ada za vyama vyao ili kusaidia shirikisho hilo
kujiendesha lenyewe,
Alisema shirikisho hilo linatakiwa kujiendesha kwa kutegemea michango na ada za wanachama wao.
Aidha aliwaonya viongozi wa wafanyakazi
ambao wamegeuka wasaliti wa shirikicho hilo kuacha kufanya hivyo kwani
ikibidi watatajwa hadharani na na kupigiwa kura za kuwaondoa
madarakani.
No comments :
Post a Comment