Friday, October 20, 2017

LUPITA NYONG'O AVUNJA UKIMYA NA KUSEMA WEINSTEIN ALITAKA KUMRUBUNI

Nyota wa filamu wa Hollywood Mkenya Lupita Nyong'o amekuwa miongoni mwa wanawake waliojitokeza hadharani kumtuhumu bilionea Mtayarishaji filamu Harvey Weinstein kwa kumtaka kimapenzi ili amsaidie kumtoa katika filamu.

Lupita mshindi wa tuzo ya Oscar kwa uhusika wake kwenye filamu ya '12 Years a Slave', ameeleza kuwa bilionea huyo alijaribu kumshawishi kufanya naye mapenzi wakati akiwa mwanafunzi muigizaji katika shule ya Uigizaji ya Yale.

Lupita amesema alikutana na Weinstein mwaka 2011 katika tamasha la filamu na kumualika nyumbani kwake kwenda kuangalia filamu mpya aliyoitayarisha, ambapo alikubali na kwenda kuangalia.

Amesema wakiwa nyumbani waliangalia filamu hiyo na watoto wake, kisha akamuita Lupita akampeleka katika chumba na kumuambia anataka kumfanyia masaji, jambo ambalo Lupita alidhani kuwa ni mzaha.

Lupita katika kujaribu kujiokoa akamtaka Mtayarishaji huyo ndiyo alale chini ili amfanyie masaji ili iwe rahisi kumdhibiti iwapo atataka kumbaka kuliko yeye kulala chini na Weinstein kumfanyia masaji jambo ambalo lingemuhatarisha.

Wakati Lupita akimfanyia masaji Weinstein, alitaka kuvua suruali yake ili amfanyie masaji sehemu ya chini ya kiuno, ndipo Lupita alipogoma na kumuambia hatojisikia vizuri na baada ya hapo waliagana na kuondoka.
  Mtayarishaji filamu bilionea Harvey Weinstein anakabiliwa na tuhuma za kuwadhalilisha kingono waigizaji filamu wakike kadhaa

No comments :

Post a Comment