Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey
Mwanry ambaye alikuwa ni Mwenyekiti wa mkutano wa ujirani mwema wa Mikoa
11 akitoa tamko la kumpongeza Rais Magufuli, kulia kwake ni Mwenyeji wa
Mkutano huo Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi.
Wajumbe wa kamati za Ulinzi na
Usalama za mikoa 11 iliyoshiriki Mkutano wa Ujirani mwema wakifurahia
mada zilizowasilishwa katika Mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa
ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida.
Wajumbe wa kamati za Ulinzi na
Usalama za mikoa 11 iliyoshiriki Mkutano wa Ujirani mwema wakifuatilia
mada zikiwasilishwa katika Mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa
ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey
Mwanry (katikati) ambaye alikuwa ni Mwenyekiti wa mkutano wa ujirani
mwema wa Mikoa 11 akipokea maoni na mawazo ya wajumbe wa kutano huo,
kulia kwake ni Mwenyeji wa Mkutano huo Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.
Rehema Nchimbi.
Mwenyeji wa Mkutano wa ujirani
mwema baina ya mikoa 11, Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi
akizungumza na wajumbe wa mkutano huo.
……………………………………………………………………………..
race Singida.
Wakuu wa Mikoa 11 wametoa tamko la kumpongeza Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kutokana na kazi ya
kizalendo ya kutetea na kulinda rasilimali za Watanzania kwa maslahi ya
taifa zima.
Tamko hilo limetolewa jana jioni
wakati wakuu hao wakihitimisha mkutano wa kawaida wa
ujirani mwema baina
ya mikoa hiyo ambao umefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya
Mkuu wa Mkoa wa Singida.
Wakiongozwa na Mwenyekiti wa
mkutano huo ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanry wakuu wa
mikoa ya Singida, Rukwa, Katavi, Kagera, Dodoma, Manyara, Geita,
Shinyanga, Mwanza na Kigoma wamesema wanamuunga mkono Rais na
wataendelea kuzingatia maelekezo yake katika utendaji wao.
“Sisi wasaidizi wake (rais
Magufuli) tutaendelea kutekeleza na kuzingatia maelekezo katika
utendaji wetu wa kila siku. Aidha, wakati wote tutakuwa pamoja na
wananchi na kuwatumikia kwa kutimiza wajibu wetu kwa uaminifu, uadilifu
na tutahakikisha maslahi ya wananchi na taifa yanapewa kipaumbele cha
kwanza”, sehemu ya nukuu ya tamko hilo.
Katika tamko hilo pia wametoa
wito kwa wananchi na wawekezaji wote halali wa ndani na nje ya nchi
kumuunga mkono rais Magufuli kwa kazi nzuri ya kulinda rasilimali za
taifa na wakati wote wazingatie sheria za nchi.
“Tutumie fursa nyingi
zinazoendelea kutengenezwa kwa hatua hizo za kizalendo anazochukua
mheshimiwa mpendwa wetu rais Dkt. Magufuli Kwa mafanikio, maendeleo na
tija kuelekea Tanzania ya uchumi wa kati na uchumi wa viwanda”, sehemu
nyingine ya tamko hilo.
Katika Mkutano huo Mwenyekiti
Mwanry amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Singida kwa kuandaa mkutano huo na
kupendekeza mikutano ya ujirani mwema ya mikoa ifanyike kikanda ili
kuimarisha ulinzi na usalama wa taifa pamoja na kubadilishana uzoefu na
kupeana taarifa mbalimbali za kimaendeleo.
“Tumekutana hapa kwa mapenzi ya
nchi yetu na ya rais wetu Magufuli. Tuliokutana leo hii changamoto za
mikoa yetu zinafanana. Changamoto hizi ni pamoja na uharibifu wa
mazingira, uhaba wa mvua, kilimo cha kuhama hama na uhamiaji haramu”,
amesema Mwanry na kuongeza;
“Kwa hiyo tukiacha kila Mkoa
utatue changamoto hizi kivyake hatutafanikiwa kizitatua. Tumekubaliana
kukutana mara kwa mara ili changamoto zinazotukabili sote tuzipatie
ufumbuzi wa kudumu kwa pamoja”.
Aidha, mwenyekiti huyo amesema
wamekubaliana kusimamia matumizi bora ya ardhi pia kusimamia ulinzi na
usalama hasa kwa Mikoa ile iliyopo mipakani na nchi jirani.
Kwa upande wake Mwenyeji wa
Mkutano huo Dkt Rehema Nchimbi amesema mkutano huo umekua wa manufaa
makubwa kwa mikoa iliyohudhuria pamoja taifa kwakuwa wameweza
kubadilishana mawazo kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wote.
No comments :
Post a Comment