Monday, May 1, 2017

Uhuru raises minimum wage by 18 per cent

Workers follow the proceedings of a COTU meeting. The minimum wage has been raised by 18 per cent. PHOTO | DENNIS ONSONGO | NMG Workers follow the proceedings of a COTU meeting. The minimum wage has been raised by 18 per cent. PHOTO | DENNIS ONSONGO | NMG 

Wafanyakazi Wakipita Mbele Ya Rais Magufuli


ESRF YAKUTANISHA WADAU KUIJADILI BAJETI YA 2016/2017 KATIKA SEKTA ZA ELIMU NA KILIMO

Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) imewakutanisha wadau mbalimbali wa maendeleo nchini kuijadili bajeti ya Tanzania ya mwaka wa fedha 2016/2017 ambao unaelekea kuisha.

Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida alisema mdahalo huo ni sehemu ya shughuli ambazo zinafanywa na ESRF ili kutazama ni njinsi gani Taasisi inaweza kuisaidia Serikali kuweka mipango thabiti kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

Dkt. Kida alisema mdahalo huo ulihusu bajeti ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kuangalia utekelezaji wa bajeti zilizopitishwa kwa mwaka wa fedha 2016/2017, changamoto zilizopo na nini kifanyike katika bajeti ya 2017/2018.
Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida akitoa neno la ufunguzi.

“ESRF imekuwa ikishirikiana na wadau ili kuangalia ni jinsi gani tunaweza kusaidia mchakato wa maendeleo wa nchi yetu kwa njia ya utafiti mbalimbali, uchambuzi na utayarishaji wa sera na kuongeza wadau uwezo kupitia mafunzo mbalimbali.

“Kama jinsi mnavyojua nchi yetu imekuwa na mipango ya maendeleo ambayo inatekelezwa kupitia bajeti kwa kuangalia mambo yenye umuhimu kwa Taifa, bajeti imekuwa ikipangwa kila mwaka kwa kuzingatia maeneo ya kuyapa kipaumbele ili kuleta maendeleo kwa nchi.” alisema Dkt. Kida.

Kwa upande wa mtoa taarifa ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Joviter Katabaro (Mkufunzi katika, shule ya Elimu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam) alisema pamoja na serikali kutoa elimu bure katika ngazi fulani ya elimu nchini lakini bado kuna changamoto mbalimbali katika elimu ambazo zinahitaji kutafutiwa ufumbuzi katika bajeti ya 2017/2018.
Mhadhiri Mwandamizi wa Shule Kuu ya Elimu Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Dk. Joviter Katabaro akitoa taarifa kuhusu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

“Pamoja na jitihada kubwa ya Serikali katika elimu bado kuna upungufu wa majengo 10,000 ya shule nchini kitoke, kuna upungufu wa maktaba 15,000, vyoo bado havitoshi,” alisema Dk. Katabaro.

Kwa upande wake, Prof. Haidari Amani (Mtafiti Mshirki mwandamizi ESRF) ambaye alitoa taarifa kuhusu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi alisema pamoja na sekta ya kilimo kuwa na changamoto ambazo zinajitokeza serikali inatakiwa iweke mfumo mzuri kuanzia wakulima wadogo ili waweze kunufaika na kilimo ambacho wanakifanya.
Mtafiti Mwenza wa ESRF, John Shilinde akitoa taarifa kuhusu Bajeti ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
Mtafiti Mwenza Kiongozi wa ESRF, Prof. Haidari Amani akijibu maswali ya baadhi ya washiriki waliohudhuria.
Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida akifafanua jambo wakati wa kuijadili bajeti ya 2016/2017 katika sekta za Elimu na Kilimo.

MVUA ZABABISHA MAPOROMOKO YA ARDHI NA MADARAJA KUKATIKA KISIWANI PEMBA

MITI mbali mbali ikiwa imeanguka katika moja ya sehemu ya Barabara ya Chake-Mkoani, kufuatia mvua kubwa iliyonyesha Kisiwani Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA) Kwa hisani ya ZanziNews
MAGUNIA 518 ya Karafuu Kavu zikiwa hazikuharibika katika ghala la kuhifadhia karafuu la Shirika la ZSTC Mkoani, baada ya ghala hilo kuanguka sehemu ya Ukuta na gunia tisa kufukiwa na dongo zikiwa na karafuu kavu.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
SEHEMU ya Ghala la Kuhifadhia karafuu la ZSTC Mkoani, likiwa limebomoka baada ya kuangukiwa na mti uliokuwa katika mlima na kupelekea Gunia Tisa za Karafuu Kavu zenye thamani ya Zaidi ya Milioni 5 kufukiwa na dongo kutokana na mvua kubwa iliyonyesha Kisiwani Pemba.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
WATOTO wadogo wakisafisha kwa kutoa dongo nje katika Msikiti wa Mbuyuni Wilaya ya Mkoani, baada ya sehemu kubwa ya msiki huo kuangukiwa na Udongo ulioporomoka na kuharibu Msikiti, kama unavyoonekana katika Picha.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
WATOTO wadogo wakisafisha kwa kutoa dongo nje katika Msikiti wa Mbuyuni Wilaya ya Mkoani, baada ya sehemu kubwa ya msiki huo kuangukiwa na Udogo ulioporomoka na kuharibu Msikiti, kama unavyoonekana katika Picha.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
WANANCHI wa Mbuyuni Wilaya ya Mkoani, wakitoa msaada kwa kuondosha Udongo, ili kutoa Vitu vilivyofukiwa na Fusi baada ya Nyumba ya Fadhil Amour Mohamed kuangukiwa na Udongo na kutokupata hata kitu Kimoja.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
SOMA ZAIDI »

JAMII YATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA UPIMAJI WA ARDHI.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akimkabidhi mkazi wa Lamadi, Mama Juma hati miliki ya eneo lake.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akizungumza na wananchi wa Lamadi juu ya kuwa na hati miliki ya maeneo yao
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi akifurahia jambo na wakazi wa Lamadi.

Na Shushu Joel,BUSEGA.

JAMII imetakiwa kuchangamkia fursa zinazoendelea kutolewa na serikali katika ufanikishaji wa wananchi wote kupima maeneo yao ili waweze kuwa

MVUA KUBWA ZA MASIKA ZALETA MAAFA KISIWANI PEMBA

Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Pemba, Bibi Salama Mbarouk Khatib, akiwa pamoja na Uongozi wa Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais na Watendaji wengine, wakiangalia maafa yaliosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea
kunyesha hukoa katika Kijiji cha Kipapo Shehia ya Chonga.
Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Pemba, Bibi Salama Mbarouk Khatib, akiwa pamoja na Uongozi wa Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais na Watendaji wengine, wakiangalia maafa yaliosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea
kunyesha hukoa katika Kijiji cha Kipapo Shehia ya Chonga.
Baadhi ya vitu mbali mbali vikiwa vimewekwa pahala pamoja baada ya Nyumba kuingia maji huko katika kijiji cha Kipapo , Shehia ya Chonga kufuatia mvua kubwa inayoendelea kunyesha Kisiwani Pemba.
Daraja lililokatika kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha na kusababisha Nyumba zaidi ya 13 kuathirika na nyengine kuanguka.
Msaidizi wa makamo wa pili wa Rais Pemba, Amran Massoud Amran, akionyesha Daraja lilivyoathirika na mvua hiyo na kusababisha gari zinazotoka Mgelema kwenda Chake Chake kusitisha safari yake hapo.
 
Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Pemba, akikaguwa baadhi ya maeneo yaliothirika na mvua huko katika kijiji cha Kipapo shehia ya Chonga Pemba.


Picha na Marzouk Khamis -Maelezo -Pemba. Kwa hisani ya ZanziNews

SWANSEA YAIZUIA MANCHESTER UNITED KUSOGEA KATIKA NAFASI YA NNE

Mpira wa adhabu uliopigwa kiufundi na Gylfi Sigurdsson umeipatia Swansea pointi muhimu ikihaha kubakia katika Ligi Kuu ya Uingereza na kuharibu hesabu za Manchester United kutinga katika nafasi ya nne.

Sigurdsson alipiga shuti la kuzungusha kutoka umbali wa yadi 30 lililotinga wavuni huku kipa akibaki anauangalia mpira, na kufanya matokeo kuwa 1-1 baada ya awali Wayne Rooney kufungwa kwa mkwaju wa penati.
Kwa matokeo hayo Manchester United imebakia katika nafasi ya tano, pointi moja nyuma ya mahasimu wao Manchester City ambao wanapointi 66 sawa na Liverpool iliyokatika nafasi ya tatu zikiwa zimecheza michezo sawa.
   Wayne Rooney akifunga kiufundi mpira wa penati kwa kumpoteza mahesabu kipa
     Mpira wa adhabu uliopigwa kiufundi na Gylfi Sigurdsson ukielekea kutinga wavuni

TOTTENHAM HAIJAKATA TAMAA YAENDELEA KUIFUKUZIA CHELSEA

Tottenham imejihakikishia kuwa inaendelea kuwa nyuma ya vinara wa Ligi Kuu ya Uingereza Chelsea kwa tofauti ya pointi nne baada ya kuwafunga wapinzani wao Arsenal kwa magoli 2-0 katika dimba la White Hart Lane.

Ushindi wa Chelsea 3-0 dhidi ya Everton uliipa presha Tottenhma lakini walijibu mapigo kwa staili nao kwa kupata ushindi na kuendelea na kiwango bora, ikilinganishwa na cha Octoba 1960 waliposhinda michezo 13 mfululizo.
Mchezo wao huo dhidi ya Arsenal uliamuliwa na magoli yaliyofungwa na Dele Alli katika dakika ya 55 likiwa ni goli lake la 21 katika msimu huu, na kisha baadaye Harry Kane akafunga goli la pili kwa mkwaju wa penati.
                    Mchezaji nyota kijana Dele Alli akifunga goli la kwanza la Tottenham 
Harry Kane akijipinda na kuachia shuti la mkwaju wa penati aliopiga kiufundi na kufunga goli la pili

CHELSEA IMEDHAMIRIA KUTWAA UBINDWA LIGI KUU YA UINGEREZA

Vinara wa Ligi Kuu ya Uingereza Chelsea wamepiga hatua kubwa katika kuelekea kutwaa ubingwa baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Everton katika dimba la Goodison Park.

Chelsea ilipata goli la kwanza kwa shuti kali la Pedro la umbali wa yadi 25, kisha Gary Cahill alifunga la pili kwa shuti la karibu kabla ya Willian kufunga la tatu na kuifanya iendelee kuongoza kwa tofauti ya pointi nne.
Kwa ushindi huo Chelsea hata wakipoteza pointi tatu katika michezo minne iliyosalia bado wataweza kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza, hata kama Tottenham watashinda michezo yote iliyosalia.
                                    Pendro akiachia shuti kali lililozaa goli la kwanza la Chelsea
                                      Gary Cahill akiifungia Chelsea goli la pili katika mchezo huo