Monday, May 1, 2017

MAKAMU WA RAIS AUNGANA NA RAIS MAGUFULI NA WAZIRI MKUU MAJALIWA KWENYE KILELE CHA SHEREHE ZA MEI MOSI MJINI MOSHI JUMATATU





Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akilakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Said Mecky Sadick na viongozi wengine wa mkoa huo, mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa wa Kimataifa wa Kilimanjaro KIA, Aprili 30, 2017. Makamu wa Rais anaungana na Rais John Pombe Magugfuli na Waziri Mkuu Majaliwa kwenye kilele cha sherehe za siku ya Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi, zitakazofanyika kitaifa mjini Moshi, Jumatatu. (PICHA NA VPO)
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na viongozi mbalimbali waliofika awanjani hapo kumlaki. Anatarajiwa kuhudhuria sherehe za wafanya kazi, Mei Mosi zitakazofanyika kitaifa mkoani Kilimanjaro Jumatatu.

PPF WAUNGANA NA WENZAO KUADHIMISHA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI



NA K-VSI BLOG/Khalfan Said
WAFANYAKAZI wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wameungana na wenzao jijini Dar es salaam kuadhimisha siku ya wafanyakazi Duniani maarufu kama Mei Mosi.
Kitaifa sherehe hizo zinaongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli mjini Moshi ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni “Uchumi wa Viwanda uzingatie Haki, Maslahi na Heshima ya wafanyakazi.”
Aidha jijini Dar es Salaam, Wafanyakazi wa PPF na wengine kutoka sekta ya Umma na Binafsi, walifanya matembezi kutoka eneo la Mnazi Mmoja hadi uwanja wa Uhuru huku wakiongiozwa na brass band ya Jeshi la Magereza.
Kwa upande wao wafanyakazi wa PPF  walianza kwa kukusanyika kwenye ofisi za Makao Makuu ya Mfuko huo barabara ya Samora/Morogoro ambapo walipewa maelekezo ya umuhimu wa ushiriki wao katika maetembezi hayo na kujiunga na wenzao eneo la kuanzia matembezi pale Mnazi moja.
Mgeni rasmi katika sherehe za Mei Mosi jijini Dar es Salaam, alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeka, Bw. Felix Lyaviva, ambaye alipokea maandamano ya wafanyakazi na magari kadhaa kutoka taasisi za umma na binafsi yakionyesha huduma zitolewazo na taasisi hizo.
Huduma zitolewazo na PPF ni pamoja na kulipa Mafao ya Uzeeni, Mafao ya Wategemezi,Mafao ya Elimu, Mafao ya Kiinya Mgongo, Mafao ya Kifo, Mafao ya Ugonjwa na Mafao ya Uzazi. Lakini pia kazi nyingine za Mfuko huo ni kusajili wanachama kupitia mfumo wa uchangiaji wa hiari ujulikanao kama “Wote Scheme”

Baadhi ya wafanyakazi wa PPF, wakiwa kwenye matembezi ya kuadhimisha Mei Mosi jijini Dar es Salaam Leo.

Kiongozi wa kundi la wafanyakazi WA PPF, wwlioshiriki matembezi ya kuadhimisha siku ya wafanyakazi duniani, Mohammed Siaga, (kushoto), akizungumza muda mfupi kabla ya kuanza matembezi hayo.









DKT..MABODI AWATAKA BARAZA LA WAZEE PEMBA KUSIMAMIA MAADILI YA VIJANA. MABO1

MABO1
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdalla Juma Saadala “Mabodi” akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Wazee wa CCM Kisiwani humo katika Ofisi ya Kitengo cha Uratibu wa CCM Chake Chake Mkoa wa Kusini  Pemba.

NA IS-HAKA OMAR, PEMBA.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt. Abdalla Juma Saadala” Mabodi” amewasihi Wazee wa Chama hicho kisiwani Pemba kusimamia ipasavyo suala la Maadili kwa

TPDC yang’oa vikombe lukuki Mei Mosi. tp2

tp2
Shamrashamra za ushindi mnono na vikombe kwenye michezo minane kati ya kumi ambayo timu za michezo TPDC ilishiriki katika mashiondano ya Mei Mosi.

tp1
Timu za michezo za TPDC zikiwa na mafuriko ya vikombe vya ushindi zilizoupata kwenye mashindano mbalimbali ya Mei Mosi.


………………………………………………………………………..
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) lafanikiwa kubeba vikombe vinanena na medali nne katika michuano ya mashindano ya Maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani-Mei Mosi yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo cha Ushirika Mkoani Kilimanjaro.
Katika mashindano hayo yaliyoanza tarehe 19 hadi 29 Aprili, 2017 yaliyoandaliwa na

TANESCO YAPONGEZWA KATIKA MAONESHO YA WAKALA WA AFYA NA USALAMA MAHALI PA KAZI (OSHA)

Na Magreth Subi,Moshi
Shirika la umeme Nchini Tanzania (TANESO) limeibuka kidedea katika maonesho ya wakala wa Afya na Usalama Mahali pa Kazi (OSHA) ambayo yamefikia kilele chake Aprili 28, 2017 Mjini Moshi.
 Mgeni Rasmi katika maonesho hayo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama,(pichani katikayi), alitoa pongeza kwa TANESCO kwa Huduma nzuri inayotolewa katika kuhudumia jamii na kuwataka Wafanyakazi kuwa na ari siku zote pamoja na changamoto wanazokutana nazo kwani changamoto ndio chachu ya maendeleo kuelekea Nchi ya Viwanda kama kauli mbiu ya Mhe. Rais inavyo sema.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Mhagama alitoa shukurani kwa washiriki na kutangaza washindi katika Nyanja mbali mbali na TANESCO kuibuka mshindi wa kwanza wa masuala ya Afya na Usalama kazini mahala pa Kazi katika Sekta ya Huduma kwa Wateja.

Kwa upande wake, Afisa Mkuu kitengo cha Afya na Usalama Kazini Bw. Fred Kayega alitoa maelezo ya vifaa mbalimbali vya vinavyotumiwa na Wafanyakazi kujikinga na ajali pahala pa kazi kwa Mhe. Mhagama alipotembelea banda la TANESCO kabla maonesho hayo hayajafikia hitimisho.

Baadhi ya Wafanyakazi wa TANESCO Makao Makuu, pamoja na Wafanyakazi wa Mkoani Kilimanjaro, walifurahia ushindi huo kwani utazidi kuongeza hari kwa Wafanyakazi na kufanya vizuri Zaidi katika utendaji wa Kazi.
Mfanyakazi wa TANESCO akitoa maelezo kwa Mhe. Waziri

DR.MABODI AWATAKA BARAZA LA WAZEE PEMBA KUSIMAMIA MAADILI YA VIJANA.


Mheshimiwa Nabii Mkuu Dr GeorDavie Royal Mkuu ,   jana amezindua rasmi kitabu cha " KUKIWA NA FOLENI" kilichoandikwa na Wiseman Luvanda.
Pia Nabii Dr.GeorDavie alimpongeza kwa kitendo chake  alichoamua kufanya kwa kuwa balozi wa barabarani  kwa kutoka Jijini Dar es salaam hadi mkaoni Arusha wa usafiri wa baiskeli
Akizungumza na wadau waliohudhuria hafla hiyo mtunzi wa kitabu hicho alisema vijana wanapaswa kutumia vipaji vyao kwa kujituma, kuthubutu na kufanya kazi kwa nguvu  na si kulalamika kila siku,  jambo linalopelekea kuibuka kwa makundi mbalimbali kama vile Panya Road na mengineyo.
Aidha mwandishi huyo amewataka wadau mbalimbali kumuunga mkono katika kukinunua kitabu hicho cha " KUKIWA NA FOLENI" , ambacho pia amekiandika kwa lugha ya Kiswahili  ili kuweza kukisambaza nchi nzima.
Tazama baadhi ya picha za tukio hili hapo chini

Pichani ni Mwandishi wa kitabu hicho Wiseman Luvanda, Akizungumza na baadhi ya wadau waliohudhuria kongamano hilo jana Jijini Arusha. Picha na msumbanews blog

Nabii Mkuu Dr GeorDavie Royal Mkuu akipokea kitabu kutoka kwa Mwandishi Wiseman Luvanda.Picha na msumbanews blog

Baadhi ya wadau mbali waliojitokeza kwenye kongamano  la kuinuliwa viwango na uzinduzi wa kitabu hicho.Picha na msumbanews blog

Mwandishi Wiseman Luvanda akifuatilia kwa makini kongamano la kuinuliwa viwango ambalo lilifuatana na uzinduzi wa kitabu chake.Picha na msumbanews blog

SMZ YAAHIDI KUUNGA MKONO JUHUDI ZA ZANUSO KATIKA SEKTA YA UJASIRIAMALI.


NA JUMA FARID, ZANZIBAR.
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar  imeahidi kuendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na baadhi ya Jumuiya za wanafunzi wa Vyuo Vikuu nchini zinazoonyesha nia ya kuthamini  fani ya Ujasiriamali kama chanzo mbadala cha kupunguza tatizo la Ajira nchini.
Ahadi hiyo imetolewa na  Mkurugenzi  wa Viwanda Zanzibar, Saleh Suleiman Hamad  kwa Niba ya  Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko  Balozi Amina Salum Ali Wakati akifunga warsha ya Mashindano ya miradi ya Ujasiriamali kwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Zanzibar yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Zanzibar ( ZU) huko Kampasi Kuu ya Chuo hicho Tunguu.
Amesema ubunifu ulionyeshwa na wanafunzi hao katika uandishi, mikakati na bidhaa  za miradi ya Ujasiriamali waliyoiwasilisha katika Mashindao hayo inajenga ushawishi kwa serikali na mashirika mengine ya kimataifa kuwaunga mkono ili wafikie malengo yao ya kujiajiri na kuwaajiri vijana wengine wasiokuwa na ajira.
Amesema bado wanafunzi wengi wanaohitimu elimu ya ngazi ya vyuo vikuu nchini hawajatumia fursa zinazopatikana katika fani ya Ujasiriamali ambayo imekuwa ikitegemewa na mataifa mbali mbali duniani kupunguza  tatizo la ajira hasa kwa vijana.
“ Nasaha zangu kwenu kabla ya kuanzisha mradi wowote fanyeni tathimini na utafti wa kitaalamu kubaini aina ya ujasiriamali unaotaka kufanya una maslahi gani na wateja wako wahitaji bidhaa za aina gani sambamba na kuwa wabunifu wa kufanya miradi isiyofanana.”, alisema Katibu huyo.
Aidha alieleza kwamba kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Masoko, Balozi Amina Salum Ali serikali itaendelea kudhamini miradi itakayoonyesha ustawi na maendeleo endelevu.
Pia  katika juhudi za kuwajengea uwezo wajasiriamali hao alieleza kwamba serikali itashawishi makampuni na mashirika ya kimaita ya kibiashara kufanya kazi kwa karibu na jumuiya hizo ili zipate soko la uhakika la kuuzia bidhaa zao.
Hata  hivyo ametoa nasaha zake kwa wajasiriamali hao kutengeneza bidhaa bora zitakazokubalika katika soko la kimataifa pamoja na kujiongeza kitaaluma kupitia mafunzo mbali mbali ya fani hiyo.
Mapema  akizungumza  Mlezi wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar(ZU), Bw. Juma Rashid Khamis  ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo hicho aliwasihi washiriki wa mashindao hayo kuendelea kujifunza zaidi kupitia kwa wajasiria mali wakongwe ili wapate ujuzi wa ziada wa kukabiliana na ushindani wa bidhaa na miradi ya ujasiriamali ndani na nje ya Zanzibar.
Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya SISI Consultants, Mohamed  Wario  aliwataka Wasomi hao kutumia  vizuri  fursa hiyo ya ujasiria mali kwa kuangazia  sehemu tofauti  ambazo bado hazijatumiwa  vizuri  kibiashara  zikiwemo  Sekta ya Utalii, Uvuvi na Ufugaji ili kuzalisha bidhaa bora zinazotokana na rasilimali hizo na kuzishindanisha katika soko la ndani na nje ya nchi.
“ Kampuni  ipo tayari kushirikiana na nyinyi  wakati wowote  lakini lazima mjiongeze zaidi kufikia lengo la kufanya miradi bora na inayoendana na mahitaji ya sasa ili mpate mafanikio zaidi”, alisisitiza Mkurugenzi huyo.
Kwa upande wake mshiriki wa mashindano hayo aliyeshindanisha mradi wa usindikaji wa bidhaa aina ya Jam inayotumia kwa chakula cha mkate iliyotengenezwa kwa matunda ya Maembe, Ehlam Ali Khamis alisema wazo la kutengeza bidhaa hizo ni kutokana na kukosekana kwa matumizi mazuri ya matunda hayo hasa wakati wa msimu wake hali inayosababisha kuharibika kwa kukosekana kwa viwanda vya kusindika matunda hayo.
Akitoa ufafanuzi juu ya  Warsha hiyo,  Mwanzilishi na Msimamizi  wa Mashindano hayo  Jumuiya ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Zanzibar  ZANUSO,  Mohamed Omar  alifafanua kwamba awali mchakato huo ulishirikisha jumla ya vyuo Sita na ulipopita mchujo vikabaki vitatu ambavyo ni Zanzibar University (ZU), State University  of Zanzibar(SUZA) na Summait University.
Mashindano hayo wamepatikana washindi saba ambao wamepewa Zawadi mbali mbali zikiwemo simu za Adroid, lakini nafasi ya kwanza ambayo imeshikiliwa na Issah Eugenio kwa mradi wa Handbags Made in Jeans, nafasi ya pili ni Ehlam Ali Khamis kwa mradi wa Mango Jam na Tatu Ibrahim ahmad abdalla na Sabrina  Khamis Machano wa mradi wa Teke knowlge solutions company  wote kutoka vyuo tofauti vilivyoshiriki kwa awatua hiyo.


Mkurugenzi wa Kampuni ya SISI Consultants, Mohamed  Wario ambayo ni miongoni mwa wadhamini akitoa nasaha zake kwa wanafunzi walioshiriki katika mashindano hayo yaliyoandaliwa na  jumuiya ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Zanzibar(ZANUSO) huko ZU kampasi kuu ya Tunguu.


Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Viwanda Zanzibar, Saleh Suleiman Hamad akiutubia wakati wa kufunga mashindano yaliyoandaliwa na  jumuiya ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Zanzibar(ZANUSO) huko ZU kampasi kuu ya Tunguu.



Picha ya pamoja ya washiriki wa mashindano hayo

Picha ya pamoja ya washiriki wa mashindano hayo pamoja na Viongozi wa ZANUSO na ZU pamoja na mgeni rasmi.