Mheshimiwa Nabii Mkuu Dr GeorDavie Royal Mkuu , jana amezindua rasmi kitabu cha " KUKIWA NA FOLENI" kilichoandikwa na Wiseman Luvanda.
Pia
Nabii Dr.GeorDavie alimpongeza kwa kitendo chake alichoamua kufanya
kwa kuwa balozi wa barabarani kwa kutoka Jijini Dar es salaam hadi
mkaoni Arusha wa usafiri wa baiskeli
Akizungumza
na wadau waliohudhuria hafla hiyo mtunzi wa kitabu hicho alisema vijana
wanapaswa kutumia vipaji vyao kwa kujituma, kuthubutu na kufanya kazi
kwa nguvu na si kulalamika kila siku, jambo linalopelekea kuibuka kwa
makundi mbalimbali kama vile Panya Road na mengineyo.
Aidha
mwandishi huyo amewataka wadau mbalimbali kumuunga mkono katika
kukinunua kitabu hicho cha " KUKIWA NA FOLENI" , ambacho pia amekiandika
kwa lugha ya Kiswahili ili kuweza kukisambaza nchi nzima.
Tazama baadhi ya picha za tukio hili hapo chini
Pichani
ni Mwandishi wa kitabu hicho Wiseman Luvanda, Akizungumza na baadhi ya
wadau waliohudhuria kongamano hilo jana Jijini Arusha. Picha na
msumbanews blog
Nabii Mkuu Dr GeorDavie Royal Mkuu akipokea kitabu kutoka kwa Mwandishi Wiseman Luvanda.Picha na msumbanews blog
Baadhi ya wadau mbali waliojitokeza kwenye kongamano la kuinuliwa viwango na uzinduzi wa kitabu hicho.Picha na msumbanews blog
Mwandishi Wiseman Luvanda akifuatilia kwa makini kongamano la kuinuliwa viwango ambalo lilifuatana na uzinduzi wa kitabu chake.Picha na msumbanews blog
No comments :
Post a Comment