PICHA: MAKTABA
Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Jumanne Muliro.
Watu 30 wametiwa mbaroni kwa tuhuma za kughushi nyaraka mbalimbali zinazohusiana na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa lengo la kujipatia malipo kwa njia ya udanganyifu kutoka kwenye mfuko huo.
Watu hao wamekamatwa na Jeshi la Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na maofisa kutoka NSSF baada ya kufanya msako na uchunguzi kwa nyakati tofauti kuanzia Desemba 2023 hadi Aprili 2024.
Watuhumiwa hao wamekamatwa na nyaraka bandia mbalimbali zinazohusu kuacha kazi, vyeti vya huduma, taarifa za uongo za ugonjwa, hati za uongo za kufukuzwa kazi pamoja na fomu za kugushi za kuomba mafao ya NSSF.
Waliokamatwa ni pamoja na Diocress Kahwa (35), mkazi wa Mbezi; mwalimu wa Shule ya Msingi Maxmilian ya Segerea, Barnabas Bonivencha na wenzake 11 wa kampuni binafsi ya ulinzi ya G4S waliowasilisha taarifa za uongo za kuacha kazi ili wapate mafao wakati bado wapo kazini.
Katika waliokamatwa yumo Gregory Rweikiza (44), mkazi wa Goba na Carolina Mushi (37) Mkazi wa Upanga, Ilala ambaye ni mtumishi wa Benki ya Stanbinc kwa tuhuma za kughushi taarifa za hospitali za ugonjwa za ili apate fao la matibabu.
Waliokamatwa wengine ni Michael Mpogolo (38) na Sabato Thomas (27), wakazi wa Madale Mivumoni Dar es Salaam kwa tuhuma za kughushi nyaraka za wafanyakazi wawili marehemu (Servas Tesha na Korodias Shoo) waliokuwa wanafanya kazi katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM).
No comments :
Post a Comment