Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa shule ya sekondari ya bweni ya wasichana ya Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyopo wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.
Ujenzi utakapokamilika shule hiyo itachukua wanafunzi kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha sita.
Ujenzi wa shule hiyo Mpya unatekelezwa kupitia Mradi wa kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) kwa gharama ya shilingi bilioni 4.
Ujenzi unatekelezwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza ya utekelezi wa mradi huo ulianza tarehe 6 April 2022 na unatarajiwa kukamilika tarehe 30 Januari 2023 na itatumia fedha Kiasi cha bilioni 3.
Katika awamu hii ya kwanza vinajengwa vyumba vya madarasa 12, jengo la utawala 1, maabara 4, matundu ya vyoo 16, chumba cha jenereta 1, bwalo 1,mabweni 5, mitaro ya maji, kichomea taka 1, matanki ya chini ya maji, matanki ya plastiki, uzio, njia za kutembea na nyumba za walimu 2.
No comments :
Post a Comment