Na Mwandishi Wetu, Michuzi Blog
WATANZANIA wakiwemo watumishi wa umma wameshauriwa kujiepusha na uwekezaji usio salama ikiwemo upatu usio rasmi pamoja na upatu wa mitandaoni na badala yake kutumia mifuko rasmi ya uwekezaji ya Serikali ili kuepukana na janga la kutapeliwa kisha kupoteza vipato walivyo navyo.
Ushauri huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri Ofisi ya Rais ,Utumishi na Utawala Deogratius Ndejembi wakati akizindua mauzo ya awali ya hisa katika mfuko wa uwekezaji unao milikiwa na Watumishi Housing Investment “Faid Fund”.
Ametumia nafasi hiyo kueleza kumeibuka wimbi la watanzania wengi kulalamikia utapeli kupitia mitandao jambo ambalo linatokana na wengi wao kuwekeza katika sehemu hatarishi kama upatu usio rasmi ambao unepelekea kutapeliwa kwa wananchi wengi.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Dkt. Freddy Msemwa amesema mfuko huo wa Faida Fund umelenga kujumuisha pia makundi yasiyo rasmi katika uwekezaji kupitia vipato vidogo vidogo nje ya uwekezaji katika hati fungani za serikali ambao umekuwa ukitumika na watu wenye vipato vya kati na juu.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deogratius Ndejemb akisoma hotuba yake wakati wauzindua rasmi uuzaji wa vipande vya hisa za mfuko wa Faida Fund Leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Shirika la Watumishi Housing Ivestiment,Hosea Kashimba akisoma hutuma yaka wakati wa uzindua rasmi uuzaji wa vipande vya hisa za mfuko wa Faida Fund Leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Dkt. Freddy Msemwa akisoma utuma yaka wakati wa uzindua rasmi uuzaji wa vipande vya hisa za mfuko wa Faida Fund Leo jijini Dar es Salaam.(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MASSAKA WA MICHUZI TV)
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Shirika la Watumishi Housing Ivestiment Hosea Kashimba na Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Dkt. Freddy Msemwa kwa pamoja Leo wakikata utepe kuzindua rasmi uuzaji wa vipande vya hisa za mfuko wa Faida Fund Kutoka shirika la Watumishi Housing Investment Katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Kisenga Makumbusho jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Shirika la Watumishi Housing Ivestiment Hosea Kashimba na Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Dkt. Freddy Msemwa wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua uuzaji wa hisa hizo.
No comments :
Post a Comment