Wednesday, November 30, 2022

SHAHADA YA UDAKTARI WA HESHIMA NI UTHIBITISHO WA KAZI KUBWA ANAZOZIFANYA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Shahada ya Udaktari wa Falsafa wa Heshima ikiwa ni Shahada ya Udaktari wa Juu katika Humanitia na Sayansi Jamii na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika Mahafali ya Hamsini na mbili (52) ya Duru ya Tano ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City tarehe 30, Novemba, 2022. (PICHA NA IKULU)

NA MWANDISHI MAALUM.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) tumeguswa na kufurahishwa na uamuzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kumtunuku shahada ya udaktari wa heshima Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mahafali ya 52 duru ya 5 yaliyofanyika leo Jumatano, 30 Novemba, 2022 ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Uamuzi huo ni uthibitisho wa dhahiri wa kazi kubwa na nzuri inayofanywa na serikali ya CCM, awamu ya sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuleta ustawi wa maisha na maendeleo endelevu kwa Nchi yetu. 

Kati ya kazi kubwa iliyofanyika na kutumika kumtunuku shahada hiyo ya heshima ni pamoja na mageuzi ya kiuchumi, uimarishaji wa misingi ya demokrasia, utawala bora, maendeleo ya jamii, ameleta furaha na tumaini jipya miongoni mwa wananchi ambayo yote ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025 uliochagizwa na utashi wake wa kisiasa, ukomavu na umahiri alionao katika uongozi wake

Shahada hii ya heshima ni fahari kwa Chama Cha Mapinduzi na watanzania wote kuwa tunaye Rais anayewajibika kwa maslahi ya wote na tunaimani ya kwamba itampa moyo kuwa watanzania wanaona kazi nzuri anazozifanya kwa Taifa hivyo kumpa ari na nguvu ya kuendelea kutekeleza wajibu wake.







No comments :

Post a Comment