Friday, November 18, 2022

MUHIMBILI KUANZISHA "SOBER HOUSE" NA KLINIKI YA MAGONJWA YA AKILI


Hospitali ya Taifa Muhimbili ina mpango wa kuanzisha Kliniki ya Magonjwa ya Afya ya Akili ikiwemo huduma  jumuishi za waraibu wa dawa za kulevya katika Kijiji cha Marekebisho ya Afya ya Akili, kilichopo Vikuruti Kata ya Chamazi ili kupunguza msongamano uliopo MNH-Upanga.

Tiba Jumuishi (Medical Assisted Treatment-MAT) hutolewa kwa waathirika wa dawa za kulevya  ikihusisha ushauri nasaha, matibabu ya kurekebisha tabia pamoja na utoaji dawa aina ya Methadone, ambapo katika Kliniki  iliyopo MNH Upanga jumla wa wananchi 1,100 wenye uhitaji huo wanahudumiwa kwa siku.
 Kijiji cha Vikuruti Bw. Beno Kalunga alisema kuwa kwa sasa kijiji kinahudumia wagonjwa 7-10 kwa mwezi, na pia kinajihusisha na kilimo na ufugaji ikiwa ni sehemu ya tiba kazi kwa  wagonjwa.

Amesema wagonjwa wanaohudumiwa Vikuruti ni wale waliopata changamoto za afya ya akili na kutibiwa hivyo hupelekwa kijijini hapo kwa lengo la kuendelea na tiba kazi ili afya zao ziimarike vizuri.

No comments :

Post a Comment