Monday, November 21, 2022

BENKI YA DUNIA YAIPA TANZANIA TRILIONI 1.24 KAMA MKOPO NAFUU

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba na Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini, Bw. Nathan Belete (kushoto), wakiwaonesha wanahabari, mikataba ya mikopo nafuu ya dola za Marekani milioni 535 sawa na shilingi trilioni 1.24, kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo. Kulia ni Waziri wa Nishati Mhe January Makamba.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba na Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini, Bw. Nathan Belete (kushoto), wakisaini mikataba ya mikopo nafuu ya shilingi trilioni 1.24 kwa ajili ya miradi miwili ukiwemo Mradi wa REA na Mradi wa kukabiliana na mafuriko katika Bonde la Mto Msimbazi. Anayeshuhudia ni Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba. 


Benki ya Dunia imeipatia Tanzania mikopo nafuu ya jumla ya dola za Kimarekani Milioni 535 sawa na shilingi za Kitanzania trilioni 1.24 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya

maendeleo.

Hafla ya kutia saini mikataba hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Hazina jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba na Mwakilishi wa Benki ya Dunia hapa nchini Bw. Nathan Belete ambapo pia Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba alihudhuria.

Taarifa inaonyesha miradi iliyolengwa ni pamoja na mradi wa kusambaza umeme vijijini (REA) na Mradi wa kukabiliana na mafuriko katika Bonde la Mto Msimbazi eneo la jangwani.

No comments :

Post a Comment