The repayment period for loans for small businesses through the Hustlers Fund will be capped at 14 days in a plan that looks set to open a window for small businesses to access cheaper credit.
Pages
Wednesday, November 30, 2022
Inflation slows for the first time in 9 months amid CBK rate hikes
Inflation has slowed down for the first time in nine months on the back of a drop in food and fuel prices and rate hikes to contain the cost of living measure.
Letter linked to Joho family SGR cargo deal goes missing
The Auditor-General has flagged missing documents in a contract that saw a logistics firm linked to the family of former Mombasa Governor Ali Hassan Joho offered the deal to operate at a taxpayer-funded terminal for standard gauge railway (SGR) cargo.
SHAHADA YA UDAKTARI WA HESHIMA NI UTHIBITISHO WA KAZI KUBWA ANAZOZIFANYA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Shahada ya Udaktari wa Falsafa wa Heshima ikiwa ni Shahada ya Udaktari wa Juu katika Humanitia na Sayansi Jamii na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika Mahafali ya Hamsini na mbili (52) ya Duru ya Tano ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City tarehe 30, Novemba, 2022. (PICHA NA IKULU)
NA MWANDISHI MAALUM.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) tumeguswa na kufurahishwa na uamuzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kumtunuku shahada ya udaktari wa heshima Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mahafali ya 52 duru ya 5 yaliyofanyika leo Jumatano, 30 Novemba, 2022 ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Uamuzi huo ni uthibitisho wa dhahiri wa kazi kubwa na nzuri inayofanywa na serikali ya CCM, awamu ya sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuleta ustawi wa maisha na maendeleo endelevu kwa Nchi yetu.
Kati ya kazi kubwa iliyofanyika na kutumika kumtunuku shahada hiyo ya heshima ni pamoja na mageuzi ya kiuchumi, uimarishaji wa misingi ya demokrasia, utawala bora, maendeleo ya jamii, ameleta furaha na tumaini jipya miongoni mwa wananchi ambayo yote ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025 uliochagizwa na utashi wake wa kisiasa, ukomavu na umahiri alionao katika uongozi wake
Shahada hii ya heshima ni fahari kwa Chama Cha Mapinduzi na watanzania wote kuwa tunaye Rais anayewajibika kwa maslahi ya wote na tunaimani ya kwamba itampa moyo kuwa watanzania wanaona kazi nzuri anazozifanya kwa Taifa hivyo kumpa ari na nguvu ya kuendelea kutekeleza wajibu wake.
RAIS SAMIA ATUNUKIWA SHAHADA YA HESHIMA YA UDAKTARI WA FALSAFA NA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM
WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AHIMIZA ELIMU YA BIMA BARANI AFRIKA
“Hapa Tanzania, Rais wetu, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amekuwa akitoa kipaumbele kwenye suala la kuwezesha jamii kwa kuwainua kiuchumi wanawake na vijana ikiwa ni utekelezaji wa Azimio la Ouagadougou (“Ouagadougou+10”) la Utekelezaji wa Mpango wa Ajira na kutokomeza umaskini ambalo lilipitishwa na Wakuu wa Nchi wa Umoja wa Afrika Januari 2015 kama Ajenda ya AU ya 2063.
“Ni wakati muafaka mifuko yetu ya jamii kusaidiana na Serikali zetu kuondoa umasikini miongoni mwa watu wetu. Nitoe rai kwa washiriki wa mkutano huu muangalie uwezekano wa kujadili kwa mapana kuhusiana na namna ya mifuko ya hifadhi ya jamii inavyoweza kusaidia kuinua uchumi wa watu wetu na kusaidia kuondoa umaskini hasa kwa wanawake, vijana na wakulima.
Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na washiriki hao, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba alisema eneo la bima lilishatolewa maelekezo na Rais Samia Suluhu Hassan Aprili 22, 2021 wakati alipohutubia Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma.
“Mheshimiwa Rais alielekeza kwamba suala la bima ya kilimo na bima ya afya kwa wote liangaliwe kwa ukaribu zaidi na kuwekewa mfumo mzuri wa kisheria utakaoainisha namna bora ya utekelezaji wake.”
Alisema Serikali iliangalia pia suala la ukingaji wa majanga kwenye maeneo ya mikusanyiko kama vile masoko, shule na maduka na ikaamua kuweka mfumo wa kisheria wa namna ya kuyakinga majanga haya kwa njia ya bima kwa kupitisha Sheria ya Fedha Na. 05 ya Mwaka 2022 itakayosaidia kukinga maeneo yenye mikusanyiko kama vile masoko, vivuko na majengo ya biashara.
“Wizara ya Fedha kwa kushirikiana na Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania tunaandaa mwongozo wa bima ya kilimo, mifugo na uvuvi ili kuhakikisha kundi hili kubwa linapata uhakika wa uzalishaji wa mazao, mifugo na uvuvi hasa kwenye kipindi hiki chenye changamoto kubwa za mabadiliko ya tabia nchi.”
MFUMO WA TAARIFA KWA MWEKEZAJI WAZINDULIWA LEO JIJINI DAR, VIPAUMBELE VYATAJWA
SERIKALI imetaja vipaumbele katika uwekezaji ambavyo ni Kilimo, Usalama wa Chakula, Nishati (Nishati jadidifu), Elimu, Utalii na Miundombinu.