.
Na.Ashura Mohamed,Arusha
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mkoani Arusha Mhandisi Richard Ruyango amesema kuwa serikali itaendelea kutengeneza mazingira mazuri wilayani humo ili kuwawezesha wawekezaji kuendelea kufanya kazi katika mazingira wezeshi.
Alisema kuwa ni vema wawekezaji wakaendelea kuwekeza katika wilaya hiyo kwa kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kuwapa,kipaumbele ili waweze kufanya shughuli zao Vizuri.
Ameyasema hayo wakati wa Mahafali ya Tatu ya Kidato Cha nne,darasa la Saba na watoto wadogo wanaoingia darasa la kwanza (Kindergarten),katika shule ya Turkish Maarif iliyopo eneo la Ngaramtoni wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha.
"Wawekezaji kama hawa wanatusaidia Sisi watanzania wametoka nchini mwao,kuja kuendeleza watoto wetu wa kitanzania na umeona hapa kuwa kuna mambo mengi mazuri wanafanya kwa vijana hawa wa kitanzania,Vipaji vikubwa lakini kitu kizuri hawajaacha kufundisha Mila na desturi za kitanzania tumeona hawa vijana wadogo"Alisema Mhandisi Richard
Aidha alitumia wasaa huo kuwapongeza walimu kwa jitihada kubwa wanazozifanya kwa kuwalea watoto kimaadili na kitaluma kuanzia wakiwa wadogo mpaka Sasa wanapohitimu masomo Yao.
Pia aliwasisitiza wazazi kuendelea kuwasaidia vijana na kusimamia,maadili kwa kuwa wazazi ni wana asilimia 50 ya kuhakikisha kuwa Taifa linapata vijana ambao wanauzalendo na weledi wa kutosha.
Nae Mkuu wa shule ya Msingi Turkish Bw.Raphael Sabaya alisema kuwa ni vema jamii ikabadili mtizamo kwa kuendeleza vipaji vya watoto ili kuondoa dhana kuwa elimu ya darasani inaweza kuwatoa kimaisha.
Bw.Sabaya alisema kuwa sio lazima Mtoto ategemee elimu ya darasanj,bali elimu ya vitendo inaweza kusaidia kujiajiri na kuondokana na changamoto ya ajira iliyopo nchini na duniani kwa Ujumla.
Jumla ya wanafunzi 33 wamehitimu kidato Cha nne,31 darasa la saba na watoto wadogo (kindergarten) 28
No comments :
Post a Comment