Mkuu wa majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda amefunga rasmi mafunzo kwa askari wapya kundi 41/22 yaliyofanyika katika viwanja vya kambi ya Jeshi Oljoro-Arusha. katika sherehe hizo zilizofanyika siku ya tarehe 30,Septemba 2022 Jumla ya Askari 2457 walihitimu mafunzo yao yalioendesha katika Shule ya Awali ya Mafunzo ya Kijeshi RTS-Kihangaiko takribani Miezi sita.
Mkuu wa majeshi Jenerali Jacob John Mkunda amewataka Askari waliokula kiapo katika sherehe hizo kukiishi kiapo chao kwani Mwanajeshi asiyeishi kwenye kiapo sio mzalendo, amewataka kuwa watii,wanyenyekevu na uhodari katika utumishi wao waliouanza rasmi. Kwani kiapo hiki leo ndio mwanzo wa Maisha yenu Jeshini.
Mkuu wa Majeshi pia Amewataka askari wapya kuilinda katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Mipaka yetu kwani hilo ndio jukumu letu kubwa kimsingi.Mkuu wa Majeshi pia amewasihi askari wapya kuishi vizuri na wananchi huko ambako watapangiwa kwani Ulinzi wa Taifa unahitaji ushirikishwaji wa wananchi.
Aidha Mkuu wa Majeshi amewasihi askari wapya kutunza afya zao kwani Jeshi ni afya bila ya afya kazi yetu ni ngumu inahitaji kujitoa kiakili na mwili kutekeleza majukumu yetu, hivyo basi afya ndio mtaji wa kazi yetu.
No comments :
Post a Comment