Thursday, October 27, 2022

BoT, FRONTCLEAR WAKUBALIANA KUSAIDIA SEKTA YA FEDHA NCHINI

 

Naibu Gavana, Sera za Uchumi na Fedha, Dkt. Yamungu Kayandabila(kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Maendeleo ya Masoko ya Fedha- Frontclear Philip Buyskes wakipeana mikono baada ya kusaini hati ya makubaliano ya kuendeleza sekta ya fedha nchini.

BENKI Kuu ya Tanzania (BOT), imesaini makubaliano na Kamisheni ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa Afrika kwa kushirikiana na Taasisi ya Frontclear ya nchini Uholanzi kwa ajili ya kutoa dhamana kwa taasisi za kifedha za ili ziwe zinakopesheka na kukuza uwezo wa taasisi hizo za fedha.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT), Naibu Gavana wa Fedha na Uchumi wa BoT Dk. Yamungu Kayandabila, amefafanua BoT imeingia makubaliano hayo kwa niaba ya Serikali ili kuzijengea uwezo taasisi za kifedha za ndani nchini zimudu ushindani na kukuza uchumi.
“Tasisi hii ambayo tumeingia nayo makubaliano ni taasisi za kifedha ambayo inaingia ushirikiano nan chi mbalimbali kupitia Benki Kuu katika kukuza masoko ya fedha , na katika kukuza huko masoko ya fedha wanafanyaje.
“Mnafahamu kuhusu  Ukwasi , kwa mfano mabenki yanakopeshana yenyewe kwa yenyewe wakati mwingine zile benki kubwa huwa sio rahisi kuzikopesha benki ndogo kwa hiyo wale wakubwa wanakopeshana wenyewe kwa wenyewe na benki ndogo wanaenda kwa wadogo wenzao.
“Kwa hiyo hii taasisi inakuja kuwa katikati maana yake naweza kufafanua bila kutaja benki , kwa benki A inataka mkopo Benki C basi taasisi hii itasimama kati na kutoa hiyo dhamana,”amesema Dk.Kayandabila.
Amefafanua kuwa hatua hiyo itawezesha kukua kwa soko la fedha nchini, uhakika wa usalama wa kifedha na kukuza mitaji kutoka hatua moja kwenda nyingine hivyo kuchochea uchumi wa nchi.
“Katika hatua hiyo kwa pamoja watahakikisha taasisi za fedha zikiwemo benki zinamudu uwezo wa kukopa nje na kujikopesha zenyewe,  taasisi hizo za kimataifa zikitoa uhakika wa dhamana ili kuzifanya benki kuwa na usalama wa kifedha,”amefafanua Dk.Kayandabila.
Ameongeza nchi za kama Uganda, Rwanda, Zambia, Ghana, Kenya ni wanufaika wa makubaliana hayo kwa muda mrefu ambayo ni fursa kwa kuwa taasisi za fedha nchini zitakuwa na dhamana ya uhakika.
 
Pia amesema taasisi hiyo itakuwa inazijengea uwezo benki mbalimbali kwenye utaalam wa masuala ya mambo ya masoko.“Kwa hiyo tutakuwa tunapata utalaamu mbalimbali kwa watu wetu kwa ujumla kwenye sekta ya fedha.
“Na sio sio kwenye benki peke yake bali sekta zote za fedha.Lakini sekta kubwa kwa maana ya mabenki watanufaika zaidi. Tumekuwa tukiona benki kubwa zimekuwa zikiwasahau benki ndogo.
“Wanasema  huyu hawezi kunirudishia pesa yangu au akija anasema nitalipisha karibu kajuu kidogo,”amefafanua Dk.Kayandabila alipokuwa akielezea kazi ya taasisi hiyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa City Benki ambaye pia ni  Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa benki za Tanzania (TBA) Geofrey Mchangila, amesema makubaliano hayo ni hatua kubwa ya kimapinduzi kwenye sekta ya fedha.
“Soko la fedha kwa benki zaidi ya 45 nchini lilikuwa na changamoto ya kukosa dhamana hasa kwa zile benki za chini, kati na juu kuweza kukopeshana kwa muda mfupi.Katika mgawanyo huo wa benki tulikuwa hatuwezi kukopeshana sawa au kuwa na riba zinazofanana kutokana na
kutoaminiana,”amesema.
Amesema  lakini dhamana hiyo  itasaidia kukua kimitaji kwakuwa benki ndogo inaweza kukopa sawa na benki kubwa kwa sasa kulingana na dhamana iliyopo na hali hiyo itakuwa chachu kwa benki hizo kuwa na uhakika wa usalama wa kifedha na kukuza mitaji kutoka hatua moja kwenda nyingine hivyo kuchochea uchumi wa nchi.
Wakati huo huo Mkuu wa Fedha , Ubunifu na Masoko ya Mitaji Idara ya Maendeleo ya Sekta Binafsi na Fedha katika Kamisheni ya Uchumi ya Umoja wa Barani Afrika(ECA) Sonia Essobmadje ameeleza  makubaliano hayo yanakwenda kuendeleza soko la fedha nchini.Naibu Gavana, Sera za Uchumi na Fedha, Dkt. Yamungu Kayandabila(kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Maendeleo ya Masoko ya Fedha- Frontclear Philip Buyskes wakisaini makubaliano itakayowezesha kuendeleza sekta ya fedha nchini.Naibu Gavana, Sera za Uchumi na Fedha, Dkt. Yamungu Kayandabila(kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Maendeleo ya Masoko ya Fedha- Frontclear Philip Buyskes wakipeana mikono baada ya kusaini hati ya makubaliano ya kuendeleza sekta ya fedha nchini.Wadau mbalimbali kutoka taasisi za fedha nchini wakiwa kwenye ukumbi wa Benki Kuu Tanzania(BoT) wakishuhudia tukio la utiwaji saini makubaliano ya kuendeleza sekta ya fedha nchini yaliyofanywa kati ya BoT na Taasisi ya Frontclear ya nchini Uholanzi.
Naibu Gavana, Sera za Uchumi na Fedha, Dkt. Yamungu Kayandabila akifafanua jambo kwa wadau wa sekta ya fedha.

    

No comments :

Post a Comment