RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amemteua Angellah Jasmine Kairuki kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wakati huo huo amemteua kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI.
RAIS amefanya uteuzi huo Oktoba 2, 2022 KATIKA mabadiliko madogo aliyoyafanya kwenye Baraza lake.
Mhe. Kairuki sio mgeni kwenye Baraza hilo, ameshawahi kuteuliwa mara kadhaa.
Taarifa kamili iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasilisho ya Rais Ikulu iliyosainiwa na Mkurugenzi wake Bi. Zuhra Yunus inaeleza zaidi hapo chini.
No comments :
Post a Comment