Tuesday, October 4, 2022

Airtel Yazindua Maadhimisho Ya Wiki Ya Huduma Kwa Wateja




Wafanyakazi wa Kitengo cha Huduma kwa wateja wakiongozwa na Mkurugenzi wa Kitengo hicho Adriana Lyamba (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni wakishiriki kwenye kukata keki kuashiria kuzindua maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa wateja. Airtel imetangaza matukio tofauti ambayo yataambana na maadhimisho hayo ikiwemo kutoa msaada kwa watoto walio kwenye mazingira magumu.


 Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja Airtel Tanzania Adrian Lyamba (kushoto akiongea na Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Mary Msuya (wa pili kulia) na Meneja Elimu na Uhamashishaji wa Baraza hilo Hillarly Tesha ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa wateja. Wa pili kushoto ni Meneja Uhusiano Airtel Jennifer Mbuya.


Mkurugenzi Mtendaji Airtel Tanzania Dinesh Balsingh (kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa kampuni hiyo Adriana Lyamba wakimsikiliza mfanya kazi wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja mara baada ya kuzindua Wiki ya Huduma kwa wateja. Airtel imetangaza matukio tofauti ambayo yataambana na maadhimisho hayo ikiwemo kutoa msaada kwa watoto walio kwenye mazingira magumu.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa wateja ambapo kwa wiki nzima hii, Airtel itakuwa ikifanya maonyesho ya huduma na bidhaa zake.


Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa maadhimisho hayo, Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa wateja Airtel Tanzania Adriana Lyamba alisema kuwa hii Wiki ya Huduma kwa wateja inatoa fursa nyingine kwa Airtel kujiweka karibu na wateja wake ambao ni watu muhimu sana kwenye biashara yetu. ‘Huku kauli mbiu ya Wiki ya Huduma kwa wateja ikiwa ni furahia huduma, Airtel inajivunia kwa Watanzania kuwa wateja wetu na tunahidi kuendelea kutoa huduma bora na za kisasa, alisema Lyamba.

‘Moja kati ya hatua ambazo Airtel tuweza kuzipiga vizuri na tunazojivunia ni teknolojia. Tunayo furaha kubwa kuwa kwa sasa wateja wetu wanaweza kutumia teknolojia na kujihudumia papo hapo. Wateja wa Airtel kwa wanaweza kupata LUKU TOKEN kwa kujihudumia mwenyewe, kurudisha muamala uliokosewa, kurudisha laini ya simu iliyopotea bila kuongea na mtoa huduma wa Airtel. Huduma zote hizi mteja anaweza kuzipata kwa urahisi na hii ni moja ya faraja yetu tunayojivunia kwenye teknolojia kama watoa huduma, Lyamba alisema.

Meneja Huduma kwa wateja Celina Njuju alisema kuwa kwenye maadhimisho haya ya wiki ya huduma kwa Airtel itajikita kwenye kushiriki kwenye matukio yanaogusa jamii moja moja. ‘Airtel kwa muda mrefu tumekuwa tukishirikiana na jamii inayotuzunguka kwenya masuala ya afya na elimu. Kwenye wiki hii ya maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa wateja, tutaembelea na kuwapa faraja watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu kama ishara ya kuonyesha upendo, Njuju alisema.

Njuju aliongeza kuwa ili kuendana na kauli mbiu ya Wiki ya Huduma kwa wateja kwa mwaka huu ya – Sherehekea Huduma, Airtel itaendelea kutoa huduma zenye ubora wa ili kuendelea kuendana na mabadaliko ya teknolojia. Alisema pia Airtel imeendelea na juhudi za kulete huduma zake karibu kwa wateja ambapo mpaka sasa tunayo maduka ya Airtel Money Branches Zaidi ya 3,000 nchini kote ambayo yanatoa huduma na bidhaa zake zote bila mteja kutembea kwa umbali mrefu.

No comments :

Post a Comment