Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma NSSF, Bi. Lulu Mengele (kushoto), akimueleza Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Uundaji na Uendelezaji wa Vikundi vya Huduma Ndogo za Fedha Kanda ya Nyanda za Juu Kuisini (MVITA) yenye ofisi zake jijini Mbeya, Bw. Bosco Ndelwa jinsi Mpango wa Sekta Isiyo Rasmi unavyoweza kuwasaidia wanachama wa MVITA.
Afisa Uhusiano Mwandamizi NSSF, Bi. Aisha Sango (kushoto) akimkabidhi zawadi ya T-shirt Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Uundaji na Uendelezaji wa Vikundi vya Huduma Ndogo za Fedha Kanda ya Nyanda za Juu Kuisini (MVITA) yenye ofisi zake jijini Mbeya, Bw. Bosco Ndelwa mara baada ya kutembelea baanda la NSSF Agosti 4, 2022.
Afisa Uhusiano Mwandamizi NSSF, Bi. Aisha Sango (kulia) akitoa elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa wananchi waliotembelea banda la Mfuko huo Agosti 4, 2022.
Afisa wa NSSF, Bi. Fatma Nyasama (kulia), akitoa elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa mwananchi huyu aliyetembelea banda la NSSF Agosti 4, 2022.
Afisa Uhusiano Mwandamizi NSSF, Bi. Aisha Sango (kushoto) akitoa elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa wananchi waliotembelea banda la Mfuko huo Agosti 4, 2022.
NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, MBEYA
MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya Uundaji na Uendelezaji wa Vikundi vya Huduma Ndogo za Fedha Kanda ya Nyanda za Juu Kuisini (MVITA) yenye ofisi zake jijini Mbeya, Bw. Bosco Stephan Ndelwa, amesema amevutiwa na Skimu ya NSSF ya Mpango wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii kwa Sekta Isiyo Rasmi kwani inakwenda sambamba na lengo la kuundwa kwa vikundi vyao.
Bw. Ndelwa ameyasema hayo alipotembelea banda la NSSF kwenye Maonesho ya Nanenane Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya Agosti 4, 2022.
“Furaha yangu kubwa ni kwamba wataalamu hapa wamenielimisha umuhimu wa Mpango huo na binafsi nimefarijika na kuvutiwa sana, mimi mwenyewe nimeshawishika kujiunga na mpango huo wa uchangiaji wa Hiari.” Alisema
Alisema kwa sasa MVITA ina jumla ya wanachama 887 na wako katika wilaya nne za Mkoa ambazo ni Mbeya Mjini, Mbeya Vijijini, Rungwe na Kyela.
Akifafanua zaidi alisema vikundi vya mijini vina wanachama kati ya 20 hadi 25 wakati vilivyoko vijijini vina wanachama wanaofikia 30 kwa kila kikundi.
“Vikundi vya mijini sehemu kubwa wanajishughulisha na biashara wakati wenzao wa vijijini shughuli zao kubwa ni kilimo na biashara.” Alifafanua Bw. Ndelwa.
Alisema vikundi hivyo vinahusu maisha ya watu na wanapofundisha kuhusu masuala ya fedha wamebaini kuwa huduma ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii hususan NSSF bado haijawafikia.
“Kupitia elimu hii niliyoipata hapa nimetamani kwa kiwango cha juu sana pia iwafikie wanachama wetu ili waweze kujiunga na kuchangia kwenye Mfuko huu kwa manufaa yao wenyewe.” Alisisitiza.
Awali Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma, NSSF, Bi. Lulu Mengele alisema Mpango huo wa Sekta Isiyo Rasmi unalenga makundi ya Wajasiriamali na wote ambao wanajipatia kipato halali.
“Kama wanafanya kazi na wanapata kipato, sehemu sahihi ya kujiwekea akiba yao ni Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii, (NSSF), ili pale uwezo wa kufanya kazi unapokoma, NSSF inakuwa kama sehemu yao ya kuwapatia mshahara.” Alisema.
Alisema Mwanachama aliye katika Mpango huu atatakiwa kuchangia kila mwezi na kima cha chini cha uchangiaji ni shilingi elfu 20,000/=.
Alisema Wananchi wote wanaofanya kazi ya kujipatia kipato halali, Mfuko wao wa Hifadhi ya Jamii ni NSSF, na lengo la kuwepo kwenye Maonesho hayo ni kutoa elimu ya Hifadhi ya Jamii na kwamba Mfuko uko tayari kushirikiana na MVITA kutoa elimu zaidi kwa wanakikundi ili waweze kuelewa umuhimu wa kujiwekea akiba kwa manufaa ya sasa na baadaye.
No comments :
Post a Comment