Monday, August 22, 2022

NBM YATENGA KIFURUSHI MAALAUM KUWAHUDUMIA WAALIMU SONGEA

Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi- Bi Aikansia Muro(watatu kulia) akipongezana na Mkuu wa Wilaya ya Songea, Mhe. Pololet Mgema wakati wa Uzinduzi wa Kifurushi cha Mwalimu Spesho Mkoani Songea. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Labani Thomas.

 

Kwa kutambua umuhimu wa walimu na mchango wao katika mafanikio ya Benki ya NMB, taasisi hiyo kubwa kuliko zote za fedha nchini imeanzisha kifurushi maalum wa kuihudumia kada hii nyeti katika ujenzi wa taifa.

Kifurushi hicho cha “Mwalimu Spesho – Umetufunza Tunakutunza” kimetangazwa rasmi jana huko Songea Mkoani Ruvuma wakati wa kongamano la walimu lililoandaliwa na benki hiyo.

Akiitambulisha Kifurushi hiyo, Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi, Bi Aikansia Muro, alisema Mwalimu Spesho ni suluhisho inayojumuisha huduma zote za kumwezesha mwalimu kukidhi mahitaji yao mbalimbali Mkoani Songea.

Huduma hizo ni pamoja na mikopo yenye riba nafuu, ikiwemo ya walimu kujiendeleza kielimu yeye na watoto wake na kuwasomesha watoto wao, mikopo ya biashara ndogondogo, ujenzi, vyombo vya moto kama bodaboda na pikipiki za miguu mitatu.

Walimu pia watapata mkopo wa bima yaani Insurance Premium Finance (IPF), ambayo inawezesha kulipa bima kujikinga na majanga mbalimbali. Lakini pia, mikopo ya pembejeo na mashine za kilimo; fursa za kushiriki promosheni na kujishindia zawadi mbalimbali pamoja na kupata elimu ya masuala ya kifedha na faida nyingine lukuki.

Mgeni rasmi kwenye shughuli hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Labani Thomas, alisema NMB ni benki ya kuigwa linapokuja swala la kuwajali walimu na kuwasihi walimu hao kuelewa vizuri huduma zinazotolewa na benki hiyo ili waweze kunufaika nazo.

Mpaka sasa, NMB kupitia Mwalimu Spesho imewafikia Walimu wa Mikoa ya Dodoma, Singida, Morogoro, Manyara, Arusha, Kilimajaro, Tanga, Mwanza, Kagera, Mkuranga, Dar es Salaam, Nachingwea na Songea na bado wanaendelea kufikia Mikoa mingine.

No comments :

Post a Comment