Monday, August 1, 2022

Dar kuwa jiji kubwa ifikapo 2030

jijipic

By Mwandishi Wetu

Dar es Salaam imeingia katika majiji tisa yanayotegemewa kuwa megacities ifikapo mwaka 2030 wakati idadi ya wakazi wake itakapoongezeka kwa asilimia 45.

Megacity ni jiji ambalo idadi ya wakazi wake imefikia au kupita watu milioni 10 na hivyo kuwa kitovu cha shughuli za kiuchumi kwa nchi yake.

Kwa mujibu wa tovuti ya jarida la Element, kwa sasa Dar inakadiriwa kuwa na watu milioni 7.4 na ifikapo mwaka 2030 inatarajiwa kuwa na watu milioni 10.79, ikiwa ni ongezeko la asilimia 45.

Katika nchi nyingi za kipato cha juu, kama Marekani, Canada, Australia, Japan na nchi nyingine za Mashariki ya Kati, zaidi ya asilimia 80 ya watu wake wanaishi mijini, wakati katika nchi maskini wengi wanaishi vijijini na hivyo uwezekano wa wengi kuhamia mijini ni mkubwa. Kwa hiyo majiji mengi yanayotarajiwa kufikia hadhi ya megacity yako katika nchi zinazoendelea.

Majiji mengine yaliyo katika orodha hiyo ni Seoul, nchini Korea Kusini ambao una watu milioni 9.98 na ifikapo 2030 litakuwa na watu milioni 10.16, London (watu milioni 9.5-- milioni 10.2, Chengdu- China (milioni 9.5- milioni 10.7), Nanjing- Cjina (milioni 9.4- milioni 11.01 na Tehran-Iran (milioni 9.4- milioni 10.2)

Miji mingine ni Ho Chi Minh-Vietnam yenye watu milioni 9.08 na inatarajiwa kufikisha watu milioni 11.05, Luanda-Angola (milioni 8.95 - milioni 12.1, Ahmedabad-India yenye watu milioni 8.45 na itafikisha watu milioni 10.15 ifikapo mwaka 2030.

No comments :

Post a Comment