Tuesday, July 5, 2022

ZAIDI YA ASILIMIA 85 YA HUDUMA ZA WCF ZINAPATIKANA MTANDAONI


Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma (kulia) akimuhudumia mwananchi aliyetembelea banda la Mfuko ili kupata uelewa wa Fidia kwa Wafanyakazi
Bi. Fransisca Kweka, (kulia), Mwanasheria Mwandamizi, WCF, akitoa elimu kuhusu shughuli za Mfuko.
Bw. Josephat Mshana, Afisa Mfawidhi WCF, Temeke (kulia), akimuhudumia mwananchi aliyefika kwenye banda la Mfuko huo.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. Masha Mshomba (kulia) akizungumza na Bw. Tenga alipotembelea banda la WCF, Julai 4, 2022.
Mkuu wa Kitengo cha Takwimu  Bw. James Tenga, (kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Elimu kwa Umma, Bi. Laura Kunenge wakijadiliana
Bw. Mshomba akisalimiana na wafanyakazi wa WCF alipotembelea banda hilo.
Bi. Fransisca Kweka, (kulia), Mwanasheria Mwandamizi, WCF, akitoa elimu kuhusu shughuli za Mfuko.
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba wakiwa kwenye banda la PSSSF.

NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID.

MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umepiga hatua kubwa katika matumizi ya TEHAMA ambapo licha ya uchanga wake karibu asilimia 85 ya huduma zake sasa zinapatikana mtandaoni.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Dkt. John Mduma amesema hayo kwenye banda la WCF kwenye Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye viwanja vya Julius Nyarere (maarufu Sabasaba).

“Sio tu tunawaondolea usumbufu na kuokoa muda lakini pia huduma hii inawapunguzia gharama wateja kwa maana ya waajiri na wafanyakazi kwasababu hawana haja ya kuja moja kwa moja kuonana na sisi watapata huduma hizi wakati wowote mahali popote huko huko waliko kupitia mtandao.” Alisema.

Akifafanua kuhusu huduma zitolewazo kwenye banda hilo la WCF lililoko mtaa wa Mabalozi wakati huu wa Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Elimu kwa Umma, Bi. Laura Kunenge alisema wanachama wa WCF na wananchi kwa ujumla watakapotembelea kwenye banda hilo watapata elimu kuhusu Malipo ya Fidia kwa Mfanyakazi aliyeumia, kuugua au kufariki kutokana na kazi anazofanya kwa mujibu wa mkataba, lakini pia uelewa wa jumla kuhusu shughuli zinazotekelezwa na WCF.

Aidha utakapotembelea banda hilo licha ya kupata  uelewa hiyo, pia mwaajiri anaweza kujisajili na kupata cheti chake cha usajili lakini mfanyakazi naye anaweza kupata taarifa za michango inayowasilishwa na mwajiri wake kwenye Mfuko, alifafanua zaidi Mkuu wa Kitengo cha Takwimu  Bw. James Tenga.

No comments :

Post a Comment