Thursday, July 7, 2022

MAONESHO SABASABA 2022: MWENYEKITI WA BODI WCF ATEMBELEA BANDA LA MFUKO NA KURIDHISHWA NA HUDUMA BORA

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Emmanuel Humba (wapili kulia), Makamu wake, Bi. Rifai Mkumba (wakwanza kulia) na Mjumbe wa Bodi Bw. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Emmanuel Humba (wapili kulia), Makamu wake, Bi. Rifai Mkumba Makamu wake, Bi. Rifai Mkumba (katikati) na Mjumbe wa Bodi Bw. Abdulaziz Alladin Shambe wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma kutembelea banda hilo.
Mwenyekiti wa Bodi na ujumbe wake walipotembelea banda la USHIRIKIANO la Mifuko ya PSSSF na NSSF.
Mwenyekiti wa Bodi Bw. Emmanuel Humba na ujumbe wake akiwemo Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma walipotembeela banda la BoT.

Ujumbe wa Mwenyekiti wa Bodi ukiwa banda la NIC
Ujumbe wa Mwenyekiti wa Bodi ukiwa banda la NHIF
Ujumbe wa Mwenyekiti wa Bodi ukiwa band ala USHIRIKIANO  la NSSF na PSSSF
Ujumbe w aMwenyekiti wa Bodi ukiwa katika banda la BoT
Ujumbe wa Mwenyekiti w aBodi ukiwa banda la Bakhresa Group
Ujumbe w aMwenyekiti wa Bodi ukiwa banda la COSTECH.

NA MWANDISHI WETU, SABASABA

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Emmanuel Humba amewahimiza Waajiri na Wafanyakazi wanaotembelea kwenye Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, (Maarufu Sabasaba) kufika katika

banda la WCF ili kujionea jinsi Huduma zitolewazo na Mfuko huo zinavyoendeshwa kisasa.

Bw. Humba ameyasema hayo Julai 6, 2022 wakati yeye na baadhi ya wajumbe walipotembelea Banda la Mfuko huo ili kujionea jinsi Wafanyakazi wa WCF wanavyotoa Huduma kwa wananchi.

“Lakini pia nawaomba Watanzania wote wanaotembela viwanja vya Sabasaba kwenye Maonesho haya wapite kwenye banda la Mfuko huu ili waweze kujifunza masuala ya Fidia wataona jinsi Mfuko ulivyo jipanga kuhakikisha Wafanyakazi wanapoumia, kuugua au wategemezi wa Mfanyakazi aliyefariki kutoakna na Kazi wanavyofaidika na Mafao yatolewayo na Mfuko.

“Niwahakikishie wote wanaotembelea katika banda nimeridhiahwa na jinsi Huduma zinavyotolewa na watahudumiwa kwa haraka na hizo ni sawa na zile zinazotolewa kwenye ofisi za Mfuko.” Alisisitiza.

Pia aliwaasa Wafanyakazi wa WCF wanaotoa huduma katika banda hilo, kuhakikisha wanawasikiliza wote wanaofika kuhudumiwa na kutatua changamoto zao kama zitakuwepo ili wanapotoka wawe wameridhika na Huduma za Mfuko.

Aidha Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini, Bi. Rifai Mkumba alisema kulingana na kauli mbiu ya Mwaka huu inayosema “Tanzania Mahali Sahii pa Biashara na Uwekezaji, Mfuko unauthibitishia Umma kuwa unaunga mkono Uwekezaji na Biashara na ndio maana waajiri wamepunguziwa dhima ya kuangalia usalama na maisha ya wafanyakazi wanapopata ajali wakiwa kazini na sasa kazi hiyo inafanywa na Mfuko.

Naye Mjumbe wa Bodi Bw. Abdulaziz Alladin Shambe ameonyesha matumaini yake kuwa katika Maonesho hayo Mfuko utavuna wanachama kwani wanaoshiriki ni taasisi na wafanyakazi ambao ndio wadau wakubwa wa Mfuko.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma, alisema Mfuko wa umepiga hatua kubwa katika matumizi ya TEHAMA ambapo licha ya uchanga wake karibu asilimia 85 ya huduma zake sasa zinapatikana mtandaoni.

“Sio tu tunawaondolea usumbufu na kuokoa muda lakini piahuduma hii inawapunguzia gharama wateja kwa maana ya waajiri na wafanyakazi kwasababu hawana haja ya kuja moja kwa moja kuonana na sisi watapata huduma hizi wakati wowote mahali popote huko huko waliko kupitia mtandaoni.” Alisema.

Ujumbe huo wa Mwenyekiti wa Bodi pia ulitembelea katika Mabanda ya wadau wa WCF, yakiwemo ya COSTECH, NSSF na PSSSF, BoT na Bakhresa Group of Companies.


No comments :

Post a Comment