Waziri wa Tamisemi, Innocent BashungwaBy Beldina Nyakeke
Tarime. Waziri wa Tamisemi, Innocent Bashungwa amemsimamisha kazi
mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Masasi mkoani Mtwara, Apoo Tindwa kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za kusaidia maendeleo kwa jamii (CSR) kutoka mgodi wa dhahabu wa Barrick North Mara.Apoo ambaye kabla ya kuhamishiwa mkoani Mtwara alikuwa mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Tarime vijijini ambapo pamoja na watu wengine wanatuhumiwa kwa ubadhirifu wa zaidi ya Sh5.6 bilioni zilizotolewa na mgodi huo kwaajili ya miradi ya maendeleo katika vijiji 11 vinavyozunguka mgodi huo uliopo wilayani Tarime.
Bashungwa amtengaza maamuzi hayo leo Mei 6, 2022 katika kijiji cha Genkuru wilayani Tarime baada ya kufanya ukaguzi wa ujenzi wa kituo cha afya cha Genkuru kilicho gharimu zaidi ya Sh700 milioni ambacho hadi sasa hakijakamilika licha ya kugharimu kiasi hicho cha fedha, fedha ambazo ni sehemu ya fedha za CSR.
No comments :
Post a Comment