Sunday, May 15, 2022

ROYAL TOUR YAINUFAISHA TANZANIA, WATALII WAMWAGIKA


Na Janeth Raphael - Dodoma
Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Kasim Majaliwa amesema Filamu ya Royal Tour imefanikiwa kuleta watalii zaidi ya mia saba ambapo amesema hayo yote ni matokeo ya filamu ya Royal Tour

Majaliwa amebainisha hayo leo Mei 15,2022 katika uzinduzi wa Filamu ya “Tanzania The Royal Tour mkoa wa Dodoma ,unaoendelea usiku huu katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre.

Waziri Mkuu Majaliwa akizungumza kwa niaba ya Makamu wa Rais ,Dkt. Philip Mpango katika uzinduzi huo amesema Filamu ya Royal Tour ina mchango mkubwa katika kuchochea utalii hapa nchini hivyo ni vyema kila mmoja kuiunga mkono.

“Filamu hii imeleta tija kubwa katika sekta ya utalii hapa nchini na takriban watalii 796 wamekuja kutokana na Royal Tour”amesema.

Kutokana na umuhimu wa filamu hiyo,waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka watanzania kuwa wamoja huku akitoa onyo kwa wale wanaobeza kuacha mara moja tabia hiyo.


Kuhusu kuhusu mkoa wa Dodoma ,Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema mkoa wa Dodoma una fursa nyingi za utalii ikiwemo utalii wa hoteli kubwa za kisasa ,hivyo ni muhimu kila mmoja kuchangamkia fursa hizo katika uwekeza

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Royal Tour Dkt. Hassan Abbas amesema Filamu hiyo inakwenda kuwafikia watu bilioni mbili Duniani na makisio ya awali ilikuwa ni Zaidi ya watu bilioni moja lakini pamekuwa na msukumo mkubwa .

Naye,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka amesema serikali ya mkoa wa Dodoma ina nafasi kubwa katika kuufanya mkoa wa Dodoma kuwa mkoa wa utalii nchini.

Mtaka amesema Mkoa wa Dodoma una sehemu mbalimbali za utalii ikiwemo utalii wa michoro ya mapango Kondoa , Dodoma ,utalii wa Zabibu.

Aidha,Mtaka amesema ,katika mkoa wa Dodoma una utalii wa miradi mbalimbali na kuwataka watanzania kuchangamkia fursa za mkoa.

“Dodoma tuna utalii wa miradi,tunatamani kila mtanzania apate fursa ya kuwekeza katika mkoa wa Dodoma ,tutahakikisha tunachepusha sekta binafsi mkoa wa Dodoma,na kuhakikisha unakuwa mkoa kila mfanyabiashara ananufaika na makao makuu ya nchi”amesema.

Kuhusu utalii wa mikutano Mkuu huyo wa mkoa amesema sasa mkoa wa Dodoma una una sehemu mbalimbali ya mikutano hivyo imekuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa sekta binafsi.

“Tunahamasisha utalii wa mikutano,watu waone ni fursa kubwa katika mkoa wa Dodoma ,Dodoma ni mji wa serikali itapendeza Zaidi katika kusaidia na kuchochea ukuaji wa sekta binafsi.

Uzinduzi wa Royal Tour Mkoa wa Dodoma umezinduliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Kassim Majaliwa kwa niaba ya Makamu wa Rais Dkt.Philip Mpango na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali ikiwemo mkuu wa Mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere,Waziri wa Maliasili na Utalii,Pindi Chana,Spika wabunge Dkt.Tulia Ackson ,wananchi na wafanyabiashara mkoa wa Dodoma ambapo unarushwa mbashara kupitia vyombo mbalimbali vya habari nchini.
















No comments :

Post a Comment