Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan
ameridhia mapendekezo ya nyongeza ya mshahara ikiwemo kima cha chini kwa
watumishi wa umma kwa 23.3%.
Mapendekezo hayo yaliyowasilishwa Ikulu ni mwendelezo wa kikao cha Mhe.
Nyongeza hiyo imefanyika kwa kuzingatia Pato la Taifa (GDP), mapato ya ndani
yanayotarajiwa kukusanywa katika mwaka 2022/2023 na hali ya uchumi wa ndani
na nje ya nchi.
Kutokana na hatua hiyo katika mwaka wa fedha 2022/2023, Serikali imepanga
kutumia kiasi cha Shilingi trilioni 9.7 kwa ajili ya kugharamia malipo ya mishahara
ya watumishi wote katika Serikali Kuu, Serikali za Mitaa, Taasisi na Wakala za
Serikali.
Hivyo bajeti ya mishahara ya mwaka 2022/23 ina ongezeko la Shilingi trilioni 1.59 sawa na 19.51% ikilinganishwa na bajeti ya mwaka wa fedha 2021/22.
Wakati huo huo, Rais Samia amepokea mapendekezo ya kanuni mpya ya Mafao ya
Pensheni kama Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA)
lilivyoomba Mei mosi, 2022.
Mhe. Rais Samia ameridhia na kuielekeza wizara yenye dhamana na masuala ya
hifadhi ya jamii kuendelea kushirikiana na TUCTA na Chama cha Waajiri nchini
(ATE) ili kukamilisha taratibu za kuhakikisha malipo ya mkupuo ya 25%
yaliokataliwa na wadau mwaka 2018 yanapandishwa hadi 33%.
Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu
No comments :
Post a Comment