Tuesday, May 31, 2022

BENKI YA NBC YATOA MAFUNZO KWA WAJASIRIAMALI ZAIDI YA 200 KILIMANJARO, YAWAWEKA KARIBU WATEJA WAKE

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Benki ya Taifa ya Biashara Dk Kassim Hussein (watatu kushoto), akikabidhi cheti cha kuhudhuria mafunzo ya uboreshaji wa uwendeshaji Biashara kwa Mteja wa Benki hiyo Procles Visent wakati wa hafla ya mafunzo hayo yalioandaliwa na Benki ya Nbc, Mkoa wa moshi wengine pichani kutoka kushoto ni Mkuu wa Kigengo cha wajasiliamali wa Benki ya Nbc Mussa Mwinyidaho, Mkurugenzi wa Biashara Elvis Ndunguru pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Taifa ya Biashara NBC, Nd Elibariki Masuke
Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya Taifa ya Biashara NBC Elvis Ndunguru (wapili kushoto) akitoa cheti cha kuhudhuria mafunzo ya uboreshaji wa uwendeshaji Biashara kwa  Mteja wa Nbc  Mkoa wa Moshi Laija  Mtenga wakati wa hafla ya mafunzo ya uboreshaji wa uwendeshaji Biashara yaliyotolewa kwa wateja wa NBC Mkoa wa Moshi wengine pichani ni Mkuu wa Kigengo cha wajasiliamali wa Benki hiyo Mussa Mwinyidaho, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NBC Dk Kassim pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Taifa ya Biashara NBC, Nd Elibariki Masuke.
Maofisa kutoka Benki ya NBC na uongozi wa mkoa wa Moshi wakiwa katika picha ya pamoja na Wahitimu wa mafunzo ya uboreshaji wa uwendeshaji Biashara yaliyotolewa na Benki ya Biashara NBC.

BENKI ya NBC imeendesha mafunzo ya ujasiriamali na uendeshaji wa biashara kwa wajasiriamali wa Mkoa wa Kilimanjaro kwaajili ya kuwaongezea ujuzi wa

kuendesha biashara zao, Mafunzo hayo yamefanyika Kiirumbe Social Halls, Mjini Moshi.

Zaidi ya mafunzo hayo, Benki ya NBC pia ilipata fursa ya kuwa na  wateja wenyeji zaidi ya 200 na kupata chakula cha jioni katika Dinner Gala iliyoandaliwa maalum na Benki ya NBC. 

Aidha Meneja wa Tawi la Benki ya NBC Moshi,Lazaro Mollel alisema lengo kubwa la kuwapa mafunzo na kuwaalika chakula cha jioni ni dhamira ya benki hiyo kutaka kuwaweka wateja wao karibu zaidi.


No comments :

Post a Comment