Friday, May 6, 2022

ALIYEKUWA MKUU WA WILAYA YA HAI OLE SABAYA AACHIWA HURU

Mahakama Kuu Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ya imemuachia huru aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro Lengai ole sabaya na wenzake wawiliwaliokua wamekata rufaa ya kupinga kuhukumiwa miaka 30 kwenda jela kila mmoja.

Uamuzi huo umetokea baada ya kubaini kuwa kulikuwa na mapungufu katika mwenendo mzima  kesi,pamoja na kutofautiana na mashahidi

"Hata hivyo,  Sabaya ataendelea kukaa mahabusu kutokana na kukabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi."

Rufaa hiyo ya jinai namba 129/2021 imeletwa na Sabaya na wenzake hao wakipinga hukumu ya kifungo cha miaka 30 jela iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Aidha Sabaya na wenzake walikuwa wakipinga hukumu dhidi yao kwakuwa Mnamba mbili Silvester Nyegu na namba tatu Daniel Mbura hawakupewa haki ya kumhoji Shahidi namba mbili wa Jamhuri na kutokufanya hivyo kunawanyima haki yao ya msingi.

Waomba rufaa hao wanawakilishwa na  Majura Magafu, (wakili)Moses Mahuna(wakili) Fauzia Mustafa,( wakili)Sylvster Kahunduka(wakili) Edmund Ngemela na Fridolin Bwemelo(wakili )ambao kwa pamoja walipinga hoja za wajibu rufaa na kuomba mahakama iridhie hoja zao 14 za rufaa na kuwaachia wateja wao huru.

Wajibu rufaa hiyo Upande wa Jamhuri uliwakilishwa na Mawakili wa Serikali waandamizi Ofmedy Mtenga, Verediana Mlenza na Baraka Mgaya ambao, wanapinga hoja za mawakili wa waomba rufaa na kuiomba mahakama itupilie mbali rufaa hiyo.

Awali Oktoba 15, 2021 Hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo aliwahukumu Sabaya na wenzake wawili kifungo cha miaka 30 kila mmoja, baada ya kuwatia hatiani kwa makosa matatu ikiwamo unyang'anyi wa kutumia silaha.

No comments :

Post a Comment