Monday, April 25, 2022

Vodacom, Smart Lab Watoa Fursa Kwa Kampuni Chipukizi Za Kiteknolojia Kwa Tsh 500 Mil

Mkuu wa Kampuni ya Smart Lab, Edwin Bruno akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu uzinduzi wa pili wa programu maalumu kwa ajili ya wajasiriamali chipukizi ujulikanayo kama “Vodacom Digital Accelerator” kwa ushirikiano na shirikisha kampuni yake na kampuni ya Vodacom. Kushoto ni Mkurugenzi wa Digitali na Huduma ziada wa Vodacom Plc, Nguvu Kamando.
Mkurugenzi wa Digitali na Huduma ziada wa Vodacom Plc, Nguvu Kamando, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa pili wa programu maalumu kwa ajili ya wajasiriamali chipukizi ujulikanayo kama “Vodacom Digital Accelerator”kwa ushirikiano na kampuni
ya Smart Lab. Kulia ni Mkuu wa Kampuni ya Smart Lab, Edwin Bruno.

KATIKA kuendelea kukuza uchumi na vipaji kwa vijana, kampuni ya Vodacom Tanzania PLC kwa kushirikiana na Smart Lab wamezindua msimu wa pili wa programu maalumu kwa ajili ya wajasiriamali chipukizi, ijulikanayo kama “Vodacom Digital Accelerator.”

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo leo Aprili 26, 2022 jijini Dar es Salaam,

Mkurugenzi wa Dijitali na Huduma za Ziada za Vodacom, Nguvu Kamando amesema programu hiyo imetenga kukuza kampuni chipukizi zilizojikita kwenye teknolojia na kuziwezesha kutengeneza faida.

Amesema kupitia programu hiyo jumla ya Sh. Milioni 500 zitatumik,a ambapo wajasiliamali mbalimbali watawezeshwa na kupatiwa uzoefu ili kuendelea kukuza chachu za kufanya ubunifu zitakazoleta tija kwa jamii nzima.

“Uvumbuzi na ujarisiamali ndiyo mzizi mkuu katika kuhakikisha zana yetu ya kuipeleka Tanzania katika ulimwengu wa kidijitali, inatimia, ushirikiano wetu na Smart Lab, ambao wamejikita kutoa mafunzo na kuwaongoza wajasiriamali wanaoshiriki umetupatia uzoefu zaidi,” amesema Kamando.

Mafanikio ya programu hii ni kuona maendeleo yanayofanywa na kampuni chipukizi zinazoshiriki ikiwa ni pamoja na kukuza mtaji kutoka kwa wawekezaji, kumalizika kwa uundwaji wa bidhaa na kukua kwa watendaji wa kampuni.


Amesema, msimu wa kwanza uliozinduliwa mwaka 2019 jumla ya maombi 500 yalipokelewa kutoka mikoa 18 na kampuni chipukizi nne ziliibuka washindi ambazo Smartclass inayojihusisha na masuala ya elimu, Hashtag Pools inayoshughulika na masuala ya biashara ya kimtandao na kampuni mbili za masuala ya afya ambazo ni Nisiima eDispensary na MyHI.

"Tunatarajia programu ya mwaka huu kuwa kubwa na bora zaidi na itaendelea kujikita kufanya kazi na kampuni chipukizi zinazojihusisha na masuala ya mawasiliano, habari, afya, elimu, kilimo, utalii na biashara ya kimtandao.

Utelekezaji wa programu hii utashirikisha wadau na washirika mbalimbali.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Smart Africa Group (SAG), Edwin Bruno ambaye pia ni mshirika wa Smart Lab, amesema, “tunafurahi kuwa sehemu ya ‘Vodacom Accelerrator’ na kwa pamoja tunatarajia kutengeneza fursa kwa vijana waliojikita kwenye teknonojia ili kukuza kampuni na kazi zao na kuonyesha kuwa vijana wa kitanzania wanaweza kushindana kwenye kiwango cha kimataifa kwenye masuala ya ujasiriamali uliojikikita kwenye ya teknolojia.

Amesema shughuli za kivumbuzi nchini zimepiga hatua kubwa, miaka michache iliyopita na Smart Lab pamoja na Vodacom Tanzania tumeongoza njia hasa hasa kwenye uvumbuzi kupitia makampuni ya biashara na kuonyesha vijana kuwa inawezekana kujenga kampuni zikafanikiwa nchini, kama ambavyo Smart Africa Group na Vodacom zilijengwa nchini Tanzania.

No comments :

Post a Comment