Monday, April 11, 2022

SERIKALI YATAJA HATUA ZA KUPUNGUZA BEI ZA BIDHAA

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akitoa taarifa juu ya hali ya uchumi na kupanda kwa bei za bidhaa wakati wa mkutano na waandishi wa habari akiwa na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (hayupo pichani), Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akielza jambo juu ya toa taarifa juu ya kupanda kwa bei za bidhaa wakati wa mkutano na waandishi wa habari akiwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani), Jijini Dar es Salaam.

SERIKALI imetaja hatua inazokusudia kuchukua ili kupunguza bei za bidhaa nchini.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.Mwigulu Lameck Nchemba wakati wa mkutano wa pamoja (joint press conference) na

Waziri wa Uwekezaji, viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya hatua hizo Dkt. Nchemba alitaja "Tutapunguza kodi ya sukari kwa kiwango so chini ya asilimia 10%, baada ya hapo tutaangalia mwezi mmoja au miwili na tutakapokuwa tunapitisha sheria mpya ya kodi tutaangalia mambo yanaendeleaje." Alisema.

"Tutapunguza sehemu ya gharama ambayo ilikuwa inaongezeka katika vifaa vya usafiri, tukipunguza gharama kwenye mafuta na vifaa hivyo moja kwa moja tunaamini itashusha gharama na bei za bidhaa nyingine,"alisisitiza Mhe. Waziri wa Fedha.

Pia alisema, Serikali itaangalia gharama ambazo zinaihusu kwenye mafuta ili kuona kiwango ambacho itapunguza.

"Timu yetu ya wataalamu itakaa ndani ya wiki moja na inaweza kuwa imeshapata jibu ili tuweze kuchukua hatua." Alibainisha Dkt. Nchemba.


No comments :

Post a Comment