Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (kulia), akizungumza katika Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Serikali ya Tanzania na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), katika Hoteli ya Sea Cliff, jijini Dar es Salaam, leo. Wapili kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akismikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula alipokuwa akimfafanulia jambo, baada ya kufunguliwa kwa Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Serikali ya Tanzania na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), uliofanyika katika Hoteli ya Sea Cliff, jijini Dar es Salaam, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula, akizungumza katika Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Serikali ya Tanzania na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), uliojadili masuala mbalimbali ya Wakimbizi Nchini, katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Sea Cliff, jijini Dar es Salaam, leo. Katikati ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, na kushoto ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Nchini, ZIatan Milisic. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (watatu kushoto waliokaa), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (wanne kulia), Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio (kushoto), na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine (wanne kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali ya Serikali na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), walioshiriki Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Serikali na UNHCR, jijini Dar es Salaam, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments :
Post a Comment