Monday, March 28, 2022

Profesa Ngowi aliliwa kila kona

professangoipic

By Elizabeth Edward

Dar es Salaam. Kifo cha gwiji wa uchumi na mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Profesa Honest Ngowi kimepokelewa kwa mshtuko na watu wa makundi tofauti na

wametumia kurasa zao za mitandao ya kijamii kumuelezea.

Habari za kifo cha Profesa Ngowi zilisambaa asubuhi ya leo zikieleza kuwa amefariki kwenye ajali kufuatia gari aliyokuwa akisafiria kuangukiwa na kontena eneo la Chalinze mkoani Pwani leo Machi 28, 2022.

Mbali na mchumi huyo ajali hiyo imegharimu pia maisha ya dereva wake aliyekuwa akimwendesha kuelekea mkoani Morogoro.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram mwanaharakati Godlisten Malisa ameandika, “Dunia imempoteza mtu muhimu sana, taifa limepoteza lulu sisi marafiki zako tumepoteza mtu aliyegusa maisha yetu kwa namna ya kipekee. Kwaheri kaka mkubwa, kwaheri Profesa Ngowi. Kwaheri mwalimu.”

Naye Mkuu wa wilaya ya Morogoro Albert Msando ameandika, “Pumzika kwa amani Profesa Ngowi, ulikuwa zaidi ya mwalimu. Ulitusimamia utafiti kwa upendo mkuu. Ulituelimisha kama rafiki zako. Ulitaka wakati wote tuwe bure kielimu na kifikra. Ulitujenga. Mzumbe na taifa limepoteza mtu muhimu sana.”

Mbunge wa Chalinze Ridhiwan Kikwete ameandika, “Sad indeed (huzuni kubwa) kumpoteza msomi na mchumi nguli. Mungu ndiye anajua sababu za kuletwa na kutwaliwa kwako. Pumzika kwa amani msomi. Mchango wako utaenziwa milele.”

No comments :

Post a Comment