Thursday, March 31, 2022

NMB Yanogesha Maonesho Njombe,Kuelekea Uzinduzi Wa Mbio Za Mwenge Kitaifa

Mkuu wa mkoa wa Njombe Waziri Kindamba akisaini kitabu baada ya kutembelea banda la benki tawi la Njombe katika maonesho yanayofanyika katika uwanja wa sabasaba.
Mkuu wa mkoa wa Njombe Waziri Kindamba akipongeza benki ya NMB kwa kujitokeza na kuonyesha ushirikiano kwa wananchi waliojitokeza katika uwanja wa Sabasaba mjini Njombe kuelekea zoezi la uzinduzi wa mbio za Mwenge mkoani Njombe.

Gudluck Shirima ni meneja wa tawi la benki ya NMB Njombe akielezea shughuli zinazofanywa na benki hiyo.

Na Amiri Kilagalila,Njombe


Wananchi mjini Njombe wameendelea kujitokeza kwa wingi katika maonesho yanayoendelea katikia uwanja wa sabasaba mjini Njombe kuelekea uwashaji wa mwenge kitaifa huku

wengi wao wakivutiwa na kutembelea banda la benki ya NMB na kuendelea kunufaika na elimu inayotolewa katika banda hilo.

Gudluck Shirima ni meneja wa tawi la benki ya NMB Njombe,akizungumza mara baada ya kutembelewa na mkuu wa mkoa wa Njombe katika banda hilo amesema mami ya wananchi wameendelea kunufaika na elimu mbali mbali ikiwemo ya ujasiriamali inayotolewa na benki hiyo.

“Tunawapa elimu ya ujasiriamali wateja wetu,elimu ya kibenki kwa maana ya akaunti mbali mbali,elimu ya mikopo inayopatikana ndani ya benki,bima pamoja na kujibu maswali mbali mbali amabyo yamekuwa yakiulizwa na wateja wetu”alisema Shirima

Vile vile amesema katika kuendelea kukuza uchumi wa wateja wao wameendelea kutoa mikopo kwa ajili ya usafirishaji.

“Tumekuwa tukitoa mikopo kwa ajili ya usafirishaji na katika shughuli ya uongezaji wa thamani ya nafaka tumekuwa tukiifanya,tuombe wananchi washirikiane na benki yetu ili waweze kuongeza mitaji na uwezo wao katika shughuli ambazo wamekuwa wakizifanya kila siku”alisema Shirima

Aidha kwa niaba ya benki hiyo ameishukuru serikali kwa kutoa nafasi ya maonesho na kutoa wito kwa wananchi kuendelea kujitokeza katika maonesho hayo.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Njombe Waziri Kindamba ameshukuru wadau hao kwa kujitokeza katika maonesho ili kuunga mkono juhudi za serikali pamoja na kuwafuata wananchi ili kuendelea kutoa elimu na huduma mbali mbali.

“Bila ya watu shughuli hainogi ninawashukuru sana kwa kuja na ninawaomba tuendelee kuwa pamoja mpaka inapofika shughuli ya uzinduzi wa Mwenge kwa umoja wetu”alisema Kindamba.

 

No comments :

Post a Comment