Mkurugenzi wa Oparesheni wa MDH Dkt. Nzovu Ulenga (kushoto) akikabidhi vifaa vya Tehama na machapisho vyenye thamani zaidi ya Mil. 105 kwa Kaimu Mkurugenzi msaidizi Epidemiolojia na udhibiti wa magonjwa kutoka Wizara ya Afya Dkt. Rogath Kishimba (kulia) leo jijini Dodoma.
Na. WAF - DODOMA
Na. WAF - DODOMA
Serikali kupitia Wizara ya Afya imepokea vifaa vya Tehama na machapisho vyenye thamani zaidi ya Mil. 105 kwa ajili ya kusambazwa kwenye vituo vya Afya ili kuboresha huduma za ufuatiliaji na udhibiti magonjwa ya milipuko nchini Tanzania.
Vifaa hivyo vimetolewa leo Februari 17,2022 na Shirika lisilo la kiserikali la "Management and Development for Health –(MDH)" kupitia ufadhili wa rasilimali fedha na ushauri wa kitaalam kutoka kituo cha kudhibiti magonjwa cha Marekani-CDC, ofisi ya Tanzania.
Akiongea wakati wa makabidhiano hayo Mkurugenzi wa Oparesheni wa MDH Dkt. Nzovu Ulenga amesema wamekabidhi vifaa hivyo ni pamoja na Kompyuta mpakato (laptops), vishwikwambi (tablets), projectors, Printers na vifaa mbalimbali vya stationary kwa ajili ya kazi za machapisho ya ripoti za kisayansi na maabara.
"MDH kupitia ufadhili huu, inapenda kutoa shukrani za dhati kwa wafadhili wetu CDC, Wizara ya Afya na TAMISEMI pamoja na wadau wetu wengine katika kubuni na kutekeleza mikakati yote ya Kisera na Kitaalam katika kufuatilia na kuthibiti magonjwa ya mlipuko yanayoathiri mfumo wa njia ya
upumuaji."amesema Dkt. Ulenga
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi msaidizi Epidemiolojia na udhibiti wa magonjwa kutoka Wizara ya Afya Dkt. Rogath Kishimba baada ya kupokea amesema vifaa hivyo vitakwenda kusaidia kutoa taarifa kwa vituo rasmi vya kukusanya taarifa za Magonjwa yanayoambukiza na yasiyoambukiza.
"Natoa Shukran kwa shirika la kudhibiti na kuzuia Magonjwa pamoja na shirika la MDH kwa kutoa vifaa hivi vitakavyo kwenda kurahisisha utendaji kazi na kuwahudumia wagonjwa kwa haraka." amesema Dkt. Kishimba
Vifaa hivyo pia vitakwenda kusaidia Katika kupambana na magonjwa ya mlipuko, katika maeneo matatu ambayo ni uwezo wa kutambua / kugundua visababishi vya magonjwa, pili ni kutoa taarifa kwa haraka na ubora na tatu ni kuchukua hatua sahihi za kupambana na ugonjwa husika kwa kufuata taraibu za Nchi na za kimataifa.
No comments :
Post a Comment